View attachment 1861764

View attachment 1861765
View attachment 1861766

Usiku majira ya saa tisa, Polisi walivamia Hoteli aliyokuwa amefikia Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na wageni wengine pamoja na wenyeji wao.

Waliochukuliwa:
1. Freeman Mbowe
2. John Pambalu
3. John Heche
4. Rose Mayemba
5. Masenya(Mwenyekiti BAVICHA Ilemela)
6. Steven Odipo
7. Dr. Rwaitama
8. Seti (Dereva kanda ya Victoria)
9. Apollo (Afisa Habari Taifa)
10. Frank Novatus (CHASO)
11. Mwakiaba (Mwenyekiti Nyamagana)
12. Benja (BAVICHA Kinondoni)

Mpaka sasa haijajulikana wamechukuliwa kwa kosa gani.

=====

My Take.
Uonevu, uvunjifu wa haki za kiraia, kutoheshimu katiba ya nchi unaendelea kwa kasi katika serikali ya Samia Suluhu Hassan.
Anyway, Aluta continua, uonevu huu utaisha oneday, dawa tutaipata tu.

Nimkumbusha Samia kuwa alikuwepo mtu katika nchi hii anaitwa Magufuli, tulimuita Chuma, Jiwe—Leo yuko wapi?

====

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)

Taarifa Kwa UMMA

Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe..Freeman Mbowe alivamiwa na Jeshi la Polisi hotelini alipokuwa ( Kingdom Hotel) majira ya saa nane na nusu usiku na kumkamata pamoja na viongozi wengine waliokuwa naye.

Viongozi wengine walipelekwa Kituo cha Kati cha Polisi Mwanza,Ila Mwenyekiti Mbowe haijulikani alipelekwa wapi na mpaka Muda huu hakuna taarifa zozote za mahali alipo.
Waliokamatwa ni wafuatao;

1. Mhe .Freeman Mbow
2. Mhe.John Pambalu
3. Mhe. John Heche
4.Mhe. Rose mayemba
5. Masenya( Mwenyekiti Bavicha ilemela)
6. Steven Odipo
7.Dr. Azavel Lwaitama
8. Seti ( Dereva Kanda ya Victoria)
9. Apolinary Appolo (Afisa habari Taifa)
10. Frank Novatus (Chaso Mwanza)
11. Mwakiaba (Mwenyekiti Nyamagana)
12. Benjamin Kambarage ( M.kiti Bavicha kinondoni)

Tunalitaka Jeshi la Polisi kujitokeza na kusema alipo Mwenyekiti wa Taifa na sababu za kumkamata zilikuwa nini.

Tunalaani ukandamizaji huu wa Haki za Watanzania Kwa nguvu zote , na hizi NI dalili za wazi kuwa Udikteta uliokuwepo enzi za utawala wa Rais Magufuli bado unaendelea .

Tutatoa taarifa kadiri ya Muda na jinsi tutakavyozipokea .

====

UPDATES:

=====

Jeshi la polisi mkoani Mwanza limefunga barabara ya Bwiru maarufu kona ya Bwiru jirani na ukumbi uliopangwa kufanyia kongamano la Chadema la kudai Katiba, hakuna kinachoendelea kwa sasa polisi wametanda barabara nzima wakiwa na magari na silaha za moto

IMG-20210721-WA0021.jpg
 
Samia Hawa washauri wake kina mwigulu wanataka kumuharibia, alishaanza kujitengenezea sifa nzuri kimataifa, anaanza mapema kujiharibia aisee, kikwete amshauri huyu mama kuwa masalia wa dikteta wanataka kumuharibia mama, wapinzani inatakiwa kupambana nao kwa hoja Kama kipindi Cha ccm hile ya kina NAPE na Kinana
Si mlikuwa mnasema Jakaya Kikwete ndio anaendesha nchi nyuma ya Samia, haya pambaneni na huyo Jakaya sasa
 
Mkuu wa mkoa kaweka zuio la mikusanyiko. Makamanda wa Chadema wanasema watakusanyika kwa nguvu kufanya kongamano.

Usiku wa manane wanadakwa. Maana mkuu wa mkoa anazo taarifa za kiusalama.

Je, hapa nani amefanya kosa?

Tusilaumu bila ya kuwa na argument za msingi.
Hotelini saa 9 usiku kuna kusanyiko?
 
Habari hii imeeneza habari za Kongamano la Katiba kuliko hata kongamano lenyewe lingefnyika huko hotelini.
 
Unaonekana tangu baada ya kifo cha mumeo bado una msongo wa mawazo.

Wewe ni mjane ambaye unahitaji msaada maana hata huna sifa ya kupata urithi kutoka kwa marehemu.
Acha ufara kwa mtandao,kaandamane huku kumuunga mkono bwana ako😃😃.
Ila nyie jamaa wajinga aisee😃😃
Kabisa mlijiaminisha kwamba unauungwaji mkono wa kiasi hicho😃
Mwingine yupo busy kwenye Twitter kutoka ubeligiji kuwaambia vijana wa Rock City waingie barabarani wakati yeye anakata mauono huko kwa beberus 😃😃
 
Mkuu wa mkoa kaweka zuio la mikusanyiko. Makamanda wa Chadema wanasema watakusanyika kwa nguvu kufanya kongamano.

Usiku wa manane wanadakwa. Maana mkuu wa mkoa anazo taarifa za kiusalama.

Je, hapa nani amefanya kosa?

Tusilaumu bila ya kuwa na argument za msingi.
Hizi amri zenye hila za kijinga hata akina Mandela walipewa sana na makaburu, tukawa tunamsifia Nyerere kwa kumuunga mkono Mandela na weusi wa Afrika kusini kugomea amri zisizo halali. Ni hivi, lile Katazo la mkuu wa mkoa sio halali. Hapo Mwanza mwanamuziki wa DRC Falii Ipupa, atakwenda kutumbuiza na hakuna Katazo lolote la hiyo corona, kwa hiyo mnaona sifa raia wa nchi nyingine kupata uhuru ambao watanzania wenye madai halali hawaruhusiwi kukutana?
 
Back
Top Bottom