Mkurugenzi JKCI: Zingatieni mtindo bora wa maisha kuepuka magonjwa ya moyo 'tusipoteze nguvu kazi ya Taifa'

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dr. Peter Richard Kisenge ametoa rai kwa wananchi kuzingatia mtindo bora wa maisha kwa kuzingatia ulaji bora na kuepuka matumizi ya vitu ambavyo uchangia magonjwa ya moyo.

Akizungumza Machi 15, 2024 katika mkutano na wadau wa sekta ya afya uliojadili mitaala ya kozi za utaalamu wa masuala ya moyo ambazo zinatarajiwa kutolewa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa kushirikiana na JKCI, Mkurugenzi huyo amesema kuwa matatizo ya moyo yamekuwa yakiongezeka na kupelekea baadhi watu kupoteza maisha ikiwemo vijana, suala ambalo amedai kuwa jitihada mbalimbali zipofanyika Taifa lanaweza kupoteza nguvu kazi.

"Magonjwa ya moyo yanazidi kuongezeka kwa kasi karibia watu milioni 47 wana matatizo ya magonjwa ya moyo na kati ya hao karibia milioni 22 wanapoteza maisha yao kwa sababu ya hayo magonjwa ya moyo"amesema Kisenge

Amesema sababu ambayo imekuwa ikichangia kiwango cha watu wengi kupoteza maisha ni pamoja na matatizo hayo kutogundulika mapema, ambapo ameeleza kuwa inapotokea magonjwa hayo yakagundulika mapema inasaidia kupata matibabu kabla matatizo hayajawa makubwa.

Kufuatia ongezeko hilo amesema "Niwaombe wananchi wafuate hali bora ya maisha kwa kuzingatia vyakula bora, kufanya mazoezi, kuacha kuvuta sigara na unywaji wa pombe uliokithiri. Hii itakuwa njia moja wapo ya kupunguza matatizo hayo"

Aidha ameongeza kuwa wataalamu wanaotarajia kuwapata kupitia kozi hizo wataongeza wigo wa wataalamu wa moyo nchini na kusaidia katika utoaji wa huduma kwa kuwafikia watu wengi wenye matatizo hayo.

Akizungumzia faida hiyo Prof. Projestine Muganyizi kwa niaba ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambaye ni Daktari Bingwa wa mogonjwa ya Wanawake, kutoka ndaki ya UDSM Mbeya inayohusika na Afya pamoja na Sayansi Shirikishi, amesema kuwa wataalamu

Amesema mafunzo hayo yataenda kusaidia kuongeza wataalamu watakaoenda kusaidia watu wengi endapo michakato ikikamilika kama wanavyokusudia.

Amesema Chuo hicho ndaki ya Mbeya tayari kimepata eneo la ekari 1000, ambapo amesema kuwa wanatarajia kulitumia kimkakati kwa ajili ya kuweka miundombinu itakayowesha kupata wataalamu hao wa afya.

Wataalamu hao ambao ni sehemu ya walengwa wamekutanishwa katika hatua ya awali kujadili mitaala inayolengwa kutumika, ambapo wamepata fursa ya kuelezwa mashirikiano hayo pamoja na tija inayoweza kutokana na kozi hizo.

Moja ya programu (kozi) inayotarajiwa kuanzishwa ni upasuaji wa moyo ambayo imedaiwa itakuwa yakwanza Afrika Mashariki na Kati, lakini vilevile programu nyingine ni upasuaji kupitia tundu dogo la moyo.

David Mzava ambaye ni msajili kutoka Baraza la Madaktari amesema kuwa kozi hizo ni muhimu katika kuongeza wataalamu wa magonjwa ya moyo wataowahudumia wananchi wengi zaidi wanaobainika na matatizo hayo.

Pia amesema kuwa wataalamu hao wakiongezeka itakuza suala la 'tiba utalii' kwa kuwa watu wengi watashawishika kupata huduma nchini kutokana kuwepo kwa wataalamu wa kutosha wenye uweledi.
images%20-%202024-03-16T184739.735.jpg


Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom