kax bedui Jr
Senior Member
- Aug 11, 2015
- 134
- 96
Ufafanuzi zaidi kwenye hili.Naona viatu vya Makonda vinampwaya ndugai,
Kupata viatu kwa size ya mguu anayovaa ni shida sana acha tu avae vikubwaNahisi Ndugu Ndugai Bado anapwaya sana katika nafasi yake ya uspika, ni mwaka wa tatu sasa hatujaona hata meno ya Bunge kuiwajibisha serikali katika masuala nyeti na Muhimu,
Nakumbuka kipindi cha jamaa Kikwete Bunge limewajibisha serikali Mara kibao sana na nashangaa mpaka Leo tuna mengi ya kuhoji lakin Bunge linaiogopa serikali,
Kuna masuala nyeti sana lakin Bunge Lipo kimya,
Naona viatu vya Makonda vinampwaya ndugai,
Hata wakati wa mwalimu Nyerere ambaye tunaamini ndo alikuwa mkali na ndo alikuwa rais kweli, lakin Bunge lilihoji na kuisimamia serikali ipasavyo mpaka saa nyingine kuikataa miswada na Nyerere ku surrender
Kipindi hicho Adam Sapi Mkwawa akiwa spika bunge lake lilikataa muswada wa Rais na kuurudisha na Rais akabwaga manyanga. Tena siyo hawa marais wa kuja bali ni Rais anayeheshimiwa hata miaka 200 ijayo yaani Rais Julius Nyerere. Je, ilikuwaje? Ilikuwa hivi.
Mwaka 1969 Waziri wa Elimu, Solomon Eliufoo aliugua na ikaonekana anaweza asiendelee kuwepo serikalini. Serikali kwa ku-panic ikapeleka muswada bungeni unaohusiana na mafao au maslahi ya mawaziri hasa wanaougua.
Muswada huo ulileta mgawanyiko bungeni ukizingatia kwamba ni miaka miwili tu tangu siasa ya Ujamaa na Kujitegemea itangazwe pia miiko ya uongozi.
Bunge likaukataa muswada ule likamrudishia Rais Nyerere ili ikiibidi afanye lolote na kama ni kuurudisha tena basi na iwe ili hatimaye wavunje bunge na nchi irudi kwenye uchaguzi.
Rais Nyerere mwenyewe alipohojiwa na waandishi alinywea na kusema "the parliament had a point" yaani bunge lilikuwa na hoja na hakuthubutu kuupeleka tena bungeni.
Haya, niambieni ni bunge lipi tena lililowahi kufauluujasiri kama huu. Wote waliobaki na mnaowataja wafyata mkia watupu, tena kukiwa na hatauwezekano wa kuhama vyama.
Leo hii Viatu vya Makinda ni vikubwa mno kwa ndugai
Utamuonea bure Ndugai. Rais tuliyenaye, ndio kila kitu. Umesahau alivyompongeza kwa kufuata maelekezo vizuri huko Bungeni?
Hapo ndo aoneshe makeke yake sasaMizizi mliambiwa inatofautiana sana kuna uliojichimbia kuzidi mingine!! So was it democratic or dictatorship!!
Ufafanuzi zaidi kwenye hili.
Ni wazi spika Ndugai amekuwa adui wa wananchi kwa kutozimgatia maslahi ya umma na utawala bora na kuwa mpiga mihuri ya serikali. Mambo mengi ya ovyo ameshindwa kusimamia kama hoja ya 1.5 trioni, hoja ya Lugumi serikali pamoja na akina Kangi ni Sarakasi tu serikali inafanya hasa ukizingatia terms of contracts management na sheria ya PPA, 2011 na kanuni zake 2013 na 2016.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo tayari kna shida maana ccm bungeni ndy wengi na kama uwajuavyo ccm wazee wa ndiyo lazima watataka spika abaki
Nani wa kumuondoa sasaAONDELEWE TU HAKUNA NAMNA SASA, sauti ya PINDAAA