Mwitikio wa kutisha mgombea wa CHADEMA alipotangaza nia Arumeru Mashariki

Tatizo la Pro-Chadema JF mnakuwa na haraka sana ya ushindi mkishindwa mnasema wameiba kura.

Umeongea ukweli wana viherehere wanauza mbinu zote jamvini ,ndio tunapenda habari lakini nyingine mungeweka vifuani mwenu munawasaidia sana chama cha ******* kupata mbinu za kupambana nanyi embu tulizeni mizuka yenu
 
Hakuna kulala tumechoka kushika nafasi ya pili ktk chaguzi ndogo Arumeru tunatakiwa kuonyesha kuwa tumedhamilia.
 
Duble Chris,
Kwanza unatakiwa hujue kuwa JF sio mali ya Chadema..

Vile vile haiwezekani members wote wa JF wawe Pro-Chadema, lazima mkubaliane na fikra tofauti kwa hiyo mambo ya blog sio muhimu nadhani JF inatosha.
Viongozi wako walishasema JF ni ya CHADEMA na hivi karibuni walizungumzia kuifunga je wewe ni CHADEMA na kama wewe siyo chadema una fanya nini JF.....
 
Ndg wana JF, tar11/02/2012 siku ya jumamosi nilifanikiwa kuhudhuria hafla fupi pale Kibo Palace Hotel Arusha, wakati Kijana Machachari wa Chadema Arumeru Mashariki Kamanda na mpambanaji Joshua Nassary alipotangaza nia yake ya kuomba kuteuliwa na Chama chake cha Chadema aweze kupeperusha bendera ya chama hicho ktk kinyang`anyiro cha uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni hapo.
Mwitikio niliouona umenifanya nishawishike kushiriki nanyi kilichojiri,
1. Idadi ya watu waliojitokeza kumuunga mkono ilikuwa ni nyingi mno tofauti na matarajio ya wengi, kinababa kinamama bila kujali itikadi zao za chama,vijana wa kiume na kike walijitokeza kwa wingi kumuunga mkono, watumishi mbalimbali wa serikali walijitoa kwa hali na mali na kuahidi kuwa naye bega kwa bega hadi wahakikishe wanaupata ukombozi kamili,
2. Michango ya papo kwa hapo ilifanyika na ndani ya dakika chache zikapatikana kianzio cha zaidi ya Tsh 11,000,000/= Milioni kumi na moja ikiwa ni cash na ahadi, Magari nane yenye uwezo wa kwenda sehemu korofi pamoja na mafuta yake kwa wakati wote wa kampeni yalipatikana kama kianzio , Vyombo vya Kupazia sauti vya uhakika kwa muda wote wa kampeni, watu mbalimbali walijitolea nyumba na vyakula sehemu tofauti tofauti, pia walijitolea vijana wa kike na kiume, wababa na wamama kwenda kuweka kambi vijijini kwa muda wote wa kampeni hadi wakati wa kumalizika uchaguzi na kutangazwa matokeo. hii imeonyesha ni jinsi gani watu wanamkubali huyu kujana na ni wazi watu wameichoka CCM hata vijijini.

Watanzania chonde tusirudie kosa la kuchagua ccm tuchague damu changa kutoka CDM ilituondoe mafisadi. Tubaki na watu makini wenye moyo wakweli wa kuisadia Tanganyika huru.
 
Kuna Njia Ilitumika Igunga Kuiba Kura Igunga ambayo ni wachache Waliigundua ila mimi nimeipata kutoka Jikoni!! Waliweka Mabox Yenye Kura zilizochakachuliwa Chini ya Mlima!! Na walipofika Juu Dereva aliandaliwa kuzima Gari na Kusema Samahani Gari imezima Naomba Mshuke Msukume ili liweze Kuwaka!! Then Wote waliitikia na Kushuka na Kusukuma Gari!! Then Dereva akashtua na kuteremka hadi Bondeni!! Then wale mawakala wakaachwa Mbali Kidogo wakawa wanakuja kwa Miguu!! Wanafika mabox yameshabadilishwa na kuwekwa mengine Yaliyochakachuliwa!! Naandika Haya ili lisije Kujitokeza tena kwa Arumeru!! Hi ni njia ambayo ni hatari sana kuua Demokrasia!!
Hahaha, wewe ni lazima utakuwa msukuma.
 
Poleni sana,mawazo yenu ni kishabiki.mnachofanya ni kujipa moyo kwa ushindi hewa, Kama wafanyavyo washabiki wa mpira. Huwa wanatabiri ushindi kabli mpira haujaanza,wakifungwa wanaishia kutafuta mchawi. Ms ninyi mnajitabiria ushindi hewa mkishindwa muanze kusema tumeibiwa. Huyo Nassary wenu alikataliwa na wananchi wa meru wakachagua mzee Sumari akiwa anaumwa. Sasa ushahidi kwamba wameru hawapendi CCM uko wapi?
 
Kuna Njia Ilitumika Igunga Kuiba Kura Igunga ambayo ni wachache Waliigundua ila mimi nimeipata kutoka Jikoni!! Waliweka Mabox Yenye Kura zilizochakachuliwa Chini ya Mlima!! Na walipofika Juu Dereva aliandaliwa kuzima Gari na Kusema Samahani Gari imezima Naomba Mshuke Msukume ili liweze Kuwaka!! Then Wote waliitikia na Kushuka na Kusukuma Gari!! Then Dereva akashtua na kuteremka hadi Bondeni!! Then wale mawakala wakaachwa Mbali Kidogo wakawa wanakuja kwa Miguu!! Wanafika mabox yameshabadilishwa na kuwekwa mengine Yaliyochakachuliwa!! Naandika Haya ili lisije Kujitokeza tena kwa Arumeru!! Hi ni njia ambayo ni hatari sana kuua Demokrasia!!

Duh,hii kali mkuu!
 
Hizi kampeni za JF utadhani CDM itashinda.
Jipeni moyo
OTIS
 
Pitia drum la tindikali nyumbani kwangu.Huu ni mchango wangu kwa CDM.
Visu na mapanga hutachangia? maana naambiwa wewe ndio mlezi wa green gurd na sungusungu waliofanya gwaride la vitisho pale Mwanza tarehe 5/2/2012.
 
Back
Top Bottom