Nauli za daladala kupanda Dar

EEee mungu wa israel na isaka tunusuru nchi hii tupe akili na mawazo ya kuwachinja wale wote wanaopelekea haya kwa kuanza na mmiliki wa DOWANS pamoja na wengine wote ambao kwao Nauli kupanda na umeme sio tatizo kwani wanatumia bure na zinalipwa na serikali kwa kutumia Kodi zetu walalahoi.

Hutawasikia wakichangia kitu kwani kwao sio la muhimu maana maumivu hakuna eee baba yetu tusikie na utupe nguvu.

AMEN.

Amen tutendewe kama ulivyonena.
 
Dowans ,,Dowans ufisadi na ulafi sasa ndio ule muda KUSAGA MENO umewadia.

Kila mtu atachangia DOWANS whether direct or indirect.

hawa wa mikoani watasaga meno saaana maana wengi wao ndio wale waliokuwa WAKIRUKARUKA KAMA NDAMA KUSHANGILIA CCM na vifulana vya KIJANI NA MANJANO.
Sasa hivi hawana hata sabuni ya kufulia hivyo vifulana na kofia zimejaa jasho.

Mie naona sawa ili waanze kusoma majira na nyakati maana tukisema kwa maneno hawaelewi kabisa.

Sasa inabidi kuwafundisha kwa mifano maana MIOYO YAO NI MIGUMU KUELEWA na WEPESI WA KUSAHAU.

Kuongeza nauli pia ni mkakati wa serikali kupunguza idadi ya wahamiaji katika miji mikubwa.
 
majadala unaendelea na maelezo kwa sasa yanafafanuliwa tuongee asubuhi star tv........inaonekana ata wanajeshi na polisi kuanza kulipa nauli kama wananchi wa kawaida
 
I really don't understand it; asilimia 61 ya Watanzania wamewachagua na kuwarudisha madarakani watu wale wale. Halafu walitarajia nini? Huwezi kufanya uamuzi au uchaguzi bila kuwa tayari kulipa gharama yake.

Ivi hiyo figure ya 61% umeiamini? Matokeo halisi ya uchaguzi 2010 hatuna, hivyo huwezi kusema watu wameichagua ccm! Watu wamenyimwa haki yao ya kuchagua na sasa wanaibiwa kwa nguvu!
 
Hao wanajeshi si wanapanda bure? Wanaitwa MAWE, unadhani wana akili ya kufanya rev wakati washapewa kombat mpya?
Wanajeshi hawawezi kumpindua jk maana kabla ya uchaguzi wamehongwa sana. Kambi zote zimekarabatiwa na nadhani mambo yao yako vizuri hasa wale matop. Atakayeleta mabadiliko tz ni mlalahoi atkapojitambua kuwa anadhurumiwa na bora kufa kuliko huu utumwa wa kuwatumikia RA,EL na JK
 
Pamoja na haya yote bado kuna mijitu inafagilia serikali inayotupeleka kuzimu huku tukiangalia.Laiti watu wangekomaa wakati wa uchaguzi...haya yote yasingetokea sasa hivi!Tunafuga mafisadi kwahiyo hatuwezi kutegemea kitu kingine zaidi ya ufisadi!
 
Ila nadhani wananchi sio wa kuwalaumu sana coz waliwakataa bt wao wakafanya hila.. cjui ndio wanawakomoa..
 
Huu ndo upuuzi mwingine wa nchi yetu, tutapata maisha bora kwa kila mtanzania kweli?

acheni muumie tu si mliichagua wenyewe ccm.!!!watanzania wanafki sana acha wabamizwe.,,wanaonywa tokea mwanzo lakini kwa ushabiki na kupenda tshirts,pilau na khanga,..umieni tu mpaka mpate akili mi nafurahi
 
Nimesikiliza mapendekezo ya nauli mpya za mabasi zikanistua sana, nikaogopa sana na kujiuliza nchi hii tunaelekea wapi..?

Kumbuka kupanda kwa nauli hizi kutasababisha kupanda kwa bei za bidhaa karibu zote hapa nchini na sana sana mikoani kwa ndugu zetu ambao maskini wa Mungu kipato chao....


Ndugu Wana JF, kama watanzania tufanyeje kuepusha balaa hili?

"Hii post imekaa kidini zaidi, kwanini unauliza hili swala huku ukijua haya ni matokeo ya uongozi wa Kikwete na kikwete ni Muislam", kwahiyo unapinga uislam? Hii ndo hali iliyopo Tanzania kila changamoto inayo kosoa utawala wa Kikwete unaitwa ni udini.
 
Sumatra kutangaza nauli mpya za daladala
Tuesday, 18 January 2011 21:26

Zaina Malongo
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi Kavu na Majini (Sumatra), itatangaza nauli mpya za daladala na mabasi ya mikoani kabla ya Januari mwishoni.

Hatua hiyo, inafuatia baada ya kukamilika shughuli ya kukusanya maoni ya wadau wa usafirishaji uliofanyika hivi karibuni.

Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake jana Ofisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo, David Mzirai alisema tayari wamepokea mapendekezo hayo ya wadau na kuanza kuyafanyia kazi.

“Suala la kupandisha nauli upo katika taratibu na kanuni za usafirishaji. Tumepokea mapendekezona tayari tumeanza kuyapitia na kuyajadili, nauli mpya tutatangaza kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Januari,”alisema Mzirai.

Alifafanua kwamba baada ya kuyapitia maombi na kutoa mapendekezo yao, Sumatra itakaa tena na wadau wa usafirishaji ili kuweka mambo sawa.

“ Baada ya hapo tutaamua iwapo nauli za daladala na mabasi ya mikoani zitapanda au la,” alisema. Hivi karibuni Sumatra na wadau wa vyombo vya usafiri walikutana katika ukumbi wa Karimjee jijini na kujadili mapendekezo ya kupanda nauli.

Kwa mujibu wa wadau hao ambao ni wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani na yale ya daladala walipendekeza kupandishwa kwa nauli wakidai kupanda kwa gharama uendeshaji.

Wadau hao walipendekeza ongezeko la Sh51.2 kwa kila kilometa moja kwa nauli za daladala na mabasi ya mikoani walipendekeza ongezeko la Sh26 kwa kila kilometa
 
Tulijitutumua na soko huria sasa ni dhahiri limetushinda ..............................and we are back to where we fully belong...................price controls...........................................
 
kama wafanyakazi wa sumatra wenyewe ndiyo wanaomiliki daladala mijini huoni kuongeza nauli haliepukiki!.
 
"Ili kuhakikisha kuwa kuna uwiano kati ya viwango vipya vya nauli na ubora wa huduma ya usafiri, Mamlaka imetoa maagizo kwa wamiliki kuboresha maeneo yanayohusiana na huduma ya usafiri kama ifuatavyo:
(i) Kufuata Sheria, Kanuni na Masharti ya Leseni ya usafirishaji abiria
(ii) Kuandika katika mlango wa kuingia abiria viwango vya nauli inavyotoza katika njia anayotoa huduma ya usafiri
(iii) Kutoa tiketi kwa kila abiria ikionyesha jina la mmiliki, namba ya usajili wa basi, kituo cha mwanzo na mwisho wa safari, nauli na tarehe ya safari
(iv) Kuzingatia usafi wa mabasi na sare za wafanyakazi wao, kutotumia wapiga debe, kutotumia lugha chafu, kutokatisha njia na kutowabugudhi wanafunzi
(v) Kubeba idadi ya abiria kulingana na uwezo wa basi na kuwepo na nafasi ya kutosha na sehemu ya kushika kwa abiria wanaosimama ndani ya mabasi makubwa
(vi) Kuhakiksha basi linabeba idadi ya abiria ambao wanapaswa kubebwa kwa mujibu wa idadi iliyoidhinishwa na mtengenezaji wa basi
(vii) Kuwepo na Bima inayowalinda abiria wote wa basi husika
(viii) Abiria wanawajibika kurejesha utamaduni wa kupanga mabasi kwa mstari na mabasi nayo yanapaswa kupakia abiria kwa mstari." (kama ilivyoletwa na PAW).

Cha ajbu ni kwamba mbona,hakuna kipengele kinachowabana wenye daladala kukarabati magari yao-service na hali ya viti-kuna baadhi ya DALA2 zimebaki na vyuma tu na mara nyingi abiria wanajikuta nguo zao zinmetobolewa au kuchanika, ama muda mwingine hata kuumizwa na vyuma hivo, hili halijazungumziwa na DAR-"KOBOA"! wanajali tu maslahi yao bila kujali usalama wa wateja wao! jamani watu wa "KIJANI" mtuonee huruma cc walalahoi! au kwakuwa nyie hampandi Dala2, na mnapewa mafuta ya Bure na allowance kedekede! inasikitisha kuwa hata yule anayejinadi kuwa mtoto wa mkulima amejisahau au anatulaghai: sishangai maake ni MWONGO hodari sana!

 
Back
Top Bottom