Mwitikio wa kutisha mgombea wa CHADEMA alipotangaza nia Arumeru Mashariki

Mafie PM

JF-Expert Member
Mar 19, 2011
1,317
207
Ndg wana JF, tar11/02/2012 siku ya jumamosi nilifanikiwa kuhudhuria hafla fupi pale Kibo Palace Hotel Arusha, wakati Kijana Machachari wa Chadema Arumeru Mashariki Kamanda na mpambanaji Joshua Nassary alipotangaza nia yake ya kuomba kuteuliwa na Chama chake cha Chadema aweze kupeperusha bendera ya chama hicho ktk kinyang`anyiro cha uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni hapo.
Mwitikio niliouona umenifanya nishawishike kushiriki nanyi kilichojiri,
1. Idadi ya watu waliojitokeza kumuunga mkono ilikuwa ni nyingi mno tofauti na matarajio ya wengi, kinababa kinamama bila kujali itikadi zao za chama,vijana wa kiume na kike walijitokeza kwa wingi kumuunga mkono, watumishi mbalimbali wa serikali walijitoa kwa hali na mali na kuahidi kuwa naye bega kwa bega hadi wahakikishe wanaupata ukombozi kamili,
2. Michango ya papo kwa hapo ilifanyika na ndani ya dakika chache zikapatikana kianzio cha zaidi ya Tsh 11,000,000/= Milioni kumi na moja ikiwa ni cash na ahadi, Magari nane yenye uwezo wa kwenda sehemu korofi pamoja na mafuta yake kwa wakati wote wa kampeni yalipatikana kama kianzio , Vyombo vya Kupazia sauti vya uhakika kwa muda wote wa kampeni, watu mbalimbali walijitolea nyumba na vyakula sehemu tofauti tofauti, pia walijitolea vijana wa kike na kiume, wababa na wamama kwenda kuweka kambi vijijini kwa muda wote wa kampeni hadi wakati wa kumalizika uchaguzi na kutangazwa matokeo. hii imeonyesha ni jinsi gani watu wanamkubali huyu kujana na ni wazi watu wameichoka CCM hata vijijini.
 
big up makamanda kila la heri hakuna kulala mpaka kieleweke uzini tumekuwa wa pili.mapambano yanaendelea kufikia 2015 nchi yetu peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeees!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!11
 
Mwanzo mzuri. Namtakia mafanikio mema huyo kijana. Nawaasa CDM (hasa timu yake ya kampeni hapo arumeru) wazibe mianya ya wizi wa kura wakati ukifika.
 
Tatizo la Pro-Chadema JF mnakuwa na haraka sana ya ushindi mkishindwa mnasema wameiba kura.
ritz kimsingi mnafeli sana kupromote chama chenu sijui mpo blog gani maana mambo muhimu ya chama chenu hamuyasemi badala yake kazi yenu ni kuropoka tu hapa JF karibu wote wa genge lenu tabia ni moja.

mngefanya kama Nape alivyo kuwa anafanya labda ingesaidia kukinusuru chama chenu ila kwa sasa kinakufa nanyi mnachangia sana kukiua (RIP)

Uzini matokeo umeyapata ??? sijasikia kama umeitimiza ahadi yako
 
Duble Chris,
Kwanza unatakiwa hujue kuwa JF sio mali ya Chadema..

Vile vile haiwezekani members wote wa JF wawe Pro-Chadema, lazima mkubaliane na fikra tofauti kwa hiyo mambo ya blog sio muhimu nadhani JF inatosha.
 
usikimbie swali ndugu je ahadi metimizaaaaa?
 
Huyu kijana anafaa sana.

angalieni msije mkatoa vijana kutoka eneo lake la kupigia kura na kwenda kuwa wakala sehemu asiyopiga kura. Hapo ni karibu na ngome nyingi za chadema i hop suala la kulinda kura litakuwa jepesi. Sasa hivi ni kutafuta watu wa kuwapigia kura. Chonde chonde kuna vijana wengi wanaoweza kuwa mawakala ambao watasimamia kura kwa uaminifu.
 
big up makamanda kila la heri hakuna kulala mpaka kieleweke uzini tumekuwa wa pili.mapambano yanaendelea kufikia 2015 nchi yetu peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeees!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!11

powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ritz ya chadema waachie pro-chadema. Wewe shughulikia ya *******. Wabunge wako wanalilia posho na baba mwanahawa kawawekea ngumu.

yule ni baba mwanaasha mkuu. sasa hivi wanajuta kumfahamu.
 
Natumaini kutakuwa na upinzani mkali zana kuqahi kutokea katika siasa za Bongo. Kila mmoja anausaka ushindi kwa udi na uvumba, itabidi nihamie Arusha kampeni zikianza kwa ajili ya kutoa updates.

PakaJimmy na kundi lako naomba ushirikiano hasa mtu anyeitwa Crashwise.
 
Back
Top Bottom