TEMILUGODA
JF-Expert Member
- Feb 11, 2012
- 1,389
- 285
Ndg wana JF, tar11/02/2012 siku ya jumamosi nilifanikiwa kuhudhuria hafla fupi pale Kibo Palace Hotel Arusha, wakati Kijana Machachari wa Chadema Arumeru Mashariki Kamanda na mpambanaji Joshua Nassary alipotangaza nia yake ya kuomba kuteuliwa na Chama chake cha Chadema aweze kupeperusha bendera ya chama hicho ktk kinyang`anyiro cha uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni hapo.
Mwitikio niliouona umenifanya nishawishike kushiriki nanyi kilichojiri,
1. Idadi ya watu waliojitokeza kumuunga mkono ilikuwa ni nyingi mno tofauti na matarajio ya wengi, kinababa kinamama bila kujali itikadi zao za chama,vijana wa kiume na kike walijitokeza kwa wingi kumuunga mkono, watumishi mbalimbali wa serikali walijitoa kwa hali na mali na kuahidi kuwa naye bega kwa bega hadi wahakikishe wanaupata ukombozi kamili,
2. Michango ya papo kwa hapo ilifanyika na ndani ya dakika chache zikapatikana kianzio cha zaidi ya Tsh 11,000,000/= Milioni kumi na moja ikiwa ni cash na ahadi, Magari nane yenye uwezo wa kwenda sehemu korofi pamoja na mafuta yake kwa wakati wote wa kampeni yalipatikana kama kianzio , Vyombo vya Kupazia sauti vya uhakika kwa muda wote wa kampeni, watu mbalimbali walijitolea nyumba na vyakula sehemu tofauti tofauti, pia walijitolea vijana wa kike na kiume, wababa na wamama kwenda kuweka kambi vijijini kwa muda wote wa kampeni hadi wakati wa kumalizika uchaguzi na kutangazwa matokeo. hii imeonyesha ni jinsi gani watu wanamkubali huyu kujana na ni wazi watu wameichoka CCM hata vijijini.
Ninapo ona taarifa hii napata picha ya namna wananchi wanao tafuta tiba ya maradhi'political,economical na social healing'.USE YOUR HEART WITH INTELIGENCE FOR INTELIGENCE SPRINGS YOUR LIFE VALUES.NGUVU YA UMMA.......