Rais Samia alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM 2022 zilikuwa ni Baraka za yeye kuwa Rais wa JMT hadi 2030. Ni mtu mjinga tu asiyeelewa hili!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,036
142,119
Binafsi nilishangaa sana kumsikia Komredi Kinana akizungumza suala la Fomu Moja kana kwamba ndio anatoa Mwongozo

CCM kupitia mkutano mkuu wa taifa ilishamchagua kwa Kura Dr Samia kuwa Rais wa JMT hadi 2030

2025 ni wakati wa Vyama Vya Upinzani kujaribu bahati yao kama wataweza kumtoa kwa kura halali za Wananchi

2025 Sisi CCM Jukumu letu ni kutetea urais Wetu wa JMT unaoshikiliwa na Mwenyekiti Wetu Dr Samia kwa kuwahimiza Wananchi watuunge mkono

Happy New Year
 
Siyo kwamba mnatetea urais kwa kupenda. Samia ndiye kashika rungu la uenyekiti, hivyo anaamrusha nn kifanyike.

Pia mkono mwingine kashika panga ra urais. Ukikataa kutekeleza anachokitaka anakushughulikia.

Ccm mnaburuzwa
 
Sidhani kama kuna mtu wa kupambana na rais nje na ndani ya chama,wakitaka taarifa zaidi wamuulize Lowasa na associates wake
 
Binafsi nilishangaa sana kumsikia Komredi Kinana akizungumza suala la Fomu Moja kana kwamba ndio anatoa Mwongozo

CCM kupitia mkutano mkuu wa taifa ilishamchagua kwa Kura Dr Samia kuwa Rais wa JMT hadi 2030

2025 ni wakati wa Vyama Vya Upinzani kujaribu bahati yao kama wataweza kumtoa kwa kura halali za Wananchi

2025 Sisi CCM Jukumu letu ni kutetea urais Wetu wa JMT unaoshikiliwa na Mwenyekiti Wetu Dr Samia kwa kuwahimiza Wananchi watuunge mkono

Happy New Year
Hakuna mwanaccm asiyefahamu ni Samia mitano tena, Bali kinachoendelea ni settings za matumbo yasibaki empty.

Kassimu Kule Ruangwa anamwaminisha mama yeye yupo royal kwake lakini lengo kuu la Kassimu asitupwe nje serikali itakapoundwa baada ya uchaguzi wa 2025 Kwa watu wenye akili tunajuwa ni Samia ndio mshindi, wasiokuwa nguvu ya sitting President wajifunze Congo Tshisekedi alivyowapiga kata funuwa Mose Katumbi na wenzanke.

Kuna wale ndani ya CCM wanaojifanya kama Wana vuguvugu wagombea Urais 2025 hawa nao ni walewale, tumbo settings activated mode.

Siri ya CCM ukitaka madaraka uwe mtata ndio utakuwa unapewa vyeo vya kunyamazishwa, si kila unayeona ameteuliwa unadhani ameteuliwa Kwa wateuzi kumpenda, Bali kumziba mdomo.

Mwana CCM ukitaka ukumbukwe na wewe pokea kijiti cha Humphrey Polepole anzisha shule ya uongozi ila kuna risk yake kama huna mizizi, usipozibwa mdomo Kwa uteuzi basi utazibwa mdomo jumla na Nec Kwa kufutwa uanachama.
 
Katiba yetu ndiyo iliyompa yeye Urais wa nchi baada ya kifo cha Rais Magufuli. CCM haikuwa na choice yeyote bali ni kumchagua awe mwenyekiti wao ili kuendeleza ule uonga wao kwamba Mwenyekiti wa CCM ni lazima awe Rais wa nchi ili chama kiwe salama.

Mtoa hoja unafikiri hatujui kwamba kuna kundi lilitaka kugoma ila dola ikashughulika nalo kimya kimya. CCM hakuna demokrasia bali kuna mkono wa chuma.
 
Binafsi nilishangaa sana kumsikia Komredi Kinana akizungumza suala la Fomu Moja kana kwamba ndio anatoa Mwongozo

CCM kupitia mkutano mkuu wa taifa ilishamchagua kwa Kura Dr Samia kuwa Rais wa JMT hadi 2030

2025 ni wakati wa Vyama Vya Upinzani kujaribu bahati yao kama wataweza kumtoa kwa kura halali za Wananchi

2025 Sisi CCM Jukumu letu ni kutetea urais Wetu wa JMT unaoshikiliwa na Mwenyekiti Wetu Dr Samia kwa kuwahimiza Wananchi watuunge mkono

Happy New Year
Mjinga ni wewe ambaye unaamini kwamba urais ni WA CCM pekee na kwamba ukishakuwa mwenyekiti wa CCM basi ni Hadi 2030. Hakika wewe ni mjinga na kama nchi hii inawajinga wengi kama wewe basi kazi ipo.
 
Ndugu Samia Suluhu alipitishwa mwaka 2022 na MM Taifa kuwa Mwenyekiti Taifa wa CCM baada ya nafasi hiyo kuwa wazi kutokana na kifo cha JPM. Lakini kuhusiana na suala la urais wake hakuna kikao chochote kile kimewahi kumpa idhini ya kugombea nafasi hii.

Si kikao cha KK, Halmashauri Kuu ya Taifa wala MM Taifa wa chama chake kimewahi kufanya hivyo. Aliyepewa ridhaa hiyo na vikao hivi ni JPM. Sijui katiba ya CCM inasemaje kuhusiana na hili, lakini mimi naona ni kinyume hata na mila na utamaduni wao.

Mwaka 2015 zilitolewa fomu nyingi, mwaka 2020 ilitolewa fomu moja ili kumpisha JPM amalizie awamu yake. Sasa 2025 zinapaswa zitolewe nyingine nyingi ili makada wapimane ubavu kwa ajili ya kumpata yule anayekubalika zaidi. Acheni uoga, kama Samia anakubalika sana ndani ya chama chake, basi si aache taratibu zichukue mkondo wake!
 
Hakuna Ukweli Wowote Kwenye Hili Zaidi Wote Wanaolitetea Wanafanya Kwa Maslahi Yao Mapana. Utaratibu Wa o Wote Wanajua Kinachoendelea Ni Batili Tupu Zaidi Ubabe
 
Mjinga ni wewe ambaye unaamini kwamba urais ni WA CCM pekee na kwamba ukishakuwa mwenyekiti wa CCM basi ni Hadi 2030. Hakika wewe ni mjinga na kama nchi hii inawajinga wengi kama wewe basi kazi ipo.
Lowassa akikusoma hapa atacheka mno

Ni mjinga tu anayeamini Tanzania kuna vyama Vya Upinzani chini ya Mtungi

Huyo Magufuli kama unavyojiita 2020 alijichagua na kuchagua Wabunge wote hadi akina mama wa Chadema na CUF dadeki🐼
 
Ndugu Samia Suluhu alipitishwa mwaka 2022 na MM Taifa kuwa Mwenyekiti Taifa wa CCM baada ya nafasi hiyo kuwa wazi kutokana na kifo cha JPM. Lakini kuhusiana na suala la urais wake hakuna kikao chochote kile kimewahi kumpa idhini ya kugombea nafasi hii.

Si kikao cha KK, Halmashauri Kuu ya Taifa wala MM Taifa wa chama chake kimewahi kufanya hivyo. Aliyepewa ridhaa hiyo na vikao hivi ni JPM. Sijui katiba ya CCM inasemaje kuhusiana na hili, lakini mimi naona ni kinyume hata na mila na utamaduni wao.

Mwaka 2015 zilitolewa fomu nyingi, mwaka 2920 ilitolewa fomu moja ili kumpisha JPM amalizie awamu yake. Sasa 2025 zinapaswa zitolewe nyingine nyingi ili makada wapimane ubavu kwa ajili ya kumpata yule anayekubalija zaidi. Acheni uoga, kama Samia anakubalika sana ndani ya chama chake, basi si aache taratibu zichukue mkondo wake!
2022 Nafasi zote za Uongozi wa CCM zilikuwa Wazi kikatiba hivyo ukafanyika uchaguzi kuanzia Shimano hadi Taifani

Nakukumbusha tu
 
Jaribu kumsitua huyo mwenyekit wenu,
Mwambie wafuasi wake kila wakisimama wanaongelea madarasa yalijengwa!
Wenye akili wanauliza, inashindikana vipi kujenga majengo ya ghorofa?
Eneo moja utakuta shule zaidi ya nne. Utasikia hii inaitwa maziwa, ile inaitwa maandazi, ile sikukuu nk.
Majengo yametapakaa ovyo!
 
Binafsi nilishangaa sana kumsikia Komredi Kinana akizungumza suala la Fomu Moja kana kwamba ndio anatoa Mwongozo

CCM kupitia mkutano mkuu wa taifa ilishamchagua kwa Kura Dr Samia kuwa Rais wa JMT hadi 2030

2025 ni wakati wa Vyama Vya Upinzani kujaribu bahati yao kama wataweza kumtoa kwa kura halali za Wananchi

2025 Sisi CCM Jukumu letu ni kutetea urais Wetu wa JMT unaoshikiliwa na Mwenyekiti Wetu Dr Samia kwa kuwahimiza Wananchi watuunge mkono

Happy New Year

Kwa hivyo alishapitishwa na chama kuwa mgombea? Ndio maana kampeni zimeanza mapema.
 
Katiba yetu ndiyo iliyompa yeye Urais wa nchi baada ya kifo cha Rais Magufuli. CCM haikuwa na choice yeyote bali ni kumchagua awe mwenyekiti wao ili kuendeleza ule uonga wao kwamba Mwenyekiti wa CCM ni lazima awe Rais wa nchi ili chama kiwe salama.

Mtoa hoja unafikiri hatujui kwamba kuna kundi lilitaka kugoma ila dola ikashughulika nalo kimya kimya. CCM hakuna demokrasia bali kuna mkono wa chuma.
Kugoma ndani ya CCM haiwezekani
 
Binafsi nilishangaa sana kumsikia Komredi Kinana akizungumza suala la Fomu Moja kana kwamba ndio anatoa Mwongozo

CCM kupitia mkutano mkuu wa taifa ilishamchagua kwa Kura Dr Samia kuwa Rais wa JMT hadi 2030

2025 ni wakati wa Vyama Vya Upinzani kujaribu bahati yao kama wataweza kumtoa kwa kura halali za Wananchi

2025 Sisi CCM Jukumu letu ni kutetea urais Wetu wa JMT unaoshikiliwa na Mwenyekiti Wetu Dr Samia kwa kuwahimiza Wananchi watuunge mkono

Happy New Year

Huyu SSH angesimama kuomba kura ya Urais yeye kama yeye 2015, 2020 CCM ingekuwa imeshatolewa Madarakani.

Ni zipi Sera zake, mipango yake, maono yake, mikakati yake, uthubutu wake? Yupo pale kufanya nini kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania?
 
Back
Top Bottom