Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,305
33,924
Rais wa nchi anayetokana na CCM kuwa mwenyekiti wa CCM Taifa ni utamaduni tu ndani ya CCM na wala si takwa la kikatiba la chama hicho.

Kwa sasa Mwenyekiti wa CCM ni Samia Suluhu Hassan kutokana na mwana CCM huyo kuwa Rais wa Tanzania. Lakini kabla ya kuwa Rais, Samia alikuwa ni mjumbe tu wa Kamati Kuu ya CCM na sidhani kama asingekuwa Rais angeweza hata kupendekezwa kuwa Makamu wa mwenyekiti wa chama hicho.

Nape Nnauye ni mwanasiasa mzowefu ndani ya CCM na ni mwanasiasa maarufu kuliko wanasiasa wengi sana ndani ya CCM, na imani yake kwa chama hicho inazidi imani ya wanazi wengi tu walio kwenye madaraka ya juu CCM. Ni wakati sasa bila ya kujali tamaduni ya kumfanya Rais wa nchi kuwa mwenyekiti wa CCM, Nape awe Mwenyekiti wa Taifa CCM sasa

Nape amepambana sana kwa niaba ya CCM. Hata yale mambo ya goli la mkono kwenye chaguzi yeye ndiye muasisi wa falsafa hiyo.
 
Wewe unajua maana yake!?

Yaani Rais apoteze kiti chake KWA kuamua mwenyewe yaani kinana Ndio achukue kiti KWA kuachiwa!!

Acha KABISA Wewe!

Andiko kubwa sana hilo usirudie TENA!
 
Ndani ya CCM hakuna kiongozi bora kama Nape!!
Ikiwa kipimo chako angalau kwa awm6 ila awm5 alifeli mazima hata kufikia mahali awm5 ilimtema. Huamini kwenye baadhi ya zile sheria za mwendo kasi za habari alishiriki kikamilifu,na hata leo ni mzigo na mateso kwa taifa na wa Tanzania 🤔
 
Mzigo na mateso kwa watanzania ni CCM na ndiyo maana tunataka Nape awe mwenyekiti wake ili aibadilishe iwe na utu ndani mwake.
CCM na sheria za kulinda maslahi yao, wenyewe kamwe hawawezi kujipunguzia maslahi yao zaidi ya kutaka kujiongezea 🤔
 
Rais wa nchi anayetokana na CCM kuwa mwenyekiti wa CCM Taifa ni utamaduni tu ndani ya CCM na wala si takwa la kikatiba la chama hicho.

Kwa sasa Mwenyekiti wa CCM ni Samia Suluhu Hassan kutokana na mwana CCM huyo kuwa Rais wa Tanzania. Lakini kabla ya kuwa Rais, Samia alikuwa ni mjumbe tu wa Kamati Kuu ya CCM na sidhani kama asingekuwa Rais angeweza hata kupendekezwa kuwa Makamu wa mwenyekiti wa chama hicho.

Nape Nnauye ni mwanasiasa mzowefu ndani ya CCM na ni mwanasiasa maarufu kuliko wanasiasa wengi sana ndani ya CCM, na imani yake kwa chama hicho inazidi imani ya wanazi wengi tu walio kwenye madaraka ya juu CCM. Ni wakati sasa bila ya kujali tamaduni ya kumfanya Rais wa nchi kuwa mwenyekiti wa CCM, Nape awe Mwenyekiti wa Taifa CCM sasa

Nape amepambana sana kwa niaba ya CCM. Hata yale mambo ya goli la mkono kwenye chaguzi yeye ndiye muasisi wa falsafa hiyo.

Konde gang mnataka kuipiku sukuma gang
 
Una kichwa cha panzi! Unafikiri CCM ni utumbo utumbo kama mawazo yako!
Jipe nafasi ya kujifunza! Nape ni mwasiasa ndiyo lakini siyo wa kuwa Mwenyekiti wa CCM.
 
Back
Top Bottom