Nani atakuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa endapo Dr. Magufuli atashindwa Urais wa Tanzania?

Watasambaratika .....hakutskuwa na chama tena maana sasahv kinachowaunganisha ni madili ya noti tu syo chama.
 
Habari ni ya kufiria na kuadhania ,,,,kwa haina maana yoyote ,,,,ndio maana endapo ,,unatuletea hoja ya endapo ..tujadilini mambo yaliyopo tuachane na hoja za kufikiria na kudhania .usje cku moja ukauliza endapo bahari ya Hindi itakauka itakuwaje .
 
CCM tangu kuanzishwa kwake imekuwa na desturi ya kuongozwa na Mwenyekiti wa Taifa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jambo hilo limetokea kwakuwa CCM imekuwa ikishinda kwenye uchaguzi na kutoa Rais.

Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa. Mzee Ali Hassan Mwinyi alikuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa. Utamaduni na utaratibu huo ulimhusu pia Rais Mstaafu Mzee Benjamin Mkapa. Hata sasa,Rais Jakaya Kikwete ni Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Uenyekiti wa Rais Kikwete unakoma mwaka 2017 kwakuwa alichaguliwa mwaka 2012 kwa mara ya pili ya miaka mitano. Sasa,uenyekiti wa CCM Taifa utakuwaje au nani atakuwa Mwenyekiti endapo Dr. John Magufuli atashindwa kwenye Urais hapo Oktoba 25?

Nenda kasome katiba ya ccm inafafanua uzuri namna ya kumpata m/kiti wa taifa.
 
asante mkuu,kwahyo ukawa tayar mshathnk about tommorrow!xo tel me mkishndwa lowassa atapewa cheo gan cdm?duni haji atarud cuf?sumaye je?nan ataendeleza harakat za dr.slaa na zitto juu ya ufisadi?

Why cant you write properly? Nimeshindwa kuelewa unamaanisha nini?
 
Habari ni ya kufiria na kuadhania ,,,,kwa haina maana yoyote ,,,,ndio maana endapo ,,unatuletea hoja ya endapo ..tujadilini mambo yaliyopo tuachane na hoja za kufikiria na kudhania .usje cku moja ukauliza endapo bahari ya Hindi itakauka itakuwaje .
yani wewe inawezekana kweli uwe unaishi bila plan ... ndo maana kweli uko CCM... kila kitu kwenye maisha lazima kiwe na pande mbili na Mungu aliiumba hivyo usipoenda mbinguni utaenda Jehanam.. ili uweze kuchagua moja..
 
Hapana ndugu! Hilo ni swali la msingi kabisa kwani latusaidia kujiandaa kisaikolojia kwa jambo ambalo linawezekana kabisa kutokea: vile vile uongozi na wanachama wote wa ccm inabidi waandaliwe kisaikologia kwa uwezekano wa kuwa kile kitu ambacho hawajawahi kuwa na uzoefu (experience) nacho, yaani, chama kikuu cha upinzani. Na pia chama kiwezacho kuwa chama tawala (UKAWA) hakina budi kijiandae kukabiliana na chama mahiri na machachari cha upinzani ambacho hakijawahi kupatikana katika nchi hii! Kwa namna yoyote wananchi hatutategemea chama kipya tawala kifanye kwa viwango cha Ccm ilipokuwa madarakani! Kipimo chao itakuwa kufanya mara dufu ya ccm! Hii ina maana wakichemka kidogo tu, hawatasalia madarakani zaidi ya miaka 5!
 
Endapo Magufuli akibahaitika kuwa Rais wetu kwenye Uchaguzi Mkuu ujao basi Chama chake CCM kitamnyima Uenyekiti kwa kubadilisha Katiba yake ili kutengua kipengele kinachoruhusu Rais kupitia CCM ndie kuwa Mwenyekiti wa Chama pia.
Watafanya hivyo kwa Hila japo waanzisha mchakato huo watatoa sababu zitakazoonekana ni za msingi mbele ya Wanachama.


Sababu za Msingi Zitakozoletwa
Sababu kubwa itakayotolewa na Wanamchakato ni kua Rais hapati Muda wa kutosha kukitumikia chama kwa nafasi ya Mwenyekiti ipasavyo kutokana na kuzongwa na majukumu ya Taifa kama Rais. Hivyo Rais asiwe Mwenyekiti wa Chama ili atumie 100% ya muda wake kutumika kama Rais.

Sababu nyingine ni kuondoa UCCM ndani ya utendaji wa Rais, ili Maamuzi ya Rais yasihusishwe na maamuzi ya Chama moja kwa moja na hivyo kuyapa maamuzi ya Raisi picha ya Utaifa na sio Uchama.

Sababu za maana zipo nyingi sana kama ambavyo mtakumbuka Katibu Mkuu CCM ndugu Kinana amewahi kuzielezea katika Ziara zake za kukileta Chama karibu na Wananchi.

Sababu za Hila na za Kulinda Maslahi Binafsi
Pamoja na kua sababu za msingi zina nguvu ya Hoja lakini zinasukumwa zaidi na Hira na Maslai binafsi miongoni mwa Wanachama ambao watazurika na maamuzi ya Magufuli kama Mwenyekiti.

Wanamuogopa Magufuli kwani wanajua fika hatakua rafiki wa mambo ya kuleanaleana kupitia Chama.
Wanamuogopa Magufuli kwani siyo yeye alieandaliwa na Mfumo ili alinde Maslai yao baada ya Kikwete kuondoka, mtu waliemuandaa hakufanikiwa kua mgombea.

Wanamuogopa Magufuli kwani ni dhahili Magufuli sasa ana Nguvu na anakubalika kuliko Chama kiasi hata cha kumtangaza Magufuli zaidi kuliko Chama wakati wa Kampeni hivyo wanahofu kua akiwa Mwenyekiti hatosikia ushauri wao kwani Magufuli atakua Mbishi kwa sababu anajua Chama kilishinda kutokana na yeye na sio Chama kama Chama.

Watafanya hivyo ili kumuondolea Magufuli nguvu ya kisisa na hivyo wataweza kumtisha kama hatotekeleza Matakwa yao.
Ni dhahili kua ndani ya CCM kuna watu wengi wasio Waadilifu, Mafisadi nk, hivyo kumnyima Magufuli Uenyekiti kutawalinda wao dhidi ya Mabadiliko yaliyodhamiliwa na Mh Magufuli.
Kwa kumnyima Magufuli Uenyekiti kutamuweka kwenye Remote Control kuamua watakavyo.

Kwa ujumla CCM hawapo tayari kubadilika kwani wana Maslai ktk mfumo uliopo na wapo tayari hata kubadilish Katiba ya Chama ili iendane na kulinda Maslai binafsi kuliko ya Taifa.

Magufuli mwenyewe anaweza kuleta Mabadiliko ila hawezi akiwa na CCM kama nilivyoeleza hapo juu.
Kama kweli unataka Mabadiliko ya kweli basi angalia njia nyingine ila sio kupitia CCM na Magufuli.
Magufuli alistahili kua Mgombea Binafsi kuliko kugombea akiwa na CCM.

Chagua UKAWA kwa Mabadiliko ya Kweli.
 
Mkuu umeongea ukweli uyu jamaa akiwa rais atawatia jambajamba mpaka basi
 
Mbona Umepanic Mkuu,lowassa Akishindwa Atapewa Cheo Gan?Na Sumaye Je?Duni Haji Atarud Cuf?Katibu Mkuu Atakua Nan Chadema?Ukawa Itaendelea Kuwepo?Nan Ataendeleza Harakat Za Dr.Slaa Na Zitto?
Nini itakuwa kaulimbiu ya CHADEMA.?
 
Back
Top Bottom