Nape: Bajeti Mbadala ya Kambi ya Upinzani inadhihirisha uongo wa CHADEMA

NARUDIA : KATI YA AHADI HIZI HAPA CHINI NI ZIPI HAZINA UKWELI NA SI KWA MANUFAA YA TAIFAAhadi za Kikwete:
  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
  2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
  5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
  6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
  7. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
  8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
  9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
  10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
  11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
  13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
  14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
  15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
  16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
  17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
  19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
  20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
  21. Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba
  22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
  23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
  24. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
  25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
  27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
  28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
  29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
  30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
  31. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
  32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
  33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
  34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
  35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
  36. Kulinda haki za walemavu- Makete
  37. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
  38. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
  39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
  41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
  42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
  43. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  44. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
  45. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
  46. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
  47. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  48. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
  49. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
  50. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
  51. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
  52. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
  53. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
  54. Kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
  55. Kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
  56. Kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  57. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kibandamaiti mjini Zanzibar
  58. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
  59. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
  60. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
  61. Kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
  62. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
  63. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  64. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
  65. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
  66. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
  67. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha
Ahadi za Dk Slaa:
  1. Kujenga nchi isiyo na ufisadi
  2. Kurejesha maadili ya taifa, utumishi wa umma
  3. Kuanza mchakato wa katiba mpya ndani ya siku 100
  4. Kufufua Tanganyika ili irejee mezani kujadili muungano na Zanzibar
  5. Kufufua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo
  6. Kukata asilimia 20 ya mshahara wa rais
  7. Kupunguza mishahara ya wabunge kwa asilimia 15
  8. Kuweka Mwenge wa Uhuru Jumba la Makumbusho
  9. Kutoa huduma bora za afya bure
  10. Kutoa elimu bure chekechea hadi kidato cha Sita (elimu ya lazima)
  11. Kufuta kodi ya vifaa vya ujenzi
  12. Kuwalipa wazee wa EAC fedha zao ndani ya siku 100
  13. Kuwalipa wanaoidai DECI
  14. Kubana matuzi ya serikali
  15. Kupunguza ukubwa wa serikali (Mawaziri 15, manaibu watano)
Ahadi za Profesa Lipumba
  1. Elimu ya bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu
  2. Kubana matumizi kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri
  3. Kuunda serikali shirikishi
  4. Kusimamia rasilimali
  5. Kuimarisha miundombinu
  6. Kusimamia na kuboresha afya
  7. Kuboresha kilimo, viwanda na uwekezaji
  8. Kurudisha chakula cha bure mahospitalini
Asante sana mkuu!Nadhani wakati mkwereee anatoa hizi ahadi hakukuwa na ushirikiano kati ya ubongo na mdomo! Maji yalikuwa yako kidevuni nusura kuzama! Hata mkimuuliza leo na asivyo makini pengine hamna analokumbuka labda wamkumbusha. Alichokuwa anataka ni urais at any cost!
 
Jamani hivi ina maana tukipata vyeo/promosheni tukaingia kwenye system tuwe waoga kukubali maana itatubidi tuishi tusivyokuwa sisi yaani ndani wengine nje sisi. Mifano ni mingi ila wawili tu kwa sasa ni kama Nape na Mzee Salva pale State House!
 
Pamoja na kuwa na kodi kwenye cement inayotoka nje pakistan ,lakini inauzwa bei sawa na ya twiga inayozalishwa ndani?nape ajiulize inakuaje?suala la elimu bure nakumbuka Maghembe nae ali COPY NA KUPASTE dakika za mwisho kabla ya uchaguzi baada ya kuona hawana kura ktk uchaguzi uliopita jee ccm imejiandaaje na tamko lile ktk bajeti hii?
 
kwani ani kasema Chadema adui zetu? Tuanajadili posho hapa au bajeti?
Nape sasa ccm nchi imewashinda, kila siku unashindana na cdm kwanini msitatue kero za wananchi kama elimu, afya bora na maji kuliko kupoteza mda mkishadadia mambo ya cdm hasa ww, au kwasababu mlishawafanya wananchi kama kondom ukiwa na shida ndo unaitumia ukimaliza shida unaitupa au sio!
 
Hoja yake kwamba alitegemea kuona ahadi za CDM kwenye bajeti mbadala kama ambavyo tunategemea kuona bajeti za meli, barabara za juu na reli mpya kwenye bajeti ya serikali si ya kubezwa. Labda kitu alichosahau NAPE ni kuwa Serikali ya CDM isingekuwa na ukubwa wa Serikali ya sasa hivyo kwa kupunguza hivyo vyeo pesa nyingi ingeokolewa na kwenda kwenye huduma za jamii ikiwemo elimu bure. Embu fikiri kupunguza baraza la mawaziri la sasa toka takribani 50 mpaka labda 25 ni pesa ngapi ingeokolewa kwa maana ya mishahara na posho, wasaidizi wa waziri, ofisi/vitendea kazi, magari na gharama za kuhudumia hayo magari. Vile vile ukifuta vyeo vya wakuu wa mikoa na wilaya ni pesa ngapi itaokelewa.Kitu muhimu cha kufahamu ni kuwa bajeti mbadala ya CDM imeandaliwa kwa kufuata mfumo wa sasa wa serikali.
Wakuu wa mikoa, maDC ma katibu tawala na ghrarama zoa zoote zingeondoka! Ni mambo mengi ya kumfumo waliyokuwa wameahidi chadema...lkn jamani, kweli huyu Nape kaamua kuwa juha kiasi hiki! Au nae kaana kuwadharau wa Tz anadhani hawawezi kuchambua mambo!
 
Nimepitia maelezo yake , kukosoa si jambo baya ila kinachosikitisha ni kwamba anaongea kama mbumbumbu, ameongelea suala la CHADEMA kutoa elimu bure sekondari mpaka elimu ya juu, inamaana nape hajui kuwa kwenye ilani kuna mikakati ya utekelezaji na inaenda kwa hatua, kwa mwaka 2011/2012 bajeti imeeleza kufuta ada kwa wanafunzi wa kike na kiasi cha asilimia 50 kwa wavulana, hajui bado hapo kuwa kungekuwa na miaka mingine minne ya kwenda hatua nyingine hatimaye kutekeleza sawasawa na ilani ya CHADEMA, kadhalika katika mambo mengine ambayo yeye ameyaona kama mapungufu.

Mbona nasikia baba yake huyu alikuwa mtu makini... huyu kilaza alipatikanaje ? anatia aibu

Kaka nawe unataka kuwa kama Nape ? Was there any need of you starting an new thread about the same thing badala ya kujibia pale pale ? Nape ni mtupu sana ulikuwa hujui ?
 
Nimepitia maelezo yake , kukosoa si jambo baya ila kinachosikitisha ni kwamba anaongea kama mbumbumbu, ameongelea suala la CHADEMA kutoa elimu bure sekondari mpaka elimu ya juu, inamaana nape hajui kuwa kwenye ilani kuna mikakati ya utekelezaji na inaenda kwa hatua, kwa mwaka 2011/2012 bajeti imeeleza kufuta ada kwa wanafunzi wa kike na kiasi cha asilimia 50 kwa wavulana, hajui bado hapo kuwa kungekuwa na miaka mingine minne ya kwenda hatua nyingine hatimaye kutekeleza sawasawa na ilani ya CHADEMA, kadhalika katika mambo mengine ambayo yeye ameyaona kama mapungufu.

Mbona nasikia baba yake huyu alikuwa mtu makini... huyu kilaza alipatikanaje ? anatia aibu
Labda................. anyway siri kubwa atakuwa nayo mama yake!
 
Nimesoma comments zenu, bahati nzuri wengi nawafahamu kwa majina yenu halisi kwahiyo sishangai sana kwa mliyotukana na kukejeli, nawashukuru. Kwa wale wanaotaka tujadili hoja karibuni.
Kwanza ni kweli kuwa CHADEMA hawako madarakani na kwamba bajeti yao inalenga kuonyesha maeneo ambayo serikali haikuyaona au hayakuwekwa sawa kwa faida ya nchi. Na ndo maana waliotulia na kusoma kituo kwa kituo watakumbuka nilianza wa kumpongeza Zitto kwa hotuba nzuri, na nikasema hata hivyo yako maswali machache ya kuyapitia.

1. SWALA LA ELIMU
Chadema haiko madarakani lakini kama walivyoshauri kwenye maswala ya madini, misamaha ya kodi nk NILITEGEMEA WASHAURI HIVYOHIVYO KWENYE IMANI YAO KATIKA ELIMU BURE,inawezekana kabisa kuishawishi serikali kutekeleza ushauri huo kwa faida ya Watanzania.. kwani yako mambo kadhaa ambayo najua yametokana na ushauri wa kambi ya upinzani.

