MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,563
...asante mwj1....
...unapozungumzia changes una maanisha nini? kwa muono wako, wadhani mabadiliko haya yameanza lini kiasi cha kulinganisha uzamani wa wazazi wetu na huu usasa wa kikwetu?
...mtazamo wangu wa ndoa za kisasa nalinganisha waliooana 1980's kuja mpaka leo hii 2011....kasi ya watu kuoana na kuachana imekuwa kubwa kulikoni wazee wetu waliokuwa wameoana miaka ya 60's na kurudi nyuma...au?
Mbu kwanza kabisa naunga mkono hoja zote za waliochangia tayari. Nakubaliana na maelezo sawia aloyatoa AshaDii na wengineo ila naomba nitoe ufafanuzi kidooogo.
Kuhusu women's rights au kujitambua kwa wanawake kama ilivyosemwa na wengi waliotangulia. Kwa mtazamo wangu hiki si kitu kibaya hata kidogo. Sidhani kama ni vibaya kuwa au kuzitambua haki za kila mmoja wetu. Tatizo nilionalo hapa ni namna tulivyoyapokea haya "Mahubiri" ya Women's Rights. Wanawake wengi tumejikuta tukishabikia haki hizi kama wafungwa washabikiavyo msamaha wa rahic bila kufikiria ukitoka jela humu utaishije ili usiharibu tena. Wanawake wengi wamepotea mahubiri haya kwa ushindani ule wa ...haya sasa nasie tuna haki. Ushindani ambao umepelekea wengi wetu kujikuza na kujikweza huku tukizisahau staha zetu, heshima zetu na ustaarabu wetu.
Laiti tungeyapokea 'mahubiri' haya na kuyajazia kwenye kikapu chetu chenye staha, heshma na ustaarabu apaswao mwanamke badala ya kuzitoa staha, heshima na staarabu zetu na kuzitupa nje ili Women's rights zipate nafasi. (hapa ninayo mengi kuongea utafikiri nimelipwa na TAMWA)
Kuhusu Upendo:
Kwa mtazamo wangu mie haya mapenzi ya "Egoli" tuliyoyaiga toka kwa wazungu yamechangia kwa kiasi kikubwa udhaifu katika ndoa nyingi za siku hizi. Hii kujidai unataka kufall in love ndo uoe/olewe imetupelekea kuiumbia na kuikubali counterprt ya falling in love ambayo ni falling out of love. Siku hizi si jambo la kushangaza kujikuta unaitwa kwenye kusuluhoisha ndoa ambayo mmoja wa wanandoa hao alilala tu usiku na kuamka asubuhi akiwa ameshafall out of love na sasa anadai talaka au anataka kuvunja ndoa. Na ajabu sana kuna kila aina ya justification ya hii falling out of love ambayo mwisho wa siku tunalazimika kukubaliana na muota ndoto huyo.
Wazee wetu wa zamani hawakuwaga na falling in love bali walikuwa na Growing in love...it just keep on growing hakuna kufall out na ndio maana walikuwa wavumilivu. Kwa kuwa unaishi kwenye ndoa ambayo kadri siku ziendavyo love inajijenga, kukua na kukomaa hata ukifanyiwa kosa gani wewe unajihisi kumpenda zaidi ingawa kwa manung'uniko kwa ndani! Ndoa za siku hizi kwa kadri unavyokosea mwenzio ndivyo anavyoendelea kuizungusha door knob ya love na mwisho anaufunguua na baaam amefall out.
Samahani imekuwa ndefu.