Mali za Lowassa hazisemwi kama alivyokuwa Mubarak madarakani penginehuelewi nafasi ya Lowassa ndani ya chama kulingana na mjadala huu, nimeyasema mengi sana. Kama EL ataondolewa madarakani kabisa, na hakubaliki na wananchi kama Mubarak mali zake zitakuja julikana wala sii zake tu na wenigine wote waliokuwa chini yake ama pamoja naye - Lowassa hajaondoka bado.Mkuu. Hakuna mahali mimi nimezungumzia ukali wa Lowassa au kufaa kwake bali hoja yangu imejikita kwenye ulinganisho wa uwiano. Kama Mubarak mali zake zimejulikana hatimaye kutaifishwa kwa nini kila siku tunaambiwa kwamba Lowassa ni tajiri wa kutupa wakati wanaosema hivyo hawajawahi kutuambia kwamba Lowassa ANAMILIKI nini. Mara zote mimi hupenda kujitenga na USHABIKI.
Kwenye siasa kufaa na kushinda UCHAGUZI ni vitu viwili tofauti. Wakati kushinda uchaguzi ni mikakati ya kikampeni na uzowefu wa kuratibisha minyukano ya kisiasa kuweza ni ubora miongoni mwa wanaoomba kuchaguliwa kuwa viongozi. Kama Ufisadi wa Lowassa umejikita kwenye kufikirishwa na wanasiasa wenzake ambao wengi wao ni maadui zake, mimi nitaendelea kuwa TOMASO ili niupate UKWELI.
Sikuwahi kumuunga mkono Lowassa na wala sina haja ya kufanya hivyo lakini najua athari za kuachia watu wengine washambuliwe bila ya wanaotoa mashambulizi kutakiwa kutoa ushahidi. Hata pale Mwembe Yanga Slaa alimtaja Lowassa kuwa fisadi kwa kufanya maamuzi yaliyoligharimu taifa lakini si kwa kukwapua mali za umma.
Kuna kisa hiki ambacho nimekibadili kifae kwa mazingira ya kwetu Tanzania. Kulikuwa na wamakonde, wachaga, wahaya, wanyakyusa na Wahadzabe wametekwa na majambazi. Wale majambazi wakaita "Wahaya tokeni mbele' Wahaya wakatoka na kuuawa mbele ya wenzao, waliendelea kuitwa hivyo mpaka ilipofika zamu ya kundi la Mwisho , jambazi mmoja akasema, "hao waue hapo hapo" wale mateka wakasema "sisi ni wamakonde msituue" na wao pia WAKAUAWA!!
Pili, kinachonifanya kutompenda Lowassa sii utajiri wake narudia tena sii utajiri wake bali UFISADI wake sijui anapokea kiasi gani ktk madeal ya Citywater, Richmond, Buzwagi, Bulyanhulu, Mara, TRC, ATC, Bank kuu na kadhalika list ni ndefu sana, maamuzi mabaya yalifanyika chini ya uongozi wake na kutugharimu hadi leo acha mbali hesabu za siku zake akiwa madarakani.
Tatu, maadam mimi na explore reality nakuomba nambie hivi kweli Lowassa akiwa rais, Chadema wataweza kuzungumzia Ufisadi tena? kuna mtu anaweza kusimama na kulaani Ufisadi chini ya jicho lake..JF kweli itapona au itakuwa hii ya leo.... na mtu anayesema JK achukue maamuzi magumu.. Unamkumbuka T. Mhando alipo sukuma issues za Chadema ilikuwaje? Mwandishi wa rais Rweyemamu akimwandikia yeye barua ya kuomba ajira na sio ofisi ya rais. Mawaziri wakijipendekeza kwake wachaguliwe uwaziri na hadi ubunge bado huoni ubaya wa huyu mtu hadi ujue mali zake?. wabunge ili wapate kutumikiwa majimbo yao lazima wajipange naye ktk kumlamba miguu..
Ebu nambie wewe siku Ile Dr.Slaa alipomtaja Lowassa kama fisadi ulielewa vipi kama unajua haikuhusiana na kukwapua mali za Umma..Na Je, wewe unasubiri pato la Taifa liibiwe lenyewe na sio mikakati inayolikosesha Taifa mapato sio wizi sio?..Basi watu tunatazama vitu tofauti sana maana wewe unatazama kimachinga wakati mimi natazama sera na mikakati..
Siwapingi na Chaguo lenu, lakini tafadhali msitake kuupoteza Umma kama nyie mnamchagua Lowassa mchagueni kwa matakwa yenu lakini kumpigia chapuo hapa JF kama vile sisi mijinga iliyolala hapo wakuu zangu mnatupeleka kusiko... tumjadili kwa sifa zake na mziweke wazi lakini sio tu Lowassa hana madhambi wanamsingizia.. Huyu mtu ni hatari na sioni tofauti yake na Dikteta wa Syria au Ghadaffi ana agenda chafu sana.