2. SWALA LA VIFAA VYA UJENZI
Kama ilivyo kwa elimu bure na mengine nilitegemea Chadema waeleze wangefanyaje kuifikisha saruji mfuko tshs 5000.

Bahati nzuri mmoja amekiri hapa kuwa tatizo Nape tumetumwa kukutukana ndo maana hatutajadili hoja lakini tutakuporomoshea matusi yote, sishangai, mara zote mtu akiishiwa hoja huishia kutukana na akizidiwa hapo pia hupigana. Nitaendelea kuwa hapa JF kwani sikujiunga jana na bahati nzuri nafaidika na wanaoamua kujadili kwa hoja kuliko matusi, nimejifunza kutosoma matusi na kejeli badala yake nawaachia wanaotaka kusoma, lakini tutajadili hoja kwa wanaotaka.

Wanaodhani nimekurupuka wana haki pia kwasababu si busara kumfanya mtu afikiri utakavyo. Kwa wale walikuwa sobber nawashukuru sana kwa comments zenu. Uzalendo kwa nchi unapaswa kuzidi ule wa chama.
Nashukuru umejitoeza mwenyewe na kujaribu kujibu michango yote iliyotolewa. Wwengine tulikuwa kuchangia kuhusu hoja yako lakini tukakuta wengine wameshachangia pia. Ila ushauri wangu wa ziada tofauti na hoja hii ya bajeti ni kwamba ebu jaribu kutumia busara na kuwa mvumilivu kuliko kuwa unakurupuka na kuanza kujibu kila kinachosemwa kuhusu chama chako. Kuwa msemaji wa chama au mwenezi haimaanishi utajibu chochote kitakachosemwa kokote kuhusu chama chako.
Mimi nadhani walikupa nafasi hiyo sio kwa sababu ni msemaji mzuri ila sababu ni kijana hivyo utaweza kuwashawishi vijana wengi zaidi kujiunga nanyi, ila umeshindwa kulifahamu hilo sababu hoja nyingi unazozitoa kwa vijana wa enzi hizi haziwaingi akilini hata kidogo sababu hazina mashiko na wanahisi wewe ni sawa na wale wazee waliokusukumia huo msala maana unabisha wakati mwingine bila kutoa sababu kisa yametoka kwenye kinywa cha mpinzani wako.
Mimi nikushauri iba busara za katibu wenu wa sasa Bw. Mkama maana amekuwa sio mtu wa kukurupukia hoja km yule Mzee Makamba. Pia jitahidi kusoma zaidi ili kuogeza uelewa wa mambo mengi zaidi na sio kila kitu unadhani ni siasa kama ulivyofanya kwenye suala hili la bajeti kivuli hoja zako ni za kisiasa tupu hakuna uchambuzi wakisomi hata kidogo wakati wewe ni graduate bwana. Kwa leo ni hayo tu na niwie radhi kama nitakuwa nimekukwaza na wala usijenge chuki ni mtazamo tu.
 
Wakuu wa mikoa, maDC ma katibu tawala na ghrarama zoa zoote zingeondoka! Ni mambo mengi ya kumfumo waliyokuwa wameahidi chadema...lkn jamani, kweli huyu Nape kaamua kuwa juha kiasi hiki! Au nae kaana kuwadharau wa Tz anadhani hawawezi kuchambua mambo!

Heshima yako!! Ujuha wangu ni upi? Nilichouliza kwanini haukuwekwa kwenye bajeti huo mchanganuo? Pengine tujipe muda kuona wenzetu wanafanyaje kwenye bajeti za kambi ya upinzani bungeni. Kaangalie Labour Party pale uingereza, lakini hata rafiki zenu wa chama cha Cons.ya uk wakiwa kambi ya upinzani bajeti zao zilikuaje? Nadhani si swala la ujuha wa Nape bali ukweli unauma..
 
who is nape in this country???

Tunaweza kumdefine kama
1)Anayetumiwa na wajanja
2)Ajui analolifanya
3)Mtu mwenye sifa na asiyejua ni kitu gani anakifanya

Akishakaaga na wajinga wenzake basi anaakuja kutuletea shobo
 
mtu wa ajabu sana anajadiri mshahara wa milioni 7 wa slaa na kuacha TRLIONI 2.4 zilizoibiwa kwenye budget ya mwaka jana
lakini tusishangae ungetegemea aseme nini anyway ndio matatizo ya degree za INDIA hayo.
 
Nashukuru umejitoeza mwenyewe na kujaribu kujibu michango yote iliyotolewa. Wwengine tulikuwa kuchangia kuhusu hoja yako lakini tukakuta wengine wameshachangia pia. Ila ushauri wangu wa ziada tofauti na hoja hii ya bajeti ni kwamba ebu jaribu kutumia busara na kuwa mvumilivu kuliko kuwa unakurupuka na kuanza kujibu kila kinachosemwa kuhusu chama chako. Kuwa msemaji wa chama au mwenezi haimaanishi utajibu chochote kitakachosemwa kokote kuhusu chama chako.
Mimi nadhani walikupa nafasi hiyo sio kwa sababu ni msemaji mzuri ila sababu ni kijana hivyo utaweza kuwashawishi vijana wengi zaidi kujiunga nanyi, ila umeshindwa kulifahamu hilo sababu hoja nyingi unazozitoa kwa vijana wa enzi hizi haziwaingi akilini hata kidogo sababu hazina mashiko na wanahisi wewe ni sawa na wale wazee waliokusukumia huo msala maana unabisha wakati mwingine bila kutoa sababu kisa yametoka kwenye kinywa cha mpinzani wako.
Mimi nikushauri iba busara za katibu wenu wa sasa Bw. Mkama maana amekuwa sio mtu wa kukurupukia hoja km yule Mzee Makamba. Pia jitahidi kusoma zaidi ili kuogeza uelewa wa mambo mengi zaidi na sio kila kitu unadhani ni siasa kama ulivyofanya kwenye suala hili la bajeti kivuli hoja zako ni za kisiasa tupu hakuna uchambuzi wakisomi hata kidogo wakati wewe ni graduate bwana. Kwa leo ni hayo tu na niwie radhi kama nitakuwa nimekukwaza na wala usijenge chuki ni mtazamo tu.

Mwanakwetu, kwanzan nakushukuru sana kwa ushauri mzuri. Lakini pengine nadhani watu hawakuzoea kuona chama kikijibu mambo mbalimbali yanayotokea nchini, jambo ambalo nadhani halikuwa zuri sana kwa chama. Na si kweli kwamba najibu kila kitu hapana, yako mengi sana nakaa kimya nayaangalia tu, mengi sana so wanaposema najibu kila kitu si kweli hata kidogo....Mfano unakumbuka walisema CCM imepeleka visu kwenye mkutano wa BAVICHA nilipuuza kwasababu ulikuwa upuuzi. Kwa hili la bajeti nilidhani watu wangeamua tukajadili bila ushabiki unaendelezwa hapa tungefikia kuwa na constructive op.nchini na hasa bungeni.
Sikukurupuka hata kidogo, nimemsikiliza waziri kivuli, nimesoma hotuba yake kabla na kwakweli nilitegemea waje na baadhi ya mambo waliyoyaainisha kwenye ahadi zao kama cama ambayo yangekuwa mbadala wa yaliyopo. Na kwakweli nilitegemea yangewajenga hata wao. Hili la kufanya mambo mengine nafanya mengi sana na ndo maana kwasasa niko full time ofisini si kama zamani huku ilikuwa kama part time job....
Lakini naheshimu sana ushauri wako na nitaufanyia kazi.
 
Ndio degree za India hizo mkuu usishangae.

Kwenye hilo sio kweli, sema labda ndio tatizo la kujihusisha na magamba! Kuna vichwa hatari vya Mzumbe na Ilboru vilikuwa chuo alichosoma huyu gambaboy! Nadhani hapa tatizo ni kuchakachuliwa na mawazo mgando ya magamba wenzie.
 
Nimesoma comments zenu, bahati nzuri wengi nawafahamu kwa majina yenu halisi kwahiyo sishangai sana kwa mliyotukana na kukejeli, nawashukuru. Kwa wale wanaotaka tujadili hoja karibuni.
Kwanza ni kweli kuwa CHADEMA hawako madarakani na kwamba bajeti yao inalenga kuonyesha maeneo ambayo serikali haikuyaona au hayakuwekwa sawa kwa faida ya nchi. Na ndo maana waliotulia na kusoma kituo kwa kituo watakumbuka nilianza wa kumpongeza Zitto kwa hotuba nzuri, na nikasema hata hivyo yako maswali machache ya kuyapitia.

1. SWALA LA ELIMU
Chadema haiko madarakani lakini kama walivyoshauri kwenye maswala ya madini, misamaha ya kodi nk NILITEGEMEA WASHAURI HIVYOHIVYO KWENYE IMANI YAO KATIKA ELIMU BURE,inawezekana kabisa kuishawishi serikali kutekeleza ushauri huo kwa faida ya Watanzania.. kwani yako mambo kadhaa ambayo najua yametokana na ushauri wa kambi ya upinzani.

2. SWALA LA VIFAA VYA UJENZI
Kama ilivyo kwa elimu bure na mengine nilitegemea Chadema waeleze wangefanyaje kuifikisha saruji mfuko tshs 5000.

Bahati nzuri mmoja amekiri hapa kuwa tatizo Nape tumetumwa kukutukana ndo maana hatutajadili hoja lakini tutakuporomoshea matusi yote, sishangai, mara zote mtu akiishiwa hoja huishia kutukana na akizidiwa hapo pia hupigana. Nitaendelea kuwa hapa JF kwani sikujiunga jana na bahati nzuri nafaidika na wanaoamua kujadili kwa hoja kuliko matusi, nimejifunza kutosoma matusi na kejeli badala yake nawaachia wanaotaka kusoma, lakini tutajadili hoja kwa wanaotaka.

Wanaodhani nimekurupuka wana haki pia kwasababu si busara kumfanya mtu afikiri utakavyo. Kwa wale walikuwa sobber nawashukuru sana kwa comments zenu. Uzalendo kwa nchi unapaswa kuzidi ule wa chama.

Kama una imani kuwa hukukurupuka, basi kuna tatizo kubwa katika uwezo wako wa kuchambua mambo. Nilikuwa nakushabikia sana lakini matamshi yako tangu ushike hatamu ya CCM yamekuwa yananikatisha tamaa sana. Umekuwa kama mpinzani wa Chadema badala ya kuwa mjenga hoja wa CCM inayotawala. Ni jukumu la wapinzani kupinga lile linalotolewa na watawala, na ni kazi ya watawala kufafanua yale yanayopingwa na wapinzani. Hiyo ni kwa sababu mwelekeo wa nchi unategemea sera za watawala siyo sera za wapinzani. Lakini badala yake umekuwa na porojo nyingi sana kuhusu CHADEMA. Elewa kuwa hataka kama CHADEMA wanakukosesha usingizi, ni lazima uwe na namna nzuri ya kukabiliana nao bila kugeuka kuwa mpinzani wao.

Wapinzani hawakuwauliza CCM kwa nini hawakuweka zile ahadi za Kikwete kwenye bajeti bali walichambua ile bajeti mliyotoa na kuwapa mbadala wake. Sasa wewe badala ya kujibu mapungufu ya ile bajeti ile mbadala, unauliza ahadi za CHADEMA za uchaguzi; hiyo busara gani ati. Ndiyo maana nina-question sana uwezo wako kiakili. Ulipoanza kugombea huko CCM ukitokea India, uliandika maneno yasiyokuwa na mpangilio kwenye blogu ya michuzi, nikakuambia kuwa kama unataka siasa jijenge kuwa na mantiki kwa unayoandika, naona hujafanya hivyo.

Sheria za kazi Tanzania zinamruhusu kila mwajiri na mwajiriwa kupanga namna ya kulipana ujira mradi hawavunji sheria; sheria hizo hazizuii mtu kufanya kazi kwa kujitolea, na vile vile hazizuii mwajiri kumlipa mwajiliwa posho. Mpaka sasa sheria za nchi zinasema kuwa posho haikaatwi kodi. Mtu anayefanya kwa kulipwa posho tu huwa halipwi kiinua mgongo anapoacha kazi, kwani anafanya kwa kujitolea. Kama Dr. Slaa amejitolea kuitumikia CDAM bila malipo, halafu CDM ikajitolea kumpa posho, basi hayo ni makubaliano ya CDM na Dr. Slaa; hawajavunja sheria yoyote ya nchi. Wewe kama kiongozi unakuwa mpuuzi kukomalia jambo ambalo ni sahihi kisheria na wala halihusu nchi, bali linawahusu wanaCHADEMA peke yao. Ukitaka alipe kodi basi lazimisha kuwepo sheria ya kulipa kodi kwa posho zote nchini. Kwa nini usiongelee viongozi mbalimbali serikalini ambao hawalipi kodi pamoja na kuwa wana mishahara minono pamoja na posho mbalimbali ukiachia mbali kuwa watapata viinua mgongo wanapoacha kazi. kwa mfano, rais, majaji, nadhani na wabunge.
 
Ukwel upi Nape?hujaelewa nn? embu acha uvivu na soma bajet ya upinzan vizur na taratibu utapata majibu ya maswal yako yote ..tatizo unakariri afu umepania sana..
 
Ningekuwa mwalimu wako nimekupa kazi kufanya riview ya bajeti kivuli na kutoa maoni yako ningekupa ziro kwani ulichofanya hapo ni inconsistency and irrelevant. Jifunze toka kwa Mnyika, Zitto na vijana wengine namna wanavyojibidisha kujifunza, kujisomea na kukubali changamoto. Kiri kwanza kwamba wewe ni kilaza na ndani ya chama chenu toka mwenyekiti hadi wanachama hamjisomei chochote, mathalani nikuombe linapokuja suala la msing kama hili acha kherehere cha propaganda za kijuha. From al the above comments i rate ur argument as a mere crap as wel as an alphabetical diaohrea and infact it dehydrates ur leadership dignity. Otherwise wait for a number of standing ovation toka kwa waosha vinywa wako ulowatuma hapa kuzoa uharo wako kila unapochafua Mr. Nape sir.
 
Heshima yako!! Ujuha wangu ni upi? Nilichouliza kwanini haukuwekwa kwenye bajeti huo mchanganuo? Pengine tujipe muda kuona wenzetu wanafanyaje kwenye bajeti za kambi ya upinzani bungeni. Kaangalie Labour Party pale uingereza, lakini hata rafiki zenu wa chama cha Cons.ya uk wakiwa kambi ya upinzani bajeti zao zilikuaje? Nadhani si swala la ujuha wa Nape bali ukweli unauma..
Nape unazidi kujidhihirisha udhaifu wako kwa kiasi kikubwa...Wewe huwezi kutaka chadema waige labour party pale uingereza wakati wewe mwenye kutawala na ccm yako hamfikii hata robo ya robo ya conservative!Hivi chama tawala uingereza kinaweza kuwa na bajeti ya maendeleo yao inayotegemea wahisani kwa asilimia tisini?Au niseme hivi, hiyo uingereza uliyochukulia mfano chama chako mmeiga nini kizuri toka huko? Ufisadi, kuwaogopa mafisadi,kagoda,deepgreen finance ambayo mtoto wa raisi ameshiriki kukwapua!Usipokuwa makini hta watoto watakuona Juha yaani watakudhrau mno! Watanzania waleo huwezi kuwapiga sanaa wasikushtukie, angalia mwenyekiti wako anavyorarauliwa hata na watoto! Hii ndio inaelekea kukupata..Tafakari...
 
ningekuwa mwalimu wako nimekupa kazi kufanya riview ya bajeti kivuli na kutoa maoni yako ningekupa ziro kwani ulichofanya hapo ni inconsistency and irrelevant. Jifunze toka kwa mnyika, zitto na vijana wengine namna wanavyojibidisha kujifunza, kujisomea na kukubali changamoto. Kiri kwanza kwamba wewe ni kilaza na ndani ya chama chenu toka mwenyekiti hadi wanachama hamjisomei chochote, mathalani nikuombe linapokuja suala la msing kama hili acha kherehere cha propaganda za kijuha. From al the above comments i rate ur argument as a mere crap as wel as an alphabetical diaohrea and infact it dehydrates ur leadership dignity. Otherwise wait for a number of standing ovation toka kwa waosha vinywa wako ulowatuma hapa kuzoa uharo wako kila unapochafua mr. Nape sir.

bukanga ningekuwa na sifa kama uzisemazo usingehangaika mpaka saa hizi kunijibu humu...karibu sana mdogo wangu
 
Ningekuona mstaarabu kama ungeelezea kwa undani mambo yanayopingwa toka ktk bajeti yenu ambayo itapita(kwa 7bu ya upumbavu wa wabunge wa Ccm)maana wao ni ndiyo mzee,kuliko kupinga bajeti ambayo haitapita,na hata ingekuwa na mazuri hamwezi kuchukua(kwa ujinga wenu)tetea hoja za chama chako achana na Cdm,au una maumivu ya kunyimwa kugombea Ubungo?
 
Back
Top Bottom