Mwanamke mjamzito kupata kichefuchefu na kutapika: Chanzo na tiba yake

Aende kwa daktar kuna dawa znaitwa nosic ztamsaidia kutoa adha zote za mimba
 
Mkuu hiyo hali ni kawaida kwa baadhi ya wanawake hasa kwenye first trimester ( kipindi cha miezi 3 ya kwanza ya mimba ) itakwisha au kwa wengine inaendelea kwa kipindi chote cha ujauzito ila anaweza kutumia vidonge vya Nosic kutwa mara 2 kwa siku 5 au vidonge vya Vomidoxin.

Ni kweli dawa hizi ni sahihi kbsa
 
Salaam wakuu,mke wangu ana ujauzito wa mwezi 1,lakini ana matatizo mawili yanayomsumbua sana,kichefuchefu muda wote hujisikia kutapika,mdomo kujaa mate muda wote,je kuna dawa yeyote kuzuia hali hii isiendelee?naomba msaada wa mawazo tafadhali.
Kujisikia kichefuchefu na kutapika wakati wa ujauzito (Morning Sickness)

Nusu ya wanawake wote wajawazito hupatwa na tatizo la kujisikia kichefu chefu na kutapika; ni mojawapo ya dalili kuu za ujauzito.


Husababishwa na kuongezeka kwa hormone mwilini, mara nyingi huanza katika wiki ya sita ya ujauzito na huweza kutokea muda wowote wa siku.


Madaktari wengine huwa wanaamini ya kuwa ni dalili nzuri kwani humaanisha ya kuwa placenta inafanya kazi vizuri.


Kwa wanawake wengine tatizo hili huisha katika wiki ya kumi na mbili ya ujauzito. Lakini kwa wengine huweza kuendelea kwa kipindi kizima cha ujauzito.


Mara nyingi ni kitu cha kawaida ambacho kinakuja na kuondoka lakini pale ambapo mama anatapika kupita kiasi mpaka anashindwa kubakisha chakula au maji mwilini basi anahitaji kumuona daktari.





Vitu vya kufanya kusaidia au kupunguza tatizo hili:



  1. Kula milo mingi midogo mara kwa mara badala ya kula milo mikuu mitatu kwa siku. Hii itasaidia kwasababu wakati mwingine tatizo hili linasababishwa na kutokuwa na sukari ya kutosha kwenye damu(low blood pressure). Sukari hii ndio chanzo cha nguvu mwilini. Ukila mara kwa mara chakula kitapokelewa mwilini na kutengenezwa sukari na mwili kuwa na nguvu ya kutosha.
  2. Kunywa vinywaji nusu saa kabla au baada ya chakula. Usinywe vinywaji na kula chakula kwa wakati mmoja.
  3. Kula mkate wa kukausha(toast au crackers) au matunda yaliyokaushwa dakika 15 kabla ya kumka asubuhi.
  4. Kunwya maji mara kwa mara ili kuzuia mwili kuishiwa na maji (dehydradtion). Jaribu kunywa litre 2.5 kwa siku ikiwa pamoja na maji, chai au juice natural zisizo na sukari ya kuongeza.
  5. Jitahidi usile au kupita sehemu zenye harufu ya chakula zinazozidisha tatizo hili.
  6. Pumzika vya kutosha na pata usingizi wa mchana.
  7. Usikae sehemu zenye joto jaribu kukaa ndani kwenye feni au ac au nje sehemu zenye upepo. Kwasababu joto huzidisha tatizo hili. Pia usiende sehemu zenye watu wengi.
  8. Ndimu, tangawizi zinasaidia, pia unaweza kunywa maji ya ndimu au kula tunda la tikiti maji (watermelon) kupunguza kichefu chefu.
  9. Kula viazi vya kukausha na chumvi.
  10. Fanya mazoezi.
  11. Usilale baada ya mlo
  12. Usiache kula
  13. Usile au kupika vyakula vyenye pili pili (spicy) au mafuta mengi.
  14. Usinywe kahawa au vinywaji vikali
  15. Kula vyakula vya protein kabla ya kwenda kulala usiku
  16. Fungua madirisha au Tembea nje ili kupata upepo na oxygen ya kutosha.
  17. Weka kijiko kimoja cha maji ya Apple Cider Vinegar kwenye 8 ounces ya maji ya uvuguvugu kisha kunywa asubuhi kabla ya kuamka.

[TD] [/TD]



18. Kunywa chai za Rasberry leaf, Spear mint/ pepper mint, Anise seed, Fennel seed kabla ya kuamka asubuhi.
[TR]
[TD] [/TD]



[TR]
[TD] [/TD]





[TR]
[TD] [/TD]







Umwone daktari kama:


Unatapika kupita kiasi mpaka unashindwa kubakisha chakula au maji tumboni au kama kutapika kunaambatana na homa au maumivu.Mwanamke, Uzazi na Afya ("Healthy Living"): Afya
 
Nosic ni dawa nzuri sana kwa kichefuchefu cha ujauzito. Maana kuna kichefuchefu kingine kikikupata unataman hata kulia, kutapika hutapiki ila cha moto unakiona.

Dah... hii hali ilinisimbua mpaka nikakosa hamu ya mtoto aise... usiombe
 
ni hali ya kawaida na ukimuona mjamzito anapitia hali hiyo utamuonea huruma.Pata ushauri wa daktari. au pia sisi tuna virutubisho ambavyo ni pure Asili vya kukusaidia wkt unapitia hali hiyo.Tunapatikana kupitia 0719 252523
 
Jf Doctors

Naomba kujua dawa ya kusimamisha kutapika kipindi cha ujauzito kwani hali ya wife si shwari, mpaka amekonda
 
Kitaalamu inaitwa emesis gravidarum/hyperemesis gravidarum ni vizur mama aende hosp wakamcheki kama anamagonjwa mengne kama malaria,Uti nk na kama ameshakonda ni dalili mbaya vizuri aende amwone dr ili kama una uwezekano wa kuongezea maji kwa njia ya mishipa.

Kuna dawa kama vile promethazine/phenergan,metoclopromide ila vizuri aende hosp kwanza.
 
nawashukuru wana JF kwa msaada wenu. Wife anafurahia uumbaji sasa. Tunatarajia mapacha tena hiv karibuni. Ndo kazi iliyobaki kujaza dunia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom