Nauli za daladala kupanda Dar

Haya tumeyataka wenyewe, tuendelee tu kuipenda serikali yetu hata kama inatuumiza, tulikuwa na nafasi ya kuyabadili haya tukafanya utani sasa wala tusilie. Bado miaka minne na miezi kumi ya maumivu!
 
mimi naombea maisha yawe magumu zaidi hasa kwa mikoa ya LINDI, MTWARA, PWANI, RUVUMA nk. ili watu wakule waamke kutoka usingizini, na wafahamu kuwa pesa zinazolipwa dowans ni zao.

Mkulu, maisha yalishakuwa magumu siku nyingi sana, labda useme Maisha yakiwa magumu zaidi. Na yakiwa magumu zaidi yatakuwa ni ya watz wote, labda uitenge hiyo mikoa uliyoitaja isiwe tz.
 
Mkiandamana tena kupinga nauli hizi tutaua twice as much, tulia tuliii, nchi itawalike bila mizengwe.

Mnataka kuanzisha chokochoko kwenye Kisiwa cha Amani?

umechanganyikiwa nini? Wewe hiyo amani unaiona wapi? Watu wanauawa, wanaweka migomo gharama za maisha zinapanda unategemea watakuwa na amani? Kama umesoma basi elimu yako haijakukomboa!
 
Nimesikiliza mapendekezo ya nauli mpya za mabasi zikanistua sana, nikaogopa sana na kujiuliza nchi hii tunaelekea wapi..?

Kumbuka kupanda kwa nauli hizi kutasababisha kupanda kwa bei za bidhaa karibu zote hapa nchini na sana sana mikoani kwa ndugu zetu ambao maskini wa Mungu kipato chao....

Ndugu Wana JF, kama watanzania tufanyeje kuepusha balaa hili?

We Great Visionaries here JF we warned the Government, the -ve consequences of electricity bill increments, people opposed physically in Arusha & some killed, bcoz Govnmt has been such a BLIND & DEAF & CORRUPT doesn't listen to its people, all
the burden go to INNOCENT, POOR CITIZENS, once these poor citizens they wake up,
& now is almost 5:00 am, no ONE, no Government, no Fisadi will stop them, they will
need thru their physique power a sincere, honest Government of their people,
na ni ugumu wa Maisha utakao wakurupusha, This Gornmnt doesn't see any
BIG DANGER it lies ahead, bcoz of its reckless, corruption & poor governance,
hata ukisema hakuna wa kusikia, wala wa kutetea wananchi, watakuambia
ww you organize kugoma, demonstrations, ww mdini, ww. unasbbisha UVUNJIFU WA AMANI< AMANIIIIIII....!!!??????? na huu mwaka utakuwa
mgumu mnoooo, hatari sana few can see these.
 
I really don't understand it; asilimia 61 ya Watanzania wamewachagua na kuwarudisha madarakani watu wale wale. Halafu walitarajia nini? Huwezi kufanya uamuzi au uchaguzi bila kuwa tayari kulipa gharama yake.

MM mkuu, subiri kidogo tu, wananchi wakipata TAABU KUU, DHIKI, na tayari hali imeshaanza, watakurupuka, no one can stop them,
serikali haipo kwa ajili ya wananchi, we warned till we tired, ni kama kamari vile wananchi wamedanganywa na asiye watumikia, patamu
 
MFUMO wa ulipaji nauli kwa mabasi ya abiria jijini Dar es Salaam na miji mingine nchini maarufu kama daladala, express na vifodi, uko mbioni kubadilika kwa abiria kulazimika kulipa nauli kwa kilometa watakazosafiri.

Hayo yamo katika mapendekezo ya Chama cha Wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (DARCOBOA), kinachopendekeza ongezeko la nauli, lakini katika mfumo wa kulipa kwa kilometa.

Imependekezwa, mtumiaji wa daladala alazimike kulipia Sh 51 kwa kilometa, ili wamiliki wa vyombo hivyo vya usafiri wamudu gharama za uendeshaji ambazo zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku.

Hii ina maana kwamba, endapo pendekezo hilo litapita, kwa abiria anayetoka kwa mfano Bunju kwenda katikati ya Jiji, atalazimika kulipa Sh 1,530 kwa safari moja, na kama atarudi, basi kwa siku atalipa Sh 3,060.

Darcoboa walitoa mapendekezo hayo jana katika kikao cha wadau cha kukusanya maoni na kufanya mapitio ya ongezeko la viwango vya nauli za daladala Dar es Salaam yatakayoisaidia Mamlaka ya Udhibiti wa Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), kupanga nauli.

Akitoa maoni yake, Mwenyekiti wa Darcoboa, Sabri Mabruk, alisema matumizi ya mafuta kwa kilometa moja ni lita tatu, huku bei ya mafuta kwa sasa ikiwa ni Sh 1,800 kwa lita, hali ambayo imekuwa ikiumiza wamiliki na kushindwa kuyafanyia matengenezo magari yao.

Alisema mwaka 1995 umbali usiozidi kilometa 10, nauli ilikuwa ni Sh 150 huku mafuta yakiuzwa Sh 385 kwa lita, lakini bidhaa nyingine zimekuwa zikipanda kwa kasi zikiiacha nauli chini huku vipuri na mafuta vikiendelea kupanda.

“Kwa kipindi cha miaka 10 nauli ya daladala peke yake imebaki chini, yaani nauli imezidi kukandamizwa wakati tunasafirisha askari bure na watu wenye vitambulisho wakiwamo wanafunzi … jamani tuitendee haki sekta ya usafirishaji,” alisema.

Alisema pamoja na kiasi hicho kidogo cha nauli wanachotoza, lakini gharama za uendeshaji ni kubwa, miundombinu mibovu hali inayofanya safari kutoka Ubungo hadi Buguruni, kutumia saa moja hadi nne kutokana na foleni, ambapo pia uchakachuaji wa mafuta unawaathiri zaidi katika kutoa huduma hiyo.

“Kutokana na hali hii tunapendekeza nauli iwe Sh 51 kwa kila kilometa, kwa maana kwamba anayetoka kilometa 30 azidishe mara 51 … kila mtu alipe nauli kulingana na umbali ili kila mtu abebe mzigo wake,” alisema.

Aidha, utaratibu huo ukikubalika, wanapendekeza kupimwa na kuwekwa alama zitakazoonesha umbali, kwa maana ya kilometa kwa lengo la kupunguza malalamiko ya abiria.

Chama cha Kutetea Abiria (Chakua), kilipinga mapendekezo hayo na kuwataka wamiliki kuboresha magari yao ambayo mengi ni kero hasa wakati wa mvua na kusema zipo njia nyingi za kuwaongezea mapato, ikiwamo kuondoa wapiga debe ambao wamekuwa wakilipwa kila siku.

Akijibu hoja hiyo, Katibu Mkuu wa Darcoboa, Mujengi Gwao, alisema ni kweli wana magari
mabovu, lakini hawatayarekebisha kwa nauli ya Sh 250 na kwamba wapiga debe hawawahitaji na walishazindua mpango wa kuwaondoa, lakini Serikali imeshindwa kuusimamia.

Aidha, waliiomba Sumatra kuelekeza makosa ya mtendaji na kumhukumu badala ya kila kosa la dereva kuelekezwa kwa mmiliki na wakati mwingine kudaiwa faini kubwa kwa kosa la kwanza tena bila onyo.

Madereva nao walisema hata nauli ikipandishwa na kuwa Sh 500, yasipoondolewa magari mabovu barabarani, bado itakuwa ni hasara kutokana na wenye magari hayo kushusha nauli ili kuvutia abiria.

Kwa upande wao Baraza la Watumiaji wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra CCC),
walipinga ongezeko hilo na kutaka kila kilometa itozwe Sh 29 na kutaka tatizo la msongamano wa magari liondolewe na kuboreshwa miundombinu ili kupunguza gharama za uendeshaji.

Akihitimisha mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Israel Sekirasa, alisema wanaendelea kupokea maoni hadi Januari 15 na kuwataka wasafirishaji hao kutowaona askari Polisi, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Magereza kuwa ni mzigo, kwa sababu kila wanapokuwa katika vyombo hivyo, wako kazini na kuongeza kuwa, baadhi ya majeshi yameendelea kununua magari kwa ajili ya watumishi wao.
 
Kweli haya ndio maisha bora kwa kila mDanganyika!Kwa hali hii tutafilisika kabla hata hatujatajirika!
 
Wamiliki wa daladala kama wanaona hiyo biashara hailipi kwa nini wanaendelea nayo?

Ningekuwa kiongozi wa sirikali ninayehusika na usafiri jijini nisingekubali hii proposal.
 
Maisha bora kwa kila Mtanzania...........Wajitokeze sasa wale waliokuwa wakishabikia kijani na manjano tuwasikie..........Watu wanachakachua mafuta wanajulikana na wanaachwa, polisi wanakula tushwa na kurusu magari mabovu barabarani wanaachwa............makonda wanakatisha route hakuna sheria za kuwabana..............Nitafurahi hii proposala ya Bunju posta kuwa sh.1500 ili siku tukisema tuandamane basi watu wote watakuwa barabarani
 
Hizo noti mpya zishaingia kwa mtaa?If possible tubandikieni hapa,at least nipate picha
 
"Kupanda kwa nauli hakukwepeki" kidumu chama cha mapinduzi na fikra za mwenyekiti!!!!!!!
 
I really don't understand it; asilimia 61 ya Watanzania wamewachagua na kuwarudisha madarakani watu wale wale. Halafu walitarajia nini? Huwezi kufanya uamuzi au uchaguzi bila kuwa tayari kulipa gharama yake.

hakuna sababu ya kuendelea kuwablame hao 61% maana washafanya walichokifanya ingawa hadi 39% tunaathirika.
 
Nataka Nauli Ipande.

Imani yangu ni kwamba Kupanda kwa nauli kutaambatana na Kupanda kwa hasira za Watanzania na kuwaamsha kutoka kwenye usingizi mzito wa Pono waliolala wakiwa wamejifunika kwa shuka wanalozimishwa na wanasiasa kujifunika nalo la 'Amani, Utulivu na Mshikamano'!


Ni Kupanda kwa nauli tu ndipo tunaweza kuanza kujihakikishia kuwa na 'Arusha' nyingi zaidi iwezekanavyo kuelkea UHURU wa Kweli. A LUTA CONTINUA.
 
Nimesikiliza mapendekezo ya nauli mpya za mabasi zikanistua sana, nikaogopa sana na kujiuliza nchi hii tunaelekea wapi..?

Kumbuka kupanda kwa nauli hizi kutasababisha kupanda kwa bei za bidhaa karibu zote hapa nchini na sana sana mikoani kwa ndugu zetu ambao maskini wa Mungu kipato chao....


Ndugu Wana JF, kama watanzania tufanyeje kuepusha balaa hili?

Watanzania tun uwezo wa kuwalazimisha kushusha hizo bei. Always nguvu ya UMMA ndiyo silaha ya maskini.
 
Back
Top Bottom