BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Profesa Joyce Ndalichako amewagiza waajiri kuweka mifumo kwa wafanyakazi wao ya kuwewezesha kufanya mazoezi ikiwemo ‘gym’ ili kuwa na wafanyakazi wenye afya njema.
Waziri huyo amesema moja ya sababu ya kutaka gym ziwepo maeneo hayo ya kazi ni kutokana na waajiri kuhitaji watu wenye afya njema ili kuwa na uzalishaji wenye tija hivyo suala la kuweka mfumo wa kufanya mazoezi litakuwa jambo jema.
Jingine amesema ni kupunguza magonjwa yasiyoambukiza yanayochangiwa kwa kiasi kikubwa na mfumo wa maisha ikiwemo kutofanya mazoezi.
“Magonjwa hayo yasiyo ya kuambukiza kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), yamekuwa yakichangia asilimia 33 ya vifo vyote duniani.
“Lakini ukiacha vifo, pia yamekuwa na gharama katika kuwatibu wagonjwa wake na hivyo kuiongezea serikali mzigo, fedha ambazo zingeweza kufanyia shughuli nyingine za kuwaletea wananchi maendeleo, hivyo tufanye mazoezi kuyapunguza,” amesema.