Mwanangu na Kikwete

kwa sasa Mheshimiwa yuko kwenye ratiba kali sana ya kampeni kwa hiyo hata ukienda kumuona watakupangia tarehe za mbele sana labda baada ya Desemba halafu kama unataka kumwona Rais unatakiwa kujaza fomu na kueleza sababu ya kwenda kumuona sasa sidhani kama hiyo sababu yako ni ya msingi

Ushauri: Najua unampenda sana mwanao ila sio kitu anachosema mtoto wazazi mkitekereze maana mtoto bado akili yake inakuwa hivyo inatakiwa kuelekezwa kinachowezekana na kisichowezekana sidhani kama ni sawa kwa mtoto wenu mdogo kutaka kuonana na Rais siku ya kuzaliwa kwake maana sidhani kama kwa umri wake atakuwa na lolotela kumwambia Rais. Pia ukiwa kama mzazi jaribu kumwongoza mtoto katika misingi ya kumfanyia mambo yanayowezekana na pia jaribu ku-reason kabla hujatenda maana wazazi wasiku hizi tumekuwa kama malimbukeni ktk malezi ya watoto tunawapenda na kuwadekeza kupita kiasi na kupita uwezo wetu ambapo matokeo yake mtoto anaharibika kisaikolojia kwa kujua kila anachotaka wazazi watampa hata kama hawana uwezo

Jaribu kumlea mtoto ktk misingi mizuri na inayowezekana sio kumlea kama maigizo kiasi kwamba anaposema anataka kumwona Rais na wewe unaumia kichwa mwisho wake atakwambia anataka kwenda kumsalimia Obama au kumwamkia Osama sijui hapo utafanyaje. Grow up kuwa kama mzazi ambaye ni mwelekezi kwa mtoto na sio mtoto ndio anaku-drive huo sio ulezi mzuri
 
Mwanao ana umri gani hivi?

Nenda pale Lumumba mwone Makamba ata organize tu na unaweza pewa t-shirt, khanga na kofia juu kisha unasafirishwa na mwanao kwenye kampeni kama ni Pemba au Unguja utakula shavu tu.

Ni mtoto wa chekechea. Tungependa aonane nae pasipo gharama za kusafiri kwenda nje ya Dar es Salaam na wala dhumuni sio kutaka kula shavu.
Asante kwa mchango wako.
 
Ushauri wangu: Mkifanikiwa kupata ruhusa ya mwanao kumuona kikwete, fanya juu chini amuone kwa mbali la sivo mwanao anaweza kupata ugonjwa wa kuanguka anguka, na ukimuanza katika umri mdogo hivo ni hatari sana!

Hizi nazo ni akili mbovu.
 
Majuma matatu kutoka sasa mtoto wangu anayesoma elimu ya chechechea ataadhimisha siku ya kuzaliwa kwake. Kasema mwaka huu hataki zawadi wala keki, anataka aende kumtembelea Raith Kikwete.

Naombeni ushauri wa jinsi ya kumkutanisha mwanangu huyu na Mheshimiwa Kikwete.

Natanguliza shukrani kwa yeyote aliye tayari kunisaidia.

Kikwete ni mtu wa Watu nenda tu sehemu ya Kampeni na kofia ya chama mueleze shida yako, ataku-attend
 
VALUER, SAFARI, KONYAGI FOR YOU ON THE HOUSE UTACHAGUA KATI YA HIZO

The Following User Says Thank You to Acid For This Useful Post:

The Finest (Today)​

Thanks cousin, unajua huwa sielewi role ya mzazi inaanzia wapi na kuishia wapi sometimes... kama kweli una access ya jk unaweza ukapromise mtoto, otherwise ni kuanza kumwambia ukweli kwamba jk ni nani, what it takes to see him and what is their position of the parents na uwezo wao

haya mambo ya ntakununulia roketi na ntakupeleka mbinguni huwa yanaleta taifa la uongo na false expectatiosn from day 1
 
