Itakuwa ni uwendawazimu na ukichaa kwa wana Mbeya kumtoa Dkt. Tulia jimbo la Mbeya Mjini

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,343
9,770
Ndugu zangu watanzania,

Naifahamu Mbeya ,Nawafahamu Wana Mbeya ,Nimekaa na kuishi Mbeya,Nimesoma Mbeya,Naendelea kwenda Mara kwa Mara Mbeya,Nazifahamu siasa za Wana Mbeya,Nafahamu Fikira za wanambeya,Nafahamu misimamo ya wanambeya,Nafahamu Tabia za wanambeya,Nazifahamu kero za Wana Mbeya,Nafahamu Mahitaji na kiu ya wanambeya.

Niseme tu kuwa Wana Mbeya siyo wajinga ,siyo wendawazimu,siyo vichaa na Wala siyo mbumbumbu, kwa kuwa Mbeya imeelimika na watu wake wameelimika hata kwa yule ambaye hajapita vidato anauelewa Mpana Sana wa mambo mbalimbali ambapo huwezi mdanganya kitu Wala kumburuza Kama mnyama asiye na utashi alionao mwanadamu.

Wana Mbeya siku zote walihitaji muwakilishi wa kuwasemea kero zao na kuzitafutia majibu na suluhisho,walihitaji mtu atakayezungumza na kuielewa lugha Yao juu ya Mahitaji Yao,walihitaji mtu atakaye kwenda bungeni na ajenda zao,walihitaji mtu atakaye waletea mrejesho akitoka bungeni,walihitaji mtu asiyelalamika muda wote kuwalaumu wengine maana kiasili na kitabia watu wa Mbeya Ni majasiri Sana na shupavu na hivyo hawahitaji mtu legelege na dhaifu kimsimamo kuwa mwakilishi wao,

Kwa Bahati mbaya katika miaka kumi walipoteza Kura zao kwa mtu ambaye aliingia katika ubunge Kama sehemu ya kujineemesha,kujimwambafai,kujikuza yeye binafsi ,kutunishaa akaunti yake benki,kuleta usera na ujanja janja,matokeo yake jiji likasimama kimaendeleo,likakosa mwakilishi ,likawa kama Lina mbunge hewa mpiga makelele na mavurugu kuanzia bungeni Hadi jimboni ,likakosa heshima ya kuitwa jiji,halimashauri ikaongozwa kiupofu pasipo mipango madhubuti kwa manufaa ya jiji na wanambeya,hoja zenye mashiko zikakosekana kutokana na mbunge wake kuwa na upeo mdogo wa kujenga hoja zaidi ya kuleta lugha za vichochoroni,kwa hakika yakawa ni majuto kwa wanambeya kulikokuwa kumetokana na kukosa mbadala.

Kukawa Hakuna ujenzi wa chochote kuanzia zahanati Hadi vituo vya Afya, Barabara za mitaa zikawa Ni matope na madimbwi matupu,maana Jimbo lilikuwa na mbunge kimvuli asiyefahamu wajibu wake Kama mbunge,Asiyejuwa ashirikiane na Nani kufanikisha Jambo fulani,asiye juwa apite wapi ili apate Jambo fulani, Asiyejuwa aseme Nini kwa Nani kupitia wapi kwa Nani ili Jambo fulani litokee,Alikuwa Ni mbunge wa maneno maneno tu.

Hatimaye Mwenyezi MUNGU akamuinua na kumpa kibali mwanadada msomi na nguli wa Sheria Dr Tulia Ackson Mwansasu,Dada mcha Mungu na mwenye hofu ya Mwenyezi MUNGU,mstaarabu na mwenye kifua Cha hekima,anayejuwa wakati gani azungumze na azungumze nini,Anayejuwa utu na ubinadamu ,aliyetokea na kukulia katika mazingira ya chini na ya kipato Cha chini ya kuuza vibama na mboga za majani anayejuwa shida za watu,anayejuwa maana ya kulala na njaa na kukosa chakula,anayejuwa maana ya maisha na Hali ngumu,aliyepitia katika maisha magumu lakini akafanya juhudi za kusoma kwa bidii Nidhamu na uchungu wa kutaka kuona siku moja anarejea nyumbani kumfuta machozi na kumsaidia mama yake , hatimaye Akainuliwa na Mwenyezi MUNGU Kama ilivyokuwa kwa yusufu , mwenye Tabia njema na aliyetukuka kwa huruma upendo unyenyekevu na ukarimu kwa watu wake.

Mwenye kuguswa na shida za watu ,mwenye kumhurumia kila mtu,mwenye kutoa msaada kwa kila aliye mbele yake,mwenye kumshika mkono kila mtu,asiyejikweza Wala kujitutumua Wala kujisifu Wala kuhitaji kutukuzwa Wala kuabudiwa, mwenye moyo wa kusaidia, asiye na mipaka ya kusaidia na kugusa maisha ya watu ndio sababu siku moja alikuja mkoani Songwe wilayani Mbozi kata ya mlowo Kijiji Cha ivwanga kitongoji Cha mabatini B akatoa msaada wa mabati katika shule ya msingi Mabatini ambapo kwa Sasa wanafunzi wanasomea na kujifunzia katika mazingira ya kutia moyo na hamasa ya kusoma,Huo wote Ni upendo mkubwa uliojaa katika kifua chake.

Tangia amekuwa mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini mabadiliko makubwa yametokea na maendeleo makubwa yamepatikana kwa kushirikiana na serikali ya Rais Samia mama shupavu na madhubuti,Ambapo kila secta imepiga hatua kubwa za kimaendeleo,kuanzia Miundombinu,Elimu Afya ,kuinua na kusaidia wajasiriamali,vijana akina mama wazee na watu wenye ulemavu,kila utakako kwenda lazima utaona Alama na mikono ya mh Dr Tulia Ackson,Na Sasa kwa juhudi zake na ushawishi wake kwa serikali, kunakwenda kujengwa kwa Barabara zingine zitakazo punguza msongamano wa magari,ajali na kuweka usalama kwa watembea kwa miguu pamoja na kuokoa muda.

Ndio maana wanambeya wanasema Dr Tulia Atosha na ndio chaguo lao uchaguzi ujao,Ndio mbunge wa ndoto Yao ,Amekata kiu Yao ya muda mrefu na amekidhi matarajio Yao ya wakati wote na amegusa mioyo Yao kwa utendaji kazi wake uliotukuka wa kujitoa na kujitolea.

Wanasema itakuwa ni Uwendawazimu na ukichaa wa hali ya juu kumtoa Dr Tulia katika ubunge ili kumrejesha aliyeshindwa kwa miaka yote kumi kufanya kazi hata robo tu ya Ile aliyofanya Dr Tulia kwa muda mfupi wa ubunge wake. Dr Tulia ndio sauti ya wanambeya na mtetezi wa wanambeya,Ameiheshimisha Mbeya na kuipa Hadhi ya kuitwa jiji,Mbeya imechanua kwa maendeleo na kustawi kila Kona ,Ameinua matumaini ya vijana waliokuwa wamekata Tamaa Baada ya kuwa wametumika na kutupwa Kama taka na aliyekuwa mbunge kimvuli.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa , kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
Ndugu zangu watanzania,

Naifahamu Mbeya ,Nawafahamu Wana Mbeya ,Nimekaa na kuishi Mbeya,Nimesoma Mbeya,Naendelea kwenda Mara kwa
Kwani kuna ubaya gani wana Mby tukimpa Sugu urais wake? Tulia aende kwao Rungwe/Busokeko.

Mbeya Mjini bora temperature Matthew Mwaikambo a.k.a Kambosonic, Kuliko tumpe yule binti wa kina Mama Machibya, Mama Mosha, Mama Msyani na Baba Watende na mzee Kajange pale getini.

Mtoto wa geti kali anazijua wapi shida za watu?
 
Kwani kuna ubaya gani wana Mby tukimpa Sugu urais wake?. Tulia aende kwao Rungwe/Busokeko. Mbeya Mjini bora temperature Matthew Mwaikambo a.k.a Kambosonic, Kuliko tumpe yule binti wa kina Mama Machibya, Mama Mosha, Mama Msyani na Baba Watende na mzee Kajange pale getini. Mtoto wa geti kali anazijua wapi shida za watu?
Dr Tulia kalituliza jiji na kulipatia maendeleo waliyoyahitaji Wana Mbeya kwa miaka yote,Heshima aliyolipatia jiji na mkoa wa Mbeya ni kubwa sana ambayo wanambeya hawawezi kukubali kuipoteza kwa kumpa Kura mtu mwingine yeyote Zaid ya Dr Tulia Mwenyewe aliyeleta heshima hiyo jijini na mkoani mbeya
 
Hana mpinzani wa kushindana Naye maana Wana Mbeya wameamua kumrudisha Tena Bungeni uchaguzi ujao maana Ameiheshimisha Mbeya na wanambeya
Majimbo yapo zaidi ya 300 lakini kila siku ni mada zake kwamba anakubalika kuliko sugu kama ni hivyo si atulie mchecheto wa nini? Mbona majimbo mengine wapo kimya, ila ajue yule aliyempa hilo jimbo 2020 hayupo tena
 
Dr Tulia kalituliza jiji na kulipatia maendeleo waliyoyahitaji Wana Mbeya kwa miaka yote,Heshima aliyolipatia jiji na mkoa wa Mbeya u kubwa Sana ambayo wanambeya hawawezi kukubali kuipoteza kwa kumpa Kura mtu mwingine yeyote Zaid ya Dr Tulia Mwenyewe aliyeleta heshima hiyo jijini na mkoani mbeya
Wewe ongelea mambo ya kina tumugoje/ tumukeshe. Mchunane ngozi ndio burudani yenu.

Hujui chochote kuhusu siasa za Mbeya Mjini. Kwanini jengo la CCM Mbeya mjini ni jengo baya zaidi kuliko majengo yote ya makao makuu ya CCM mikoa aliyoiacha Nyerere?
 
Tunatamani hata kesho aondoke betina.
Sauti za wanambeya zinamhitaji Dkt. Tulia Kuendelea kuwa mwakilishi wao na mbunge wao, vijana wameridhishwa na uchapa kazi wa Dkt. Tulia na namna alivyowasaidia kupata mikopo kupitia halmashauri na hata yeye mwenyewe binafsi amewasaidia vijana wengi Sana kuwapatia mitaji bila kusahau akina mama wazee na watu wenye ulemavu.

Lakini pia amewasaidia wengi Sana wasio jiweza kuwakatia bima ya Afya ili wasipate shida na changamoto ya kupata huduma hospitalini wapatapo changamoto ya kiafya
 
Sauti za wanambeya zinamhitaji Dr Tulia Kuendelea kuwa mwakilishi wao na mbunge wao,vijana wameridhishwa na uchapa kazi wa Dr Tulia na namna alivyowasaidia kupata mikopo...
CCM ime spoil kwa kiasi kikubwa maendekeo ya Mbeya. Kuanzia uhuru ccm imeshindwa kuuoanga vizuri mji wa Mbeya. Idara ya upimaji na ramani walikuwa wanafanya nini miaka nenda rudi?
 
Ndugu zangu watanzania,

Naifahamu Mbeya ,Nawafahamu Wana Mbeya ,Nimekaa na kuishi Mbeya,Nimesoma Mbeya,Naendelea kwenda Mara kwa Mara Mbeya,Nazifahamu siasa za Wana Mbeya,Nafahamu Fikira za wanambeya,Nafahamu misimamo ya wanambeya,Nafahamu Tabia za wanambeya,Nazifahamu kero za Wana Mbeya,Nafahamu Mahitaji na kiu ya wanambeya.
Huko kwenu Mbozi ccm imewafanyia nini? Tunduma , Magufuli mchana kweupe alisema hawaletei maendeleo. Wewe ni msaka Tonge ndio maana kila uzi wako unaandika namba ya simu ili upate uteuzi. Umefeli Big time
 
Majimbo yapo zaidi ya 300 lakini kila siku ni mada zake kwamba anakubalika kuliko sugu kama ni hivyo si atulie mchecheto wa nini? Mbona majimbo mengine wapo kimya, ila ajue yule aliyempa hilo jimbo 2020 hayupo tena
Kwani wewe Nani aliyekuzuia kuzungumzia hayo majimbo mengine? Kazi kubwa alizofanya Dr Tulia zinambeba na kumfanya aendelee kuchanja mbuga katika mioyo ya wanambeya ambao wanamuona Kama mkombozi wao na aliyewapa heshima ya kipekee kabisa
 
Huko kwenu Mbozi ccm imewafanyia nini? Tunduma , Magufuli mchana kweupe alisema hawaletei maendeleo. Wewe ni msaka Tonge ndio maana kila uzi wako unaandika namba ya simu ili upate uteuzi. Umefeli Big time
CCM imefanya makubwa sana katika wilaya ya Mbozi, imejenga vituo vya Afya kila Kona,shule kila mahali,zahanati kila sehemu,usambazaji wa maji Safi na salama, utolewaji wa mbolea za Ruzuku.

Pia serikali yetu Ina mpango wa kujenga Barabara ya kutoka mlowo Hadi kamsamba kwa Kiwango cha lami hali itakayo fungua fursa za kiuchumi.

Kuchochea na kurahisisha biashara,kupunguza Bei ya usafirishaji wa mazao na mizigo mingine Kama vile mpunga kutoka kamsamba, mahindi maharage kahawa alizeti kutoka maeneo tofauti Tofauti,kukuza na kuongeza miji kidogo kidogo Kama vile igamba
 
CCM ime spoil kwa kiasi kikubwa maendekeo ya Mbeya. Kuanzia uhuru ccm imeshindwa kuuoanga vizuri mji wa Mbeya. Idara ya upimaji na ramani walikuwa wanafanya nini miaka nenda rudi?
Sasa Mbeya IPO katika mikono salama na Tulivu ya Dr Tulia ,hivyo Apewe ushirikiano ili aendeleze kazi kubwa aliyoianza ya kulijenga jiji la Mbeya kimaendeleo,Hakuna jiwe litakalobakia mbele ya Dr Tulia ,Hakuna mfupa mgumu kwake mh Dr Tulia Dada mchapa kazi na mbunifu ,
 
Back
Top Bottom