Mwanamke mjamzito kupata kichefuchefu na kutapika: Chanzo na tiba yake

Kahema

JF-Expert Member
May 21, 2010
202
43
Swali No 1
Tafadhari naombeni msaada kwa yeyote anayejua nini chanzo cha mama mjamzito kutapika na kichefuchefu kila mara.

Kama kuna dawa please nisaidieni nijue kwani nina ndugu yangu anapata taabu sana.

Swali No 2 kutoka kwa sijui nini

Salaam wanaJF, mi ni mara yangu ya kwanza ndani ya jukwaa hili.

Nina tatizo moja naombeni ushauri wenu, tunatarajia kupata mtoto wa kwanza mwezi ujao Mungu akipenda, ila tatizo linakuja mke wangu anatapika sana hqasa kipindi hiki cha miezi ya mwishoni (hapo mwanzo alikuwa poa kabisa) ila tangu alipoingia kwemye mwezi wa saba hivi akaanza kutapika.

Ilianza kwa kudai anasikia kiungulia sana na baadae ikamletea kutapika, nilimpeleka hospital wakasema ni hali ya kawaida na wakampa dawa za kuzuia kutapika na kiungulia na kweli ile hali ikapoa ila baada ya mguda mfupi tu ikarudi tena, tukaenda tena wakampa dawa kiungulia kikaisha kabisa ila ikabaki kutapika.

Nikimuuliza mke wangu kama ana chochote cha ziada anachojisikia kama maleria au kuumwa kitu kingine chochote anadai hamna kabisa yuko poa na hajisikii kuumwa popote ila bado anatapika, hospitali wanasema ni hali ya kawaida na inatokea ila mpaka napata wasiwasi (unajua tena ndo first born anakuja).

Yaani anaweza kukaa nyumbani wiki moja au mbili inayofta yupo hospitali wamemlaza kumuwekea drip za maji (wakati mwengine na sindano za kuzuia kutapika) yaani hali ndo hivyo.

Sasa kama kuna ushauri mwingine wowote please nisaidieni waungwana.

Swali No. 3 kutoka kwa MsakaGamba

Habari zenu mabibi na mabwana.

Naomba msaada wenu wa hali na mali wenye michango yakinifu na yenye mashiko itakayo nisaidia kumtibu mke wangu.

Mwenzangu kila anapo kuwa mjamzito huwa anasumbuliwa sana na kutapika, mimba ya kwanza ilikuwa balaa sana maana alianza kutapika ikiwa na mwezi mmoja na hali hiyo ikaendelea mpaka alipofikisha miezi tisa. Ilikuwa kila anacho kula hakikai anatapika kiasi kwamba ilifika wakati akawa anatundikiwa drip ya maji ambayo imechanganywa na dawa ya kuzuia kutapika na haikuwa inampa nafuu ya kudumu.

Niliambiwa kwa sababu ni mimba ya kwanza nivumilie, nimekaa apumzike miaka 5 kwa kuwa niliigopa sana ile hali lakini pia kuweka interval nzuri kati ya mtoto wa kwanza nawa pili.

Tumeamua tupate mtoto wa pili ila kinacho nishangaza mwezi bado niwa kwanza na ameanza tena kutapika kama kipindi akiwa na ujauzito wa kwanza! Kwa sasa kila anachokula anatapika, hii inanipa woga kuwa huenda akazoofu kama jinsi alivyo kuwa kwenye mimba ya kwanza.

Wabobezi na wataalamu wa haya maswala naombeni msaada wenu. Miaka 5 iliyo pita sikuwa memba humu. Hivyo naomba jf dokta iwe msaada kwangu katika kipindi hiki kigumu kwangu.

Naomba watakao changia wawe ambao wako tayari kunisaidia kwa ushauri/dawa au matibabu. SITAKI DHIHAKA TAFADHARI.

Swali No 4 gidytitus - Mjamzito kutapika baada ya tendo la ndoa

Wataalam wa afya na wale wakongwe waliomo kwenye ndoa kwa muda mrefu naombeni ushauri wa kitaalam na kiuzoefu!

Mke wangu anatapika mara nyingi baada ya tendo la ndoa hasa pale anapokuwa na amefikia mshindo (Kileleni) au kumaliza.

Hali hii imeanza kumtokea akiwa na ujauzito wa miezi 5, na kwa kuwa sisi ni wageni katika hii taasisi ya ndoa tumekuwa na hofu na mara nyingine kudhani kuwa ni disorders za preg but kwa kweli inatupa hofu na mara nyingine hata kuogopa kufurahia tuzo yetu tulopewa na mwenyezi Mungu.

Tunaomba ushauri, Je kuna madhara yanayoambatana na kutapika huku?

Asanteni.

Mchango,Maoni ya WanaJF

Mkuu gidytitus Je, ujauzito sasa hivi umefikia wiki ngapi?

Kama kutapika kunasababishwa na tendo la ndoa ninakushauri uahirishe tendo hilo kwa kipindi kilichobaki. Hii ni kwasababu ukiendelea inaweza kusababisha premature birth ambayo itakuwa na madhara kwa mtoto iwapo hatapata neonatal support ya kiwango.

Kiujumla, katika ujauzito mwili wa mwanamke hubadilika kwa namna mbalimbali na iwapo kuna chochote kinachomletea madhara basi solution yake ni kuacha nacho.

Kutapika sio kitu cha kawaida, ni dalili ya tatizo na kutapika itself kunaweza kuleta matatizo zaidi ya kiafya.

Chanzo cha mama mja mzito kutapika au kujihisi kutapika (kichefuchefu) ni mabadiliko ya mfumo wa hormone mwilini mwa mwanamke anapopata ujauzito.

Mzunguko wa mwezi wa mwanamke unatawaliwa na hormones (follicle stimulating hormone, lutenizing hormone, estrogen na progesterone) ambazo levels zake kwenye damu zinbadilika kutokana na kipindi cha mzunguko.

Lakini pindi anapopata mimba kunakuwa na mabadiliko ya baadhi ya hizi hormones (zinapungua sana kiasi chake kwenye damu au kupotea kabisa), na hormone inaitwa human chorionic gonadotropin inakuwa kwa kiasi kikubwa kwenye damu na kuchochea hali hiyo.

Haya mabadiliko huwa yanatokea miezi miwili hadi mitatu ya kwanza ya ujauzito, na ndio katika kipindi hicho mwanamke mwenye ujauzito anajisikia kichefuchefu, kutapika na mabadiliko mengine mfano kukosa usingizi, kula sana au kutokula, hamu ya kula vitu kama udongo etc.

Kama anatapika sana kiasi cha kuhatarisha kupoteza maji na/au madini mwilini (hyperemesis gravidarum) basi mgonjwa atahitaji sindano za kuzuia kutapika (antiemetic) na/au drip za kuongeza maji.

Kutapika ni dalili inayojitokeza kwa mama mjamzito hasa kipindi cha awali ingawa tatizo la kutapika au kuhisi kichefuchefu linaweza kutokea katika maradhi mengine mbali na ujauzito.

Hali ya kutapika kwa mama mjamzito imegawanyika katika makundi mawili.Kwanza ni kichefuchefu na kutapika wakati wa kipindi cha mwanzo cha ujauzito ( Early pregnancy) na pili ni kipindi baada ya hicho cha awali (Late pregnancy).

Tukiingia kiundani kila kundi limegawanyika katika sehemu mbili.Ingawa hatutazama ndani zaidi,ila jambo la msingi ni kwamba katika hali ya awali (Early pregnancy),kutapika na hali ya kichefuchefu inaweza kuwa ya kawaida na isimletee shida kubwa mama (Morning sickness) na kutapika kidogo (emesis Gravidarum) na kuwa mgonjwa hata asiweze kufanya shughuli nyingine.

Mama huumwa hadi kuishiwa maji mwilini kwa kutema mate,kutapika na kushindwa kula na wakati mwingine hulazwa hospitali, hali hii huitwa kitalaam “Hyperemesis gravidarum.”

Yapo magonjwa mengine yanayosababisha kichefuchefu na kutapika ambayo yanaweza kumpata mama mjamzito na asiye mjamzito.
Magonjwa haya ni kama vile minyoo (Intestrial Infestations) maambukizi ya njia ya mkojo(Urinary Track infections),magonjwa ya

ini(Hepatitis),ugonjwa wa kisukari (pale sukari inapokuwa juu) (Ketoacidosis of Diabetes),mkojo kuingia katika mfumo wa damu(uraemia),ugonjwa wa kidole tumbo (Appendicitis),vidonda vya tumbo (peptic ulcer) kuziba kwa tumbo (Intestnal obstruction) matatizo ya nyonga kifuko cha mayai (Twisted Ovarian cyst) na uvimbe katika kizazi (uterine fibroid).

Kutapika kunakoendelea wakati wa ujauzito (late pregnancy) huwa ni muendelezo wa hali hiyo.Tangu mwanzoni hali ya awali (Early pregnancy) hutokea mimba inapokuwa chini ya miezi minne lakini hii hali ya pili ‘Late pregnancy inatokea mimba inapokuwa zaidi ya miezi minne.Hapa mama huendelea tu kutapika na vilevile inahusiana na dalili za magonjwa mengine kama dalili za awali za kifafa cha mimba.

CHANZO CHA TATIZO
Mbali na maradhi mengine yanayohusiana na tatizo hili la kutapika wakati wa ujauzito,chanzo cha ugonjwa au tatizo hili ni pale mimba inapokuwa changa hadi baada ya kufikisha kati ya miezi mitatu na minne inakoma au ina weza kuendelea hadi miezi sita au hadi mama anapojifungua.

Tatizo hili linaweza kutokea katika mimba ya kwanza tu,wengine hutokea ya pili au wengine hutokea mimba zote.
Hali hii au tatizo hili linaweza kusababishwa na kuwepo kwa kiasi kikubwa cha hormone au kichocheo cha HCG mwilini au Human Chronic Gonadotrophin ambacho kikizidi kinakuwa sumu na kuanza kuchefua mwilini.

Hali ya kisaikolojia (psychogenic) pia huchangia kuamsha kichefuchefu kwa kutotamani baadhi ya vitu au vyakula au harufu.

Mama akiwa na hali hii hasa vyakula vya wanga hasa nyakati za usiku,asubuhi ataamka na njaa na kichefuchefu na kuanza kutapika na kuchoka.

Chakula cha wanga kama wali na ugali ni muhimu kwani vinatia nguvu na joto,vilevile uwepo wa vitamini B za kutosha nao husaidia sana.

Tatizo hili la kichefuchefu na kutapika pia huchangiwa na mzio (Allergies ) mbalimbali na tumbo kutofanya kazi vizuri (Decreased gastric motility).

NINI CHA KUFANYA

Hali hii ni tatizo sugu kwa baadhi ya akinamama kwani kila wapatapo mimba inakuwa shida.Tatizo hili linapoanza na ukawahi kumuona Daktari haliwezi kusumbua kwa kiasi kikubwa.

Mgonjwa atachunguzwa kama ana baadhi ya maradhi tuliyoyaeleza au kama kuna hitilafu zozote zilizosababishwa na ugonjwa.Mgonjwa baada ya uchunguzi atapatiwa tiba kadiri daktari atakavyoona inafaa.

Tiba mojawapo ni kuongezewa maji na dawa zitakazomsaidia kuondoa au kupunguza kasi ya kichefuchefu.
Mgonjwa akazane kula hasa vyakula vya jamii ya wanga pale hali inapokuwa nafuu,kunywa maji mengi na mara kwa mara ili hata kama hali hiyo itajirudia awe salama asisumbuke sana.

Je, umri wa hiyo mimba ni wiki ngapi? Kama bado ni mimba changa(below or around 12 weeks) ni kawaida kwa mjamzito kuexperience hali hiyo.

Je, ameshaanza clinic? Kama bado, nakushauri aanze clinic, na huko atapata msaada zaidi kuhusu hali hiyo.

Mara nyingine kunakuwa na vitu vinavyosababisha hali hiyo ya kutapika kuzidi sana, kama vile mimba ya mapacha,na matatizo yanayohusiana na mimba.

Aende hospitali afanyiwe na vipimo ikiwemo ultra sound ya hiyo mimba ili ku-rule out vitu kama ujauzito wa mapacha(multiple gestation), then daktari atamuanzishia dawa kadri inavyofaa na kwa dosage sahihi, usikubali kumuanzishia dawa tuu kienyeji, kila mgonjwa ni tofauti na daktari atatoa dawa sahihi na dozi sahihi kulingana na ugonjwa, na atamuongezea dozi au dawa au kumpunguzia kadri ya maendeleo yake yatakavyokuwa.

Nakutakia malezi mema ya ujauzito wa mkeo, umtunze na kumuangali vizuri zaidi katika kipindi hiki, ahsante sana
 
Hutokana na mabadiliko ya mlingano/uwiano wa vichocheo (hormones) wakati wa ujauzito, kuna baadhi ya vichocheo vinapanda kwa kiasi kikubwa na kusababisha kichefuchefu na kutapika.

Dawa za kuzuia kutapika zilizo nyingi huleta usingizi na kulegea mwili, lakini kunabaadhi cheche hazina tabia hiyo, kwa mfano dawa inaitwa NOZICK, ni vema ukakurana na dakitari bingwa wa akina mama i.e OBSTETRICIAN.
 
Asante ndugu yangu, mwanzo mzuri.
 
Chanzo cha mama mja mzito kutapika au kujihisi kutapika (kichefuchefu) ni mabadiliko ya mfumo wa hormone mwilini mwa mwanamke anapopata ujauzito.

Mzunguko wa mwezi wa mwanamke unatawaliwa na hormones (follicle stimulating hormone, lutenizing hormone, estrogen na progesterone) ambazo levels zake kwenye damu zinbadilika kutokana na kipindi cha mzunguko.

Lakini pindi anapopata mimba kunakuwa na mabadiliko ya baadhi ya hizi hormones (zinapungua sana kiasi chake kwenye damu au kupotea kabisa), na hormone inaitwa human chorionic gonadotropin inakuwa kwa kiasi kikubwa kwenye damu na kuchochea hali hiyo.

Haya mabadiliko huwa yanatokea miezi miwili hadi mitatu ya kwanza ya ujauzito, na ndio katika kipindi hicho mwanamke mwenye ujauzito anajisikia kichefuchefu, kutapika na mabadiliko mengine mfano kukosa usingizi, kula sana au kutokula, hamu ya kula vitu kama udongo etc.

Kama anatapika sana kiasi cha kuhatarisha kupoteza maji na/au madini mwilini (hyperemesis gravidarum) basi mgonjwa atahitaji sindano za kuzuia kutapika (antiemetic) na/au drip za kuongeza maji.
 
Chanzo cha mama mja mzito kutapika au kujihisi kutapika (kichefuchefu) ni mabadiliko ya mfumo wa hormone mwilini mwa mwanamke anapopata ujauzito. Mzunguko wa mwezi wa mwanamke unatawaliwa na hormones (follicle stimulating hormone, lutenizing hormone, estrogen na progesterone) ambazo levels zake kwenye damu zinbadilika kutokana na kipindi cha mzunguko. Lakini pindi anapopata mimba kunakuwa na mabadiliko ya baadhi ya hizi hormones (zinapungua sana kiasi chake kwenye damu au kupotea kabisa), na hormone inaitwa human chorionic gonadotropin inakuwa kwa kiasi kikubwa kwenye damu na kuchochea hali hiyo. Haya mabadiliko huwa yanatokea miezi miwili hadi mitatu ya kwanza ya ujauzito, na ndio katika kipindi hicho mwanamke mwenye ujauzito anajisikia kichefuchefu, kutapika na mabadiliko mengine mfano kukosa usingizi, kula sana au kutokula, hamu ya kula vitu kama udongo etc.

Kama anatapika sana kiasi cha kuhatarisha kupoteza maji na/au madini mwilini (hyperemesis gravidarum) basi mgonjwa atahitaji sindano za kuzuia kutapika (antiemetic) na/au drip za kuongeza maji.
thanks man. good advice.
 
Good explanation man!
 
Salaam wanaJF, mi ni mara yangu ya kwanza ndani ya jukwaa hili.

Nina tatizo moja naombeni ushauri wenu, tunatarajia kupata mtoto wa kwanza mwezi ujao Mungu akipenda, ila tatizo linakuja mke wangu anatapika sana hqasa kipindi hiki cha miezi ya mwishoni (hapo mwanzo alikuwa poa kabisa) ila tangu alipoingia kwemye mwezi wa saba hivi akaanza kutapika.

Ilianza kwa kudai anasikia kiungulia sana na baadae ikamletea kutapika, nilimpeleka hospital wakasema ni hali ya kawaida na wakampa dawa za kuzuia kutapika na kiungulia na kweli ile hali ikapoa ila baada ya mguda mfupi tu ikarudi tena, tukaenda tena wakampa dawa kiungulia kikaisha kabisa ila ikabaki kutapika.

Nikimuuliza mke wangu kama ana chochote cha ziada anachojisikia kama maleria au kuumwa kitu kingine chochote anadai hamna kabisa yuko poa na hajisikii kuumwa popote ila bado anatapika, hospitali wanasema ni hali ya kawaida na inatokea ila mpaka napata wasiwasi (unajua tena ndo first born anakuja).

Yaani anaweza kukaa nyumbani wiki moja au mbili inayofta yupo hospitali wamemlaza kumuwekea drip za maji (wakati mwengine na sindano za kuzuia kutapika) yaani hali ndo hivyo.

Sasa kama kuna ushauri mwingine wowote please nisaidieni waungwana.
 
Kwa kweli dawa ya kutibu kuacha kutabikakwa mjamzito ni ngumu kwa sabababu ni mabadiriko ya hormone kwenye mwili,cha msingi hospitali wakupe dawa za kuzuia kutapika,atumie machungwa,akitapika sana nenda waongeze drip,vinginevyo ni kwa miujiza ya Mungu.
 
Lakini umeenda kwa wataalamu wa masuala ya uzazi au ni hospitali tu ili mradi? Najua kutapika huwa ni kawaida lakini hadi kufikia ilo la kuwekewa drip,..
 
Tumejaribu kwenda hospitali za serikali na sasa tumeamua kwenda za binafsi pia..zote wanasema ni hali ya kawaida tu na wamempima wanasema hawaoni tatizo lolote na isitoshe wanasema dogo(mtoto) yuko poa kabisa na wameshapiga mapa tarehe inayowezekana akajifungua kutokana na hali ya mtoto ...ila hata mimi huku kutapika huku..!?? lah..:A S-confused1:
 
Dada walichokuambia ni ukweli kabisa ni mambo ya kawaida ukiwa mjamzito acha mawazo jitahidi kunywa maji,juice, na kula vyakutosha wakati unapoacha kutapika kurudisha maji na madini unayopoteza ukitapika.
 
dada walichokuambia ni ukweli kabisa ni mambo ya kawaida ukiwa mjamzito acha mawazo jitahidi kunywa maji,juice, na kula vyakutosha wakati unapoacha kutapika kurudisha maji na madini unayopoteza ukitapika.
Asante...ila nikurekebishe kidogo am not she!! otherwise thanks na nitajaribu kumshauri hivyo..
 
Hakuna shida ujumbe niliuelekeza kwa mhusika ndo maana nikasema she,hata hivyo wewe na yeye ni mwili mmoja mnaweza tumia she/he kwa pamoja maadam hakuna madhara.
 
Kwa kawaida kutapika hotokea sana miezi minne ya mwanzo, na baadaye huenda kunapungua kadri mimba inavyokua. Kama umeanza kutapika miezi ya mwishoni ni vizuri kwenda kwa wataalamu waliobobea kwenye magonjwa ya kina mama na uzazi utasaidiwa.
 
