Ndugai abanwa bungeni na kuahirisha bunge saa 5.30

Tatizo ni kwamba hawataki wananchi wajue kuwa mapendekezo ya CHADEMA yanachukuliwa na kufanyiwa kazi. Huu ni ujinga kabisa kwani pale ni kwa ajiri ya taifa na sio chama
 
nimeona mkuu,siku hiyo mwenyekiti alikuwa mabumba.mhe. lissu amefafanua juu ya kifungu ambacho AG alikuwa akikizungumzia kutetea utaratibu uliofanywa.Lissu Oyeeeeeeeeeeeeh

Mkuu ushabiki mwingine umepitiliza sana utadhani bunge umeangalia peke'ko
Aliyeelezea kifungu na kueleweka ni AG, Kwa maelezo yake yule M/kiti alifanya makosa kwa kulazimisha kufanya mabadiliko yeye peke'ke ambayo yalishafanywa na bunge. Alichosema AG serikali inajiandaa kuja kuleta muswada wa kufanyia mabadiliko hicho kifungo, kwa maana hy yale maamuzi ya M/kiti yalikuwa ni batili.
Na alichofanya Lissu ni ufafanuzi tu wa hoja ya Mnyika na Machali kuwa walikuwa wanataka muongozo kuhusu utaratibu wa M/kiti kufanya mabadiliko ye mwenyewe wakati yalishapitishwa na bunge.
 
Kwamba mh. Spika alibadili maamuzi ya Bunge bila kufuata kanuni stahili. Ni kwamba wakati bunge session ijumaa bunge kama kamati lilipitisha kutopitisha mswada flani (siukumbuki) na kupigiwa kura na Wabunge wote. Bi Spika yeye kwa makusudi ama kupitiwa maana kanuni anazijua, aliamua kama Spika kuupitisha kwa jinsi alivyoona yeye binafsi unafaa bila kuhoji tena Wabunge. Sasa leo Machali, Mnyika na Kafulila wamekomalia hadi ikabidi mh. Ndugai akiri na kuahidi kulishughulikia

hawa ndio watanzania great thinker humu!!! hivi kwa nini hii tabia mods haikomi watu kuanzisha thread ilimradi tu waonekane wameanzisha thread?

huna uhakika kwa nini unapost na kuquote long informations


kwa faida ya wengine, ijumaa bunge lilikaa kama kamati na aliekuwa anaongoza bunge hakuwa maadam spika alikuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge mh. sylvester massele mabumba mbunge wa Dole ccm, kulikuwa na mabadiliko ya mh. mnyika kuwa adhabu ingezeke kutoka kifungo cha miaka mitatu na wahusika walipe kiasi kile cha mali iliyohusika maana makosa ya money laundering yanahusisha kiasi kikubwa cha pesa mpaka bilioni na kuendelea wakati sheria inataka kuwa watuhumiwa walipwe kati ya milioni mia mpaka mia tano

sasa wakati anawahoji alitakiwa kusema kifungu hicho kinaafikiwa? instead yeye akasema kifungu hicho pamoja na mabadiliko yake kinaafikiwa? yaani marekebisha mnyika aliyotaka yaongezwe! na wabunge wakasema ndiyo

baada ya hapo bunge likamaliza kukaa kama kamati na likapitisha maazimio yote huku wakishangiliwa na wabunge wa chadema, kwa hiyo kabla ya kuahirisha bunge ole sendeka akaomba mwongozo ili kuweka sawa hansard akamwambia mwenyekiti uliteleza ulimi kwa hiyo na mwenyekiti akasema anabadilisha maneno yake ambacho ni kinyume cha kanunu za bunge mwenyekiti au spika kutengua maamuzi ya bunge.

ndipo leo AG akasema ataleta hoja ya kubadili hile kauli ili bunge lipitishe na wakati huo huo Tundu Lissu akahoji kwa nini mwenyekiti avunje kanuni na wakati akijua kuwa anavunja kanun!

tusubiri maamuzi ya kamati ya kanuni za bunge.

nachokiona hapo kuwa mh. Mambumba kiti hakiwezi na hata siku moja mh. Halima mdee aliwahi kumwambia kiti hicho kitakushinda ukiendekeza ushabiki! na kweli huyu jamaa maamuzi yake utafikili yupo nyumbani kwake vile anafuata tu ushabiki bila hoja na kufuata sheria.
 
bunge haliwezi kukurupuka kama miswada haijakamilika no bora kuahirisha kuliko kuileta bungeni hivyo hivyo.
acha kutudanganya mkuu,hayohayo yaliyopitishwa na bunge hilohilo leo yamerudishwa bungeni ili yafanyiwe marekebisho,huoni kuwa bado kuna tatizo ktk bunge letu hususani ktk upitishaji wa hoja kwa njia ya kukomoana?
 
hakubanwa kaelezwa kwamba alivunja kanuni alitakiwa baada ya kamati kujadili Ndugai angerudhisha kwa wabunge wote jambo ambalo hakufanya. Ni mambo ya kanuni si kubanwa.

Semantics tu, ukweli uko pale pale alibanwa na akabanika na kuomba msaada kwa Ole sendeka na AG. Raia Mwema kama kweli wewe ni Raia Mwema, jadili hoja sio semantics, tutumie vichwa vikuu kufikili.
 
Wabunge wa CCM wameamua kugoma ati kwa sababu Rais amekubali mapendekezo ya CDM kuhusu muswaada wa sheria ya mabadiliko ya Katiba na suala la kugomea posho zao. Kwa hiyo, wamesema miswaada ya Serikali itakwamishwa Bungeni.

Mhhh! hivi walitoa mapendekezo gani! tuwekee hapa ili tujadili.
 
Baada ya maswali na majibu leo hakuna hoja yeyote ya serikali itakayojadiliwa naona wabunge wamegoma na serikali inaogopa kuleta miswaada.bunge litahairishwa saa nne asubuhi posho kibindoni

Ulisikiliza Bunge kweli au ulikurupuka tu ulipoona Naibu Speaker akiahilisha Bunge na wewe kwa kiherehere chako ukaona uje hapa JF uandike chochote tu ili uonekane na wewe upo?
 
kurekebisha vifungu, kuvunjwa kwa kanuni bungeni sio jambo jipya ama kwa spika au kwa wabunge wenyewe na wao wanavunja kanuni pasipo kujua ndio maana likaitwa bunge liko pale kunyoosha mambo kabla hayajawa sheria.
 
Ijumaa iliyopita, Bunge lilipitisha marekebisho ya sheria ya fedha haramu. Serikari ilipendekeza adhabu ya jela miaka 3, Mh. Mnyika akapendekeza iongezeke na bunge kuridhia na kupitisha. Ghafra Ole Sendeka akakurupuka na kuleta pendekezo kwa mwenyekiti wafute kwenye hansadi mabadiliko aliyopendekeza Mh. Mnyika. Mwenyekiti bila kulishirikisha bunge akaagiza hansadi ifutwe yote yaliyochangiwa na Mnyika yabaki ya serikali. Na yakafutwa.
Leo

Mh Machali na Mh Mnyika walitaka mwongozo wa spika juu matumizi ya kiti kubadili maamuzi halali ya bunge. Olesendeka akatoa pumba zake eti walitakiwa wawasilishe kwa Katibu wa Bunge. AG akaona tatizo hilo ila akataka kulikwepesha kwa kutosema kama Kiti kilikosea kubadili bali eti serikali inataka ilete mabadiliko yale yajadiliwe tena ili kubariki aliyoamua Mwenyekiti. AG kamponda Olesendeka.

Mh. Lisu katolea ufafanuzi bila kuuma maneno kuwa hoja ni je Kiti kinauhalali wa kufuta maamuzi ya Bunge na kurekebisha sheria iliyopitishwa?


Nimekusoma mkuu wangu;

KWani mnashangaa nini wakati ikiwa nia sawa na kumchukua shmba boi wa IKULU kumpa cheo cha kuwa Waziri katika Wizara??

Watu tulichagua Spika na Naibu wake kwa kuangalia Itikadi za Chama na siyo uwezo wa mtu katika kukiongoza chombo hiki muhimu katika nchi. Na si naibu Spika tu kwa hata Spika mara nyingi amekuwa akileta mambo ambayo ni tofauti hata mtoto awa Nursery School anaona kabisa hapa kuna tofauti, mfano kutumia lugha za kibabe katika maamuzi.

Hivyo kwa lililotokea Ijumaa kila mbunge ambaye anajua kuwa alimpigia Kura Naibu Spika siku ile, hapashwi kulalamika bali anatakiwa kusema "NDIO MZEE" kwa kila jambo. Sasa ukipinga jamii ikueleweje wakati siku ile uliona ni kheri??

Alichofanya Ole Sendeka ni sahihi kwa sababu bado analinda uamuzi wake katika kuchagua Naibu Spika.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
MOD

1. Asante kwa kurekebisha Title. Bahati mbaya sijui.

2. Kwa kuunganisha thread mbili zenye maudhui tofauti, utawapoteza wana JF. Nashauri tu
 
Watu wengine kweli mna mambo hivi licha ya ufafanuzi huo huelewi nini. Mbona mimi sikuona ila naelewa tu jaman? Ishu hapa huyo mzanzibari alichemsha na ndugu yenu sendeka anataka kutetea magamba
 
wabunge wengi wa ccm huwa wawajui kinachoendelea bungeni,hoja km za miswada ya sheria wanakuwa kimya kazi ni ndiyo je ndio nini hawajui.
 
hakubanwa kaelezwa kwamba alivunja kanuni alitakiwa baada ya kamati kujadili Ndugai angerudhisha kwa wabunge wote jambo ambalo hakufanya. Ni mambo ya kanuni si kubanwa.

apa tunaanza kukuelewa,mleta mada kasema bunge leo litahairishwa sa4 wewe ukapinga na mpaka sasa tayari wamehairisha,sasa unabisha tena,aya ndugu...
 
Baada ya maswali na majibu leo hakuna hoja yeyote ya serikali itakayojadiliwa naona wabunge wamegoma na serikali inaogopa kuleta miswaada.bunge litahairishwa saa nne asubuhi posho kibindoni

Mbona bunge liliendelea? au unaongelea bunge gani?
 
Baada ya maswali na majibu leo hakuna hoja yeyote ya serikali itakayojadiliwa naona wabunge wamegoma na serikali inaogopa kuleta miswaada.bunge litahairishwa saa nne asubuhi posho kibindoni
Ndugai amebanwa na nani?...........

Bunge limeahirishwa baada ya shughuli zilizopangwa kufanyika leo(kwa mujibu wa order paper) kumalizika......

Kilichotokea ni wabunge Mkosamali kutoa hoja ya kutaka Bunge lijadili mauaji yaliyofanywa na Polisi Kasulu na baadae Polisi hao kuhamishiwa Kibondo(hoja haikuungwa mkono baada ya Mkosamali kukosea kifungu cha kuitetea hoja yake na Naibu Spika kumshauri aitoe wakati mwingine)....Kingine ni wabunge Manchali, Mnyika na Ole Sendeka na AG kutaka muongozo wa Spika na kutoa Taarifa juu ya uchemfu uliofanywa Ijumaa na Mwenyekiti Sylivester Mabumba(Huyu jamaa sijui kwa nini alipewa Uenyekiti maana Siku zote akikalia kiti huwa ni mchemfu na huwa hajiamini,hana uwezo wa kuongoza).....Naibu Spika alisema kwamba wameliona hilo na Kamati inayishughulika na kanuni za Bunge italishughulikia suala hilo haraka iwezekanavyo....

Ndugai hajabanwa leo mkuu....
 
Back
Top Bottom