Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
Kuna sheria iko jikoni yenye kulenga kuboresha mafao ya viongozi wa kitaifa na kuhakikisha wenza wa viongozi hao kulipwa 25% kama mafao ya kustaafu. Pia familia zao kuvuna 60% ya mshahara mara baada ya viongozi wa kitaifa kufariki dunia.
La ajabu, huu muswada pamoja na kuchochewa na mapendekezo ya mbunge na mke wa Rais mstaafu mama Salma Kikwete aliyoyatoa bungeni tarehe ya April 22, 2022 katika Bajeti ya Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (2022/23) lakini pia yamo kwenye Rasimu ya marekebisho ya katiba iliyopendekezwa na bunge maalumu la katiba.
Yapo matatizo mengi kama hili bunge litapitisha muswada huo. Tatizo kuu mafao ya viongozi wa kitaifa wastaafu ni ya kikatiba na bunge halina mamlaka ya kuyaboresha bila ya kurekebisha katiba!
Tatizo kubwa ni kupanua nyufa ambazo zinatokana na viongozi wa kitaifa kuyatumia madaraka yao vibaya ya kujipendelea wao wenyewe kila kukicha.
Sheria tajwa inalenga kuimarisha matabaka ya wanaotawala na watawaliwa kwa sababu inapokuja watumishi wa umma wasiyo wa kitaifa utaona bunge hilo hilo hukaza buti kudhoofisha haki za wafanyakazi wa ngazi za chini na kuwaongezea ufukara mara wanapostaafu.
Aidha bunge limeweka ukomo wa umri wa kulipwa haki za kustaafu kwa watumishi wa kawaida na kuwa miaka 60 wakati kabla ya hapo ulikuwa miaka 50-55. Bunge halijali mtumishi akistaafu hana kipato na kumnyima mafao ya kustaafu hadi afikishe miaka 60 ni kumwongezea umasikini.
Pili, bunge hilo hilo limejenga matabaka wako watumishi wa umma wa kitaifa na wasiyo wa kitaifa huku wa kitaifa wanacho kikotoo tofauti na wale wasiyo wa kitaifa. Kikotoo cha viongozi wa kitaifa ni asilimia ya mshahara wa sasa wa cheo kilekile alichoondokea wakati wale wasiyo wa kitaifa msingi wake kwanza haijulikani na pia hujikita kwenye majumlisho ya mtumishi husika aliyolipwa wakati wa utumishi wake na wala siyo asilimia ya cheo alichoondoka nacho.
Tatizo ni kuwa Kikotoo cha viongozi wa kitaifa kigezo chake kikuu ni kumlinda mstaafu dhidi ya mfumuko wa bei na mapato. Wakati cha watumishi wasiyo viongozi wa kitaifa kikotoo chao kinalenga kudidimiza mafao ya kustaafu kwa kuhakikisha hakuna uhusiano wowote ule na mfumuko wa bei na mapato!
Hili ni tatizo kubwa la kwanini hakuna kikotoo kimoja kwa watumishi wote wa umma? Lengo la kujitawala lilikuwa kuamini dhana ya kuwa kwa kuwa viongozi wanatoka miongoni mwetu basi watafanya maamuzi yanaboresha masilahi ya wote lakini hali halisi ni kinyume chake.
La kusikitisha sasa hata wenza na familia za wastaafu sasa kulipwa mafao endapo viongozi wa kitaifa watakuwa wamefariki dunia. Tuna maswali mengi ya kujiuliza. Mwajiriwa wa umma ni nani haswa? Tunapomwajiri kiongozi wa kitaifa huwa tunaajiri na familia yake pia? Ni wapi kwenye katiba inasema hivyo?
Katiba yetu haitambui wenza na familia za viongozi wa kitaifa kama ni waajiriwa wa umma na kutunga sheria ya mafao ya wenza wa marehemu waliokuwa viongozi wa kitaifa ambao haki zao ni za kikatiba ni ukiukwaji wa katiba. Inabidi kwanza katiba iwatambue wenza wa viongozi wa kitaifa na familia zao ni watumishi wa umma ndipo hapo haki za kustaafu zitawahusu. Bunge haliwezi kuajiri familia ya wastaafu wa viongozi wa kitaifa na kuwalipa mafao ya kustaafu wakati katiba haiwatambui. Na maelezo yanahitajika kwanini watumishi wengine wasio wa kitaifa familia zao nazo siyo sehemu ya ajira wa umma? Zoezi zima lina mwelekeo wa kuondoa misingi ya usawa.
Kama bunge linataka kuongeza nyufa za matabaka miongoni mwa watumishi wa umma basi warekebishe katiba kama rasimu ya marekebisho ya katiba iliyopitishwa na bunge haramu la katiba.
Bunge likifanya hivyo litakuwa halijakiuka katiba bali litakuwa limewabagua watumishi wengine wa umma ambao siyo viongozi wa kitaifa ambao wenza wao na familia zao hawatalipwa baada ya wao kuaga dunia.
USHAURI
Hili bunge ni kinara sana wa kupitisha maazimio na sheria zinazokinzana na katiba ni vyema sasa mkaanza kurudi kwenye mstari na kuikataa hii sheria ya mafao ya wenza na familia za viongozi wa kitaifa waliofariki dunia.
Sababu kuu ya kuikataa hii sheria ni kuwa bunge halina mamlaka ya kubuni ofisi zaidi ya zile zilizoainishwa kwenye katiba. Ili mwenza wa Rais alipwe hiyo 25% ya mshahara wa mstaafu inabidi awe alikuwa akilipwa yeye mwenyewe huo mshahara kama mtumishi wa umma. Kama hakuwa halipwi sasa hoja ya malipo tajwa inatoka wapi?