NDOA: Zamani vs Siku hizi

Kwahiyo babu wewe hisia zako kwa bibi DC zikoje?
Mnaishi kwasababu umemzoea au kwasababu unampenda?

Mhhh,

Very tricky...ila naweza kukueleza kuwa naishi naye kama mwenzangu wa karibu sana.. Lolote lake ni langu ingawa sina hakika kama kweli langu ni lake!!

Ndo maana nilisema huko nyuma kwamba siwezi kumtelekeza mke wangu kwenye tatizo lolote (however simple it might be) hata kama a few minutes ago kanifanyia kosa kubwa au kuniudhi sana!! Nadhani mafundisho ya baba hapa yanachukua nafasi. Alikuwa anatueleza kuwa hawezi kumchapa mtoto hata kama kafanya kosa gani kabla ya kula endapo ni muda wa chakula!! Mtakula kwanza halafu unapata zawadi yako!!

Kama nampenda Bibi DC au la, bado hata mie najiuliza!!!
 
Hahahaha, kwa maelezo hayo babu ni dhahiri unampenda na sio unaishi nae kwa mazoea.

Mmh nimependa hiyo ya kumwacha mtoto ale kwanza (kama ni muda) ndio aadhibiwe.Makes a lot of sense.
 
Lizzy,sijakuelewa uliposema napinga kwa sababu nampinga fulan!Pia sipo hapa kupinga bali naeleza mtazamo wangu!Pia naomba uniambie kupenda kwa tafsiri yako ni nini!
 
Hahahaha, kwa maelezo hayo babu ni dhahiri unampenda na sio unaishi nae kwa mazoea.

Mmh nimependa hiyo ya kumwacha mtoto ale kwanza (kama ni muda) ndio aadhibiwe.Makes a lot of sense.

Ahsasnte sana Lizzy,

Naamini sasa unaweza kuelewa kwa nini yule baba aliyeelezwa na Makaburini kwa maoni yangu hastahili tena kuitwa tena mume (achana na kwamba facts zilizopo hazijitoshelezi)!!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Hakuna neno Lizzy,

Mie ni miongoni mwa wale ambao hadi sasa sina hakika kama nafahamu maana ya hicho kitu mnaita kupenda. Kwa vile tunasonga mbele, naamini kwamba ama nafanya vizuri au mwenzangu keshanizoea na kukubali mapungufu yangu!!

Tuendelee kupeana shule!!

Babu acha tu.........hili neno wengi hatulielewi lakini mie nina ushuhuda wa mdada ambaye ameshakuwa na mahusiano makuu stable mawili) (meaning ndoa ya kwanza, bahati mbaya mume alifariki kwa ajali; amepata mwingine ambaye wanatarajia kufunga ndoa April 2012, kwa sababu tu aliambiwa anapendwa..................meaning yeye anarespond to being approached and loved (kwa kuwa ameapproachiwa/ na kuelezwa kuwa anapendwa) tu. Hakuhusiani na yeye kupenda na bado amekuwa na maisha mazuri sana kimapenzi.
Ukimuuliza anajibu kuwa yeye anampenda anayempenda!!!!
 
Ahsante mkwe, nimekupata. Mpaka hapo mimi nimeelewa kwamba tatizo halipo kwenye kupenda kwanza ama kuoana kwanza bali ni kwenye utayari wa watu kukabiliana na ndoa, majukumu yake na changamoto zake.

Kwa maana hiyo hata kizazi cha leo tukiachana ile dhana ya "nilimuoa akiwa mrembo na sasa amechuja. . . niliolewa nae akiwa na kazi inayomlipa vizuri na sasa hanayo. . .nilimuoa ili nisifiwe mjini na sasa sifa zimeisha " hivyo hanifai tena tutafika mbali. Uzuri wa wazee wetu ni kwamba hawakuchaguana kwa sura, mali na mengine kama hayo.Walichaguana ili wasaidiane though tunaweza kudhani kizazi cha leo ndio kinachosaidiana zaidi ila ukweli ni kwamba kizazi cha leo kimetawaliwa na ubinafsi zaidi. Mtu anaingia kwenye ndoa kwaajili yake tu, kwa mahitaji na matakwa yake tu.Namna anayoishi haimhusu mwenzi wake, hivyo hata akitoka nje (cheat) au akitaka kuachana hamfikirii mwenzake bali anajifikiria mwenyewe.

Mkwe maisha ya ndoa ya sasa mmmmhhh
taabu tupu ikiwezekana bora kutokuoana
mkwe mie tofauti hahahahahahahaa
hatapata taabu za hawa vijana :lol::lol:
 
Nimempenda huyo dada....Kuna sababu gani ya kuhangaika wakati kuna mtu ambaye amekueleza kuwa anakupenda na kukuonesha upendo kwa vitendo. Actually, hata kwa kutumia common senses, huwezi kuacha kumpenda mtu wa namna hiyo!!

Ngoja kwanza niishie hapa kwani Lizzy keshaanza kunichokonoa!!
 
Ahsasnte sana Lizzy,

Naamini sasa unaweza kuelewa kwa nini yule baba aliyeelezwa na Makaburini kwa maoni yangu hastahili tena kuitwa tena mume (achana na kwamba facts zilizopo hazijitoshelezi)!!

Hahahaha, babu najaribu kufikiria "mume kacheat na nimemfuma jana, mpaka leo hajaomba hata samahani ila kwa bahati mbaya kwake asubuhi ameamka hali sio nzuri au kaanguka akavunja hata mguu" je ntampeleka hosp au la? Katika hali ya kawaida ntampeleka ila akishatoka huko mambo yanarudi kama yalivyokua.

Yule besti wa Makaburini binafsi nashindwa kumhukumu kutokana na namna mke alivyomwaproach shemejie. Plus, lile sio swala la kufa na kupona, angeweza kuomba hata mmoja wa shoga zake wamsaidie.
 
...jamani mtanisamehe siwezi kuwa quote nyote, ila nitaanza kwa michango iliyonigusa zaidi...

Mabadiliko niliyozungumzia Mbu ni mengi, ila moja wapo ambalo nimeona kama limekuwa sugu sana kwa wanandoa ni hili litokanalo na kuingia kwa wanawake katika soko la ajira. Hili limekuwa tatizo sugu kwa kuwa pamoja na kuwa ni jambo zuri hasa katika dhana ya women empowernment and development bado limetuletea dhahma katika taasis ya ndoa. Mabadiliko haya hayajaenda sambamba na mabadiliko yetu ya kimaadili na kitamaduni.
Kwa wanawake:
Wengi tumeyapokea mabadiliko haya kivyengine yaani si kama ilivyodhamiriwa. Kuwa kwetu na uwezo au opportunities za kupata ajira na kuajiriwa, kushiriki kajika soko la ajira katika hali na ushindani sawa (na wengine wakiuza utu wao) na wanaume vimetufanya tuwe na ile hali ya kiburi na ile hali ya 'hata mie ninao uwezo, kama wewe'. Ninaposema kuwa mabadiliko haya hayajaenda sambamba na mabadiliko yetu kimaadili na kitamaduni nina maanisha kuwa pamoja na uwezo huu, bado wapo wanawake ambao wamekumbatia dhana za "Wewe ndie Baba wa familia, ni jukumu lako kuhakikisha familia inaprosper na si mimi; chako ni chetu na changu ni changu, wewe ni kichwa cha familia, utajiju n.k huku kipato chake mama kikiwa ni marufuku kutumika kwenye family matters hata kama kuna ulazima wa kufanya hivyo.

...dahhh!

Ahsante mkwe, nimekupata. Mpaka hapo mimi nimeelewa kwamba tatizo halipo kwenye kupenda kwanza ama kuoana kwanza bali ni kwenye utayari wa watu kukabiliana na ndoa, majukumu yake na changamoto zake.

Kwa maana hiyo hata kizazi cha leo tukiachana ile dhana ya "nilimuoa akiwa mrembo na sasa amechuja. . . niliolewa nae akiwa na kazi inayomlipa vizuri na sasa hanayo. . .nilimuoa ili nisifiwe mjini na sasa sifa zimeisha " hivyo hanifai tena tutafika mbali. Uzuri wa wazee wetu ni kwamba hawakuchaguana kwa sura, mali na mengine kama hayo.Walichaguana ili wasaidiane though tunaweza kudhani kizazi cha leo ndio kinachosaidiana zaidi ila ukweli ni kwamba kizazi cha leo kimetawaliwa na ubinafsi zaidi. Mtu anaingia kwenye ndoa kwaajili yake tu, kwa mahitaji na matakwa yake tu.Namna anayoishi haimhusu mwenzi wake, hivyo hata akitoka nje (cheat) au akitaka kuachana hamfikirii mwenzake bali anajifikiria mwenyewe.