Bi Lewinsky muda huu hata ukitaka Kikwete apite barabara ya nyumbani kwako atapita tu. Anataka kura. Jiweke mkao wa kumpigia kura, kofia, tshirt, chupi, suruali, sketi, skafu, picha, bendera za CCM mambo yatakuwa mswano. Ikiwezekana, kubali kuwa bango la biashara ya kura
 
kwa sasa Mheshimiwa yuko kwenye ratiba kali sana ya kampeni kwa hiyo hata ukienda kumuona watakupangia tarehe za mbele sana labda baada ya Desemba halafu kama unataka kumwona Rais unatakiwa kujaza fomu na kueleza sababu ya kwenda kumuona sasa sidhani kama hiyo sababu yako ni ya msingi

Ushauri: Najua unampenda sana mwanao ila sio kitu anachosema mtoto wazazi mkitekereze maana mtoto bado akili yake inakuwa hivyo inatakiwa kuelekezwa kinachowezekana na kisichowezekana sidhani kama ni sawa kwa mtoto wenu mdogo kutaka kuonana na Rais siku ya kuzaliwa kwake maana sidhani kama kwa umri wake atakuwa na lolotela kumwambia Rais. Pia ukiwa kama mzazi jaribu kumwongoza mtoto katika misingi ya kumfanyia mambo yanayowezekana na pia jaribu ku-reason kabla hujatenda maana wazazi wasiku hizi tumekuwa kama malimbukeni ktk malezi ya watoto tunawapenda na kuwadekeza kupita kiasi na kupita uwezo wetu ambapo matokeo yake mtoto anaharibika kisaikolojia kwa kujua kila anachotaka wazazi watampa hata kama hawana uwezo

Jaribu kumlea mtoto ktk misingi mizuri na inayowezekana sio kumlea kama maigizo kiasi kwamba anaposema anataka kumwona Rais na wewe unaumia kichwa mwisho wake atakwambia anataka kwenda kumsalimia Obama au kumwamkia Osama sijui hapo utafanyaje. Grow up kuwa kama mzazi ambaye ni mwelekezi kwa mtoto na sio mtoto ndio anaku-drive huo sio ulezi mzuri

Lililonileta hapa umeshanisaidia kwenye aya yako ya kwanza.

Asante kwa ushauri wa jinsi ya kulea mtoto. Hata hivyo hilo silo lililonileta hapa. Hauna uhakika kama ni mzazi grown up, kama namdekeza mtoto na ananidrve na simwelekezi. Ningeshukuru kama ungestick kwenye mada husika.
 
Bi Lewinsky muda huu hata ukitaka Kikwete apite barabara ya nyumbani kwako atapita tu. Anataka kura. Jiweke mkao wa kumpigia kura, kofia, tshirt, chupi, suruali, sketi, skafu, picha, bendera za CCM mambo yatakuwa mswano. Ikiwezekana, kubali kuwa bango la biashara ya kura

Makubwa. Hata hivyo tusingependa hii issue iwe kisiasa. Ningependa iwe real, kama vile ambavyo angependekeza sherehe ya kuzaliwa ifanyike kwa babu.
 
Jaribu kumuuliza mwanao, kikwete ni nani na umuulize akifanikiwa kumuona atamwambia kitu gani? kama majibu yake yatakuridhisha uanze kufanya mchakato wa kumpata. Alafu kama mkifanikiwa kumuona na mwanao ni mwanao ataongea au ni wewe? hilo ni angalizo tu.
 
Ni mtoto wa chekechea. Tungependa aonane nae pasipo gharama za kusafiri kwenda nje ya Dar es Salaam na wala dhumuni sio kutaka kula shavu.
Asante kwa mchango wako.

Naona unataka kutubadili akili hapa badala ya kufuatilia mambo ya maana na msingi na kuhakikisha tunapata kiongozi bora wewe unatuvulugia stimu
 
Nenda na huyo mwanao ktk mikutano ya kampeni ya JK na ujipange katika mstari wa mbele mahali atakapopita JK, lazima atawapa TANO
 
Lililonileta hapa umeshanisaidia kwenye aya yako ya kwanza.

Asante kwa ushauri wa jinsi ya kulea mtoto. Hata hivyo hilo silo lililonileta hapa. Hauna uhakika kama ni mzazi grown up, kama namdekeza mtoto na ananidrve na simwelekezi. Ningeshukuru kama ungestick kwenye mada husika.

pole kwa kulea Lewinski Ms, sipati picha siku mtoto atakapokuwa anataka Valuu!sijui itakuwaje tu
 
Naona unataka kutubadili akili hapa badala ya kufuatilia mambo ya maana na msingi na kuhakikisha tunapata kiongozi bora wewe unatuvulugia stimu

Samahani kama unadhani nataka kubadili akili zenu. Hivi jukwaa la mahusiano na urafiki ndipo mnapohakikisha mnapata vongozi bora. Samahani tena.
 
Majuma matatu kutoka sasa mtoto wangu anayesoma elimu ya chechechea ataadhimisha siku ya kuzaliwa kwake. Kasema mwaka huu hataki zawadi wala keki, anataka aende kumtembelea Raith Kikwete.

Naombeni ushauri wa jinsi ya kumkutanisha mwanangu huyu na Mheshimiwa Kikwete.

Natanguliza shukrani kwa yeyote aliye tayari kunisaidia.
 
Lililonileta hapa umeshanisaidia kwenye aya yako ya kwanza.

Asante kwa ushauri wa jinsi ya kulea mtoto. Hata hivyo hilo silo lililonileta hapa. Hauna uhakika kama ni mzazi grown up, kama namdekeza mtoto na ananidrve na simwelekezi. Ningeshukuru kama ungestick kwenye mada husika.
nimejaribu kukuelekeza maana unaelekewa una upeo wa mashaka, mtu aliye na upeo hawezi kumchukulia Rais kama kitu cha mchezo hivyo. Elewa kuwa Rais ana tight schedule na pia ana majukumu mengi ya kitaifa na pia kuna watu wengi sana wanaotaka kumwona kwa matatizo serious na bado wanaikosa hiyo nafasi so kama ungekuwa umefikiria critically nadhani ungekuwa umeshapata jibu na sio kuuliza hapa

Binafsi nina mashaka sana na fikra zako na huyo mzazi mwenzako nae ajakushauri chochote juu ya uwezekano wa ili. Rais ni mtu mkubwa sana na kupata nafasi ya kumwona sio rahisi kama unavyofikiria unavyomwona kwenye kampeni anavyowapa watu tano ni strategies za kuomba kura ila hayuko simple kiasi hicho

Sorry kama nimekuudhi ila fikiria kwa mapana na elewa kuwa hii nayo ni sehemu ya mada wala sijatoka nje. Na hilo swali ulilouliza naamini popote duniani utakapouliza watu watahisi una walakini im telling u
 
Thanks cousin, unajua huwa sielewi role ya mzazi inaanzia wapi na kuishia wapi sometimes... kama kweli una access ya jk unaweza ukapromise mtoto, otherwise ni kuanza kumwambia ukweli kwamba jk ni nani, what it takes to see him and what is their position of the parents na uwezo wao

haya mambo ya ntakununulia roketi na ntakupeleka mbinguni huwa yanaleta taifa la uongo na false expectatiosn from day 1

I tell you iko siku mtu atakuwa anaenda kufanya tendo la ndoa na mkewe atakuja hapa atuulize pia " Jamani leo naenda kufanya tendo la ndoa na mke wangu mnanishauri vipi"? There are somethings which you have to learn to deal with them by yourself.
 
On second thoughts inawezekana dogo anaanza kujitayarisha mapema, anaanza ku network kabisa kama hapa chini Clinton alivyokuwa ana network na Kennedy.

clinton-kennedy.jpg
 
Back
Top Bottom