CCM Taifa mkemeeni mzee Sabaya kwa kauli yake ya kibaguzi; Kinyume chake ni kauli ya CCM

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,272
2,033
Naamini CCM anayoiongoza Mwenyekiti Rais Samia haiwezi kukubali KAULI ya Hovyo na ya Kibaguzi aliyoitoa KADA wake Bw.Sabaya Mwenyekiti wa CCM Mkoa. Kauli hii haipaswi kuachwa hivi hivi kwani ni Kauli inayokinzana na juhudi zote anazifanya Mwenyekiti Samia za Maridhiano na Vyama vya Upinzani.

Mzee Sabaya kwa Umri wake hakupaswa kabisa kuwa na Mawazo ya kijinga na ya kibaguzi kama aliyokuwa nayo Mtoto wake akiwa Dc wa Hai.

CCM TAIFA toeni NENO ZITO kwa Viongozi wenu wenye mawazo ya Kibaguzi kwa WANANCHI kwa tofauti za ITIKADI inawezekana Mzee Sabaya pamoja na Umri wake HAJUI Fedha za Maendeleo ni KODI za hao hao WAPINZANI anaosema Wasipelekewe Maendeleo.

Mzee SABAYA tafadhali "CHUTAMA" Waombe RADHI WAPINZANI.

Kujishusha hakukupunguzii Cheo chako unachojidai nacho pia kumbuka CHEO ni DHAMANA.
Leo upo kesho haupo ataingia mwingine Mwanao ALIAMINI atakuwa DC MILELE leo yupo Wapi JIFUNZE kupitia MWANAO.

Pia Soma; Mwenyekiti CCM Arusha: Unachagua upinzani kisha unataka uletewe huduma ya maji?
 
Mzee yupo sahihi,ameuliza kwanini Kilimanjaro hapafanyikagi maandamano...?wanakuja Arusha kuwahamasisha vijana..au ndio ile kusema hata wakifa haiyumi kwasababu sio ndugu zao
 
Mzee Sabaya katumwa kueneza chuki ya ubaguzi wa kisiasa na hao hao ccm . Watamkemea vipi?
 
Mzee yupo sahihi,ameuliza kwanini Kilimanjaro hapafanyikagi maandamano...?wanakuja Arusha kuwahamasisha vijana..au ndio ile kusema hata wakifa haiyumi kwasababu sio ndugu zao
Mkuu maandamano gani yameua watu mwaka huu?
 
Vipi kuhusu kauli za Lema? Hakemewi Kwa sababu Walalamishi wa Taifa ni CHADEMA?
 
Mzee yupo sahihi,ameuliza kwanini Kilimanjaro hapafanyikagi maandamano...?wanakuja Arusha kuwahamasisha vijana..au ndio ile kusema hata wakifa haiyumi kwasababu sio ndugu zao
Yupo sahihi kabisa!! Lema katuna viongozi wa dini lakini CHADEMA haijamkemea!! Wapuuzi wakubwa
 
Back
Top Bottom