Mwenyekiti Wa Ukombozi Na Ufahari!

ki.
Margaret__BourkeWhite__Portrait_of_Mahatma_Ghandi.jpg


Mwenyekiti wa Chama cha kuwakomboa wananchi, anapotumia magari kama ya watawala, inasema nini kuhusu huu ukombozi? VX8, tena sio moja, Wasaidizi, Dreva, MABENDERA, KUCHELEWA KUFIKA UWANJANI, bado hajashika nchi, je akishika tutegemee nini tofauti, maana haya si ndio ya kawaida kwa watawala? Kwenye kuvaa kombati sawa lakini mengine hayo mbona sawa na watawala?

- NAOMBA KUTOA HOJA, MAANA WAKOMBOZI KINA CASTRO, CHE GUEVARA, MAO, NA SAVIMBI HATUKUWAONA NA MA-VX8, AU WASAIDIZI AU NI UKOMBOZI TOFAUTI?

- KUONGOZA SI NI MFANO ZAIDI? MUNGU AIBARIKI TANZANIA!


William.
Du kiongozi na wewe mawazo yako, sasa hapo ndio ulikuwa unamaanisha nini? sio mbaya lakini angalau umefanya ulichotumwa kuliko ungekaa kimya ungeonekana si mwenzetu.
 
Nilikuheshimu sana hasa baada ya CCM kukupendekeza ugombee ubunge, lakini ever since umekua ukikomenti mambo ya ajbu sana na hata last week kuna comment nilikuomba uindoe maana inakushushia hadhi lakini naona kama sikio lako haliskiaa sasa utavuna ulichopanda kumbe wewe ni sifuri na hata waliokunyima ubunge walikua na akili
 
Ngoja niweke sawa mambo
1.mbowe anunuliwi mafuta na chama
2.gari analolitumia sio la chama ni lakwake bnafs
3.msafara wa magari uliokutia ukichaa ni magari ya wanachama na walikuja kwa garama zao kutokea makao makuu ya chama sawa.
4.msafara wakati unaingia pale chadema square yalikuwepo gari la lema, dr slaa,mbowe, sungu, na magari mawili yalikuwa ya matangazo
5. Kumbuka miaka hiyo vx v8 ayakuwepo magari yalikuwa machache sana na garama ilikuwa kubwa sana uwezi kulinganisha na sasa sijui kama umenipa vema.
 
hiyo gari mmempa wenyewe pale mjengoni,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, endelezeni majungu muone kama yatawasaidia...................................
 
Tunaomba utuwekee picha ya gari lako na Nyumba yako.Baada ya hapo ndiyo tuzungumzie ya wengine.Pili huyu ni mwenyekiti wa CDM taifa na ni Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni, kuwa na hivi vyeo ni sawa na kuwa mtawala.
 
View attachment 54787


- Mkuu tizama nyumba aliyokuwa anaishi Savimbi!, huyo ni msaidizi amekuja kuchukua ujumbe tu, sio ma-vx8, mabendera, madereva tizama ukombozi hapo ndio maisha yake hayo juu, umemuona savimbi hapo mwenye kombati!


William.
nadhani Bwana William Malecela kama haya ndio mawazo yako unayoayaamini, basi ndio maana ulikosa ubunge wa Afrika ya Mashariki kwani wameona mali ulizonazo wakashtuka. POLE SANA KWA KUWAZA KIJIMA.
 
Heshima kwenu wanajamvi,

Mkuu W J M kauliza swali zuri sana bahati mbaya hapewi majibu ana ambulia kejeli na viroja.Wanajamvi wenzangu tuitendee haki JF kama huna uwezo wa kujibu hoja kaa pembeni magauzi ya kweli yatafanikiwa ikiwa tutakubali kukosolewa na kujisahihisha.

CDM leo ni chama cha upinzani kesho kinaweza kuwa chama tawala mambo yanayotendwa na viongozi wake leo yanatoa mwanga wakipewa dola watatutendea nini !.

Tunapinga kwa nguvu zetu zetu serekali ya CCM iachane na matumizi ya magari ya kifahari bahati mbaya mbadala wa CCM naye anatumia magari ya kifahari ?.

Mkuu
Kama sikosei wanachokipigania CHADEMA ni usimamizi wa rasilimali za nchi vizuri, ikiendana na kuacha kutumia mamilioni ya pesa kwenye magari ya kifahali lakini sio kuwakataza wananchi wenye uwezo binafsi kufanya hivyo, kwa hiyo mpaka hapo nitakaposibitishiwa kwamba Gari la Mwenyekiti limetoka kwenye pesa za chama ndio ntaona kuna hoja ya kujadili.
 
Mbona hauweki picha za nyerere, au kwa sababu yeye alifrustrate issues za mzee???
 
W.malecela naona ameshaanza mambo kama ya nape, hivi pamoja na kuishi usa bado unafikili kama mtanzania wa kawaida sana asiyejua kesho atakula nini. Kwa utajiri alionao mbowe hata asingerikuwa chadema angeweza kumiliki V8.
 
Chairman of the Party to redeem the land, he uses the car as they do, says what about this liberation? VX8, again not one, helpers, driver, banner, late Arrive field, yet keep the country, are used to hold what we should expect a difference, because these are not normal ones will not? At the same pole but other wear them why they do the same? - I beg to move, Deliverance DEEPER MEANING Castro, Che Guevara, Mao, and Savimbi HATUKUWAONA AND MA-VX8, OR JT OR IS A DIFFERENCE Deliverance? - LEADING EXAMPLE IS NOT OVER! God bless Tanzania!
@willie nimeutafsiri ***** wako kwa kiingereza angalau hata nielewe lakini nimetoka kapa
 
Nimeipenda sana hii.
Nilikuwa sifahamu Kwamba Willy ni kilaza wa uzito huu. Unajua hayo ma Vx ni old model ambayo hata mtu wa kawaida tu anayo na isitoshe huwezi ukamfananisha Mbabe wa vita Savimbi na Mbowe. Hili jamaa kumbe kubwa jinga hivi.
 
Willium ni sawa na wale wazazi wanaowaambia watoto wao enzi zetu tulienda shule bila viatu hivyo naohawatakiwi kuvaa viatu.
 
View attachment 54787


- Mkuu tizama nyumba aliyokuwa anaishi Savimbi!, huyo ni msaidizi amekuja kuchukua ujumbe tu, sio ma-vx8, mabendera, madereva tizama ukombozi hapo ndio maisha yake hayo juu, umemuona savimbi hapo mwenye kombati!


William.
Wewe ulipoenda kujidhalilisha bungeni ulienda na baiskeli?? sio wewe ndio ulikuwa unasema kwenye kila post, pamoja sana CHADEMA, pamoja sana JF, pamoja sana pamoja sana pamoja sana ka unajifunza kuongea vile, ngoja ujitie aibu leo.
 
Mkuu bombu una maana yale ni magari yao binafsi? Hata ikiwa hivyo sawa. Sasa kama wanatumia magari yao binafsi aina ya V8 wakichukua nchi ndio watatumia RAV4 au wataendelea kutumia magari yao binafsi V8?

Kwanza walithubutu vipi kulimbikiza mali kiasi hicho kama wana upendo kweli kwa watz? Hawawaoni ombaomba mtaani? Wafao kwa kukosa panado tu? Walalao kwenye maboksi nje? Watembea uchi, kuanzia baba mama hadi watoto? Waliokosa shule je? Katika nchi kama hii kuna uhalali gani wa kuishi anasa hali majority ni kapuku? Magari ya kifahari, ndege angani, tena hadi kumbi za starehe, kweli huu ni muda wa starehe kweli? Madaraka ni kwa ajili ya kututumikia kweli, au kulinda biashara zenu kama wafanyavyo ccm? Chonde watz wenzangu, tushirikiane kuondoa wezi waliopo madarakani na hawa wenzao wanaonyemelea wakitaka kuwapokea wenzao! Ccm na Chadema wanajuana, wanatupoteza maboya tu! KUAMINI WANASIASA NI ZAIDI YA KUVUA NGUO MBELE YA WATOTO WAKO!
Mungu wetu anaita!
 
Last edited by a moderator:

sasa umejiona uko upande upi wa binadamu.

1.KAZI YA MALAYA NI KUUZA MWILI WAKE.
2.MWIZI NI KUIBA.
3.MUONGO NI UZUSHI.4.lofa ni kutokujuwa anafanya, nini anaongea nini
4.lofa ni kutokujuwa anafanya nini, anaongea nini,anataka nini,anakwenda wapi na anaongea na nani.
wiliam ni lofa na zuzu mwili wa bure akili ya tea spoon.
 
You are very myopic William. Unafit sana kule facebook.
:iamwithstupid:

Huku FB amekuja tena na hili tumemkurupusha ameacha kuchangia..Naanza kumchoka , pia aelewe kuwa Mbowe pesa anayo tu hata asingeingia kwenye siasa, na pia gari ni lake na ana awezo wa kutosha kumiliki hayo magari..Ina maana ukiwa mkombozi wa watu na una pesa usitumie pesa zako kukusaidia? Mengi anatoa misaada kwa yatima na ni mfanyabiashara, kwa hiyo akienda kwa yatima aende na bodaboda au bajaj? Huyu Malecela ameanza kuchanganyikiwa baada ya kukosa ubunge wa East Africa na kunyimwa Ukuu wa wilaya.
 
Heshima yako kaka Billy.

Nakupongeza kwa ujasiri wako wa kuthubutu kuandika juu ya chama chenye wapenzi wengi sana nchini. Una uthubutu.......

Ngoja nikuonyeshe ulitakiwa kufanya nini kabla hujaandika. Itakusaidia sana siku za usoni. Unaposema....


  1. Mwenyekiti wa Chama cha kuwakomboa wananchi, anapotumia magari kama ya watawala, inasema nini kuhusu huu ukombozi? VX8, tena sio moja, Wasaidizi, Dreva, MABENDERA, KUCHELEWA KUFIKA UWANJANI, bado hajashika nchi, je akishika tutegemee nini tofauti, maana haya si ndio ya kawaida kwa watawala? Kwenye kuvaa kombati sawa lakini mengine hayo mbona sawa na watawala?

  • Umeonyesha kuwa upeo wako unahusisha utekelezaji wa sera zenye kasoro na kutumia magari ya kifahari, walinzi, bendera na kubwa zaidi dereva as if magari yalitakiwa yawe co piloted (labda unaangalia sana sinema za sciencefiction)
  • Bendera ni identity! Hata wakati ukiwa baharia wa meliza SINOTASHIP, nazo zilikuwa na bendera
  • Walinzi ni jambo liko wazi kabisa unless uwe unalindwa na watu wasioonekana kama alivyosema mtabiri Fulani
  • Kimoyoni uko Chadema nadhani maana umependa kombati!

  1. NAOMBA KUTOA HOJA, MAANA WAKOMBOZI KINA CASTRO, CHE GUEVARA, MAO, NA SAVIMBI HATUKUWAONA NA MA-VX8, AU WASAIDIZI AU NI UKOMBOZI TOFAUTI?

  • Itabidi ukae chini usome tofauti kati ya political party na resistance movement. Unachanganya masomo. Tafuta kitabu kinaitwa Waging Nonviolent Struggle: 20th Century Practice and 21st Century Potential cha Gen Sharp. Utajua kwanini siku hizi hakuna mapinduzi kama zamani. Lazima ujue kutofautisha zama, madhumuni ya mapambano na watu walio katika mfumo

  1. KUONGOZA SI NI MFANO ZAIDI? MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

  • Kuongoza ni mfano zaidi. Sasa wewe ambaye ulitaka kuongoza halafu unamiss such basic stuff? Haiyumkini kura hazikutosha
USHAURI:

  1. Soma sana uongeze maarifa. Kwa sasa, umepwaya sana. Kama itakupendeza….tutakusaidia vitu vya kusoma
  2. Take time to think kabla hujasema au kuandika. Maandishi huwa hayafutiki. Tutakuja kukuonyesha what you wrote ukiwa popote pale unagombea nafasi yeyote ile. Hili ni la muhimu sana kuzingatia
  3. Wahenga walisema “ A silent fool is counted wise”
.
Margaret__BourkeWhite__Portrait_of_Mahatma_Ghandi.jpg


- Tizama wakombozi wa wananchi hawa, wanafanana na wananchi wanaotaka kuwakomboa, ni maoni yangu tu!

William.

Kwa hiyo wewe ulivyopeleka tumbo lako kubwa bungeni ukitaka ubunge wa Africa Mashariki ulikuwa umesahau kwamba wakombozi wanatakiwa kuwa namna hii?
 
Back
Top Bottom