Ndugai abanwa bungeni na kuahirisha bunge saa 5.30

Leo Mh. Ndugai amebanwa na wabunge kwa makosa ya ubabe alioufanya Ijumaa kubadili sheria ya ant-money roundering.

AG amemuabisha pia kwa kuonyesha kuwa alichemka. Bravo Mnyika and Machali.

Ole sendeka kwisha kazi, ameanza kujiua kisiasa mwenyewe

Ubabe hakufanya Ndungai..ni jamaa mwenye utindio wa akili Mabuba..jamaa mwenye miwani ya mbao
 
Leo Mh. Ndugai amebanwa na wabunge kwa makosa ya ubabe alioufanya Ijumaa kubadili sheria ya ant-money roundering.

AG amemuabisha pia kwa kuonyesha kuwa alichemka. Bravo Mnyika and Machali.

Ole sendeka kwisha kazi, ameanza kujiua kisiasa mwenyewe
Huyu kafanya nini Broda?
 
AG vs. Lissu nani zaidi wote ni wanasheria sasa nani kati yao ametoa ufafanuzi mzuri wa kanuni ? Naibu Spika ameshindwa kabisa kutoa mwongozo mpaka imebidi ahairishe bunge huku akitupa swali kwa kamati ya kanuni ambayo kazi yake ni kumshauri Spika..... hapo ni siasa tu msitarajie kitu hapo...... Halafu Mbunge akikosea kanuni kifungu kamili lakini wazo analolisema lipo kwanini hoja ipuuzwe kama alivyofanya Ndugai ?
 
nimeona mkuu,siku hiyo mwenyekiti alikuwa mabumba.mhe. lissu amefafanua juu ya kifungu ambacho AG alikuwa akikizungumzia kutetea utaratibu uliofanywa.Lissu Oyeeeeeeeeeeeeh
 
  • Thanks
Reactions: FJM
nimesoma gafla jicho langu la kushoto likafumba......unajaribu kusema nini
 
Kaka hakuna ishu bungeni na siku imeisha posho imetuna kwenye akaunti. Kuna madaktari wanakesha usiku wakiwa zamu asubui elfu kumi tena mpaka wapige mayowe ndo elfu kumi wanapewa. Na asubui mzigo kama kawaida. Hawa jamaa leo masaa ma 2 tu hamna ishu. Nchi mbovu sana hii


Kwa mpango huu, na mimi natangaza nia kuingia kinyanganyiro katika Jimbo la Arumeru. Kama kwa masaa tu unapokea kitita kisha muda uliobaki katika siku unaenda kuendelea na biashara zako!!!!!

Kazi nzuri sana hii; maana naona hapa bunge hili la JF hakuna posho ingawa mawazo yetu ni mazuri kuliko yale yanayotolewa kule Bungeni Dodoma. Yaani hizi ni dharau kabisa yanni Serikali inatufanyia; sisi hapa tunafanya kazi bila ya kusinzia muda wote tupo makini kuangalia kuna hoja gani mpya imetupwa, na tunatoa michango yetu kujibu au kuchangia hoja ipasavyo. Lakini hawa wenzetu wanasinzia, wanapewa posho kubwa kwa siku moja ya kikao kuliko mshahara wa mwezi anaolipwa Mwalimu au Askari.

Wanachukua maoni yetu hapa wanaenda kujifanya wao ndio waanzilishi kule Dodoma. Na ndio maana wanafungua sana hii website ili kujua nini cha kuongea. Wameishiwa na sera inaonyesha hawa. Sasa leo kwa kuwa jana ilikuwa Week-end na walikuwa katika minuso hawakupata muda wa kufungua JF na kusoma mada tulizoweka ndio maana wakajifanya kuleta za kuleta ili kuahirisha Bunge.

Lakini nashangaa kwa nini hawakutaka Bunge liahirishwe mapema kabla ya Kusaini posho!!!!!

UJANJA MTUPU HUU!!!!!!

Naomba wapenzi wote wa JF mniunge mkono nikagombee Arumeru, na nikiwa Dodoma nitahakikisha hakuna atakayetoa neno la kukashifu JF hata siku moja.

Nawategemea sana JF Members!!!!!!


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Hivi tatizo ni mbio za kutaka kuwa mpashaji habari wa kwanza au nini?
Habari haieleweki hata kidogo.

Hiyo kitu huwa inanikera sana...halafu ukimwambia aeleze vizuri mtu anauchuna tu na hata wale ambao wanaangalia sasa hivi wana assume kila mtu anaona kinachoendelea.
 
Yah. Huyu jamaa anaitwa Mabumba na Ndugai hawafai hata kupewa kijiji kuwa viongozi yaani huwa sipati faraja nionapo kijana kama Ndugai anadiriki kuchezea taifa ambalo JK na mafisadi wengine wa serikali watatuachia likiwa hoi bin taabani.

Mabumba aliahirisha bunge kibabe siku ya ijumaa alhali alikwisharidhia/bunge lilikwisha ridhia marekebisho ya Mnyika. Then wanataka kurekebisha kinyemela bila kupata ridhaa ya bunge!!

Wakurupukaji wale ndo maana waongoza nchi wengi wa serikali hii ni wanafiki kwenye mambo ya msingi ya nchi wanapiga blaa blaa na kuungwa mkono na lelemama waliowekwa bungeni kwa mbelelko ama viti maalum (NDIYOOOOOOOOO: Kwa mtazamo wangu nadhani waliosema ndiyo wameshinda!!!).
 
Asilimia kubwa ya wabunge wa CCM walikuwa jijini Mwanza jana kwenye sherehe ya CCM kutimiza miaka 35. Sasa si tunajua tena, mwendo wa kutoka Mwanza hadi Dodoma ni kilomita 700+ na ni mwendo wa saa karibu 6 kwa gari; hivyo kwa kuanza safari leo asubuhi wasingeweza kuwahi, hivyo naona kuna kanuni ya bunge imepitiwa na kuona si vizuri bunge likaendelea leo.
 
Hapa hatupigi story anayejua issue vizuri atuandikie kwa ufasaha wengine hatana sehemu ya kupata habari tofauti na hapa ofisni kwenye jf (internet ya bure kwa mwajiri). Umeme umepanda bei nyumbani twalala giza hakuna tv wala radio kuwashwa.
 
Leteni habari za ukweli na kwa ufasaha sio kiduchu kiduchu.

Ijumaa iliyopita, Bunge lilipitisha marekebisho ya sheria ya fedha haramu. Serikari ilipendekeza adhabu ya jela miaka 3, Mh. Mnyika akapendekeza iongezeke na bunge kuridhia na kupitisha. Ghafra Ole Sendeka akakurupuka na kuleta pendekezo kwa mwenyekiti wafute kwenye hansadi mabadiliko aliyopendekeza Mh. Mnyika. Mwenyekiti bila kulishirikisha bunge akaagiza hansadi ifutwe yote yaliyochangiwa na Mnyika yabaki ya serikali. Na yakafutwa.

Leo

Mh Machali na Mh Mnyika walitaka mwongozo wa spika juu matumizi ya kiti kubadili maamuzi halali ya bunge. Olesendeka akatoa pumba zake eti walitakiwa wawasilishe kwa Katibu wa Bunge. AG akaona tatizo hilo ila akataka kulikwepesha kwa kutosema kama Kiti kilikosea kubadili bali eti serikali inataka ilete mabadiliko yale yajadiliwe tena ili kubariki aliyoamua Mwenyekiti. AG kamponda Olesendeka.

Mh. Lisu katolea ufafanuzi bila kuuma maneno kuwa hoja ni je Kiti kinauhalali wa kufuta maamuzi ya Bunge na kurekebisha sheria iliyopitishwa?


SWALI: Hivi wanaogopa nini adhabu ya wezi kuwa kubwa??????????????????? Ndugai na Ole sendeka watoe majibu
 
Kwamba mh. Spika alibadili maamuzi ya Bunge bila kufuata kanuni stahili. Ni kwamba wakati bunge session ijumaa bunge kama kamati lilipitisha kutopitisha mswada flani (siukumbuki) na kupigiwa kura na Wabunge wote. Bi Spika yeye kwa makusudi ama kupitiwa maana kanuni anazijua, aliamua kama Spika kuupitisha kwa jinsi alivyoona yeye binafsi unafaa bila kuhoji tena Wabunge. Sasa leo Machali, Mnyika na Kafulila wamekomalia hadi ikabidi mh. Ndugai akiri na kuahidi kulishughulikia

Issue ya Ijumaa haikuwa handled na Bi Kiroboto bali ni yule Mzenji MaBumba sijui. Huyo ndo alilikoroga bahati mbaya hakuna personalities mahala pale kwani wanasema ni kiti.
 
hakubanwa kaelezwa kwamba alivunja kanuni alitakiwa baada ya kamati kujadili Ndugai angerudhisha kwa wabunge wote jambo ambalo hakufanya. Ni mambo ya kanuni si kubanwa.
 
Ubabe hakufanya Ndungai..ni jamaa mwenye utindio wa akili Mabuba..jamaa mwenye miwani ya mbao

Mbona wote hamuelezei kilichojili huko. Mnaruka ruka tu kama sungura!!! Kwa nini basi msiandikiane kwenye PM, kuliko kuleta thread hapa kisha hamtaki kufafanua. Sisi hatutaki kujaza maneno kwa jambo tusilolielewa vizuri.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Back
Top Bottom