Nape: Bajeti Mbadala ya Kambi ya Upinzani inadhihirisha uongo wa CHADEMA

Mi nachukia sana hivyo ndg zangu! hashuriki huyu Nepi ameshakunywa maji ya Rangi ya kijani na njano.
 
Nape umidhihirisha kweli huna uwezo wa kuwa katibu mwenezi wa chama chako (ccm). Na kama kweli walikuchagua kutokana na uwezo wako katika nafasi hiyo,basi sichelewi kusema chama chako si makini na wote humo ni mambumbumbu. Nayasema haya kwa masikitiko makubwa sana kwani naumia kuona chama makini kama hicho (CCM) enzi za mwalimu,chama kilichokuwa miongoni mwa vyama BORA barani Afrika enzi za mwalimu kimefikia mahala kina fikra mtindi kama zako naumia sana.

Nape kwa fikra hizo hufai kuwa hata kiranja wa darasa la pili. Nasema hivi si kwasababu ya ushabiki wa kisiasa bali nikutokana na upeo wako mdogo katika fuatilia Mambo ya msingi. Naumia zaidi unavyotumia ujinga wa wananchi kupotosha jamii.

Nijikite sasa katika hoja zako za uongo wa chadema kama ulivyodai katika waraka wako,japo naona aibu kukujibu kiongozi kama wewe wa nafasi kubwa kama yako. Sioni aibu kwasababu najiona ni mdogo (kicheo) kwako bali najiuliza umepewaje nafasi hiyo kwa akili hiyo?


Utekelezaji wa ilani ya chadema ni matokeo ya mabadiliko mengi ya kisera kama katika ukusanyaji wa mapato ya serikali kama; ubinafsishaji wa mali za mafisadi, kuondoa misamaha ya kodi kwa makampuni makubwa, kuandaa mikakati endelevu ya kuwawezesha vijana kujiajiri na hatima kuinua uchumi wenye tija kwa wananchi wote hivyo kuchangia pato la taifa kwa kiasi kikubwa , na kupitia mikataba yote ya madini na kudhibiti uchimbaji na usafirishaji wa kiolela wa madini ya nchi yetu (ikumbukwe nchi yetu ni miongoni mwa nchi zilizo na madini mengi Duniani).

UFAFANUZI:
Hivyo ndio kusema bajeti ya zito ilisadifu mazingira yaliyopo kwamba serikali iliyopo madarakani kwa sera zile zlile. Kama kupitia serikali hii ingewezekana kutimiza ilani ya CHADEMA kusingekuwa na umuhimu wa CHADEMA kutaka kushika nchi. Kwa sera hizi za CCM hatuwezi kupata mapato ya utekelezaji wa ilani ya CHADEMA kama ulivyotaka NAPE. Nape kumbuka CHADEMA wanatoa mbadala wa Bajeti kwa kuzingatia mifumo iliyopo (every things remain constant) yaani chini ya uongozi wa CCM. Ukitaka kuyaona ya ilani ya CHADEMA yanatekelezwa subiri washike nchi mwaka 2015.

Nape unachokisema ni sawa na kufananisha mimba na kitambi, kumbuka vinafanana tu!. Ni wazi utambue kuwa kila hitaji lina mikakati yake. Na maanisha ilani ya CHADEMA itatimia tu ikiwa Serikili pia itakuwa ni ya kwao,hivyo ni kusema wangebadilisha mambo mengi ambayo yangetoa zao la utekelezaji wa ILANI yao. Nape CCJ unahamia lini? Au mmemuuza mwenzenu MPENDAZOE?
 
Msameheni nape jamani hana chakufanya anachoona kuwa mpira umewaelemea ivyo bora liende tu we unafikil ad upewe cheo cha nape ndan ya ccm unatakiwa uwe na sifa zipi moja ni iyo uropokaji makamba afadhari nape ni potelea mbali anatetemeka akimuona doctor waukweliiiiii
 
Nyie hapo juu ni wehu kweli! Badala ya kujadili content ya alichokiainisha ninyi mna attack personality ya Nape. Hebu acheni unazi kidogo jadilini alivyoviandika hivi kati yenu ninyi mnaojidai mnabongo kubwa nani kaviona ambavyo Nape kaviona? Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Katika hili ameyaona mengi ambayo wengi hamja yaona. Kukiri mapungu siyo ujinga.
 
kabla sijamaliza kusoma tayari umedanganya chadema haikusema itatoa elimu bure hadi chuo kikuu, ilisema hadi kidato cha sita. labda hiyo ni ile ahadi ya CCJ yako.

Ushindwe na ulegee mfululizo
BAJETI MBADALA YA KAMBI YA UPINZANI NI UTHIBITISHO WA UONGO WA CHADEMA


1.0 UTANGULIZI:

Leo tarehe 15/06/2011 kambi ya upinzani bungeni ambayo inaundwa na chama cha CHADEMA kupitia waziri wake kivuli wa fedha Mhe. Zitto Kabwe (Mb), imewasilisha bajeti yake aliyoiita bajeti mbadala kwa mwaka wa fedha 2011/2012.

Nichukue nafasi hii kumpongeza kijana mwenzangu kwa uwasilishaji wa bajeti na kwa baadhi ya mambo ya msingi yaliyomo ndani ya bajeti husika.Hata hivyo bajeti imeacha maswali kadhaa bila majibu.

Katika bajeti hiyo pamoja na mambo mengine kwa kiasi kikubwa imedhihirisha kuwa maneno mengi na ahadi nyingi zilizotolewa na CHADEMA wakati wa Uchaguzi kama sio zote basi nyingi zilikuwa ahadi hewa zilizolenga kuwa hadaa wapiga kura kwa nia ya kupata kura.

2.0 MANTIKI YA HOJA:

Moja kati ya misingi mikuu ya kutengeneza bajeti katika mazingira ya siasa za kwetu na nyingine nyingi duniani ni ahadi ambazo chama kimeahidi kwa Wananchi wake aidha kwa kupitia Ilani ya Uchaguzi au ahadi binafsi za Mgombea Uraisi alizozitoa kipindi cha kampeni ya uchaguzi. Kwa maneno mengine bajeti ni zao la Ilani ya Uchaguzi ya Chama husika na sera mbalimbali zilizopo.

2.1 Elimu Bure kwa Watanzania kwa ngazi zote;

Kwa mfano kupitia Ilani ya CHADEMA ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na ahadi kibao za kila mara za aliyekua mgombea urais wa chama hicho Dr. Slaa, waliahidi wakichaguliwa watatoa elimu bure kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu.

Itakumbukwa hii ni moja ya ahadi zilizovutia sana wakati huo, lakini huku wakijua kuwa wanadanganya waliendelea kutoa ahadi hiyo kwa muda wote wa kampeni hizo, sasa imefika wakati tulitegemea wangeonyesha kwa vitendo kwa kuweka kwenye bajeti yao jinsi wanavyoweza kutoa elimu bure lakini bajeti hii mbadala ya 2011/2012 ni uthibitisho wa hadaa ya CHADEMA kwa umma wa watanzania.

Hapa namnukuu Waziri kivuli wa fedha,
“..(ix)kuondoa ada kwa wanafunzi wa shule za sekondari za kutwa na kupunguza ada kwa sekondari za bweni kwa kiwango cha asilimia hamsini kwa wavulana na bure kwa wasichana...”

Lakini katika Ilani yao ya Uchaguzi ya mwaka 2010 ukurasa wa 15. Inaeleza CHADEMA itahakikisha “ Elimu ya ngazi ya msingi na sekondari itagharimiwa na serikali kuu pamoja na serikali za mitaa”.
Hapo ndipo tunapouona uongo dhahiri wa CHADEMA wa kukiri kuwa Serikali haiwezi ikatoa Elimu bure kwani katika Bajeti yao mbadala wanakiri kuwa watapunguza ada kwa asilimia hamsini kwa wavulana.

Kwa mantiki hiyo suala la wanafunzi wa sekondari kuchangia wanalikubali ila walitumia ghiliba kipindi cha kampeni ili kuwaongopea Watanzania kwa kitu ambacho hawawezi kukitekeleza.

Kinachosikitisha zaidi, kwenye bajeti hii mbadala iliyosomwa leo, inaonyesha dhahiri kwa upande wa elimu; hakuna mpango wowote unaozungumzia “Elimu ya Juu” kama vile si kitu kwao ukilinganisha na walivyokuwa wakihubiri kwenye majukwaa wakati wakitafuta kura. Hakika huu ni usanii mkubwa kumbe walikuwa wakitafuta kura za vijana hawa tu hawana mpango nao!!

2.2 Kushusha bei ya vifaa vya ujenzi;

Ahadi nyingine kubwa iliyovuta hisia za wengi ni ya kushusha bei ya mfuko wa saruji kufikia shilingi za kitanzania elfu tano, pamoja na vifaa vingine vya ujenzi. Kwenye bajeti hii mbadala tulitegemea wangewaeleza watanzania hili wangelifanyaje lakini badala yake waziri kivuli wa fedha anaishia kusema;
“..itakuwa marufuku kwa kituo cha uwekezaji kutoa ruhusa ya msamaha wa kodi kwa makampuni ya uwekezaji kwa bidhaa zinazozalishwa nchini na hasa Saruji....”

Hapa hakuna mkakati wowote wa kufanya mfuko wa saruji uuzwe shilingi za kitanzania elfu tano kama CHADEMA walivyotaka watanzania waamini wakati wa uchaguzi. Huu ni ushahidi wa hadaa ya CHADEMA.

Kwenye bajeti hii mbadala waziri kivuli anasema.... “ujenzi wa barabara za vijijni utatumia kwa kiasi kikubwa nguvu kazi watu (labour intensive)..”

Viongozi wengi wa CHADEMA wanasifika kwa kuzuia wananchi wasichangie shughuli mbalimbali za maendeleo huko vijijini, leo inashangaza kusema watatumia kwa kiasi kikubwa nguvu kazi watu, huu bila shaka ni unafiki na hadaa kwa wananchi.

2.3 Suala la kukwepa kodi;

Umejengeka utamaduni wa watu na taasisi mbalimbali kukwepa kodi na kuona kuwa suala hilo ni la kawaida. Lakini ikumbukwe kuwa kukwepa kodi kunaipunguzia mapato serikali na hivyo kupunguza uwezo wake wa kutoa huduma kwa jamii.

CHADEMA wanakiri hili kupitia Bajeti yao mabadala iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha Kivuli Mhe. Zitto Kabwe, kuwa ......”kuna watu wengi sana ambao wanapata mapato makubwa lakini hawalipi kodi......” Kauli hii ya CHADEMA inapingana na matendo yao halisi, kwani itakumbukwa wanamlipa katibu Mkuu wao Dr. Wilbroad Slaa zaidi ya shilingi Milioni saba, fedha ambayo haikatwi kodi yeyote.

Chakushangaza zaidi pamoja na CHADEMA kuendelea kumlipa Dr. Slaa mamilioni yasiyotozwa kodi, bila aibu Zitto anatoa wito kwa kila Mtanzania mwenye kipato alipe kodi ya kipato chake.
Na anaendelea kusema kuwa ... “kulipa kodi ndio ishara ya Uzalendo na ili raia aweze kuinyoshea kidole serikali yake lazima awe na uchungu na uchungu unapatikana kwa kulipa kodi.”

Kwa kauli hii ya Zitto, anauthibitishia umma wa Tanzania kuwa Dr. Slaa siyo mzalendo na wala CHADEMA pia siyo wazalendo. Kwani Dr. Slaa alitakiwa kukataa kuchukua mshahara usiokatwa kodi, na Chama chake kilipaswa kupeleka kodi za watumishi wake serikalini.



2.4 Kima cha chini cha mshahara;

Katika bajeti yao mbadala, CHADEMA wanaahidi kuongeza kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wa Umma mpaka kufikia Tshs. 315,000 kwa mwezi na kutoa motisha kwa walimu wanaofundisha Vijijini kwa kuwapa Mshahara mara moja na nusu ya wenzao wanaofundisha mijini.
Cha kushangaza hawajaainisha fedha hizo za ziada watazitoa wapi, hata katika mchanganuo wao wa mapato hawajaonesha kuwa kiasi hicho cha pesa kitatoka wapi. Huu ni usanii mkubwa na uongo ulikithiri.


3.0 HITIMISHO:

Ukipitia mambo haya machache kama mifano utagundua kuwa sehemu kubwa ya ahadi za CHADEMA kwa wananchi ni ulaghai na uongo usio na mfano, hivyo wananchi wanapaswa kuutambua mti kwa matunda yake si majani yanayoonekana na kutamanisha machoni.

Ukiifahamu kweli itakuweka huru, ni muhimu kuitafuta na kuifahamu kweli.

Imetolewa na;

Nape Moses Nnauye,
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.
15.06.2011
 
Nape keep it up! hawajakuelewa ulipo hoji hizo pesa za kupandisha mishahara na elimu bure watazitoa wapi. Hata hao vibaraka wao wanao mtete ZItto hawajui kuwa hizo fedha za Posho za wabunge ambazo wamegoma kuzichukua wamesha zichukua na wanadaiwa. Wasitufanye sisi hatujui wasijidai wao malaika nawakati ni mashetani wanaotaka utukufu kwa kuwaongopewa watanzania.
 
Zitto kwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya mashirika ya umma aliweza kuiona bajeti ya mkulo mapema ndo akaja na chakachua yake. Hebu oneni haya aliyoyasema mkulo : Bajeti hii ni ya kubana matumizi ya Serikali.

Hatua za Kibajeti:
1. Kupunguza malipo ya posho zisizo za lazima;2. Kupunguza semina na warsha; 3.Kupunguza safari za ndani na nje ikiwa ni pamoja na ukubwa wa misafara; na 4. Kusitisha manunuzi ya magari ya Serikali.

Sasa nyie mazuzu mtuambie lipi hapo ambalo Zitto kajanalo ambalo ni jipya. Acheni ushabiki wa kijinga
 
Nyie hapo juu ni wehu kweli! Badala ya kujadili content ya alichokiainisha ninyi mna attack personality ya Nape. Hebu acheni unazi kidogo jadilini alivyoviandika hivi kati yenu ninyi mnaojidai mnabongo kubwa nani kaviona ambavyo Nape kaviona? Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Katika hili ameyaona mengi ambayo wengi hamja yaona. Kukiri mapungu siyo ujinga.

Hebu na wewe tudokezee, yapi hayo Nape kayaona ambayo sisi wengine hatuyaoni ? Sasa kama mjumbe wa sekretariat na katibu wa propaganda wa chama tawala, CCM, ni kati ya wanyonge wa nchi hii, huyo mwananchi wa kawaida yukoje. Achebe, kama wewe siye Nape mwenyewe na kama una akili timamu, kweli unaweza kunipa sababu ya Nape kuanzisha mjadala kuhusu mapungufu, kama yapo, ya ilani ya Chadema wakati huu ?

Kwanza Chadema haiko madarakani na nafikiri hoja ya Nape ni mbinu chafu na ya kijinga ya kutuondoa kwenye kuijadili bajeti kama ilivyosomwa na Mkulo. Kwa upeo wa watu kama Nape, si ajabu hata kidogo kukurupuka na hoja za hovyo kama hii na majibu anayoyapata humu JF ni halali yake kabisa, kayalilia na sasa acha apewe. Ukweli ni kwamba bajeti aliyosoma Mkulo ndio imedhihirisha uwongo wa Chama Cha Mafisadi, CCM.
 
Vituko vya mwaka wamekula pesa zote za seating allowance sasa wanasema hawazitaki. Hatuna matatizo na hoja yao, warudishe kwanza zile walizokopa hapo ndipo tutaona kweli wana nia njema na watanzania. Nje ya hapo hatutawamini hata chembe.
 
Vituko vya mwaka wamekula pesa zote za seating allowance sasa wanasema hawazitaki. Hatuna matatizo na hoja yao, warudishe kwanza zile walizokopa hapo ndipo tutaona kweli wana nia njema na watanzania. Nje ya hapo hatutawamini hata chembe.
Naona unawaza kwa kutumia makamasi ukiona kijana mpaka leo yupo CCM ujue alinyonya mbolooo ya baba yake akiwa mdogo
 
Naona unawaza kwa kutumia makamasi ukiona kijana mpaka leo yupo CCM ujue alinyonya mbolooo ya baba yake akiwa mdogo
wengine humu Dr. slaa ni bwana enu yaani basha wenu ndo maana hamsikii hamuoni pambafu....majifanya kujua kutukana na mnaangaliwa tu...******* wengine bwana
 
76176_171157302905691_100000342668655_450964_5070561_n.jpg
 
Mbona hamuulizi Mkulo amenunua meli ngapi katika bajet yake ama watajenga fly over ngapi kama mkuu alivyokua anatoa ahadi.
 
2.4 Kima cha chini cha mshahara;

Katika bajeti yao mbadala, CHADEMA wanaahidi kuongeza kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wa Umma mpaka kufikia Tshs. 315,000 kwa mwezi na kutoa motisha kwa walimu wanaofundisha Vijijini kwa kuwapa Mshahara mara moja na nusu ya wenzao wanaofundisha mijini.
Cha kushangaza hawajaainisha fedha hizo za ziada watazitoa wapi, hata katika mchanganuo wao wa mapato hawajaonesha kuwa kiasi hicho cha pesa kitatoka wapi. Huu ni usanii mkubwa na uongo ulikithiri.


Kwanza Nape unawamislead wasomaji Zitto amependekeza mishahara ya walimu vijijini iwe mara moja na robo na si nusu kama unavyosema , unaonekana si makini kabisa unarembesha ku mislead watu. CDM wamerekebisha ahadi zao kulingana na uwezo na akili za watendaji wa sasa, kwani wao wangeweza kabisa kutelekeza waliyoahidi ila wanajua uwezo wa CCM utaishia hapo. kwani mwalimu anapomfundisha mwanafunzi kujumlisha na kutoa kwanza, ina maana yeye hajui kugawanya, unampa mtu ushauri kulingana na level yake ya kufikiri kwani ukizidisha utamchanganya, hata ili limekuchenga Nape inaonekana wangesuggest vyote wanavyotaka kufamnya wao ndio mngefunga bunge kabisa! CDM sio level yako Nape!

 
Sifa moja ya upinzani ni kupingana kwa nguvu ya hoja na wala sio hoja za nguvu kama ambavyo "bila magamba" wanafanya. Kwa hivyo ninatarajia 1. Itawekwa hapa bajeti halisi ya upinzani kupinga maelezo ya uongo ya Nape.
2. Katika bajeti hiyo halisi kutaoneshwa kuwa yale yaliyokuwemo katika ilani ya uchaguzi na ahadi za CDM wakati wa kampeni ndio yale yale yaliyomo katika bajeti mbadala ya upinzani, hasa katika elimu na bei za vifaa vya ujenzi.
3. Ningependa kujua ikiwa viongozi wetu, wasio magamba na wa upinzani, wanalipa kodi kutoka mishahara yao au tunalipishwa kodi sisi ambao mishahara yetu ya mkia wa mbuzi. Hivi uzalendo na kukaza mkanda ni kwa mlala hoi tu?
 
kwelil unaweza kutema pumba, yaani kwa muda mfupi tu uliweza kupitia bajeti yote na kuitolea comment?
nafikiri wewe na baba yako kikwete mna akili zinazo fanana, ni kama vile yeye anavyotoa ahadi bila kufanyia

utafiti kamilifu
 
Back
Top Bottom