Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
Hata mimi naamini hatuna haja ya kutaja majina kwa sasa kwani wenyewe kama jamii hatujawa safi kiasi cha kuuchambua usafi wa wenzetu. Kuna wakati nilisema humu ndani kama tungekuwa tunatumia majina yetu halisi wengi wetu tusingekuwa jasiri kama hivi tulivyo.mara nyingi wabongo hatuko logic, ili rais asimame nani anamsimamisha? bila shaka chama chake...km JK hafai maana yke ccm haifaii. hao unaofikiria ni safi ndani chama kwa nini hawakusimama kupinga JK kupita? kama taifa tuna mambo muhimu ya kujadili mf. uzalendo ni nini? uzalendo unajitokezaje kwa mtu moja moja? kwa chama? kwa taasisi?...je tunahitaji kiongozi mzalendo au watu wazalendo?... hatupaswi kufikiri juu ya majina.
Kuna maaskari wanamiliki magari lakini ni kutokana na ulaji rushwa. Badala ya kulalamika basi ni lazima tubadili mfumo mzima wa maisha yetu kutoka kwenye familia zetu hadi kwenye ngazi ya taifa. Kama askari ananunua gari basi iwe ni kwa njia zilizo halali na si kwa njia za kirushwa rushwa kama ilivyo sasa. Nakumbuka Mtikila alivyomwita Rostam Aziz fisadi naye RA akatoa nakala ya hundi aliyomlipa Mtikila fedha ili akajengee kanisa lake na kanisa halikujengwa na hela iliyotolewa na "Fisadi" haijulikani "msafi" Mtikila aliifanyia nini.
Ukienda kwenye NGOs wanakwambia siku hizi huwezi kupata fedha za kuendeshea shughuli bila ya kutoa dhamananyuma (Kickback) Hali hiyo iko kwenye kila nyanja kuanzia Ukandarasi, udahili wanafunzi vyuoni, upatikanaji wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu hadi mikopo ya kwenye mabenki. Siku Moja niliombwa rushwa na kiongozi wa Magerezae ili ndugu yangu apekelekwe kwenye chuo cha Magereza Kiwira hadi nikamuuliza askari anayeajiriwa kwa rushwa atakuwaje? Kwa ufupi UFISADI ni mfumo wa maisha yetu na ili tupambane nao ni LA ZIMA tuzikane nafsi zetu.