NDOA: Zamani vs Siku hizi

Nimempenda huyo dada....Kuna sababu gani ya kuhangaika wakati kuna mtu ambaye amekueleza kuwa anakupenda na kukuonesha upendo kwa vitendo. Actually, hata kwa kutumia common senses, huwezi kuacha kumpenda mtu wa namna hiyo!!

Ngoja kwanza niishie hapa kwani Lizzy keshaanza kunichokonoa!!

Hahahaha, babu mbona mimi nimetulia tu?
Honestly, mahusiano ambayo mmoja anampenda sana mwenzake na huyu mwingine anashukuru/furahia/kuenzi kupendwa huko hata kama hisia zake sio sawa na za mwenzake nafasi ya wao kufika mbali ni kubwa. Tatizo lipo pale baadhi ya watu wanapotumia mapenzi waliyonayo wenzao juu yao kama udhaifu na fimbo ya kuwapigia. Unakuta mtu anamnyanyasa mwenzie kwa kila namna kisa tu anajua anapendwa, kwa style hiyo lazima mpendaji atachoka na kuamua kuondoka.
 
Hapo (blue) tuko pamoja.....Inapobidi unamsaidia kama binadamu mwingine yeyote ambaye ungempatia msaada endapo angepata emergency mbele yako!!

Kwenye red, Makaburini aliitwa baada ya mume kukataa kutoa msaada au nimesahau??
Kilichofuata baada ndicho kinachonifanya nisiamini sana anayodai shemejie Makaburini.
 
...umeandika na kuchambua vizuri sana, na umegusia kitu kimoja kizuri sana...thamani ya ndoa.
Nakubaliana nawe sana thamani ya ndoa imeshuka kwa kiwango kikubwa, sasa je...iwapo sie wa kizazi hiki
tumefikia hapa,...huko tunakoelekea itakuwaje yarabi?....nani alaumiwe kwa janga hili?
...kuna lolote linaloweza tuepusha na gharika hizi au ndio tusubiri "mesina"
kama ya Nuhu?

Thamani na maana nzima ya ndoa imebadilika na kushuka for the original meaning ya ndoa sasa imebadilika Mbu.... Hivo maadili na kuthamini ndoa kupungua haviepukiki.... Tukiangalia kwa upana sasa hivi kuna ndoa kati ya wanadamu wa jinsia moja, kuna ndoa ambazo zimehalalishwa kabisa na kua ni za mkataba... Kuna muingiliano wa dini siku hizi... Watu wa dini tofauti waona na ndoa kufanyika bomani.... Naaamini kua nidhamu ya uoga dhidi ya ndoa; spouses wenye woga zaidi dhidi ya ndoa zao ni wale walooana kwa dini moja kuliko wa bomani.

Tukiangalia kua nani alaumiwe.... Nadhani jamii nzima inwajibika kuweza laumiwa, kupokea na kukumbatia mambo mengine yasio faa na huchangia kupotosha vijana wadogog dogo kujiingiza katika maswala mbali mbali yasio faa kama vile ushoga...

Kusema twaweza epuka gharika hili? Siamini.... Haya mambo hayalazimishwi, evolution ni inevitable let us just hope that in the long run ita evolve for the better kuliko tulipo hapa.
 
Hahahaha, babu mbona mimi nimetulia tu?
Honestly, mahusiano ambayo mmoja anampenda sana mwenzake na huyu mwingine anashukuru/furahia/kuenzi kupendwa huko hata kama hisia zake sio sawa na za mwenzake nafasi ya wao kufika mbali ni kubwa. Tatizo lipo pale baadhi ya watu wanapotumia mapenzi waliyonayo wenzao juu yao kama udhaifu na fimbo ya kuwapigia. Unakuta mtu anamnyanyasa mwenzie kwa kila namna kisa tu anajua anapendwa, kwa style hiyo lazima mpendaji atachoka na kuamua kuondoka.

Huyo ni limbukeni na lazima ipo siku atapigwa chini tu....awe mke au mume!!

Halafu mijitu ya namna hiyo huwa inasumbua sana baada ya kupigwa kiboot....Mie likirudi kwangu naliambia likaishi kwenye banda la kuku!!
 
Hhahahahha, ndio unaniingiza mjini hivyo mkwe?Usije ukamnyanyasa wakati mwenzio anakupenda alafu arudi kunililia.

mkwe upendo wangu wa kizamani haswa
mke anakuwa na mtoto wa nje na mume anajua wanapiga kimya
na mume hivyo hivyo hadi kifo
thubutu leo hata aliyezaliwa kabla hujaoa/olewa
please mkwe usiniharibie unajua jinsi nampenda
wakati mwingine wakwe wanachangia lakini sio wewe
hahahahahah
 
Hata wanaume bwana nao maadili yao yanaporomoka kwa kasi kiasi kwamba yanakaribia kwenye mstari wa zero!!

Mfano, utajiitaje mwanamume wakati unakimbia kimbia na vitoto vya majirani zako na hata wafanyakazi wao? Au unakwenda kwenye ufuska na kurudi saa 11 asubuhi!!

Wazee wetu walikuwa wanajua kuwa mama watoto ndiye nambari one...Wengine wote ni washika pembe, mama ndiye anayekamua. Sasa hivi mnawafanya wake zenu washika pembe...Is that fair??

Wazee wa zamani walikuwa wanaoa wake watatu mpaka tano kulingana na uwezo wake ila sasa ni tofauti kabisa utandawazi umeharibu kila kitu.
 
Huyo ni limbukeni na lazima ipo siku atapigwa chini tu....awe mke au mume!!

Halafu mijitu ya namna hiyo huwa inasumbua sana baada ya kupigwa kiboot....Mie likirudi kwangu naliambia likaishi kwenye banda la kuku!!
Na ndivyo ilivyo babu.
Ndio maana unasikia wajukuu wakiitana ATM, kisa tu mwanaume kampenda na kumjali kiasi cha kuamua kumsaidia hata kifedha basi tayari anaitwa ATM na maneno mengine ya ajabu ajabu watu wanayoitana siku hizi.Ukishasikia hivyo jua kama kuna mapenzi basi yapo upande mmoja na huo upande wa pili unamdharau mpendaji.
 
Thamani na maana nzima ya ndoa imebadilika na kushuka for the original meaning ya ndoa sasa imebadilika Mbu.... Hivo maadili na kuthamini ndoa kupungua haviepukiki.... Tukiangalia kwa upana sasa hivi kuna ndoa kati ya wanadamu wa jinsia moja, kuna ndoa ambazo zimehalalishwa kabisa na kua ni za mkataba... Kuna muingiliano wa dini siku hizi... Watu wa dini tofauti waona na ndoa kufanyika bomani.... Naaamini kua nidhamu ya uoga dhidi ya ndoa; spouses wenye woga zaidi dhidi ya ndoa zao ni wale walooana kwa dini moja kuliko wa bomani.

Tukiangalia kua nani alaumiwe.... Nadhani jamii nzima inwajibika kuweza laumiwa, kupokea na kukumbatia mambo mengine yasio faa na huchangia kupotosha vijana wadogog dogo kujiingiza katika maswala mbali mbali yasio faa kama vile ushoga...

Kusema twaweza epuka gharika hili? Siamini.... Haya mambo hayalazimishwi, evolution ni inevitable let us just hope that in the long run ita evolve for the better kuliko tulipo hapa.

Hilo ni tatizo la ubinafsi ambalo linawafanya watu wajifikirie zaidi wao wenyewe na raha zao (hata kwa kutumia plastic au mawe) badala ya kuwa tayari kuliwa ili nao wale!!

Ila sorry ADii...mambo ya jinsia moja siyo ndoa au??
 
Tafadhali sana sijawahi kukutukana hata siku moja, na wala sikutegemea kama utafikia kunitukana kiasi hiki!

"Ukiona mtu anaanza matusi ujuwe kashindwa hoja".
 
mkwe upendo wangu wa kizamani haswa
mke anakuwa na mtoto wa nje na mume anajua wanapiga kimya
na mume hivyo hivyo hadi kifo
thubutu leo hata aliyezaliwa kabla hujaoa/olewa
please mkwe usiniharibie unajua jinsi nampenda
wakati mwingine wakwe wanachangia lakini sio wewe
hahahahahah
Hahahah mkwe bana.Kwahiyo mnafichiana aibu sio?
Ila kweli siku hizi mune hata asipopiga mswaki kila mtu atajua, mke akipata ukurutu kila mtu atajua. Ile ya wanandoa kusitiriana haipo tena, biashara yao imekua biashara ya kila mtu.

Mpaka hapo nakukabidhi rasmi, ila sitaki kesi.
 
Tafadhali sana sijawahi kukutukana hata siku moja, na wala sikutegemea kama utafikia kunitukana kiasi hiki!

"Ukiona mtu anaanza matusi ujuwe kashindwa hoja".

Usitake kukwepa kwa ku cherry pick kineno kimoja kati ya mengi. Ujanja wa kizamani huo.

Kwanza hujatukanwa wewe. Ukisoma context utaelewa. Lakini kwa vile najua huwezi kutetea ulichoandika ndo maana umeenda huko kwenye kudai umetukanwa. Hahaaaaaaaa....jaribu tena.
 
Wazee wa zamani walikuwa wanaoa wake watatu mpaka tano kulingana na uwezo wake ila sasa ni tofauti kabisa utandawazi umeharibu kila kitu.

Bado unaweza kuoa hadi wa 4 kama ukifuata taratibu...

Najua ni vigumu kwa mwanamume kuishi na mke mmoja....Hilo wanawake wanatakiwa kulijua ila pia wanaume wanatakiwa kujitahidi ama kutohangaika na warembo wa nje au kuwa na adabu/heshima kwa wake zao pale wanapoenda kuonja onja nje!

Ila under no circumstance...cheating for women is allowed...(najua kuwa hapa nitawatibua baadhi ya watu, ila ndiyo fact)!!!
 
Usitake kukwepa kwa ku cherry pick kineno kimoja kati ya mengi. Ujanja wa kizamani huo.

Kwanza hujatukanwa wewe. Ukisoma context utaelewa. Lakini kwa vile najua huwezi kutetea ulichoandika ndo maana umeenda huko kwenye kudai umetukanwa. Hahaaaaaaaa....jaribu tena.

Tumemaliza, na umeshinda wewe. Tafadhali sana, achana na mimi, huwa sipendi kabisa kuendelea na mjadala unaowapa faida wengine kwa kutukanwa.
 
ndio maana nikasema watu hawana hofu ya mungu na wala hawafati mila na desturi zao maana najua wapo ambao hawaamini habari za mungu.

...Husninyo, unapokubaliana mpasuko huu unatokana na watu kupoteza hofu ya mungu na kuacha mila na desturi zao nakuunga mkono kwa asilimia 100, unajua kwanini?,

kwenda na wakati kama wana Beijing walivyopendekeza, ina maana wanawake waachane na mila potofu zilizokuwa zinamuongoza mwanamke, (ambazo ziliwesha kulinda ndoa za mababu zetu) na maandiko matakatifu ambayo kwa kiwango kikubwa yanalazimisha uongozi na maamuzi ya mwanaume katika maisha ya ndoa.

sijui tunakubaliana bado au?

Babu hamna niliposema mwanaume ndie wakulaumiwa, ila katika harakati za kumjibu Mbu kuhusu mume kutaka mkewe avae kiheshima ili kulinda ndoa nimegusia kwamba inatakiwa wawili hao (wenye ndoa) wawe wanajadiliana badala ya mmoja kumuendesha mwenzake (iwe mke au mume).

...sasa kuna ubaya gani kuwa mkali mke anapokataa kunisikiliza mie kichwa cha familia? mie nasimamia maandiko, mila na desturi bana...
 
Tumemaliza, na umeshinda wewe. Tafadhali sana, achana na mimi, huwa sipendi kabisa kuendelea na mjadala unaowapa faida wengine kwa kutukanwa.

Hakuna ulipotukanwa. Hiyo ni janja yako tu ya kukwepa hoja. Ila hamna neno kwa sababu nia yangu si kuchakachua sredi ya watu.
 
Usitake kukwepa kwa ku cherry pick kineno kimoja kati ya mengi. Ujanja wa kizamani huo.

Kwanza hujatukanwa wewe. Ukisoma context utaelewa. Lakini kwa vile najua huwezi kutetea ulichoandika ndo maana umeenda huko kwenye kudai umetukanwa. Hahaaaaaaaa....jaribu tena.

...easy buddy, achana na faiza foxy bana ni mgeni wangu kwenye mjadala huu,
pls bro.
 
Back
Top Bottom