Nauli za daladala kupanda Dar

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WAMILIKI wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam (DARCOBOA) wamesema kuna uwezekano wa kupandisha nauli za daladala kutokana na kupanda kwa bei ya vipuri vya mabasi ya usafirishaji wa abiria.

Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Mwenyekiti wa Darcoboa, Sabri Mabruk, alisema mgomo ambao walipanga kufanya wiki ikashindikana kutokana na serikali kukubali malalamiko yao katika mkutano wa wadau wa usafirishaji unaotarajia kufanyika Desemba na kwamba ongezeko la nauli itakuwa ni sehemu ya ajenda yao.

"Bei ya
 
hii ndio sera ya chama chetu kitukufu katika kufikia malengo ya melinium
 
Kuna habari zisizothibitishwa kwamba mkutano kati ya TABOA na SUMATRA umefikia makubaliano hayo.
 
wacha tu wapandishe, wananchi wanaochagua ccm isiyowatetea kabisa ndio watakao ona chamoto...hili liwe fundisho kwao mwaka 2015. wawe na busara wanapochagua rais.
 
tena wapandishe sana ili tuanze kutembea kwa miguu kama babu zetu wakati ule...mtu unatembea toka kigoma mpaka dar. safi kabisa...hongera ccm kwa kutimiza ilani, hata mkulo anasema uchumi umepaa hivyo wananchi wana uwezo wa kulipia hayo maongezeko ya maj, umeme, usafiri, afya n.k. hii nio maana ya maisha bora, kutumia kwa sana!!! huwezi ukawa unatumia chini ya dola moja ukasema una maisha bora.
 
tena wapandishe sana ili tuanze kutembea kwa miguu kama babu zetu wakati ule...mtu unatembea toka kigoma mpaka dar. safi kabisa...hongera ccm kwa kutimiza ilani, hata mkulo anasema uchumi umepaa hivyo wananchi wana uwezo wa kulipia hayo maongezeko ya maj, umeme, usafiri, afya n.k. hii nio maana ya maisha bora, kutumia kwa sana!!! huwezi ukawa unatumia chini ya dola moja ukasema una maisha bora.

wapandishe kwa asilimia 100.
 
Haitakuwa ajabu maana umeme umepanda kwa sababu zilezile! Tazameni bei ya vipuri ilivyo, tazama bei ya mafuta, tazama kudorora kwa shilingi yetu; inadorora kuliko sarafu zote za Afrika Mashariki.
 
ccm mhhh watapandisha mpaka malipo ya MAHARI miaka hii mitano ya utawala wao
 
wewe ndio umeleta habari halafu unadai sisi ndio tukujuze? we vipi, mwongo mkubwa!

mkutano uko scheduled for the 7th, Jan

mkuu jazba zako wapelekee CCM sio mimi,nilidokezwa na mdau mmoja nasubiri uthibitisho.kama una ukweli uweke hapa jamvini!
 
acha wapandishe, watu kila siku kwa mafungu leo tunaenda kumsalimia shangazi, kesho kwa binamu, kesho kutwa mjomba,tena wapandishe kwa 500%, tufanye na mazoezi kupunguza vitambi hasa kwa wanawake!
 
Aliskia tetesi, akazileta. Kiukweli si mwongo bali mdaku.
Mna mwone habari inaweza kuanza na tetesi halafu kukatokea na mtu anae lifahamu jambao hilo vema aka-confirm sasa mkianza kumsakama hivyo ina maana neno tetesi hapa JF halina maana.....au siku hizi tetesi hazitakiwi hapa JF....
 
Mafuta yamepanda sana!
Alafu Hute una uhakika wananchi waliichagua CCM?
 
Back
Top Bottom