....aiseee!?....Lizzy umegusia mambo ya msingi kabisa niliyokuwa nayategea kwenye mdahalo huu...

Mbu kwanza kabisa naunga mkono hoja zote za waliochangia tayari. Nakubaliana na maelezo sawia aloyatoa AshaDii na wengineo ila naomba nitoe ufafanuzi kidooogo.
Kuhusu women's rights au kujitambua kwa wanawake kama ilivyosemwa na wengi waliotangulia. Kwa mtazamo wangu hiki si kitu kibaya hata kidogo. Sidhani kama ni vibaya kuwa au kuzitambua haki za kila mmoja wetu. Tatizo nilionalo hapa ni namna tulivyoyapokea haya "Mahubiri" ya Women's Rights. Wanawake wengi tumejikuta tukishabikia haki hizi kama wafungwa washabikiavyo msamaha wa rahic bila kufikiria ukitoka jela humu utaishije ili usiharibu tena. Wanawake wengi wamepotea mahubiri haya kwa ushindani ule wa ...haya sasa nasie tuna haki. Ushindani ambao umepelekea wengi wetu kujikuza na kujikweza huku tukizisahau staha zetu, heshima zetu na ustaarabu wetu.

Laiti tungeyapokea 'mahubiri' haya na kuyajazia kwenye kikapu chetu chenye staha, heshma na ustaarabu apaswao mwanamke badala ya kuzitoa staha, heshima na staarabu zetu na kuzitupa nje ili Women's rights zipate nafasi. (hapa ninayo mengi kuongea utafikiri nimelipwa na TAMWA)

...am humbled, mwj1 ubarikiwe kwa ufunguo huu....dahhhh!?
 
Wanawake wasasa maadili yameporomoka kutokana na utandawazi kila nikijitahidi kuoa nashushwa dah.

Hata wanaume bwana nao maadili yao yanaporomoka kwa kasi kiasi kwamba yanakaribia kwenye mstari wa zero!!

Mfano, utajiitaje mwanamume wakati unakimbia kimbia na vitoto vya majirani zako na hata wafanyakazi wao? Au unakwenda kwenye ufuska na kurudi saa 11 asubuhi!!

Wazee wetu walikuwa wanajua kuwa mama watoto ndiye nambari one...Wengine wote ni washika pembe, mama ndiye anayekamua. Sasa hivi mnawafanya wake zenu washika pembe...Is that fair??
 
Ahsasnte sana Lizzy,

Naamini sasa unaweza kuelewa kwa nini yule baba aliyeelezwa na Makaburini kwa maoni yangu hastahili tena kuitwa tena mume (achana na kwamba facts zilizopo hazijitoshelezi)!!

Babu mi nataka kuoa sasa kila nae mpata vigezo havizingatiwi wasasa anapenda sana kushika shika kimeo changu cha mchini na anataka ajue nani kanipigia au kasisms hapa wasiwasi wangu mnaweza kuja kula pilau alafu baada ya wiki nikamtimua na malboro.
 
Hapo ndipo unapokosea siku zote. Hii ni kama ile ya kuleeee, unakumbuka? na hilo lako kosa la wengi sana si wewe tu, lakini nani wa kuwakosoa? kumbuka women rights, ni haki zinazowahusu wanawake ambazo bado hazijawa zao na women's rights ni tayari haki zao. (kabukuwe tena kuhusu "possessive tense"). Sikisii.

Ni haki ambazo zinawahusu wanawake ambazo bado hazijawa zao? It doesn't get any asinine than that! Unajua maana ya haki wewe?

Merriam-Webster's Learner's Dictionary

Women's rights - Wikipedia, the free encyclopedia

http://www.thefreedictionary.com/Women+Rights
 
Hahahaha, babu najaribu kufikiria "mume kacheat na nimemfuma jana, mpaka leo hajaomba hata samahani ila kwa bahati mbaya kwake asubuhi ameamka hali sio nzuri au kaanguka akavunja hata mguu" je ntampeleka hosp au la? Katika hali ya kawaida ntampeleka ila akishatoka huko mambo yanarudi kama yalivyokua.

Yule besti wa Makaburini binafsi nashindwa kumhukumu kutokana na namna mke alivyomwaproach shemejie. Plus, lile sio swala la kufa na kupona, angeweza kuomba hata mmoja wa shoga zake wamsaidie.

Hapo (blue) tuko pamoja.....Inapobidi unamsaidia kama binadamu mwingine yeyote ambaye ungempatia msaada endapo angepata emergency mbele yako!!

Kwenye red, Makaburini aliitwa baada ya mume kukataa kutoa msaada au nimesahau??
 
Mkwe maisha ya ndoa ya sasa mmmmhhh
taabu tupu ikiwezekana bora kutokuoana
mkwe mie tofauti hahahahahahahaa
hatapata taabu za hawa vijana :lol::lol:

Hhahahahha, ndio unaniingiza mjini hivyo mkwe?Usije ukamnyanyasa wakati mwenzio anakupenda alafu arudi kunililia.
 
Ahsasnte sana Lizzy,

Naamini sasa unaweza kuelewa kwa nini yule baba aliyeelezwa na Makaburini kwa maoni yangu hastahili tena kuitwa tena mume (achana na kwamba facts zilizopo hazijitoshelezi)!!

....swadaktaaaaaaa......!

ila mtazamo wangu nawe unatofautiana kwenye quotes alizoziainisha makaburini;

picha ninayoipata ni kwamba mke alinunua gari kiushindani, na mume kwa gubu lake kama zali vile siku hiyo lilipomgomea ndio naye akatapika machungu yake!

Wadhani iwapo gari hilo kwenye manunuzi yake huyo mume angekuwa ameshirikishwa bado angeendelea kumsusia?
Kumbuka mkuu, sie vijana wa zamani tuna kasumba mke hata akiwa na uwezo vipi, bado anastahiki kupata go ahead toka
kwa mumewe kufanya maamuzi makubwa ya maisha mfano kujenga, kununua gari nk....au?
 
Babu mi nataka kuoa sasa kila nae mpata vigezo havizingatiwi wasasa anapenda sana kushika shika kimeo changu cha mchini na anataka ajue nani kanipigia au kasisms hapa wasiwasi wangu mnaweza kuja kula pilau alafu baada ya wiki nikamtimua na malboro.

Fidel, ukishapata walau mmoja ukahisi anaweza kuwa mwenzi wako, basi hao wengine wape likizo umpe yeye nafasi hadi itakapothibitika kuwa haiwezi uone kama itakupa tatizo.

Sasa unataka uwe na dada wa watu wakati huo umeegesha magari kibao getini....It will never work labda upate mtaalamu wa kucheza usanii kama huo!
 
....swadaktaaaaaaa......!

ila mtazamo wangu nawe unatofautiana kwenye quotes alizoziainisha makaburini;

picha ninayoipata ni kwamba mke alinunua gari kiushindani, na mume kwa gubu lake kama zali vile siku hiyo lilipomgomea ndio naye akatapika machungu yake!

Wadhani iwapo gari hilo kwenye manunuzi yake huyo mume angekuwa ameshirikishwa bado angeendelea kumsusia?
Kumbuka mkuu, sie vijana wa zamani tuna kasumba mke hata akiwa na uwezo vipi, bado anastahiki kupata go ahead toka
kwa mumewe kufanya maamuzi makubwa ya maisha mfano kujenga, kununua gari nk....au?

Mkuu,

Katika mazingira kama hayo, you have to be a human being first and next you call yourself Mbu or DC!!

Huwezi kunipa sababu ya msingi ya mume kutomsaidia mke wake wakati wa shida halafu useme hiyo ndoa haijapata permanent damage!!

Kaka kumbuka ndoa ni ya watu wa 2...an injury to one must be an injury to both...If one is injured and the hubby anafanya tafrija...that is the beginning or even the end of things fall apart!!
 
Back
Top Bottom