Ndugai abanwa bungeni na kuahirisha bunge saa 5.30

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,598
3,671
Baada ya maswali na majibu leo hakuna hoja yeyote ya serikali itakayojadiliwa naona wabunge wamegoma na serikali inaogopa kuleta miswaada.bunge litahairishwa saa nne asubuhi posho kibindoni
 
Huyu jamaa huyu!!!''''''......hili tumbo huwa anakula nini huyu!!!

5.jpg
 
wameshasoma alama za nyakati leo magamba walikua kitu kimoja na CDM kupinga kila hoja ya serikali pangechimbika bungeni
 
Wabunge wa CCM wameamua kugoma ati kwa sababu Rais amekubali mapendekezo ya CDM kuhusu muswaada wa sheria ya mabadiliko ya Katiba na suala la kugomea posho zao. Kwa hiyo, wamesema miswaada ya Serikali itakwamishwa Bungeni.
 
Yaani kweli jamaa bila aibu ndo wanaondoka bungeni. Job ameahirisha bunge mpaka kesho!! Dah tunaliwa tukiwa tunaona hivi hivi. Hii ni tabia ya fisi hangoji windo lake life hula likiwa hai!
 
bunge haliwezi kukurupuka kama miswada haijakamilika no bora kuahirisha kuliko kuileta bungeni hivyo hivyo.
 
Washazikunja wanaenda kuopoa, wa massage na hangover za week end. Wajua kila juma3 wengi wanakuwa wanasinzia sana kwa pilika za whole weekend and night. hhahahaha, Ubunge njoo utamuu njoo.
 
kweli bunge limeahirishwa hadi kesho saa 3 asubuhi, wabunge wa ccm wameambiwa waache simu zao wazi, wataitwa muda wowote, tangazo limetolea na mwenyekiti wa wabunge wa ccm mh Jenister Mhagama hali inaonekama si nzuri ndani ya chama na serikali, tusubiri tuone
 
Leo Mh. Ndugai amebanwa na wabunge kwa makosa ya ubabe alioufanya Ijumaa kubadili sheria ya ant-money roundering.

AG amemuabisha pia kwa kuonyesha kuwa alichemka. Bravo Mnyika and Machali.

Ole sendeka kwisha kazi, ameanza kujiua kisiasa mwenyewe
 
Kwamba mh. Spika alibadili maamuzi ya Bunge bila kufuata kanuni stahili. Ni kwamba wakati bunge session ijumaa bunge kama kamati lilipitisha kutopitisha mswada flani (siukumbuki) na kupigiwa kura na Wabunge wote. Bi Spika yeye kwa makusudi ama kupitiwa maana kanuni anazijua, aliamua kama Spika kuupitisha kwa jinsi alivyoona yeye binafsi unafaa bila kuhoji tena Wabunge. Sasa leo Machali, Mnyika na Kafulila wamekomalia hadi ikabidi mh. Ndugai akiri na kuahidi kulishughulikia
 
Wakuu nimekuwa nikifuatila bunge katika kikao cha leo,baada ya maswali na majibu Machali na Myika waliomba mwongozo kutokana na makosa ya ukiukwaji wa kanuni za bunge uliofanywa na Mwenyekiti S Mabumba siku ya Ijumaa wakati wa kupitisha marekebisho ya sheria kudhibiti matumizi ya fedha haramu.

Kilichonisikitisha leo ni pale Mh Olesendeka mbunge kupitia CCM kusimama na kuendelea kupinga hoja za kina Mnyika na Machali ili mabadiliko ya sheria hiyo pamoja na mabadiliko yake yaliyopendekezwa na Mh Mnyika siku ya Ijumaa yaendelee kutumika kwa utengunzi wa Mwenyekiti wa kikao cha siku hiyo,wakati baada ya kuwahoji siku hiyo ya Ijumaa bunge lote waliitikia ndio.

Leo Sendeka anaendelea kupinga adhabu hiyo isikaziwe na kuwa kali kama mapendekezo ya Mnyika alivyowasilisha,je hii ni picha gani?je Sendeka ni fisadi na anadhani adhabu hii ikiwa kali itakuja kumkumba?je mtu anaepinga adhabu isiewe kali hii si tafsiri ya ufisadi?

Nawasilisha
 
Bunge la Jf mbona limeanza Udaku, bungeni kunaendelea vema tu.
Kaka hakuna ishu bungeni na siku imeisha posho imetuna kwenye akaunti. Kuna madaktari wanakesha usiku wakiwa zamu asubui elfu kumi tena mpaka wapige mayowe ndo elfu kumi wanapewa. Na asubui mzigo kama kawaida. Hawa jamaa leo masaa ma 2 tu hamna ishu. Nchi mbovu sana hii
 
Back
Top Bottom