NDOA: Zamani vs Siku hizi

....kuna mambo yalikuwa kama taboo kwa siku za nyuma ambayo kwa kizazi hiki imekuwa kama kawaida sasa...
mke kuanzisha bifu na mama mkwe na mawifi....

hii haikuwapo zamani, maana mke ilikuwa ni taswira ya ukoo aliotoka...
miaka ya hivi karibuni, imekuwa vice versa,....mke akiolewa inakuwa kama nani zaidi, yeye au familia ya mume!
kishindo heavy! ....pheewww, mnisamehe dada zangu, ila nanyi ni mawifi na wakwe watarajiwa...

Kuna familia naijua inamchukia mke wa kaka yao kwa vile hataki waweke picha za mtoto wa kaka yao facebook!!!! na mambo mengine ya ndani amabyo mashemeji wamemfanyia huyu binti lakini kibaya zaidi kuambizana kuwa wamtenge wifi yao, wasimwalike kwenye 'shughuli zao na wala wasiende kwake hata awaalike!

Kweli ndugu wa mume ni mzigo!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu

...haya sasa, athari za utandawazi kwenye ndoa za kisasa,...si ni suala la kuelewana tu hapo desturi zetu?
uvumilivu na uelewa umepungua sana miaka hii au na ujuaji umetuzidi?

...msidhani miaka hiyo hapakuwepo 'mashindano' haya ya kifamilia, kulikuwa na mivutano
lakini miongozo ya kimila na tamaduni ilisimamiwa na kuheshimiwa tofauti na sasa ambapo neno sio desturi zetu
linakufanye uonekane kama wa zamaani!
 
Ndo unaposhangaa mtu kuamua maisha ya familia ya ndani ya mumewe. Nadhani watu wamelipukia matumizi ya mitandao ya kijamii mfano wa mbwa aliyefunguliwa toka kwenye cage. Binafsi sidhani kama ni sahihi kuweka mapicha ya watoto wadogo kwenye mitandao, wakue waamue watakavyo.

Kimsingi ndoa za zamani zilidumu kwa vile mfumo ulikuwa kandamizi na wanawake walikuwa moulded kukubali kukandamizwa, hata kwama walikuwa wakiugua maumivu ya ukandamizwaji, udhalilishwaji kutokana na mfumo wa kijamii lulokuwepo (mfumo dume). Mwanamke anayetoka kwenye ndoa kwa kukataa manyanyaso toka kwa mume au ndugu wa mume alionekana dhaifu, asiyefaa, na anayestahili kutengwa na wanajamii wote (sio ndugu wa mume tu bali hata ndugu wa mwanamke huyo).

Hivyo basi naungana na wote waliosema kuwa uthabiti wa mwanaume katika kuonyesha msimamo wake kwa mkewe dhidi ya mashambulizi toka kwa mume una afasi kubwa sana katika kuokoa ndoa hizi.

Kingine ni kuelewana (understanding each other). Kila binadamu ana mapungufu, hakuna mtimilifu abadan. Hivyo basi pamoja na elimu tulizonazo, teknolojia tuliyonayo, maendeleo na mabadiliko ya kiutamaduni tunayokumbana nayo (hasa kwenye inter tribal na religion marriages) ni muhimu kuwa wawazi na kujadili mapungufu ya wenza wetu. Na katika kujadiliana tukubali kutokubaliana bila kuweka inferiority complex an magrudges juu ya wenza wetu. Flexibility kwenye yale yapasayo iwepo, sio mtu unakuwa na msimamo kama chuma cha pua, yaani hadio uone matokea ndio ukubali kubadilika.
 
....safi kabisa, tupo ukurasa mmoja...

...ila hapo kwenye mfumo wa ukandamizaji tunaweza debate mpaka kukuche,
mfano; lipi weye ulionalo ni ukandamizaji ambalo likiondolewa halitakuwa na athari kwenye ndoa?
 
mfano, katika familia nyingi mwanaume ni mfalme na me ni kijakazi wake. Na ndivyo ilivyokuwa kwa wengi wa wazazi wetu. Mwanamke uamke wa kwanza saa kumi na moja na ulale wa mwisho saa tano. Uwahi kuamka kuhakikisha unaandaa watoto kwenda shule wakiwa wasafi, wamestaftahi, na wamechukua kila wanachopaswa kuchukua. Wakiondoka au wakati unaandaa watoto umuandae na baba, mwisho ujiandae wewe, kama si kwenda kazini basi ni kwenda sokoni, saloon, ngomani, msibani na sehemu kama hizo. Uhudhurie misiba yote ya ndugu wa mume na ya kwenu, wagonjwa wote wa ndugu wa mume na ndugu zako, watoto waliozaliwa nk. Short of that wewe si mwanamke. Jioni chakula kiwe tayari mapema, uhakikishe mume kashiba na chakula kingine cha usiku umemlisha vizuri.

Hakuna mtu anayejali biolojia ya mwanamke, kwamba kuna siku unakuwa na hormonal imbalance, umechoka choka tu kuumwa huumwi, usipowajibika unaonekana mvivu na hufai kuwa mke. Unapouw ana maumivu ya MP ukashindwa kupaka wanja nai kuamka mapema basi ndoa imekushinda, unatafutiwa mke wa pili.

Huu ni mfano mmoja wa haraka kati ya mingi. Huu si ukandamizaji?
 
Back
Top Bottom