Nataka kuweka stop order kwa benki inayotaka kuuza nyumba yangu Mbeya Mjini

Kuna kitu hujaeleza. Ila unapaswa ukaonane na manager, umueleze hal yako kibiashara, kiwango unachomudu kwa sasa kulipa ili waweze kukurekebishia mkopo wako uendane na hali halisi.
NB. Kama bank inafata taratibu zote za kukupa mrejesho wa mdololo wa marejesho yako, hata mahakaman watashinda na nyumba itauzwa.
 
Habari wana jf, asalaam aleykum Muslimina.

Nianze moja kwa moja suala langu, nimekuwa na utaratibu wa kuomba overdraft miaka 4 iliyopita kiasi cha shilingi million 15.

Nimekuwa nikichukuwa kutumia fedha hizo kwa shughuli zangu za biashara ya mpunga na mahindi pamoja na korosho, kama kawaida, lakini kwa bahati mbaya kutokana na hali mbaya ya kiuchumi kama sote tunavyofahamu awamu ya tano haikuwa rafiki kibiashara kwa wafanyabiashara, hivyo deni lilia cumulate mpaka kufikia million 40, kutoka 15 million, hivyo nilijipigapiga katika KUEPUSHA shari nikalipa 21 million, hivyo deni kubaki nusu, lakini rekodi yangu ni nzuri katika banks hiyo na Nina imani ndani ya muda mfupi nitalimaliza deni hili, hawa jamaa hawataki kuelewa na wamenipa siku saba tu.

What should I do to stop that shits.
Kama mteja wao mzuri kuna room ya kujadili
 
Hao wapeleke Baraza la ardhi la wilaya huko utapewa zuio na hati utaipata huko utampatia mtendaji wa kata au mtaa au Mg au dalali wa mahakama ampatie wito branch manager akisaini tu mikwala yote inaishia hapo then rudi kwa karani wa mahakama yeye ndo mpanga tarehe cheza na pesa tu huko maboss huitwa wenyekiti wa Baraza watakuwa wanasogeza siku mbele huku unakaa sawa na milango itafunguka ulipe deni then nyumba haitaguswa na mtaani hawatajuaa maana madalali wakianza kuchora nyumba na kupiga PA mtaani heshima inashuka kwa Sasa nenda mahakama ya ardhi upate zuio Ila pesa kule muhimu uitoe ukizubaa zuio hupati mjengo unatembea huyo manager achana naye
Naongea kwa uzoefu hiyo hali nilipitia naijua vema sisi wapambanaji no check number mkuu.
 
Back
Top Bottom