Asante Michelle, sasa unaiona hio red hapo, kwa jinsi nilivyoona mimi ndicho kinachochangia huyu baba anakuwa karibu zaidi na huyo bi mdogo. Kuhusu kusoma na ujasiriamali wa huyu mother house nimejikuta namtupia lawama huyu baba, kwa sababu, hakumpa ushirikiano katika hilo nafikiri. Manake baba ni mkali, ni ile staili ya Shikamoo baba kumbe mume wako!!
Mwisho: Unamshauri nini huyu mama mwenye nyumba, ili aweze kuishi kwa furaha na amani katika ndoa yake?
Yaani kabla hata hujaufunga mlango wa kutokea kwenda huko unakokwenda SIKUBALIANI KABISA NA HILI Eti BABA AMEKOSEA!!
Hakukosea hata kidogo na nadhani alimpenda kwa dhati na kama alivyosema LD ni watu wazima na ndoa nyingi za wazee wetu ziko hivyo Baba ni msomi kuliko Mama. Kosa alilolifanya Mbaba huyu ni kutegemea maisha yake na maendeleo yake yaongozwe na nyumba ndogo badala ya kumwendeleza mkewe na kumpa ujuzi wa kuendesha maisha kwa pamoja ye anaendagawa ugali nje??
Kabla sijatoa sababu
Natoa msimamo wa babu,
Lakini isiwe bawabu,
La kuficha majawabu;
Msimamo wa babu:
Mzee hakukosea kuoa huyo anayeitwa mama mwenye nyumba
Na hakukosea pia kuwa na huyo anayeitwa mpango wa nje.
Ntarudi kufafanua kama hamjanielewa.
Pole but asikate tamaa si wanasema elimu haina mwisho?? kama bado ana nguvu ajienroll hata kwenye vikozi vya biashara na kisha ajichanganye. Kudispair hakutatui tatizo kunaongeza matatizo .....madepression, mapresha na mwishowe stroke.Hata mimi nimejikuta namlaumu huyu baba zaidi MJ1, halafu fikuiria na uzee huu,
mtu anajikatia tamaa, mpaka house girl anamdharau.
Anaishia kuona bora akae peke yake tu bila house girl.
Na mikazi ya nyumbani inavyochosha.
Wewe ulitaka aende kwa mpango wa kando asiye hata na akili aje kuchukua hata kidogo walichonacho hapo ndani na washindwe kuishi vizuri na familia?unajua hata kama kitu hakikubaliki,we should learn to see the good side of it....usiangalie ubaya tu wa huo mpango wa kando.....
Haiwezekani baba amfungulie mwanamke biashara ashindwe kumpa training ya kuchangamsha akili yake?huo mtaji wa biashara ni zaidi ya hiyo elimu......mwanamme mkali nini bwana,hajui tu kumpunguza makali huyo mama....mumeo mfanye rafiki,lakin unapompa status ya baba na yeye atakuwa baba......huyo mama angetaka shule angekuwa ashasoma kitambo......
Teamo c'mon baana hebu tugaie busara zako .......you always have the talent of seeing what most of us fail to see in the first glance of the thread.i hereby rest my case.....!
upinzani ni mkali zaidi by the look
Sina budi tabaruku, ushauri wako Babu
Mkewe alimtunuku, kumfanya mahabubu
Na mpango kachunuku, nyumbani uwe bawabu
Kosa lilofanya Baba, Mkewe kumdharau
Wajua Babu ni kweli baba huyu hakufanya makosa kumwoa mkewe na (kama unavyosema kwa mtazamo wako) hakufanya makosa kuwa na mpango wa kando kwani umemletea manufaa (I hope hii ingekuwa tofauti iwapo Mpango huu ungekuwa ni ule wa hasara zaidi). Hagombwi kwa kuwa na mpango huo na pengine tumpongeze kwa kuweza kuwa makini na kuchagua mpango wa kando ulio bora (I guess na wetu wangekuwa na uwezo huo wala sie tusingepiga kelele loh). Angewezafanya moja kati ya yafuatayo
1. Kuamua kumtumia mpango wa nje (kwa akili kwa ajili ya maendeleo yake na familia kwa ujumla) Bila kumnyanyasa m,kewe na kumfanya akajua kuwa kuna small dogodogo anamsaidia au
2. Angechukua maujuzi ya mpango wa kando akaminduce mkewe ili hata baadae ikitokea la kutokea basi familia isitetereke.
Lakini pia tujiulize walikotokea na mpango wa nje huo..... isijekuwa umeegemea kwenye mhimili wa TRUE LOVE kiasi kwamba mpango wa kando uko genuine loh.
LD kabla sijamalizia hii insha ya msimamo wangu naomba kukuuliza:
Mama Mwenye nyumba anajua mzee ana mpango wa nje?
mama mwenye nyumba anajua kama mpango wa nje una mtoto?
Kama majibu ni ndio na mama ameridhia.....
Baba hajakosea kuwa na mpango wa nje........Thread Klozd!
Kama majibu ni hapana....
Baba anakaribia kukosea kuwa na mpango wa nje, japokuwa atakuwa bado hajakosea.
LD kabla sijamalizia hii insha ya msimamo wangu naomba kukuuliza:
Mama Mwenye nyumba anajua mzee ana mpango wa nje?
mama mwenye nyumba anajua kama mpango wa nje una mtoto?
Kama majibu ni ndio na mama ameridhia.....
Baba hajakosea kuwa na mpango wa nje........Thread Klozd!
Kama majibu ni hapana....
Baba anakaribia kukosea kuwa na mpango wa nje, japokuwa atakuwa bado hajakosea.