Nape mnafiki? Sasa amsifu Rostam hadharani huko Igunga

Mwanzoni ilisemekana Rostamu aliweka ngumu alipoombwa akubali kuisaida CCM katika kampeni huko Igunga lakini alipoendelea kubembelezwa alitoa masharti kadhaa kubwa zaidi likiwa la jina lake kusafishwa mbele ya wananchi wa Igunga.

Aliitaka CCM ihakikishe kazi hiyo haifanywi na kiongozi yeyote mwingine ndani ya CCM zaidi ya katibu wake wa uenezi Nape Nnauye. Ilibidi maamuzi yafanyike haraka haraka kumwondolea kifungo cha kutokukanyaga Igunga huyo vuvuzela ili aweze kufika Igunga kumsafisha huyo kingmaker wa CCM.

Na kweli kama ndoto vile, Nape Nnauye katinga Igunga na cha kwanza kabisa alichofanya siyo kumnadi mgombea wa CCM Kafumu bali kingmaker mwenyewe, Rostamu Aziz - makubwa haya!

Rostam hawezi kuepuka kumpigia debe mgombea wa chama chake, amelazimishwa atake, asitake.

Kamati kuu ya ccm ilimwambia kama atakataa kumkampenia mgombea wa ccm, itaanika mambo yake hadharani. Kwahiyo mtakavyomuona Rostam kapanda jukwaani Igunga ni kwa sababu ya kuiridhisha ccm.

Lakini jamaa hana hamu na CC ya chama chake na hakutaka kabisa kushiriki ila hana jinsi, isipokuwa kuitegemea ccm ili madhambi yake yawekwe pending.

Mheshimiwa, nashindwa kukubaliana moja kwa moja na maelezo yako, naomba mwongozo wako: RA ni muasisi wa wizi wa mabilioni bot na alikuwa mshika fedha na baadae kinara wa kampeni za ******, lakini pia huyu jamaa anajua vyanzo vyote vichafu na hata visafi vya mapato ya ccm, zaidi anajua jinsi ccm inavyopwaya na kuishia kutumia dola wakati wote, anafahamu ****** hajakaa kwa ridhaa ya watz ilz kwa wizi wa kura, anajua kabisa hata hiyo meremeta, deep green ni ya nani na pesa zake zilitumikaje, kuna gazeti la kila siku liliwahi kureport kuwa RA anauwezo wa kuingiza bilioni 180 kwa mwezi, sasa swali kwa TRA kama waliliona hilo, binafsi siamini kama wanaweza kumbana kiivyo kwa kuwa jamaa mara nyingi hufanya uchafu wake kwa ufundi sana. Ni dhahili sasa mambo yanapalaganyika, mheshimiwa naomba mwongozo wako...

Hapo sioni Unafiki wowote!
Rostam aliamua kuwa Accoutable (ni watanzania wachache sana wanaoweza kuachia madaraka-Oly Rostam & Lowasa hav done that)
Alifanya mambo mengi sana Igunga na kila mwana Igunga anayakubali- ndio maana tulishuhudia vilio siku ile alipokuwa anatangaza kung'atuka.
Kitendo cha Nape kumsifia kwa aliyoyafanya ni sahihi kabisa.
Ulitaka amponde kwa aliyowafanyia watu wa Igunga ambayo yanaonekana wazi wazi?
Wewe ulianzaisha hii thread ndio mnafiki mkubwa na hujui unalozungumza.

Mwanaume ni lazima uwe na uwezo wa kusimamia kauli zako. Ajenda kubwa iliyo mbele yetu watanzania ni UFISADI na RA ni kinaa wa huo ufisadi na Nape alijitanabaisha kuwa ni mpinga ufisadi, Sasa iweje lao hii hata kabal ya hatua za kisheria nkuchukkuliwa dhidi ya kinara huyu wa ufisadi akengeuke na kuanza kumsifia? Huu ni ushahidi tosha kuwa Nape ni mtu wa kutumiwa ndio maana hata ufisadi uliokuwa ukifanyika ndani ya UVCCM aliufichua katika kinyanganyiro cha kugombea Uenyeikti wa Jumuia hiyo na sio kama mtu anayechuklia ufisadi.

images

images

Inasadikika kuwa ukiwa mnafiki wakati wa ujana kuna uwezekano mkubwa uzeeni ukawa mchawi. kwa nini nape anakuwa kigeugeu hivo? watz wa leo hawadanganyiki ng'o.Siku zao magamba zinahesabika

Huenda ndiyo wamepanga iwe sera ya ccm ktk kampeni yao ili kulipata hilo jimbo la Igunga tena

Ujinga utakaotumika ni kumwomba awapigie kampeni tena wakati wao wenyewe wamemtoa baru,,,Sasa hapa patakuwa na neo..Kila kitu tayari twasubiria kipenga Mechi ianze

Kweli wanasiasa vigeugeu hasa hii mijitu ya Chama Cha Magamba-CCM!!!!
Ukifuatilia hili sakata la ROSTAM AZIZ kujivua gamba kwa madai ya KUCHOSHWA na siasa UCHWARA zinazoendeshwa na CCM ikiongozwa na vuvuzelA NNAPE na CHILIGATI na kuwa yeye RA ameachana na siasa lakini leo unasikia Magamba hao hao waliosema aondoke kwenye Chama chao leo wanamwomba AWASAIDIE KUNUSURU JIMBO LA IGUNGA kwa kuwapigia kampeni!!!!?????...Siwaelewi kabsaaa hawa Magamba.

CCM is just a bunch of fools. Wanachofanya ni kujaribu kucheze na akili za Watanzania kwa maneno ya dharau,kebehi,longolongo na ubabaishaji mwingi.
Mtu umemwambia ajiondoe kwenye chama maana ni gamba. Iweje leo unamwomba tena akusaidie KUKUPIGIA KAMPENI wakti unamtuhumu kuwa ni JIZI NA FISADI??? NI LINI RA NA BWM wameodolewa kwenye LIST OF SHAME????

Kwanza CCM walipokaa CC yao walisema Nnape asiende Igunga maana tayari ana BIFF na RA kwa hiyo ataharibu kabisa Kampeni za CCM na hivo kuwakosesha ushindi. Leo tunaambiwa Nnape ametinga Igunga. Ameenda kufanya nini huyu kama sio UNAFIKI NA UFUKUNYUKU WA KUKIVURUGA CCM???

Mimi naomba Wana IGUNGA wote safari hii wawashikishe adabu CCM pale Igunga. Hakuna kura itakayopigwa kwa ajili ya CCM HATA KAMA NI KWA BUNDUKI!!!!!

Sitaki CCM wawafanye wana IGUNGA ni majuha ambao hawajui maana ya KUMKATAA MBUNGE WAO. Acha Igunga iongozwe na CDM CUF but not CCM. CCM hawana hati miliki ya Igunga hata mara moja. Igunga ni ya wana-igunga na ya Watanzania wote.

CCM kwa kumkataa RA maana yake wamekataa haki na uhuru wa wana Igunga wa kuwapa ridhaa ya kuwaongoza! Nitakuwa mtu wa kwanza KUWAZOMEA NA KUWABEZA Wanyamwezi wa Igunga kama kweli wataipa CCM ridhaa ya kuwaongoza tena!!!!

Rostam naye kama si mnafiki kwa kusema ameachana na siasa uchwara tutaona reaction yake
Rostam bado anahitaji kupata pesa zaidi na zaidi, sasa akiwaudhi CCM atazipataje?

Nape kaajiriwa kwa hiyo hupo kazini na kaambiwa na Boss wake akamsafishe RA na ndicho anachokifanya.

CCM hawana la maana na kwa kauli hiyo dhana nzima ya MAGAMBA ni utumbo mtupu, na ndiyo maana CHENGE NA EL wamegoma kujikoboa na mimi nawa support 100%.

Uzuri wa Rostam ni kama uzuri wa gadafi, kusaidia wananchi wake huku yeye akipura mali lukuki,ila tulivo mazuzu tutawapa tena kura CCM

Mwanaume ni lazima uwe na uwezo wa kusimamia kauli zako. Ajenda kubwa iliyo mbele yetu watanzania ni UFISADI na RA ni kinaa wa huo ufisadi na Nape alijitanabaisha kuwa ni mpinga ufisadi, Sasa iweje lao hii hata kabal ya hatua za kisheria nkuchukkuliwa dhidi ya kinara huyu wa ufisadi akengeuke na kuanza kumsifia? Huu ni ushahidi tosha kuwa Nape ni mtu wa kutumiwa ndio maana hata ufisadi uliokuwa ukifanyika ndani ya UVCCM aliufichua katika kinyanganyiro cha kugombea Uenyeikti wa Jumuia hiyo na sio kama mtu anayechuklia ufisadi.
Kaka kauli yako nzito sana.

You have to give the devil his due. Rostam alikuwa fisadi upande mmoja lakini upande mwingine ni mwanamaendeleo na mchangiaji mkubwa sana. Amesidia miradi mingi sana ndani ya Igunga na hata nje yake. Kwahiyo sidhani kama kuna tatizo tukimpa sifa zake ingawa ni kweli ameshiriki kwenye ufisadi mkubwa sana.
you can't be both!
Na kama ni fisadi mmemchukulia hatua gani? Ni fisadi kwa ushahidi gani? Alifanya vipi ufisadi?

Sifa kubwa ya mfuasi washetani ni uongo. anaitwa baba wa uongo. Anayevuliwa magamba sasa anasifiwa. jaza mwenyewe. Kazi ya shetani ni kuharibu, kuua na kuiba.

Jamani huyu nape mngemsamehe kwa sababu huwa hasemi kitu kwa matakwa yake mwenyewe huyu anaelekezwa maneno ya kusema. Aliambiwa amponde rostam siku za nyuma na sasa ameambiwa amsifu, siku nyingine akiambiwa amtukane hadharani atafanya hivyo, hana jinsi.

Back
Top Bottom