Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 56,608
- 93,379
Labda niulize sisi tuliosoma miaka ya nyuma na sasa kuna kitu gani kimebadirika?
Tulisoma bila kuwa na vitabu, hatukujuwa sylubus yoyote, Primary tuliwahi namba SAA 12 asubuhi na SAA 8 mchana ni mwisho wa masomo na kurudi nyumbani na wengi hatukusoma masomo ya ziada tuition lakini kulikuwa na vipanga balaa.
Sasa uvumilivu umenishinda, nina kitoto ni one of dependant wangu anaamka Saa 10 usiku saa 12 asubuhi anaanza tuition ya lazima shuleni anaendelea na masomo mpaka Saa 12 jioni kisa eti ni darasa la saba.
Sasa nimepitia repoti yake leo asubuhi hii ya annual examination sijafurahishwa nayo lakini remarks za class teacher ameandika Good.
Nimejiuliza sana darasa la Watoto 60 mtoto anakuwa wa 50 hii good inatoka wapi? OK average B lakini kutesa kote huku Watoto haya ndio matokeo yake? Na ieleweke wazi hii ni private school.
Sasa labda Mimi nimepitwa na wakati naomba mnielimishe huku ndio tulikofikia?
Ifike sasa Wazazi hasa kina mama tuache ushamba, ni bora kutafuta shule ya umma nzuri mtoto asome huko umuwekee usimamizi mzuri tu kuliko huu Utapeli tunaofanyiwa na hizi private school.
Anyway nisiwachoshe lakini sijafurahishwa kwakweli.