Ndiyo, Lowassa ni fisadi na hilo halina ubishi lakini ndani ya CCM yupi ni afadhali Urais 2015!

Ubinafsi ni tabia mbaya sana, mtu anaweka gazeti hapa ili mradi ajinufaishe yeye baadae.
 
Wanajamvi, bila shaka lolote kila binadamu hupenda madaraka, hupenda sifa na hupenda mali na kama yupo binadamu ambaye hapendi hivyo vitu, huyo hajaumbika nikiwa na maana ana mapungufu fulani. Kinachotutofautisha ni msukumo na kiwango cha tamaa kilicho nyuma ya jitihada zetu katika kuvitafuta. Tamaa ya wastani ni kitu kizuri kwani haitoi nafasi kwa tabia za ulafi, udanganyifu, wizi na hujuma. Lakini tamaa inapovuka mpaka, then hell breaks loose, na vyama kama CCM hugeuka na kuwa kama shamba la kuotesha na kukuza mafisadi kama Lowassa.

Edward Lowassa ni mfano tosha wa mavuno halisi kutoka shamba hilo la CCM lakini tofauti kati yake na makada wengine ni kwamba anawajibika. Aliwajibika kama Waziri Mkuu kwa kujiuzulu ili kuisetiri serikali ya CCM pamoja na Kiongozi wake mkuu, Raisi Jakaya Mrisho Kikwete. Kwa hekima fisadi msaidizi ilibidi ajiuzulu ili fisadi mkuu abaki madarakani kumlinda yeye na mafisadi wengine ndani ya chama na serikalini. Hata hivyo yanayotokea sasa ni uthibitisho tosha kuwa ushirika katika maovu hauwezi kudumu milele na ni swala la muda tu kukuru kakara huanza.

Washiriki wote katika kuisetiri serikali pole pole wanaaza kuvuna walichopanda tukianza na Mwakyembe, Sitta, na Kikwete mwenyewe. Nyumba (CCM) inayowasetiri imeanza kuungua moto na taratibu moshi wake umewaathiri wote wanaoishi humo kiasi wanashindwa hata kuonana. Lengo langu hapa si kumtetea Fisadi Lowassa, la hasha, kwangu adui mkubwa wa taifa letu si mtu moja bali ni zimwi CCM. Ndani ya CCM naamini hakuna aliye safi hata moja lakini kama ni kumla nguruwe, hakuna aliyenona kama Edward Ngoyai Lowassa, mbunge wa Monduli.

Mimi, tofauti na wengi, naamini EL pamoja na madhambi yake yote, katika kujiuzulu Uwaziri Mkuu alitumia busara. Nampongeza kwa tendo lake hilo, likifuatiwa na la juzi la kukataa kujiuzulu CCM na kumhusisha Raisi katika sakata la Richmond, jambo ambalo limezidi kuiumbua CCM na kuiacha uchi. Wakati wa Richmond kuna watu kama Hosea tulitegemea wangejiuzulu lakini hawakufanya hivyo na leo kuna watu kama Luhanjo tulitegemea watajiuzulu mara moja lakini bado wapo tu ! Tusidanganyane, Kikwete hakuwa na ujasiri wa kumfukuza Lowassa.

Karibuni mtakaodai na mimi Mag3 niko kwenye payroll ya Lowassa, hilo halinipi taabu hata kidogo, siwezi kumzuia yeyote kufikiria hivyo. Ukweli ni kuwa kama Raisi 2015 atatoka CCM (na hilo Mungu atupishilie mbali !), basi ndani ya hiki Chama cha Mafisadi, kwa sasa hakuna kama Lowassa kama taifa linataka kujinasua kwenye dimbwi la utawala legelege uliojaa usanii. Uwajibikaji, uvumilivu na ujasiri aliouonyesha ni dalili nzuri katika Uongozi kama hazitasukumwa na ulafi na tamaa, vitu ambavyo hata hivyo vimemganda kama kupe na kumwandama kama kivuli chake !

Nafanya rejea tuu na kulinganisha na hali ilivyo sasa!.
Pasco
 
Naliangalia suala hili kwa mtazamo wa maana ya uongozi na thamani zake. Kiongozi hata awe mchapa kazi kiasi gani mara zote hupimwa kwa uadilifu wake. Ninapomwangalia EL simpimi kwa suala la Richmond tu, naangalia nguvu yake ya uadilifu kwa umma wakati wa suala zima.

Alipokuwa waziri mkuu alitumia mbinu nyingi sana kulizima suala la Richmond. Ni wakati huo alikubali na kulitaarifu bunge kuwa taarifa ya PCCB ilikuwa sahihi na hakukuwa na mauza mauza katika mkataba wa Richmond. Alitoa kauli hizo akijua wazi kuwa alikuwa anaudanganya umma wa Watanzania kwani leo hii amekiri kuwa alitaka kulisitisha kabla ya taifa kutumbukia kwenye hasara kubwa.
Alijua matokeo ya uchunguzi wa Hosea na gharma za uchunguzi huo lakini akafumba macho na kuziba masikio.

Kamati ya Mwakyembe ilipotoa taarifa, EL alipewa nafasi ya kujieleza. Tunafahamu alisema nini kwa jazba na hasira. Maneno yake ya 'ninemdhalilishwa sana na ni kwasababu ya uwaziri mkuu' hayakuwa na nia ya kuwaeleza Watanzania udanganyifu wa Dr Hosea, gharama za uchunguzi achilia mbali hasara kubwa taifa iliyolipata bali uwaziri mkuu wake.

Miaka 2 anakuja kutueleza kuwa alitaka kusitisha mchakato wa Richmond akazuiwa na swahiba yake. Ameyasema haya si katika maongezi ya kawaida bali katika kujitetea asichukuliwe hatua za nidhamu. Hii nayo ni katika kulinda kitumbua chake na sio kueleza masikitiko ya hasara taifa iliyoingia.

Kiongozi mwadilifu angeyasema hayo mwanzoni kabisa hata kabla ya Hosea hajamwaga ----- wake uliomdhalilisha EL, Rais na serikali kwa ujumla. Leo Hosea anaonekana mtu hovyo mbele ya jamii na taasisi anayoongoza imepoteza imani kwa wananchi.

Hata kama anauwezo wa kusukuma ajenda mbele na kutoa matokeo EL hana sifa ya uaminfu na uadilifu achilia mbali mbinu zake chafu za kutumia ukabila na udini atimize malengo yake kama tunavyomuona akihangaika sasa.

Sidhani kuwa kwa vile kuna jambazi mtaani anatusaidia kubeba mizigo bure, kuchimba makaburi peke yake, kubeba wagonjwa tukimhitaji, kulima mashamba kwa bei nafuu sana, basi yote hayo yatufanye tusahau kuwa jambazi ni mtovu wa uadilifu na haaminiki!!!!

EL akumbuke kuwa mtu anapokuwa na ng'ombe 20 pengine hakuna anayejua mtaani kwake, lakini mtu huyo akibeba kilo moja ya nyama iliyooza basi mtaa na mji mzima utazungumzia hilo.
EL ana kilo moja ya nyama iliyooza!!
Sijui mkuu Nguruvi3 bado upo ukishuhudia haya yanayotokea au you are among those missing in action? Mkuu Mag3 nadhani sasa unaweza kupiga makofi kwa nyayo zako!
 
Last edited by a moderator:
Msome vizuri Jakaya kwenye blogu yake maalum, akiapa kuwa Lowassa si fisadi, bali alisingiziwa

attachment.php
 
Back
Top Bottom