Madereva bajaji wapanga kupandisha nauli katika mikoa mbalimbali nchini. Viongozi wa vijiwe vya bajaji wahusika

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,105
Kama mtakuwa mnafuatilia ndugu zetu wamiliki wa bajaji na madereva wameanza kujipanga kupandisha nauli mara dufu katika maeneo mbalimbali wanayofanya vizuri ikiwemo Mwanza.

Aidha, inadaiwa tozo ya trafiki kwa siku imepanda kutoka elfu moja hadi elfu mbili kwa bajaji moja hivyo kuchochea gharama kuendelea kuwa kubwa. Endapo mpango huu utafanikiwa basi nauli ya shilingi mia tano inatarajiwa kupanda hadi elfu moja au zaidi. Aidha, kupanda kwa nauli hizi kunaendana sambamba na kupanda kwa gharama za usajili katika vituo vya kupakia bajaji na tozo za siku.

Kutokana na mfumuko huu wa nauli upo uwezekano nauli za pikipiki zikapanda pia huku daladala nazo zikipandiaha gharama peak hours. Haya yote yakifanikiwa mzigo wa gharama kwa mwananchi utakuwa mkubwa kwani mishahara bado ni ileile na biashara haziendi.

Nimeleta mada hii kwenu kuwatumbua macho kuhusu mambo madogo madogo yenye athari kwa wengi yanayowanufaisha wachache. Nimewashauri kuanzia kesho futalieni nauli za bajaji mwanza, Arusha na DAr mtabaini kuna mabadiliko makubwa sana. Hoja hapa je nani anayeratibu usafiri wa bajaji? Nani anapanga bei? Kwa jiji kama DAr es salaam ambapo baadhi ya maeneo hakuna daladala kuna bajaji wananchi watamudu gharama za usafiri?
 
Kwanza wanapewa favour tuu kuingia road wanatuchafulia Miji.
 
sasa bajaji anakutia stress kivipi wakati kula yake ipo mfukoni mwako......wewe ndo unaamua leo ale samaki au mrenda..

Nunua baiskeli ruti nyingi za bajaji unaweza kwenda kwa baiskeli....sema bongo watu wengi mabishoo,kuendesha baiskeli wanaona kama umaskini.

Ila mkuu mwanza si kuna zile ganagana......ahahhahaa
 
Gari ni hitaji la msingi, japo kibongo bongo, tra huko ukiagiza ka ist ni kukomoana.

Hivi vitu lazima vipande, daladala na mabus makubwa nauli wamepandishiwa, kwanini wao wasipandishe wakati wote wanatumia nishati hizo hizo.
 
Aidha, inadaiwa tozo ya trafiki kwa siku imepanda kutoka elfu moja hadi elfu mbili kwa bajaji moja hivyo kuchochea gharama kuendelea

Fafanua kidogo kuhusu hii tozo ya traffic ni nini? Inapangwa na nani? Kwa sheria, utaratibu upi?
 
Acha waongeze,kama hamtaki kulipa nauli hiyo pigeni mguu

Ova
 
Back
Top Bottom