Naombeni msaada wapendwa!!!!!

Asante babu yangu,
Lakini sasa babu, mbona akili yangu inakataa kuamini kwamba wanaume wote lazima watoke nje ya ndo?
Kwani wanaume hawafuati sheria na amri za Mungu?
Elodiii hebu msome babu hapa chini nadhani ameshalijibu hilo

Huu ni msimamo wa babu na hauusiani na imani ya dini yoyote ya dini wala mashirika ya kutetea jinsia za watu!
 
Hao wanaozihubiri Amri za Mungu, hao mnaokwenda kwao kutubu dhambi zenu na kurudishwa sijui kundini......nawazungumzia hao hao.....ni waasherati na wazinzi wakubwa tena wazoefu!

LD kubali usikubali lakini ukweli ndio huu: Sisi waname haturidhishwi na wala hatukuumbwa kwa ajili ya mwanamke mmoja.... Na hilo si kwa binadamu tu; Angalia majogoo, mabeberu, simba, fisi, na wanyama kribia wote.

Kufuata Sheria Za Mungu huwa tunazifuata kinafiki!

Babu naona unataka kujihalalishia kutembea nje ya ndoa
 
Msimamo wa babu ambao ndio hali halisi na ukweli ni huu:

Mwanaume hajawahi na wala hatakaa aridhishwe na mwanamke mmoja
Mwanaume hajaumbwa kwa ajili ya mwanamke mmoja.

Mama mwenye nyumba hana alichokosea....hata angekuwa na upeo sawa na mumwewe, ameenda shule kama mumewe, angekuwa mjasiriamali mzuri, mzuri kama Cleopatra....bado jamaa angetoka nje.....(mwanaume haridhiki kuwa na mwanamke mmoja, msisahau)

Baba kuwa na mpango wa nje pia hajakosea.....kwa kuwa hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke mmoja.

Alichokosea huyu bwana:
Kuzaa nje ya ndoa....kama mkewe hana shida ya uzazi kilichompeleka kutotoa huko nje ni nini?
Kumdharau mke wake.....Ameshindwa nini kufanya mpango wa nje kwa siri?
Kuuachia mpango wa nje kuendesha biashara zake....Likiingia limbwata hapo, au mzee akaRIP ghafla vilio vya watoto wake wa mpango wa ndani vitamlilia mpaka jehanamu atakapokuwa.

mmmmmhhhhhhhhh,yatosha kwa leo.....
 
i have a feeling kuwa wewe wahusika na hiyo nyumba ndogo kw anamna moja au nyingine.... stay away from ndoa ya watu...HAYAKUHUSU!
 
Lakini babuuuuuuuuuuuuuu!!!!
Daaaaaa ngumu kumeza lakini........................daaaaa inatuuma sana sisi wanawake nadhani babu.
Kweli hapo pamekaaa je jamani.............hiiiiiiiiiiiii!!!!!
 
mmmmmhhhhhhhhh,yatosha kwa leo.....

Michelle darling...

habari ndio hiyo......nyie jidanganyeni tu na mjipe moyo lakini huo ndio ukweli wenyewe.

Tunachojitahidi sisi wastaarab ni kuhakikisha hamjui na hivyo mnajifariji mko peke yenu.......Laiti kuta zingekuwa zinaongea, mngeambiwa mengi sana!
 
Salamu kwenu nyote Mabibi na Mabwana, natumaini mko Salama kabisa.

Kuna jambo moja nimeliona likanipa maswali mengi, halafu nikawa sipati majibu mazuri.

Kuna ndoa moja ya mume moja na mke mmoja wote Wakristo. Sio ndoa changa wanandoa ni watu wazima kabisa. Kwenye miaka ya 50's hivi.

Baba ana elimu kubwa ni mfanyakazi na mfanya biashara pia.
Mama/mke wake wa ndoa ni mama wa nyumbani, hakubahatika kupata Elimu ya juu, tuseme ana Elimu ya msingi.

Baba huyu ana mpango wa kando (Mke mwingine nje ya ndoa) na amezaa naye mtoto mmoja. Kilichonipa maswali sasa ni kwamba huu mpango wa nje walau umeenda shule, unajua mambo hasa yahusuyo biashara na maisha kwa ujumla.

Huyu mama mwenye nyumba (mke wa ndoa) yeye ni mama wa nyumbani pure!!
Anashinda nyumbani, anaangalia tu taratibu za hapo nyumbani.

Mipango mingi inayohusu maendeleo ya biashara na maisha kwa ujumla, Baba anapanga na huo mpango wa kando, kila kitu lazima mpango wa kando ahusishwe na atoe maoni yake.

Na huo mpango wa kando unajua mambo, kufikiri, na maoni na ushauri mzuri wa kimaendeleo. Ambacho nimekigundua mpango wa kando unajua kufikiri kuliko mpango wa ndani. Yani ukimsikiliza huyo mpango wa kando na mother house katika kutoa hoja na kuchangia jambo lolote la maendeleo unagundua kabisa kuna gape kubwa la uelewa wa mambo, wakati mwingine hata utendaji wao.

Na hicho kimepelekea baba kuelemea zaidi huko kwa mpango wa kando kwa sababu huko ndiko anakopata Innovative ideas zaidi.
Ingawa analala na kukaa nyumbani kwa mke wake wa ndoa. Kiukweli ukiangalia unaona huyu mpango wa kando ana mchango mkubwa sana kwenye maswala ya maendeo ya kiuchumi zaidi kuliko mother house.

Kuna wakati huyo baba alimfungulia mother house wake biashara kubwa na nzuri tu, lakini alishindwa ku manage ikafilisika kabisa.
Lakini kuna viyu huyu mpango wa kando anaviangalia vinakwenda vizuri sana, na vina leta faida kweli kweli.

-Kama ilivyo kawaida mother house hana furaha na kile anachokifanya mume wake, kumletea hadi mtoto kwenye ndoa. Hana ujasiri kwa mume wake, ni mnyonge, hana maamuzi yake binafsi, hana uhuru wa kutosha. Yani ni tabu tupu. Anaishi tu kwa sababu kuna kuishi lakini hana furaha ya ndoa kabisa. Na kwa sababu ya hayo anazidi kuwa kituko kabisa, hata house girl anaweza akamfokea!!

1.Je huyu baba alikosea kumuoa mke ambaye hana kiwango cha elimu zaidi ya
elimu ya msingi??

2.Je kwa nini huyu baba asimwendeleze huyu mama/mke wake kielimu
kidogo ili aweze kuchangamsha akili kidogo?

3. Je ni vizuri mtu kuoa/kuolewa na mtu ambaye walau akili zenu zinaendena katika utendaji wa mambo hasa ukizingatia mipango na maono yako ya maisha?

4. Je huyu baba anafanya makosa kumfanya mpango wake wa kando
mshauri wa mipango yake ya maendeleo zaidi ya mke wake?

Mwisho: Unamshauri nini huyu mama mwenye nyumba, ili aweze kuishi kwa furaha na amani katika ndoa yake?

Mbarikiwe!!!

LD!

Sina hakika kama ulichoandika ni something real au ni hypothetical case,vyovyote iwavyo;ulichoandika katika ujumla wake kinawakilisha matatizo ya jumla kwenye ndoa nyingi za kitanzania ambazo wanandoa wako kwenye age hiyo 50's na 60's...ukweli ni kwamba wengi waliingia kwenye ndoa kwa influence ya familia zao (aidha kuchaguliwa ile purely au kushinikizwa) na siyo kwa mapenzi yao.ndicho kinacho-reflect kwenye ndoa hizo.

Well,inasikitisha sana kwani karibu asilimia 99.9 wahanga wanakuwa ni kina mama,siyo mageni hayo yapo na pengine wengi wetu tupo au tulilelewa kwenye familia kama hizo.

Kuwa mkweli kwa stage aliyofikia huyo baba hakuna kitakachorudisha mapenzi yake kwa mama,sasa hata mama leo akijiendeleza akapata elimu kidogo abaki aishi kwenye hiyo ndoa kwa mazoea au kwa mapenzi?anayempenda mke wake kwa dhati hawezi fanya yote hayo (kumzalia nje,kumleta mtoto nyumbani na bado anaendelea na huyo wa nje,aah hapo hakuna mapenzi)

Mama kwa asilimia zote ana mapenzi na mumewe lakini Baba hana mapenzi kabisa.

Ushauri wangu ni kwamba mama kama ana watoto wakubwa ambao wanaweza ku-msupport aangalie maisha yake tu,Mungu atambariki kwenye hilo...No More..aache kuishi kwa mazoea,ndiyo ambayo yamewaua mama zetu wengi au yamewafanya waishi kama watumwa kabisa (refer kwenye story yako kufokewa na house girl!!)

i have a feeling kuwa wewe wahusika na hiyo nyumba ndogo kw anamna moja au nyingine.... stay away from ndoa ya watu...HAYAKUHUSU!

Laiti ungejua ukweli ulivyo kaka angu, ungeomba nikuongoze sala ya toba kwa ajili ya hizo feelings zako.
Kama una mapenzi mema ni PM, nikwambie yale ambayo sikuyaandika ili uendelee ku feel vizuri!!
 
Babu naona unataka kujihalalishia kutembea nje ya ndoa

Nilishaweka angalizo babu mdogo!

Hiyo ndiyo hali halisi na haihusiani na imani ya dini yoyote.....

Linapokuja swala la ngono; Hakuna cha dini, imani, kabila, uhalali, umri wala nini sijui. Inatafutwa space ya faragha watu wanamaliza shida zao. Hapo ndipo unaweza kuwa mwanzo wa mahusiano au ndo mwisho wake
 
Laiti ungejua ukweli ulivyo kaka angu, ungeomba nikuongoze sala ya toba kwa ajili ya hizo feelings zako.
Kama una mapenzi mema ni PM, nikwambie yale ambayo sikuyaandika ili uendelee ku feel vizuri!!

Huko kwenye PM ntawafuata huko huko!
 
LD!

Sina hakika kama ulichoandika ni something real au ni hypothetical case,vyovyote iwavyo;ulichoandika katika ujumla wake kinawakilisha matatizo ya jumla kwenye ndoa nyingi za kitanzania ambazo wanandoa wako kwenye age hiyo 50's na 60's...ukweli ni kwamba wengi waliingia kwenye ndoa kwa influence ya familia zao (aidha kuchaguliwa ile purely au kushinikizwa) na siyo kwa mapenzi yao.ndicho kinacho-reflect kwenye ndoa hizo.

Well,inasikitisha sana kwani karibu asilimia 99.9 wahanga wanakuwa ni kina mama,siyo mageni hayo yapo na pengine wengi wetu tupo au tulilelewa kwenye familia kama hizo.

Kuwa mkweli kwa stage aliyofikia huyo baba hakuna kitakachorudisha mapenzi yake kwa mama,sasa hata mama leo akijiendeleza akapata elimu kidogo abaki aishi kwenye hiyo ndoa kwa mazoea au kwa mapenzi?anayempenda mke wake kwa dhati hawezi fanya yote hayo (kumzalia nje,kumleta mtoto nyumbani na bado anaendelea na huyo wa nje,aah hapo hakuna mapenzi)

Mama kwa asilimia zote ana mapenzi na mumewe lakini Baba hana mapenzi kabisa.

Ushauri wangu ni kwamba mama kama ana watoto wakubwa ambao wanaweza ku-msupport aangalie maisha yake tu,Mungu atambariki kwenye hilo...No More..aache kuishi kwa mazoea,ndiyo ambayo yamewaua mama zetu wengi au yamewafanya waishi kama watumwa kabisa (refer kwenye story yako kufokewa na house girl!!)

Daaa umesema kweli kabisa mpendwa, nakiri kabisa kama sio Neema ya Mungu,
na huyu mama ameuweka moyo wake kwa Mungu na kumtazame yeye kama mtetezi wake hapa duniani,
pengine tungekuwa tunaongea mengine sasa hivi.
 
Laiti ungejua ukweli ulivyo kaka angu, ungeomba nikuongoze sala ya toba kwa ajili ya hizo feelings zako.
Kama una mapenzi mema ni PM, nikwambie yale ambayo sikuyaandika ili uendelee ku feel vizuri!!
LD ulichomjibu hapa kinatosha ..... mpotezee.

BTT
Ninafikiri sasa hapa kutokana na post ya Asprin tukiishupalia sana tunawezajikuta tunapoteza mwelekeo wa thread na kuanza kudiscuss ile ya Are we Fighting the Lost Battle iliyotoka mwaka jana.

Kama nimemwelewa vema Asprin alitaka kumaanisha kuwa kuwa na mpango wa nje kwa huyo Baba tusiikomalie sana kama ni kosa kwani kwa mtazamo wake usiofungamana na upande wowote (Non- Aligned Mtazamo -NAM) angekuwa na mke msomi, mwenye akili za biashara au hata mke ambaye ndie chanzo cha mafanikio ya familia stil bado angetoka nje kwa kuwa ni hulka ya kiumbe mwanaume (Acc. to Asprin).

So kwake hapa anaashiria kusema kuwa tujikite zaidi katika kuangalia namna ya kuisaidia ndoa ya Bi Mkubwa na kumfanya Bi Mkubwa ajione yu duniani au aishi maisha na si mfano wa maisha akiwasindikiza wengine..kukazania kulaumu tendo la baba la kuchukua nyumba ndogo kwa Asprin si hoja ya msingi.
 
Daaa umesema kweli kabisa mpendwa, nakiri kabisa kama sio Neema ya Mungu,
na huyu mama ameuweka moyo wake kwa Mungu na kumtazame yeye kama mtetezi wake hapa duniani,
pengine tungekuwa tunaongea mengine sasa hivi.

LD.............naona Biblia ya Mama haina ule mstari usemao ...Jisaidie nami nitakusaidia.

Afanye kitu huku akiomba mwongozo wa mwenyezi MUNGU
 
LD ulichomjibu hapa kinatosha ..... mpotezee.

BTT
Ninafikiri sasa hapa kutokana na post ya Asprin tukiishupalia sana tunawezajikuta tunapoteza mwelekeo wa thread na kuanza kudiscuss ile ya Are we Fighting the Lost Battle iliyotoka mwaka jana.

Kama nimemwelewa vema Asprin alitaka kumaanisha kuwa kuwa na mpango wa nje kwa huyo Baba tusiikomalie sana kama ni kosa kwani kwa mtazamo wake usiofungamana na upande wowote (Non- Aligned Mtazamo -NAM) angekuwa na mke msomi, mwenye akili za biashara au hata mke ambaye ndie chanzo cha mafanikio ya familia stil bado angetoka nje kwa kuwa ni hulka ya kiumbe mwanaume (Acc. to Asprin).

So kwake hapa anaashiria kusema kuwa tujikite zaidi katika kuangalia namna ya kuisaidia ndoa ya Bi Mkubwa na kumfanya Bi Mkubwa ajione yu duniani au aishi maisha na si mfano wa maisha akiwasindikiza wengine..kukazania kulaumu tendo la baba la kuchukua nyumba ndogo kwa Asprin si hoja ya msingi.

Respect mjukuu!!

Daaa huu ukweli wa babu unauma sana!!
Ila hata mimi nilivyoangalia maisha yanavyokwenda,
Nilijikuta nafikiria, hivi kama sio huyu mama (mpango wa kando) kuna mambo fulani fulani yangekuwa,
hayaendi.
Ikiwa ngumu kwangu kusema Yes kwa mpango wa kando!!
Wakati huo huo, ikawa ngumu kwangu kukubaliana na maisha anayoishi mother house!!
 
LD ulichomjibu hapa kinatosha ..... mpotezee.

BTT
Ninafikiri sasa hapa kutokana na post ya Asprin tukiishupalia sana tunawezajikuta tunapoteza mwelekeo wa thread na kuanza kudiscuss ile ya Are we Fighting the Lost Battle iliyotoka mwaka jana.

Kama nimemwelewa vema Asprin alitaka kumaanisha kuwa kuwa na mpango wa nje kwa huyo Baba tusiikomalie sana kama ni kosa kwani kwa mtazamo wake usiofungamana na upande wowote (Non- Aligned Mtazamo -NAM) angekuwa na mke msomi, mwenye akili za biashara au hata mke ambaye ndie chanzo cha mafanikio ya familia stil bado angetoka nje kwa kuwa ni hulka ya kiumbe mwanaume (Acc. to Asprin).

So kwake hapa anaashiria kusema kuwa tujikite zaidi katika kuangalia namna ya kuisaidia ndoa ya Bi Mkubwa na kumfanya Bi Mkubwa ajione yu duniani au aishi maisha na si mfano wa maisha akiwasindikiza wengine..kukazania kulaumu tendo la baba la kuchukua nyumba ndogo kwa Asprin si hoja ya msingi.

Aisee mjukuu hebu njoo chukua MARUNYAG toti mbili hapa!

Hili la mpango wa nje si mjadala kwa kuwa haliepukiki.....

Wanachosahau watu ni kuwa hata huu mpango wa nje iko siku utajikuta na wenyewe umeletewa mpango wake wa nje.......itafika sehemu huyu baba hataridhishwa na huyu, na kama ilivyokuwa kwa jasiri haachi asili yake, huyu jamaa ataopoa kifaa kingine.....
 
LD.............naona Biblia ya Mama haina ule mstari usemao ...Jisaidie nami nitakusaidia.

Afanye kitu huku akiomba mwongozo wa mwenyezi MUNGU

Umeona eeh,
Yani ukiiangalia sana hiyo, unaona ni kama vile mtu anavyopoteza mawazo na Valuu,
Huku ikawa kinyume chake tuuuuuuuu!!!
 
Msimamo wa babu ambao ndio hali halisi na ukweli ni huu:

Mwanaume hajawahi na wala hatakaa aridhishwe na mwanamke mmoja
Mwanaume hajaumbwa kwa ajili ya mwanamke mmoja.

Mama mwenye nyumba hana alichokosea....hata angekuwa na upeo sawa na mumwewe, ameenda shule kama mumewe, angekuwa mjasiriamali mzuri, mzuri kama Cleopatra....bado jamaa angetoka nje.....(mwanaume haridhiki kuwa na mwanamke mmoja, msisahau)

Baba kuwa na mpango wa nje pia hajakosea.....kwa kuwa hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke mmoja.

Alichokosea huyu bwana:
Kuzaa nje ya ndoa....kama mkewe hana shida ya uzazi kilichompeleka kutotoa huko nje ni nini?
Kumdharau mke wake.....Ameshindwa nini kufanya mpango wa nje kwa siri?
Kuuachia mpango wa nje kuendesha biashara zake....Likiingia limbwata hapo, au mzee akaRIP ghafla vilio vya watoto wake wa mpango wa ndani vitamlilia mpaka jehanamu atakapokuwa.

Huu ni msimamo wa babu na hauusiani na imani ya dini yoyote ya dini wala mashirika ya kutetea jinsia za watu!
kwenye hizo bolded parts hizo NAPINGANA NA WEWE MOJA KWA MOJA......na pingana na wanaokusupport pia...!
SIO KWELI
HUO NI UPOTOSHAJI
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom