Mwanamke mjamzito kupata kichefuchefu na kutapika: Chanzo na tiba yake

Je, umri wa hiyo mimba ni wiki ngapi?? Kama bado ni mimba changa(below or around 12 weeks) ni kawaida kwa mjamzito kuexperience hali hiyo. Je ameshaanza clinic? Kama bado, nakushauri aanze clinic, na huko atapata msaada zaidi kuhusu hali hiyo. Mara nyingine kunakuwa na vitu vinavyosababisha hali hiyo ya kutapika kuzidi sana, kama vile mimba ya mapacha,na matatizo yanayohusiana na mimba.............
Aende hospitali afanyiwe na vipimo ikiwemo ultra sound ya hiyo mimba ili ku-rule out vitu kama ujauzito wa mapacha(multiple gestation), then daktari atamuanzishia dawa kadri inavyofaa na kwa dosage sahihi, usikubali kumuanzishia dawa tuu kienyeji, kila mgonjwa ni tofauti na daktari atatoa dawa sahihi na dozi sahihi kulingana na ugonjwa, na atamuongezea dozi au dawa au kumpunguzia kadri ya maendeleo yake yatakavyokuwa.
Nakutakia malezi mema ya ujauzito wa mkeo, umtunze na kumuangali vizuri zaidi katika kipindi hiki, ahsante sana

asante kwa ushauri mzuri na wa kitaalamu....noted!!

ni below 12 weeks,ningependa kujua kwa utaalamu wako,pale muhimbili (incase upo dsm na ni daktar wa binadamu)..naweza kuonana na daktari gani mzuri wa masuala haya ya ujauzito..ningependa apate the best treatment...ambayo naona muhimbili ndio wapo maexpert zaidi
 
Mpe pole sana ...mie nilipewa dawa zinaitwa Nosic na nikaambiwa ninywe kidonge kimoja asubuhi ,na kimoja jioni kwa siku kumi na nne inasaidia,
Kwa ushauri zaidi mpeleke kwa Gyna atapata msaada

hii siyo sahihi hata kidogo. Wewe ulipewa dawa baada ya kuonana na daktari na kumuelezea tatizo lake na yeye kukupima, sasa unavyomwambia na yeye akanunue nosic siyo sawa hata kidogo.

Kwa sababu nyingi, je kama kinachomsababishia yeye kutapika ni molar pregnancy(mimba ambayo imetungwa na mbegu ya kiume au yai la mama lisilokamilika kijenetikali), au tatizo lingine kubwa? Kwasababu vipo vitu vingi vinavyoweza kusababisha kutapika kulikopitilza wakati wa ujauzito, na ni lazima daktari ahahakikishe mgonjwa hana vitu vyote hivyo ndo aanze kumpa dawa ya kumsaidia kuzuia kutapika.

Na pia hiyo nosic inatolewa kwa dosage tofauti tofauti kulingana na judgement ya daktari, inaweza kutolewa hadi mara sita kwa siku kulingana na severity ya ugonjwa, wewe kupewa mara mbili kwa siku haimaanishi kila mgojwa atapewa hivyo hivyo, je vipi kama yeye extent ya ugonjwa wake itarequire a larger dose hauoni hapo utakuwa umempoteza mwenzio?

Pia, kuna situations ambazo mgonjwa hatakiwi kupewa nosic kutokana na sababu tofauti tofauti, je unajuaje kama huyu mgonjwa ana tatizo au condition ambayo akinywa nosic itamdhuru, huoni utakuwa umemponza mwenizio?

Watanzania wenzangu, tusipende sana hii tabia ya kuelekezana madawa mtaani tu au kwenye mitandao, "ooh mimi nilikuwa na shida kama hiyo nikaandikiwa nosic nikaambiwa ninywe mara mbili kwa siku, nikapona".
Samahani kama nimekukwaza, ni katika kueleweshana tuu ili mambo yaende sawa.
 
Nilipokuwa mjamzito kabla ya wiki 12 (1st trimester) nilitapika sana yani hata maji nilikuwa nayatapika. Nilipokwenda kwa dactari akaniambia nipige ultra sound, everything was fine, akaniambia nikivuka trimester ya kwanza nikawa bado natapika nirudi aniandikie dawa.

baada ya miezi hiyo mitatu ya mwanzo, kutapika kulitoweka kabisa sikurudi kwa daktari.

Mara nyingi ni kawaida kwa mtu kutapika sana hasa miezi 3 ya mwanzo but kama ambavyo Dr. Wansegamila alivyokushauri, usithubutu kununua dawa yoyote kabla hujamwona daktari, tena awe specialist wa wanawake, dawa nyingi zina madhara kwa wajawazito. so be careful and hongera as soon u will be called Dad.
 
Mimi ni kawaida kwangu kwa mimba zote nilizowahi kubeba, lkn nikivuka miezi mi3 kuingia wa 4 kila kitu
kinakaa sawa. Lkn kusema kweli ni hali mbaya kui experience.yani sitaki hata kukumbuka
 
Kwa wale mliopo dar naomba kujua daktar mzuri wa masuala ya kina mama wajawazito hasahasa pale Muhimbili,,,,,,,,
 
hii siyo sahihi hata kidogo. Wewe ulipewa dawa baada ya kuonana na daktari na kumuelezea tatizo lake na yeye kukupima, sasa unavyomwambia na yeye akanunue nosic siyo sawa hata kidogo......... Kwa sababu nyingi, je kama kinachomsababishia yeye kutapika ni molar pregnancy(mimba ambayo imetungwa na mbegu ya kiume au yai la mama lisilokamilika kijenetikali), au tatizo lingine kubwa? kwa sababu vipo vitu vingi vinavyoweza kusababisha kutapika kulikopitilza wakati wa ujauzito, na ni lazima daktari ahahakikishe mgonjwa hana vitu vyote hivyo ndo aanze kumpa dawa ya kumsaidia kuzuia kutapika.
Na pia hiyo nosic inatolewa kwa dosage tofauti tofauti kulingana na judgement ya daktari, inaweza kutolewa hadi mara sita kwa siku kulingana na severity ya ugonjwa, wewe kupewa mara mbili kwa siku haimaanishi kila mgojwa atapewa hivyo hivyo, je vipi kama yeye extent ya ugonjwa wake itarequire a larger dose hauoni hapo utakuwa umempoteza mwenzio?
Pia, kuna situations ambazo mgonjwa hatakiwi kupewa nosic kutokana na sababu tofauti tofauti, je unajuaje kama huyu mgonjwa ana tatizo au condition ambayo akinywa nosic itamdhuru, huoni utakuwa umemponza mwenizio?
Watanzania wenzangu, tusipende sana hii tabia ya kuelekezana madawa mtaani tu au kwenye mitandao, "ooh mimi nilikuwa na shida kama hiyo nikaandikiwa nosic nikaambiwa ninywe mara mbili kwa siku, nikapona".
Samahani kama nimekukwaza, ni katika kueleweshana tuu ili mambo yaende sawa.

Ndio maana nimemwambia amuone Gyna ..sijamwambia aanze kunywa dawa
thank you
 
asante kwa ushauri mzuri na wa kitaalamu....noted!!

ni below 12 weeks,ningependa kujua kwa utaalamu wako,pale muhimbili (incase upo dsm na ni daktar wa binadamu)..naweza kuonana na daktari gani mzuri wa masuala haya ya ujauzito..ningependa apate the best treatment...ambayo naona muhimbili ndio wapo maexpert zaidi
Sipo Dar mkuu, ila kuna chief anaitwa Dr. Kapona pale muhimbili kama alivyoelekeza mdau mmoja hapa atakusaidia ukimuona, he is a good colleague kwa kweli. Samahani kwa kuchelewa kukujibu, i was occupied kidogo
 
Wataalam wa afya na wale wakongwe waliomo kwenye ndoa kwa muda mrefu naombeni ushauri wa kitaalam na kiuzoefu!

Mke wangu anatapika mara nyingi baada ya tendo la ndoa hasa pale anapokuwa na amefikia mshindo (Kileleni) au kumaliza.

Hali hii imeanza kumtokea akiwa na ujauzito wa miezi 5, na kwa kuwa sisi ni wageni katika hii taasisi ya ndoa tumekuwa na hofu na mara nyingine kudhani kuwa ni disorders za preg but kwa kweli inatupa hofu na mara nyingine hata kuogopa kufurahia tuzo yetu tulopewa na mwenyezi Mungu.

Tunaomba ushauri, Je kuna madhara yanayoambatana na kutapika huku?

Asanteni.
 
Kutapika ni hali ya kawaida kwa mama mja mzito ila hilo la kutapika akiwa amefika kileleni kwangu ni geni ila usikute ndo namna ya kufika kileleni kwa hali aliyonayo ya uja uzito
Ila sasa akikutapikia kuna haja ya kuacha au kupunguza sex apo
 
Je, ujauzito sasa hivi umefikia wiki ngapi?

Kama kutapika kunasababishwa na tendo la ndoa ninakushauri uahirishe tendo hilo kwa kipindi kilichobaki. Hii ni kwasababu ukiendelea inaweza kusababisha premature birth ambayo itakuwa na madhara kwa mtoto iwapo hatapata neonatal support ya kiwango.

Kiujumla, katika ujauzito mwili wa mwanamke hubadilika kwa namna mbalimbali na iwapo kuna chochote kinachomletea madhara basi solution yake ni kuacha nacho.

Kutapika sio kitu cha kawaida, ni dalili ya tatizo na kutapika itself kunaweza kuleta matatizo zaidi ya kiafya.
 
Jamani wataalam wa afya na wale wagongwe waliomo kwenye ndoa kwa muda mrefu naombeni ushauri wa kitaalam na kiuzoefu! Mke wangu anatapika mara nyingi baada ya tendo la ndoa hasa pale anapokuwa na amefikia mshindo (Kileleni) au kumaliza. Hali hii imeanza kumtokea akiwa na ujauzito wa miezi 5, na kwa kuwa sisi ni wageni katika hii taasisi ya ndoa tumekuwa na hofu na mara nyingine kudhani kuwa ni disorders za preg but kwa kweli inatupa hofu na mara nyingine hata kuogopa kufurahia tuzo yetu tulopewa na mwenyezi Mungu. Tunaomba ushauri, Je kuna madhara yanayoambatana na kutapika huku???
Asanteni.

Wewe umeshampa mimba au ameshapewa mimba, unataka kumpa mimba mbili kwa wakati mmoja?

Huyo mtoto anapata vishindo tumboni, akitokea kuwa toto tundu, mtajiuliza sababu ni nini!! Mnamfundisha utundu akiwa tumboni..
 
Wewe umeshampa mimba au ameshapewa mimba, unataka kumpa mimba mbili kwa wakati mmoja?

Huyo mtoto anapata vishindo tumboni, akitokea kuwa toto tundu, mtajiuliza sababu ni nini!! Mnamfundisha utundu akiwa tumboni..

Kuwa mtaarabu basi japo kidogo ndugu yangu,huh!
Hivi ndivyo jukwaa hili linavyozidi kuzeeka na mwishowe,litakuwa kijiwe cha kupiga soga.Sidhani kama kuna ulazima wa kuchangia ikiwa mtu huoni haja ya kumsaidia mwenzako.
 
Mzee unapiga kama za ronaldhinho wakati mama tayari yuko hoi? punguza bana, piga tu haste haste kwa afya yake na ya kiumbe kilichopo huko ndani.
 
Habari zenu

Wapendwa naujauzito wa mwezi na nusu,inanisumbua natapika sana yaani kula cwezi na nikila natapika.watu wananishauri nitoe kwani naweza poteza kazi kwa hali hiyo.jamani kuna tiba kwa hili tatizo.nisaidieni sipend kuitoa.
 
Mh..jf we siku imeanza tulivu ya alhamic..umeolewa?ebu jiulize mama yako angetoa mimba yako ungekuwa hapa leo..watu wanalilia watoto kila siku wewe unataka kutoa..kaa utulie lea hiyo mimba ni miezi 3 tu ya misukosuko yote yatakwisha..ukiona shida kunywa vitu vichachu..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom