Ndiyo, Lowassa ni fisadi na hilo halina ubishi lakini ndani ya CCM yupi ni afadhali Urais 2015!

mara nyingi wabongo hatuko logic, ili rais asimame nani anamsimamisha? bila shaka chama chake...km JK hafai maana yke ccm haifaii. hao unaofikiria ni safi ndani chama kwa nini hawakusimama kupinga JK kupita? kama taifa tuna mambo muhimu ya kujadili mf. uzalendo ni nini? uzalendo unajitokezaje kwa mtu moja moja? kwa chama? kwa taasisi?...je tunahitaji kiongozi mzalendo au watu wazalendo?... hatupaswi kufikiri juu ya majina.
Hata mimi naamini hatuna haja ya kutaja majina kwa sasa kwani wenyewe kama jamii hatujawa safi kiasi cha kuuchambua usafi wa wenzetu. Kuna wakati nilisema humu ndani kama tungekuwa tunatumia majina yetu halisi wengi wetu tusingekuwa jasiri kama hivi tulivyo.

Kuna maaskari wanamiliki magari lakini ni kutokana na ulaji rushwa. Badala ya kulalamika basi ni lazima tubadili mfumo mzima wa maisha yetu kutoka kwenye familia zetu hadi kwenye ngazi ya taifa. Kama askari ananunua gari basi iwe ni kwa njia zilizo halali na si kwa njia za kirushwa rushwa kama ilivyo sasa. Nakumbuka Mtikila alivyomwita Rostam Aziz fisadi naye RA akatoa nakala ya hundi aliyomlipa Mtikila fedha ili akajengee kanisa lake na kanisa halikujengwa na hela iliyotolewa na "Fisadi" haijulikani "msafi" Mtikila aliifanyia nini.

Ukienda kwenye NGOs wanakwambia siku hizi huwezi kupata fedha za kuendeshea shughuli bila ya kutoa dhamananyuma (Kickback) Hali hiyo iko kwenye kila nyanja kuanzia Ukandarasi, udahili wanafunzi vyuoni, upatikanaji wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu hadi mikopo ya kwenye mabenki. Siku Moja niliombwa rushwa na kiongozi wa Magerezae ili ndugu yangu apekelekwe kwenye chuo cha Magereza Kiwira hadi nikamuuliza askari anayeajiriwa kwa rushwa atakuwaje? Kwa ufupi UFISADI ni mfumo wa maisha yetu na ili tupambane nao ni LA ZIMA tuzikane nafsi zetu.
 
Mnahangaika bure Lowasa hawi Rais 2015. Hii ni kwa vile Hana chama cha kumsimamisha labda Kama tukibadili katiba na kuruhusu mgombea binafsi njia ambayo ni ngumu kwa yeyote kuipita na kuwa Rais. Ukweli ni kwamba CCM bado inao watu safi na wenye uwezo wa kupipatia chama cha mapinduzi ushindi. Kama suala ni ufisadi tu hata cdm inaongozwa na mafisadi. nani hajji kilichomtoa Dr Slaa katika baraza la Maaskofu pale kurasini Kama siyo ufisadi na ufuska! Mbowe ndiyo usiseme ufisadi ndiyo Amira yake. Kwa kizazi hiki hakuna chama cha upinzani cha kuiondoa CCM madarakani. Labda kizazi kijacho.

Kwa kauli hii unaonekani bado hujajua ukweli wa mambo. Wtz wa sasa hawaifanyii majungu kazi, wanachotaka ni facts with evidence na si hizi longolongo zako za kiwendo wazimu. Your are realy behind the time, your need to walk up to ketch up with a now time! Achana na mawazo potovu we kamtu!!!
 
Bwana Wildcard,

Afadhali sisi tunakubali UDHAIFU ila tunaamini tutasonga mbele maana NIA, Mikakati na UWEZO tunao.

Lowassa all they way.

Na nyie nani all the way?
FP,
Mimi nasubiri KATIBA MPYA itupatie namna nzuri ya kumpata Rais ajae 2015. Tumeambiwa katiba hii itazinduliwa April 26, 2014. Natumaini katiba itaweka wazi WATANZANIA wagombee kwa sifa zao. Kwa uwezo wao. Wagombea waandike ILANI zao. Tujue wao wanautaka URAIS wa JMT kwa nini. Ilani za vyama vyao zitafuata baadae. Watanzania pia tutakuwa na sauti kwenye ilani ya TAIFA. Tutawambia mapema tunayotarajia kutoka kwao. Tutawapima kila mara kwa ilani hii ya TAIFA.
Vyombo vya DOLA vitaelezwa na katiba hii mpya wajibu wao. Mipaka yao ya kazi. Utendaji wao. Visimamie UCHAGUZI HURU na wa HAKI. Vitangaze matokeo ya KWELI. Katiba hii mpya itavieleza vinawajibika kwa nani na kwa kiwango gani. Kenya wameweza sielewi ni kwa nini sisi ambao tunajidai ni WAMOJA zaidi tushindwe.
Ndio maana kwa sasa napendekeza tusizungumzie watu. Tuzungumzie KATIBA pamoja na mapungufu yaliyokwisha jitokeza. Hawa tunaowazungumzia sasa huenda KATIBA ijayo isiwaruhusu kugombea kama sifa mama za KIONGOZI wa TAIFA zitawekwa vizuri pamoja na MIIKO thabiti ya uongozi.
 
Tena Wildcard.. Katiba itutengenezee ilani ya kudumu ya Taifa.Na itaje wizara muhimu kwa nchi,tenaza kudumu.Siyo kila rais anaundaunda tu wizara ili awapoze washkaji zake. Ndiyo maana tunaambiwa sisi ni irrelevant tunang'aka......
 
Kwa vyovyote KATIBA ijayo itakuwa nzuri tu. Baadhi yetu tunataka kuona haya ulioyataja ndani ya KATIBA hii. Tuiondoe serikali BUNGENI. Wabunge wasiwe mawaziri ili BUNGE liisimamie kwa dhati SERIKALI. Vyombo vya DOLA ndivyo vimeifanya CCM itutawale inavyotaka. Tumekosa Tume huru ya uchaguzi. Tumekosa MAHAKAMA huru. Tumekuwa na Rais MunguMtu.
Halafu watu tunapoteza muda kuwajadili watu watutawaleje! Watatuwala vilevile kama KATIBA itaendelea kuwa ileile. Lowasa kapewa Uwaziri Mkuu na swahiba wake kwa kutumia KATIBA hii. Kaanza kututafuna mapema. WAtu wanataka tumpe URAIS kabisaa!
 
FP,
Mimi nasubiri KATIBA MPYA itupatie namna nzuri ya kumpata Rais ajae 2015. Tumeambiwa katiba hii itazinduliwa April 26, 2014. Natumaini katiba itaweka wazi WATANZANIA wagombee kwa sifa zao. Kwa uwezo wao. Wagombea waandike ILANI zao. Tujue wao wanautaka URAIS wa JMT kwa nini. Ilani za vyama vyao zitafuata baadae. Watanzania pia tutakuwa na sauti kwenye ilani ya TAIFA. Tutawambia mapema tunayotarajia kutoka kwao. Tutawapima kila mara kwa ilani hii ya TAIFA.
Vyombo vya DOLA vitaelezwa na katiba hii mpya wajibu wao. Mipaka yao ya kazi. Utendaji wao. Visimamie UCHAGUZI HURU na wa HAKI. Vitangaze matokeo ya KWELI. Katiba hii mpya itavieleza vinawajibika kwa nani na kwa kiwango gani. Kenya wameweza sielewi ni kwa nini sisi ambao tunajidai ni WAMOJA zaidi tushindwe.
Ndio maana kwa sasa napendekeza tusizungumzie watu. Tuzungumzie KATIBA pamoja na mapungufu yaliyokwisha jitokeza. Hawa tunaowazungumzia sasa huenda KATIBA ijayo isiwaruhusu kugombea kama sifa mama za KIONGOZI wa TAIFA zitawekwa vizuri pamoja na MIIKO thabiti ya uongozi.
Mkuu wangu unacheza karata hapa wakati wildcard huna mkononi.. Hakuna katiba mpya uitakayo lazima wakati mwingine tujifunze. Hawa watu waliokuja hapa kumtetea Lowassa ni kwa sababu wanajipendekeza kama Mama Sophia Simba ambaye kisha jua the next President inline ni Lowassa na katiba itatengenezwa kwa maslahi yake kumlinda na kuwalinda mafisadi wote kama alivyokataa kujiengua Ubunge na Unachama. Kama nimemwelewa Pasco anachozungumzia yeye ni kwamba odds zote za ushindi anazo Lowassa, jipangeni nyuma yake..Ni lugha ilofunikwa kawa lakini harufu inayonukia inajieleza kimepikwa nini!..

safari hii CCM itakataa kujiengua ndani ya Katiba ili kuendelea kulinda Ufisadi, hivyo hakuna mategemeo yoyote ktk uchaguzi wa mwaka 2015 zaidi ya kutokea machafuko makubwa nchini ambayo hayajawahi kutokea. Amini maneno yangu leo hii katiba itakayotoka mwaka 2014 itakuwa sio uloitaka na tutapiga biashara zetu za machinga hadi uchaguzi 2015 bila marekebisho wala marudio, maana tungeweza kabisa kuanza mchakato wa katiba mpya mara tu JK alipoingia madarakani mwaka 2005..Kitu gani kilitulazimu kusubiri hadi leo hii ili katiba mpya itoke 2014?.

Kwa hiyo wapo vijana wengi wameisha give up na wanajua nguvu ya Lowassa. Kama alivyosema mwanaJF hapo nyuma hizi ni siasa za Bush ingawa alisema zangu mimi ndio hivyo lakini ukweli utabakia You aither with us or with enemy lazima uchague upande na wao wameisha chagua upande unaolipa hata kama hakuna haki. Hizi ndio siasa za New world order na zinauzwa dunia nzima maana neno mwanamapinduzi limekwisha ondolewa isipokuwa Magaidi - Terrorist...

Lowassa ana fit sana ktk tafsiri ya viongozi wanaotakiwa na nchi za magharibi, viongozi machinga ambao wanasubiri misaada na kuuzia wananchi wao kama maendeleo. Viongozi wanaoagiza finished product nje na kuuzia wananchi wake kama ndio maendeleo ya nchi na Commanding Heights zote wamezishika wao sharing with Western Government hivyo zinalindwa na mtawala mwenyewe ambaye pia analindwa na nchi hizo. It's all about investment na Lowassa ni mfanyabiashara mwizi mzuri sana hivyo he is the right candidate kutuibia ktk mfumo huu. Enzi za kina Mobutu zimerudi tena kwa nguvu kubwa sana ku plant viongozi wanaoweza kuibia wananchi wao rasilimali zao, viongozi wasiokuwa na haya wala uzalendo isipokuwa kwa kutumia vitabu..

Bahati mbaya tu ni kwamba kila Mtanganyika leo hii ni machinga toka rais aliyepo, wabunge hadi wasomi wetu wanapendekeza zaidi biashara ya umachinga tuletewe vitu vilivyokwisha tengenezwa (elimu, mtaji na hata nguvukazi) hata kama vipo hapa nchini waje wageni wavitengeneze kwa dhana ya kwamba sisi hatuna uwezo...Tumeuza viwanda vyote, sasa tunauza hata Uhuru wetu kwa kuuza ardhi, ajira na hata imani zetu.. HOPE imeondoka..

Leo hii haya ujenzi wa nyumba siku hizo wageni ndio wajenzi, kilimo wageni, yaani imefikia hadi ukimpelekea ndugu yako Trailer truck ataliuza maana hataki taabu ya kazi, Umachinga ndio biashara na sii uwekezaji..Tunapenda kubangaiza mjini kimachinga na udalali kuwa ndio utawala bora. Kwa mtaji huu wa elimu ya umachinga - Tumekwisha!..
 
Mkandara,
Tanzania hii ya akina CHADEMA, NGOs za nguvu namna hii, Maaskofu na Masheikh wakakamavu namna hii, blogs za nguvu kama hii JF na Mkandara, Mwanakijii, Pasco, FP, Mag3, NyaniNgabu, Invisible, ..., bado tu tutabambikiwa KATIBA? Kwa nini tumejikatia tamaa namna hii?
 
Hapana hatujakata tamaa lakini mkuu wangu kazi yangu sii ku explore reality?..katiba mpya hatuiandiki sisi na wala hatuna mamlaka ya kuiandika ni sawa na kutafuta kumzuia Lowassa asigombanie urais kwa hofu ya Ufisadi wake hutaweza kumzuia... na anaweza kweli kupitishwa kote ingawa hapendeki wamepita wangapi Iraq, Afghanstan, na hata huyo Bashir wa Sudan leo kipenzi cha Western baada ya kuwapa deal zote. Darfur watu wanakufa ovyo husikii tena yakizungumzwa, tena amesaidiwa na hawa hawa wana demokrasia hadi kumuua mpinzani wake. Bashir taratibu wanamweka sawa kumlisha sumu yake mwenyewe kama Ghadaffi..

Katiba iliyopo kama ulivyosema hapo awali imeondoa miiko na maadili ya uongozi pia katiba hiyo imeondoa nguvu zote za wananchi na mawaziri na kumwacha rais na nguvu zote za kuendesha na usimamizi kama ilivyokuwa wakati wa Ujamaa na Kujitegemea. Kwa hiyo wakati ule rais alipewa nguvu zile kusimamia Ujamaa lakini sasa tupo ktk soko huria serikali haiendeshi tena uchumi wa nchi bali kusimamia lakini rais ana nguvu zile zile za kuendesha na kusimamia kisichopo - Atatumaliza.
 
Bwana Masabuda Umesema hivi:

"hainingii akilini kwa mtu msafi kama ww ukawa na changuo la mtu MCHAFU"

Sasa ndo ujiulize, kwanini mie mtu msafi unayejua wazi kuwa rushwa kwangu mwiko, kwanini nimsapoti unayemuona ni mchafu.
Jibu ni simplo: Lowassa sio mchafu kama ulivyofanywa uamini. Na ndani ya CCM hakuna aliye msafi kuliko Lowassa miongoni mwa wagombea urais mpaka sasa wanne:

Lowassa, Bernard, Sumaye na Six.

Ukipima utendaji, uchafu na mengineo. Lowassa anaibuka kidedea wa kugombea urais 2015.

Mbona umekwepa aliyoongea Lowassa kwenye NEC ya CCM majuzi? Kama Lowassa ni mchafu kwanini hawamfukuzi CCM?

Karibu kwenye hoja yangu acha mara moja kumsapot EL kama kweli nikuelewe ww ni msafi
kuhusu kuaminishwa kuwa EL sio kweli labda uniambie alimpa kazi Mwakyembe ambambikizia kwa sababu si mtu wa kuhongwa au kuchukua rushwa kama vile ww usivyopenda kupokea rushwa namjua vizrui take it from me

So kwa kumwamini hivyo Dr ndio maana nasema ule ulikuwa ukweli mtupu!

Lowassa hafai hata kupewa ukuu wa mkoa jamani
 
Ee bwana EL hawavumi kumbe bado wamo, hii thread imefika hadi huku?

attachment.php
 
Attachments

  • Bounce back by Jacob Zuma.jpg
    Bounce back by Jacob Zuma.jpg
    21 KB · Views: 92
@ Fairplayer tusadie nasi Lowasa iwe chaguo letu

  • Unadhani moja ya ajenda za lowasa akiwa magogoni itakuwa kushughulikia UFISADI?
  • Lowasa atafanya nini cha tofauti au sawa na kilichofanyika kwenye uongozi wa mkapa na Jakaya ?
  • Nini Lowasa atatanguliza wakati wa kufanya maamuzi kati ya maslahi ya chama na taifa kama yatakuwa yanakinzana
 
Hukumalizia vizuri swali la mwisho... kuna maslahi YAKE (mafisadi) ya CHAMA na ya TAIFA...
 
Hukumalizia vizuri swali la mwisho... kuna maslahi YAKE (mafisadi) ya CHAMA na ya TAIFA...
hahahha Mkandara nilitaka kuweka hilo ngoja fairplay atusaidie maana kwa upofu wangu/ wetu na masikio yangu yasiyosikia vizuri sijawai kusikia Lowasa akiongelea na kukubali kuwa UFISADI ni tatizo

Huyu mchapakazi mkali mara nyingi akigusiwa kuhusu UFISADI analikwepa hilo swali. Siku hizi anasema tatzo ni ajira kwa vijana. Akienda mbali zaidi atakumbia ni SIASA ZA chuki.

Haya fairplay tusaidie majibu na sisi tufikie maamuzi magumu kama uliyofanya wewe. lakini usichoke tukiendelea kuhoji sababu nina maswali mengi ya kuhoji Lowasa kuwa rais kuliko maswali niliyonayo Nape Nauye au Pinda, kuwa rais.
 
@ Fairplayer tusadie nasi Lowasa iwe chaguo letu
  • Unadhani moja ya ajenda za lowasa akiwa magogoni itakuwa kushughulikia UFISADI?
  • Lowasa atafanya nini cha tofauti au sawa na kilichofanyika kwenye uongozi wa mkapa na Jakaya ?
  • Nini Lowasa atatanguliza wakati wa kufanya maamuzi kati ya maslahi ya chama na taifa kama yatakuwa yanakinzana

sawa sawa FP please

ongezea na hili

lini atakwenda bungeni na kukanusha tuhuma zote za ufisadi na aseme bungeni kuwa yeye sio fisadi na sio makanisani
 
Lowasa hata kama ni mwizi hawezi kuwa Jela sababu tayari alishakuwa PM. wa Tanzania na nchi nyingi za kiafrika hatijafiia level hiyo ya viongozi kama RAIS na PM kushatakiwa wachilia mbali kufungwa. Unachohji wewe ni NADHARIA. jibu nalokoupa ni hali halisi ya utendaji ilivyo kwenye hizi seriali zetu. Tanzania is not france, Norway ndi tunataka tufike huko. Mahakama Pekee wa sasa ya Mtu kama Lowasa ni ya kisiasa

Ni sababu hatujafikia level hiyo ndiyo maana unaona hata viongozi maadili yao mabyo yana shaka bado kuna watu waawapigia debe. Kama wewe na wengine unampigia debe lowasa basi elewen hamtatufiish kule miaka 20 ijayo tutasikia wairi mkuu au rais anasharakiwa.

Nimeuliza
  • Huyu Lowasa anayepigiwa debe hivi analinganishwa na nani mpaka aonekane ana nafuu kuliko wengine? Sijaona jibu
  • Je ben Mkapa alichohomolewa wapi mwaka ule. Huko alikochomloewa hakuna wengine?
Cheo cha rais hakitaki mchapakazi, anayeubakubalika na watu kadhaa . Cheo cha uongozi wa Urais kinataka mtu MUADILIFU. So far UADILIFU wa lowasa tayari una maswali megi bora tuletewe kina Mkapa wapya

Hivi CCM imeshiwa hivi

Tunaachana kwenye Uadilifu wa Mkapa, Kwengineko tuko pamoja.
 
sawa sawa FP please

ongezea na hili

lini atakwenda bungeni na kukanusha tuhuma zote za ufisadi na aseme bungeni kuwa yeye sio fisadi na sio makanisani

Kwa Mujibu wa Katiba Hawa Jamaa Wanatakiwa Wajaze Fobu ya Kuainisha Mali Zao, mara wanapokuwa Wabunge Hivi Wanajaza nini Hasa? ni vipi fomu hizo zinaweza kuwekwa hadharani tukaona huo Uongo na Utapeli wanaotufanyia.
 
Back
Top Bottom