Pole kaka ila ni jambo la kawaida kwani kila mimba inapotunga huwa na vibwanga vyake wengine wanakuwa wako powa hawana shida huwaoni wakitapika wala kutematema mate ama kuchagua vyakula, wengine ni kulala hasira sizizo kuwa na kichwa wala miguu, wengine jambo kidogo tu ni kulia utafikiri kafiwa.

Wengine kutapika mwanzo hadi mwisho anapojifungua na wengine miezi ya mwisho hutapika sana na kuchangua vyakula kama ndio kwanza mimba imetunga,ama wengine ni bedi resti mwanzo mwisho hivyo hiyo ya wifi yetu ni jambo la kawaida usiwe na wasiwasi huwa inatokea cha kumsisitiza ale vizuri na ikitokea kuna vitu anavyovimenda avile kwa wingi maji mengi ni mihimu na matunda kwa wingi.

Ikiwa mtakuwa na wasiwasi na hicho kijacho cha mwanzo ni vizuri mkaenda kwa madaktari bingwa wa kinamama watawasaidia, ila kwa upande wangu ni kawaida sana kwenye hiyo hali, wapo marafiki zangu wakaribu waliokuwa na hiyo hali.
 
Pole kaka ila ni jambo la kawaida kwani kila mimba inapotunga huwa na vibwanga vyake wengine wanakuwa wako powa hawana shida huwaoni wakitapika wala kutematema mate ama kuchagua vyakula, wengine ni kulala hasira sizizo kuwa na kichwa wala miguu, wengine jambo kidogo tu ni kulia utafikiri kafiwa, wengine kutapika mwanzo hadi mwisho anapojifungua na wengine miezi ya mwisho hutapika sana na kuchangua vyakula kama ndio kwanza mimba imetunga,ama wengine ni bedi resti mwanzo mwisho hivyo hiyo ya wifi yetu ni jambo la kawaida usiwe na wasiwasi huwa inatokea cha kumsisitiza ale vizuri na ikitokea kuna vitu anavyovimenda avile kwa wingi maji mengi ni mihimu na matunda kwa wingi.

ikiwa mtakuwa na wasiwasi na hicho kijacho cha mwanzo ni vizuri mkaenda kwa madaktari bingwa wa kinamama watawasaidia, ila kwa upande wangu ni kawaida sana kwenye hiyo hali, wapo marafiki zangu wakaribu waliokuwa na hiyo hali.
Asante mkuu..nitafanya hivyo!!
 
Habari za majukumu wana Jf. Nina rafiki yang ana Ujauzito wa Miezi miwili inaelekea mitatu,tatizo lake ni kwamba huwa anatapika kila wakati anapokula au kunywa maji. Hali hiyo amekua nayo baada ya wiki kama kupita tokea apate huo ujauzito.

Mwenye kufahamu suluhisho au ushauri wa kupunguza tatizo hilo naomba msaada.
 
Hii ni kawaida hasa katika miezi mitatu ya mwanzo, na hasa kwa mimba za kwanza. Hali hii huitwa morning sickness. Lakini inapozidi sana kiasi cha kuchosha itahitaji msaada wa daktari,hali hii huitwa hyperemisis gravidarum.
So kama ni serious hadi kutapika kila kitu na kila wakati mjamzito apelekwe kituo cha tiba haraka !
 
Lakn kwann utolee mfano mwenzako wakati muhanga niwewe mwenyewe? Haya fuata ushaur huo hapo juu.
 
Hii ni kawaida hasa katika miezi mitatu ya mwanzo, na hasa kwa mimba za kwanza. Hali hii huitwa morning sickness. Lakini inapozidi sana kiasi cha kuchosha itahitaji msaada wa daktari,hali hii huitwa hyperemisis gravidarum.
So kama ni serious hadi kutapika kila kitu na kila wakati mjamzito apelekwe kituo cha tiba haraka !

Kuongezea hapo ajitahidi kunywa maji ya kutosha,kutumia dawa za kuzuia kutapika,kula chakula kidogokidogo badala ya kula chakula kingi kwa wakati mmoja.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom