Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
Mkandara kwa nini umengia kwenye mtego wa kukumbatia falsafa ya George Bush ya "either you are with us or against us"? Mimi simuungi mkono Lowassa lakini pia siwaungi mkono watu wanaopenda kufanya ukasuku. siipendi tabia ya watu wanaoua mtu mwingine kwa sababu tu wamesikia sauti ya watu wengine wakimwita huyo mtu mwizi. Imeshawahi mara nyingi tu watu wameuawa kwa kuitwa mwizi na wagoni wao.Siwapingi na Chaguo lenu, lakini tafadhali msitake kuupoteza Umma kama nyie mnamchagua Lowassa mchagueni kwa matakwa yenu lakini kumpigia chapuo hapa JF kama vile sisi mijinga iliyolala hapo wakuu zangu mnatupeleka kusiko....
Mimi nasema hizi "allegations" zisipojengwa katika misingi ya kisayansi yaani kuegemea katika uthibitisho, mwisho wa siku tutakuja kuombana radhi na wale ambao leo tunawaona ni mafisadi wa kutupa. kati ya watu wanaomini kwamba Lowassa ana mapungufu makubwa ya uadilifu mimi ni mmojawapo, lakini siipuuzii nguvu ya Lowassa katika jamii na jamii ya wanasiasa hapa Tanzania.
Siku Lowassa alipofanikiwa kuwa Mwenyekiti ya kamati ya Ulinzi na mambo ya nje niliwaambia wenzangu kwamba pamoja na ufisadi wake bado ana nguvu sana kwenye siasa za Tanzania. Kama ukitaka kupambana na Barcelona na ukaichukulia nguvu yake ni sawa na Mtibwa Sugar ya Morogoro, utakuwa unajidanganya.
Kamati anayoiongoza Lowassa ndiyo inayosimamia majenerali wetu, Idara ya Usalama wa Taifa, Wizara ya mambo ya Nje ya Nchi, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. pamoja na ufisadi wote tunaoujua wa Lowassa bado jamaa ilishindikana kumzuia kupewa kamati nyeti namna hii. Mkandara hata mimi sina ndoto ya kuwa na Rais anayeitwa Edward Ngoyai Lowassa, lakini pia najua kwamba sitapiga kura peke yangu na hao wenzangu sijui mitizamo yao kuhusu Lowassa.
Hoja yangu ni lazima wale "wanaojua" madhambi ya Lowassa watupe ushahidi usiotia shaka "Beyond resoanable doubt" ili na sis tuweze kuwaeleza wengine kinagaubaga ubaya wa huyu jamaa bila ya kubuni buni mambo au kushabikia yale yanayosemwa na wengine. Ndiyo maana sipendi watu wachache tu ndiyo wayajue madhambi ya Lowassa.