Nape mnafiki? Sasa amsifu Rostam hadharani huko Igunga

Rostam naye kama si mnafiki kwa kusema ameachana na siasa uchwara tutaona reaction yake

Hapo ndipo napo pasubiri mie kuwaona ndugu zangu wananchi wa Igunga je Ni mazuzu au Maana hamuwezi ona Mbunge wenu wa Igunga katika kashifa na huku nyie mlikuwa mnamwamini yuko safi na imeonekana ni mchafu na nyie hamtaki kukusikia hilo na akaja kujiuzuru mbele yenu na mkakili hamto kichagua tena CCM sasa hapo ndipo tutakapo kuja kujua je ni kweli yule mbunge wenu aliye sema hataki tena kujihusisha na Gutter Politics means si ha sa za maji taka iweje leo hii aje kuwaumiza kidonda kuwa hato rudi tena kwenye ulingo wa si ha sa iweje leo aje tena si uchonganishi huo kati ya uongozi wa Juu ya CCM na watu wa Igunga??

My Take;

Kurudi kwa Rostam kwenye Gutter politics kama alivyosema wakati anajivua uongozi na ubunge wa Igunga ni Matusi makubwa na dharau inaashirilia kuwa wana Igunga wote walikuwa ni mafisadi.

Na kama walichukizwa sana na Uongozi wa juu wa CCM katika kufanya mbunge wao RA kujivua nyadhifa zote basi wana Igunga wanatakiwa kuidhihilishia CCM kuwa wao ni watu komavu katika siasa na wachague kiongozi wamtakao wao ni sio CCM iwachagulie kiongozi wamtakao wao.

You have to give the devil his due. Rostam alikuwa fisadi upande mmoja lakini upande mwingine ni mwanamaendeleo na mchangiaji mkubwa sana. Amesidia miradi mingi sana ndani ya Igunga na hata nje yake. Kwahiyo sidhani kama kuna tatizo tukimpa sifa zake ingawa ni kweli ameshiriki kwenye ufisadi mkubwa sana.
Mchango alioutoa haufiki hata theluthi ya pesa alizoiba,kinachouma anabwiha pesa za walipa kodi kama wewe na mimi

You have to give the devil his due. Rostam alikuwa fisadi upande mmoja lakini upande mwingine ni mwanamaendeleo na mchangiaji mkubwa sana. Amesidia miradi mingi sana ndani ya Igunga na hata nje yake. Kwahiyo sidhani kama kuna tatizo tukimpa sifa zake ingawa ni kweli ameshiriki kwenye ufisadi mkubwa sana.

Kwa wewe Unayefikiria kwa Kutumia Masaburi, Mwanamume akikugongea Mkeo let say, na kesho akajitokeza kumlipia mwanao Karo ya shule, still uta mpraise???ni kwa mtu aliyeganda Ubongo ndo anaweza kumsifia Rostam

JK mwenyewe mwongo, kawadanganya watanzania na ahadi zisizotekeleka, sembuse Nape kuwadanganya wana Igunga! Kudanganya ndiyo Itikadi ya ccm, hata majina yao sometimes ya uongo.

• Thanks
Reactions: LAT
kutumia muda mrefu kumzungumzia nape na rostam ni kupoteza muda na kuwapa umaarufu.
tuzungumze namna ya kuwatoa kwenye kiti pale igunga.

Tatizo siyo Nape bali ni CcM kwa Ujumla,wamezoea kuwadanganya watanzania hata kwa jambo ambalo haliwezekani kila kipindi cha uchaguzi,hebu fikiri Ahadi za uchaguzi za ccm zimefanywaa?
Wanawafanya watanzania wajinga mno,ili kukataa kuonekana wajinga wana Igunga msiichague ccm kabisa.

CCM ajenda yake kuu ni kushinda chaguzi hivyo mambo ya maendeleo ya wananchi sio priority yake ndio maana wanafanya wanayofanya kuwadanganya wana Igunga!! Kama Rostam alifanya mambo makubwa kwa wanaIgunga kwanini basi mumuandame kuwa atoke kwenye chama chenu kwani alikuwa gamba? Nape anatumiwa na punde atatupwa kama kondomu iliyotumika!!

You have to give the devil his due. Rostam alikuwa fisadi upande mmoja lakini upande mwingine ni mwanamaendeleo na mchangiaji mkubwa sana. Amesidia miradi mingi sana ndani ya Igunga na hata nje yake. Kwahiyo sidhani kama kuna tatizo tukimpa sifa zake ingawa ni kweli ameshiriki kwenye ufisadi mkubwa sana.

Nyie ndo walewale ambao hata ukijitahidi kuwafikisha kwa mungu mtadai mkapaone na kwa shetani pia

Hapo kwenye red,
Hivi unaona raha gani kumtukana Nape, kwa nini usiandike bila dharau? Hata kama humpendi au unataka sifa toka kwa wachangiaji, fahamu wako wengi wanaompenda Nape, haijalishi utamtukana vipi lakini ni kiongozi na anayo heshima yake kama mTZ.
Kwa taarifa yako Nape atakuja kuwa kiongozi mkubwa serikalini, hupende usipende huu ndo ukweli.
Kama unavotaka kuheshimaka mpe heshima yake nape then jenga hoja.
Mi si mwanachama wa chama chochote kwa sasa, lakini sipendi dharau kama hizi.
Wewe una nini zaidi ya Nape? Acha hizo bana

Wewe una ubia na Nnape??? Kwanini unamtetea ilhali kweli ni vuvuzela la CCM??

Central Committee walimwambia asiende Igunga maaana ataikosesha CCM ushindi KWA VILE YEYE NDIYE ALIYESABABISHA ROSTAM KUJIUZULU UBUNGE NA NYAZIFA ZOTE NDANI YA CCM. Je,wewe huyajui haya? Yaonekana hata CCM wenyewe HAWAMWAMINI NNAPE. Kwanza bado hajajibu tuhuma za KUANZISHA CCJ ndani ya CCM na hao jamaa zake kina Sitta. Nnape hana lolote ni domokaya mpiga makelele lakini hana moja wala mbili kichwani.Pambaf!

Unaposema Nnape atakuja kuwa kiongozi Mkubwa serikalini ni kwa hao MAVUVUZELA WA CHAMA CHA MAGAMBA TU na si vinginevyo.

Mi nadhani watanzania hatujaelewa nini msimamo/mwelekeo wa hiki chama, nadhani kumbukumbu ya uchaguzi mkuu mwaka jana watu mmeshasahau! M/Kiti wa chama si alipita majimbo yote ya hao 'MAFISADI' na kuwanyanyua mikono kwamba ni watu safi, timu iliyo kamilika n.k?!! Sasa leo hii tukimshangaa Nape tutakuwa tunaamua kusahau mambo ambayo hayajamaliza hata mwaka 1 tangu yatokeee.. HIKI CHAMA NDIVYO KILIVYO, Msiokuwa wanachama itakuwa ngumu sana kuelewa philosophy yao.

hizi ndio siasa za tanzania hazina mbele wala nyuma kila mtu analake hawa jamaa Nape na Rostam ukiwapima akili zao zinaweza kuwa na matatizo makubwa sana matendo yao tu yanadhibitisha haya yote

You have to give the devil his due. Rostam alikuwa fisadi upande mmoja lakini upande mwingine ni mwanamaendeleo na mchangiaji mkubwa sana. Amesidia miradi mingi sana ndani ya Igunga na hata nje yake. Kwahiyo sidhani kama kuna tatizo tukimpa sifa zake ingawa ni kweli ameshiriki kwenye ufisadi mkubwa sana.

Usingezunguka, ungesema hivi fedha alizopata ra kwenye ufisadi alikuwa kiasi kidogo akikitumia kununua wananchi wa igunga na kwingineko Tz basi.

Man huu uzushi.. una ushahidi gani kama rostam kalazimishwa....

kwa mahaba na mapenzi yake ya chama tawala ndio maana afanya hivo

Hapo kwenye wekundu hapo.

Kama RA angelikuwa na MAPENZI NA MAHABA KWA CHAMA CHAKE TAWALA ASINGELITHUBUTU KUJIVUA NYAZIFA ZAKE ZOTE NA KUWAITA CCM WANA SIASA UCHWARA-GUTTER POLITICS.

Uwezekano wa kulazimishwa kwa RA kuikampenia CCM uko wazi kabisa. Kwamba wasipomtumia kwenye kampeni zao CCM wanajua kabisa itakuwa imekula kwao na hilo jimbo halitarudi mikononi mwao.

Kwa hiyo CCM wanachofanya kwa sasa ni kutumia kila mbinu NZURI NA CHAFU IKIWA NI PAMOJA NA KULAZIMISHA,KUTUMIA MABAVU,KUIBA KURA NA IKIWEZEKANA KUUA KABISA ILMRADI IGUNGA ITAWALIWE NA CCM.

Hapa ndipo mimi nilipokuwa najiuliza na ndipo HOJA
Rostam naye kama si mnafiki kwa kusema ameachana na siasa uchwara tutaona reaction yake

You have to give the devil his due. Rostam alikuwa fisadi upande mmoja lakini upande mwingine ni mwanamaendeleo na mchangiaji mkubwa sana. Amesidia miradi mingi sana ndani ya Igunga na hata nje yake. Kwahiyo sidhani kama kuna tatizo tukimpa sifa zake ingawa ni kweli ameshiriki kwenye ufisadi mkubwa sana.
kk ina maana hata majambazi wakiiba benki na alafu wakasaidie ombaomba tuwaachie kwa sababu watakuwa wamesaidia jamiii acha upofu mkuu...... fisadi ni fisadi tu haijalishi kafanya nini....... Lyumba alikuwa anatoa misaada kibao tu kwa watu bado kafungwa

Nape Moses Nnauye ambaye siku za hivi karibuni alikuwa akipita huku na kule akiwananga mapacha watatu kwamba ni magamba, ndio yamechangia kuipa CCM ushindi mdogo, na kwamba lazima waondoke CCM. Moja ya magamba hayo ni Rostam Aziz.

Katika hatua inayoonyesha unafiki wa Nape na uongo wake uliotukuka wa kuwahadaa wananchi wa Igunga, Nape ameanza kumsifia Rostam Aziz huku akiomba watu wasimbeze kwa kuwa amefanya makubwa huko Igunga. Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania la leo, Nape amesema kazi aliyoifanya Rostam ndio kigezo cha ushindi wao huo Igunga.

Naomba watu wa Igunga msidanganyike tafadhali, huu uongo wa CCM wa kujipendekeza siku za uchaguzi unatakiwa ukataliwe kwa vitendo kwa kuwakataa huko Igunga. Nape anawafanya watanzania ni wajinga, kwamba anaweza kusema chochote leo na kesho akasema kingine na watu wakamsikiliza. Nape siasa za kuhadaa watu hazina nafasi kwenye dunia ya sasa, acha unafiki wako.

Jamani watu wafike mahali wamuogope Mungu. Hawa magamba wanachezea watu kiasi hiki utafikiri wao ndio wenye akili peke yao. Jamani watanganyika ndugu zangu hebu tufike mahali tuseme BAAAASI INATOSHA.
jana tu hawa magamba wanamsema vibaya sana huyo gamba mwenzao na kutaka aachie ngazi leo hii hata hawakumbuki walichokisema wanakuja na porojo tofauti. Hii ndiyo kuonyesha kuwa hawa jamaa wanafikiri kwa kutumia masaburi na wanawaona watanganyika ni wadanyanyika na wanaweza kucheza na akili zetu watakavyo. Hebu kuanzia sasa tuseme NOOOOO. Na tuanzie na Igunga. Watu wa Igunga tafadhalini onyesheni mfano

Hapo sioni Unafiki wowote!
Rostam aliamua kuwa Accoutable (ni watanzania wachache sana wanaoweza kuachia madaraka-Oly Rostam & Lowasa hav done that)
Alifanya mambo mengi sana Igunga na kila mwana Igunga anayakubali- ndio maana tulishuhudia vilio siku ile alipokuwa anatangaza kung'atuka.
Kitendo cha Nape kumsifia kwa aliyoyafanya ni sahihi kabisa.
Ulitaka amponde kwa aliyowafanyia watu wa Igunga ambayo yanaonekana wazi wazi?
Wewe ulianzaisha hii thread ndio mnafiki mkubwa na hujui unalozungumza.

Ni kweli Nape alitakiwa aseme ukweli tu wa yale aliyoyafanya, lakini pia asiache kusema kuwa Rostam ni fisadi na atambe kwa yeye mwenyewe kufanya juhudi ya kumng'oa kwenye uongozi. Akifika hapo hataitwa mnafiki, lakini akiishia kumsifu tu ili CCM ipate kura kupitia mgongo, huyo atakuwa mnafiki na anapaswa kuogopwa kama ukoma.

alipitwa na usemi huu "" usitukane mamba kabla hujavuka mto""

Back
Top Bottom