Hivi niulize usomi ni sifa au Cheo? Huko kwenye wizara wapo mawaziri ambao pia ni ma-professor na wengine ni PhD.sitawataja kwakuwa mnawafahamu. Kwa kudokeza tu wapo prof. Maghembe, Msolwa n.k. wamefanya nini? kama hawajafanya kitu basi tukubaliane kuwa uongozi ni karama zaid ya elimu.Tatizo ni moja tu mkuu watu waliosoma kukubali kutumika kisiasa tena chini wa wasiosoma!!!!
Ok wote hatuwezi kuwa viongozi lakini hata wanapokosea kuwaambia pia hao waliosoma hawataki!!!! Yaani wamekuwa watumwa wa wanasiasa!!!!!
Mengine ni kukosa uzalendo na kuendekeza sifa na njaa,unakuta msomi mzuri tu eti anashika mkoba wa mtu ambaye hana tija kwa Taifa ili tu awe karibu na kiongozi na hatumii usomi wake kumshauri huyo muhusika!!!!
Ukiniuliza tuanzie wapi mimi ntasema mawaziri wasiwe wabunge kwanza ili nafasi nyeti za nchi zishikwe kwa minajili ya utaalamu na uzoefu wa lile mtu alilosomea na kufanyia kazi!!!! Hii itaamsha ari na hadhi ya elimu na utaalamu na pia itajenga mipaka ya kazi na heshima kati ya wanasiasa na professionals!!!!