Nani atakuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa endapo Dr. Magufuli atashindwa Urais wa Tanzania?

Hizi ndo nyuzi tulizozizoea JF,zinafikirisha.Kwanza ndo itakuwa mara ya kwanza cccm wanafanya uchaguzi wa mwenyekiti toka chama kianzishwe,pili itakuwa ngumu kumpata volunteer wa kujitolea kipindi hicho kwani tayari wanachama wao watakuwa waoga wa kujaribu (kumbuka sasa ni nguvu tu zinatumika),kwa ninavyoona mmoja wa watoto wa vigogo atatupiwa mfupa kwa lazima,halafu kinafia rasmi kwenye chaguzi za mitaa

Hapo ndipo kitabadirishwa jina kutoka chama tawala hadi kua sungu sungu jamii!maana wale green g'wale walio mlimboka mbunge mtarajiwa ubungo!yani hii picha ni ya kutisha mwaka huu!!
 
CCM tangu kuanzishwa kwake imekuwa na desturi ya kuongozwa na Mwenyekiti wa Taifa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jambo hilo limetokea kwakuwa CCM imekuwa ikishinda kwenye uchaguzi na kutoa Rais.

Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa. Mzee Ali Hassan Mwinyi alikuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa. Utamaduni na utaratibu huo ulimhusu pia Rais Mstaafu Mzee Benjamin Mkapa. Hata sasa,Rais Jakaya Kikwete ni Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Uenyekiti wa Rais Kikwete unakoma mwaka 2017 kwakuwa alichaguliwa mwaka 2012 kwa mara ya pili ya miaka mitano. Sasa,uenyekiti wa CCM Taifa utakuwaje au nani atakuwa Mwenyekiti endapo Dr. John Magufuli atashindwa kwenye Urais hapo Oktoba 25?
Ndoto za kiseng.........rema hizi
 
Back
Top Bottom