NDOA: Zamani vs Siku hizi

Mbu,

Haya mabadiliko ya haki za wanawake ni mazuri tu. Tatizo ni kwamba yameanza na gia za juu kiasi kwamba yanazua hofu kwa wanaume!

Kwa wale tuliokulia vijijini, kuna mambo hatuyawezi kabisa...Mfano umeoa ila mwanamke anakwambia hataki mtoto au mzae baada ya miaka 10 ili kwanza mfaidi maisha...Binafsi siwezi kuelewa hapo!!
 
...sasa kuna ubaya gani kuwa mkali mke anapokataa kunisikiliza mie kichwa cha familia? mie nasimamia maandiko, mila na desturi bana...
Sasa Mbu kwanini mfikie hatua ya kugombezana kama watoto wakati wote ni watu wazima na majadiliano yangeweza kumaliza tatizo lenu?Mke akikuonyesha kiburi baada ya kumlazimisha afanye kitu jilaumu mwenyewe. Ongea nae kistaarabu uone kama hamtaishia kucheka kwa furaha badala ya kutoka amevaa vile ulivyotaka huku amenuna au hata akasusa kutoka kabisa.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Hahahah mkwe bana.Kwahiyo mnafichiana aibu sio?
Ila kweli siku hizi mune hata asipopiga mswaki kila mtu atajua, mke akipata ukurutu kila mtu atajua. Ile ya wanandoa kusitiriana haipo tena, biashara yao imekua biashara ya kila mtu.

Mpaka hapo nakukabidhi rasmi, ila sitaki kesi.

ukienda salon ndio kijiwe cha kueleza matatizo yao
hapo hujaenda kaunta ya juu na nyumba ndogo
wanajua kila kitu kama walikuwepo wakati wa tukio

mkwe usiwe na wasi hutasikia kesi labda wewe ulete kesi
maana wakwe wa siku hizi hawachelewi kusema mie nilikuwa
namlisha chakula hiki mara amezoea vile
tutakuwa tunawasiliana hapa JF na mara chache home
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Hilo ni tatizo la ubinafsi ambalo linawafanya watu wajifikirie zaidi wao wenyewe na raha zao (hata kwa kutumia plastic au mawe) badala ya kuwa tayari kuliwa ili nao wale!!

Ila sorry ADii...mambo ya jinsia moja siyo ndoa au??

Tafsiri ya ndoa hapo kale ilikua "kujumuika kwa mwanaume na mwanamke/wanawake wakiapa kuishi kama mke na mume". Siku hizi the definition does not apply tena.... For imekua pana mno (kama nilivoeleza katika my former post). Katika jamii mbali mbali ile tu kukutana kimwili kwa jinsia moja let alone kinyumbe cha maumbele ni kama vile taboo.... Hivo mzee DC naona jamii yetu bado ipo mbali saana kuweza itambua ndoa ya jinsia moja....
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Sasa Mbu kwanini mfikie hatua ya kugombezana kama watoto wakati wote ni watu wazima na majadiliano yangeweza kumaliza tatizo lenu?Mke akikuonyesha kiburi baada ya kumlazimisha afanye kitu jilaumu mwenyewe. Ongea nae kistaarabu uone kama hamtaishia kucheka kwa furaha badala ya kutoka amevaa vile ulivyotaka huku amenuna au hata akasusa kutoka kabisa.

Lizzy,

Kama ungejua, wanaume mara nyingi hawafuatilii mavazi ya wanawake. Labda kama kuna kitu kimekukera sana. Ila mpaka umshauri mama abadilishe ni kazi kweli na endapo utajaribu kutumia nguvu....Mie huwa natumia gia kwamba hajapendeza....Hapo utamkamata.

Ila mara nyingi wanawake ndo wanakuwa wakali kuwachagulia waume zao mavazi. Sasa jaribu kubisha uone!! Hapa huwa namwambia akachague mwenyewe analotaka nivae...After all I belong to her!! Furaha yake ndiyo yangu pia!!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Hahahaha, babu mbona mimi nimetulia tu?
Honestly, mahusiano ambayo mmoja anampenda sana mwenzake na huyu mwingine anashukuru/furahia/kuenzi kupendwa huko hata kama hisia zake sio sawa na za mwenzake nafasi ya wao kufika mbali ni kubwa. Tatizo lipo pale baadhi ya watu wanapotumia mapenzi waliyonayo wenzao juu yao kama udhaifu na fimbo ya kuwapigia. Unakuta mtu anamnyanyasa mwenzie kwa kila namna kisa tu anajua anapendwa, kwa style hiyo lazima mpendaji atachoka na kuamua kuondoka.

...hili nalo ni neno la maana kabisa...

unazungumzia suala la kupiga/kupigwa/ au hata kupigana katika mapenzi/ndoa.
je, hali hii inahusikanaje na uthamani wa ndoa ya mtu...

hivi waweza kupigwa bure bure tu pasipo sababu kwenye maisha ya ndoa?
unless huyo mume ni mgonjwa wa akili, kinyume na hapo narudi kule kule kwenye uongozi
wa nyumba....almuradi mume hamnyanyasi mke, au mke hamnyanyasi mume.
 
ukienda salon ndio kijiwe cha kueleza matatizo yao
hapo hujaenda kaunta ya juu na nyumba ndogo
wanajua kila kitu kama walikuwepo wakati wa tukio

mkwe usiwe na wasi hutasikia kesi labda wewe ulete kesi
maana wakwe wa siku hizi hawachelewi kusema mie nilikuwa
namlisha chakula hiki mara amezoea vile
tutakuwa tunawasiliana hapa JF na mara chache home

Hahahahaha, mkwe kama ulikuwepo.
Yani kila kinachoendelea ndani kinajulika, hata yale ambayo ni lazima yawe siri yamepoteza usiri.
Unatembea barabarani watu wanajaribu tu kukuweka kwenye mazingira waliyohadithiwa. . .NO WONDER NDOA NYINGI NI AIBU ZAIDI YA HESHIMA.

Hehehehehe, sasa mkwe hutaki nikufundishe jinsi ya kumfurahisha na kumpendezesha laaziz wako wakati mimi namfahamu zaidi yako? Ntakua nampikia chakula akipendacho mara moja moja na kumtumia.
 
Mbu,

Haya mabadiliko ya haki za wanawake ni mazuri tu. Tatizo ni kwamba yameanza na gia za juu kiasi kwamba yanazua hofu kwa wanaume!

Kwa wale tuliokulia vijijini, kuna mambo hatuyawezi kabisa...Mfano umeoa ila mwanamke anakwambia hataki mtoto au mzae baada ya miaka 10 ili kwanza mfaidi maisha...Binafsi siwezi kuelewa hapo!!

babu tatizo ni wale waliopewa dhamana ya kuyaeneza au kufikisha ujumbe wake kwa wanawake wengine. Kuna mtu alishawahinibana na kuniomba nisurvey wale wote wanaoshabikia Beijing (enzi zile inaingia kwa kasi) kisha nimletee feed back. nilichoka. Wengi walioidaka ile tenda na kuahidi au kuonyesha uwezo wa kuieneza vema ni wale walokuwa hawana ndoa au wako kwenye mazingira magumu ya ndoa. Matokeo yake ile mbegu ikaenezwa kwa chuki na hasira.

Namkumbuka Prof. M.Mb. alishawahieleza kinagaubaga kuwa pamoja na kuwa yeye si mtanzania na pamoja na kuwa yeye ni mmojawapo wa wapigania haki za wanawake Tanzania, teh moment anaporudi nyumbani kwake na mume wake ambaye ni mtanzania, u-beijing wote anauacha nje ya mlango wa kuingilia (ilmradi tu mumewe anamheshimu).

Sasa wale waso na ndoa au wenye frustrations ndo wakaja na sera za..........Sisi wote tu sawa, tuwekeane zamu ya kupika, kwenda sokoni e.t.c. e.t.c
 
Tafsiri ya ndoa hapo kale ilikua "kujumuika kwa mwanaume na mwanamke/wanawake wakiapa kuishi kama mke na mume". Siku hizi the definition does not apply tena.... For imekua pana mno (kama nilivoeleza katika my former post). Katika jamii mbali mbali ile tu kukutana kimwili kwa jinsia moja let alone kinyumbe cha maumbele ni kama vile taboo.... Hivo mzee DC naona jamii yetu bado ipo mbali saana kuweza itambua ndoa ya jinsia moja....

Kweli ADii,

kwenye jamii nyingi (za Kiafrika), naamini ndoa ilikuwa ni jambo kubwa sana. Lenye heshima ya hali ya juu na halikufanywa kirahisi rahis kama tunavyotaka kufanya siku hizi!!

Hapo kwenye blue,

Nadhani mie binafsi sitaweza kulielewa hilo kwa miaka yangu michache iliyobaki hapa duniani!! Labda nikiambiwa ni michezo fulani ya kitoto!!
 
...hili nalo ni neno la maana kabisa...

unazungumzia suala la kupiga/kupigwa/ au hata kupigana katika mapenzi/ndoa.
je, hali hii inahusikanaje na uthamani wa ndoa ya mtu...

hivi waweza kupigwa bure bure tu pasipo sababu kwenye maisha ya ndoa?
unless huyo mume ni mgonjwa wa akili, kinyume na hapo narudi kule kule kwenye uongozi
wa nyumba....almuradi mume hamnyanyasi mke, au mke hamnyanyasi mume.
Mbu kuna mtu anapigwa kwa kuwa kachelewa kuipokea simu yake hata kama sababu ilikuwa ni kumuattend mtoto!!!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Lizzy,

Kama ungejua, wanaume mara nyingi hawafuatilii mavazi ya wanawake. Labda kama kuna kitu kimekukera sana. Ila mpaka umshauri mama abadilishe ni kazi kweli na endapo utajaribu kutumia nguvu....Mie huwa natumia gia kwamba hajapendeza....Hapo utamkamata.

Ila mara nyingi wanawake ndo wanakuwa wakali kuwachagulia waume zao mavazi. Sasa jaribu kubisha uone!! Hapa huwa namwambia akachague mwenyewe analotaka nivae...After all I belong to her!! Furaha yake ndiyo yangu pia!!
Hahahahaha, sasa babu siunaona.Ni kiasi tu cha kujua wapi umkamatie, sio unamwambia "embu badili hiyo suruali. . . .usivae hilo gauni. . .ulivyovaa hivyo unataka kutamaniwa ehhh." and the likes. Unatakiwa utumie lugha laini ili mwisho wa siku akibadili abadili akifikiria kwamba unamjali sana na sio unamwendesha sana.
 
Hakuna ulipotukanwa. Hiyo ni janja yako tu ya kukwepa hoja. Ila hamna neno kwa sababu nia yangu si kuchakachua sredi ya watu.

Wewe usitake kujidai mjanja, wewe umenitukana na nnakuambia sitaki kuendelea kubishana na wewe. Umeshinda kwa kunitukana na umeshindwa kwa hoja, ungekuwa una hoja usingenitukana wala usingetumia tusi kuelezea hoja yako. Huwa sijibizani na watu wanaotumia matusi na kwa kuwa ndivyo walivyolelewa basi kwao huona hawajatukana hata wakitukana, Hapo upo tofauti na mimi, kabisa tena.

Mimi sikutakani wala sijawahi kukutukana na wala sitakutukana. Wewe mshindi. Unataka nini zaidi ya ushindi?
 
Kuna wanaoowa na bado wanakaa kwa Baba na mama, je huyu atakuwa ni mke wako au ni mke wa familia?
Na kuna walioolewa lakini kila baada ya siku mbili kiguu na njia kwa mama yake, je huyu anaweza akawa wife material?
Na kuna wazazi wanaotaka watoto waishi maisha yao wao wazazi, je inawezekana mtu kuishi maisha ya mtu mwingine?
Na kuna mawifi wao ndio wamejipa jukumu la kuverify kwamba mkeo anafaa au hafai, unadhani hapa bila mume kuwa strong kuna ndoa imara?
Kuna wanawake wengine hata ufanyaje yeye ni mtu wa kukulaumu tu kana utimizi majukumu yako nyumbani, na anataka wewe ufanane na nyani ngabu kisa nyani ngabu ni mbeba mabox maarufu basi anataka na wewe uwe na ujiko huo!

Kuna wanawake ukiwa unatumia kilevi kidogo basi ndio nongwa, ni lawama zisizoisha kana kwamba pesa yako yote unapigia mtungi, anataka umiliki kigari huku akisahau hata yeye anapaswa kununuwa gari maana wapo wanawake wenzake wanamiliki mpaka Ferari bila kuhongwa na mwanaume!
How can you build broken relationship when feeling is no longer there?
 
Tumemaliza, na umeshinda wewe. Tafadhali sana, achana na mimi, huwa sipendi kabisa kuendelea na mjadala unaowapa faida wengine kwa kutukanwa.

Wewe usitake kujidai mjanja, wewe umenitukana na nnakuambi sitaki kuendelea na kubishana na wewe. Umeshinda kwa kunitukana na umeshindwa kwa hoja, ungekuwa una hoja usingenitukana wala usingetumia tusi kuelezea hoja yako.

Mimi sikutakani wala sijawahi kukutukana na wala sitakutukana. Wewe mshindi. Unataka nini zaidi ya ushindi?

Si ushasema "tumemaliza" na nimeshinda? Sasa kwa nini unaendeleza malumbano?

Lazima kitakuwa kimekuuma.
 
...hili nalo ni neno la maana kabisa...

unazungumzia suala la kupiga/kupigwa/ au hata kupigana katika mapenzi/ndoa.
je, hali hii inahusikanaje na uthamani wa ndoa ya mtu...

hivi waweza kupigwa bure bure tu pasipo sababu kwenye maisha ya ndoa?
unless huyo mume ni mgonjwa wa akili, kinyume na hapo narudi kule kule kwenye uongozi
wa nyumba....almuradi mume hamnyanyasi mke, au mke hamnyanyasi mume.

Mbu unaongelea kupiga/pigana physically?
Hiyo wapo wanaopiga wake zao kisa tu chumvi imezidi ama imepelea kidogo kwenye mboga. Kuna watu hua hawafikirii, mkono unainuka tu.

Ila mimi nilikua naongelea ile ya mtu kumtenda mwenzake hovyo (kucheat, kumtukana, kutomjali, kumdharau na hata kumpiga kama hapo juu) kisa tu anajua anapendwa.
 
babu tatizo ni wale waliopewa dhamana ya kuyaeneza au kufikisha ujumbe wake kwa wanawake wengine. Kuna mtu alishawahinibana na kuniomba nisurvey wale wote wanaoshabikia Beijing (enzi zile inaingia kwa kasi) kisha nimletee feed back. nilichoka. Wengi walioidaka ile tenda na kuahidi au kuonyesha uwezo wa kuieneza vema ni wale walokuwa hawana ndoa au wako kwenye mazingira magumu ya ndoa. Matokeo yake ile mbegu ikaenezwa kwa chuki na hasira.

Namkumbuka Prof. M.Mb. alishawahieleza kinagaubaga kuwa pamoja na kuwa yeye si mtanzania na pamoja na kuwa yeye ni mmojawapo wa wapigania haki za wanawake Tanzania, teh moment anaporudi nyumbani kwake na mume wake ambaye ni mtanzania, u-beijing wote anauacha nje ya mlango wa kuingilia (ilmradi tu mumewe anamheshimu).

Sasa wale waso na ndoa au wenye frustrations ndo wakaja na sera za..........Sisi wote tu sawa, tuwekeane zamu ya kupika, kwenda sokoni e.t.c. e.t.c

Halafu huo ujumbe wanawapelekea akina DC waliokulia katika mazingira ambayo mwanamke ana haki moja tu, ya kusema ndiyo kwa kila kitu anachoelezwa na mume??!! Walifanya kosa kubwa na jitahada za kurudi kwenye mstari zitawagharimu!!

Tunawapenda sana wake zetu ila pia watusaidie kupita kwenye hii transition ya kutoka kwenye udume wa kweli na kuwa wanaume na baba wa kisasa!! Hii process inatakiwa isindikizwe kwa mwendo wa kobe!!
 
Back
Top Bottom