Mwanamke mjamzito kupata kichefuchefu na kutapika: Chanzo na tiba yake

Ushauri mzuri sana hasa Wa kumueleza aanze kutumia folic acid, tumekuwa tukishauri sana matumizi ya folic acid in early pregnancy! Nakugongea thanks shosti ila natumia mchina hapa

u r welcome love. Thanks for your support. Pamoja Tunaweza. :*
 
u r welcome love. Thanks for your support. Pamoja Tunaweza. :*

Thanks dear, keep on taking pregnacare iron ni muhimu kuongeza damu, tunashauri pia kuendelea kutumia hata wiki sita baada ya kujifungua. Ubarikiwe sana
 
Habari zenu mabibi na mabwana.

Naomba msaada wenu wa hali na mali wenye michango yakinifu na yenye mashiko itakayo nisaidia kumtibu mke wangu.

Mwenzangu kila anapo kuwa mjamzito huwa anasumbuliwa sana na kutapika, mimba ya kwanza ilikuwa balaa sana maana alianza kutapika ikiwa na mwezi mmoja na hali hiyo ikaendelea mpaka alipofikisha miezi tisa. Ilikuwa kila anacho kula hakikai anatapika kiasi kwamba ilifika wakati akawa anatundikiwa drip ya maji ambayo imechanganywa na dawa ya kuzuia kutapika na haikuwa inampa nafuu ya kudumu.

Niliambiwa kwa sababu ni mimba ya kwanza nivumilie, nimekaa apumzike miaka 5 kwa kuwa niliigopa sana ile hali lakini pia kuweka interval nzuri kati ya mtoto wa kwanza nawa pili.

Tumeamua tupate mtoto wa pili ila kinacho nishangaza mwezi bado niwa kwanza na ameanza tena kutapika kama kipindi akiwa na ujauzito wa kwanza! Kwa sasa kila anachokula anatapika, hii inanipa woga kuwa huenda akazoofu kama jinsi alivyo kuwa kwenye mimba ya kwanza.

Wabobezi na wataalamu wa haya maswala naombeni msaada wenu. Miaka 5 iliyo pita sikuwa memba humu. Hivyo naomba jf dokta iwe msaada kwangu katika kipindi hiki kigumu kwangu.

Naomba watakao changia wawe ambao wako tayari kunisaidia kwa ushauri/dawa au matibabu. SITAKI DHIHAKA TAFADHARI.
 
[h=3]Kujisikia Kichefu chefu na Kutapika wakati wa ujauzito (Morning Sickness)[/h]
Nusu ya wanawake wote wajawazito hupatwa na tatizo la kujisikia kichefu chefu na kutapika; ni mojawapo ya dalili kuu za ujauzito.

Husababishwa na kuongezeka kwa hormone mwilini, mara nyingi huanza katika wiki ya sita ya ujauzito na huweza kutokea muda wowote wa siku.

Madaktari wengine huwa wanaamini ya kuwa ni dalili nzuri kwani humaanisha ya kuwa placenta inafanya kazi vizuri.

Kwa wanawake wengine tatizo hili huisha katika wiki ya kumi na mbili ya ujauzito. Lakini kwa wengine huweza kuendelea kwa kipindi kizima cha ujauzito.

Mara nyingi ni kitu cha kawaida ambacho kinakuja na kuondoka lakini pale ambapo mama anatapika kupita kiasi mpaka anashindwa kubakisha chakula au maji mwilini basi anahitaji kumuona daktari.

[h=4]Vitu vya kufanya kusaidia au kupunguza tatizo hili:[/h]
  1. Kula milo mingi midogo mara kwa mara badala ya kula milo mikuu mitatu kwa siku. Hii itasaidia kwasababu wakati mwingine tatizo hili linasababishwa na kutokuwa na sukari ya kutosha kwenye damu(low blood pressure). Sukari hii ndio chanzo cha nguvu mwilini. Ukila mara kwa mara chakula kitapokelewa mwilini na kutengenezwa sukari na mwili kuwa na nguvu ya kutosha.
  2. Kunywa vinywaji nusu saa kabla au baada ya chakula. Usinywe vinywaji na kula chakula kwa wakati mmoja.
  3. Kula mkate wa kukausha(toast au crackers) au matunda yaliyokaushwa dakika 15 kabla ya kumka asubuhi.
  4. Kunwya maji mara kwa mara ili kuzuia mwili kuishiwa na maji (dehydradtion). Jaribu kunywa litre 2.5 kwa siku ikiwa pamoja na maji, chai au juice natural zisizo na sukari ya kuongeza.
  5. Jitahidi usile au kupita sehemu zenye harufu ya chakula zinazozidisha tatizo hili.
  6. Pumzika vya kutosha na pata usingizi wa mchana.
  7. Usikae sehemu zenye joto jaribu kukaa ndani kwenye feni au ac au nje sehemu zenye upepo. Kwasababu joto huzidisha tatizo hili. Pia usiende sehemu zenye watu wengi.
  8. Ndimu, tangawizi zinasaidia, pia unaweza kunywa maji ya ndimu au kula tunda la tikiti maji (watermelon) kupunguza kichefu chefu.
  9. Kula viazi vya kukausha na chumvi.
  10. Fanya mazoezi.
  11. Usilale baada ya mlo
  12. Usiache kula
  13. Usile au kupika vyakula vyenye pili pili (spicy) au mafuta mengi.
  14. Usinywe kahawa au vinywaji vikali
  15. Kula vyakula vya protein kabla ya kwenda kulala usiku
  16. Fungua madirisha au Tembea nje ili kupata upepo na oxygen ya kutosha.
  17. Weka kijiko kimoja cha maji ya Apple Cider Vinegar kwenye 8 ounces ya maji ya uvuguvugu kisha kunywa asubuhi kabla ya kuamka.

Maji ya Apple Cider Vinegar

18. Kunywa chai za Rasberry leaf, Spear mint/ pepper mint, Anise seed, Fennel seed kabla ya kuamka asubuhi.
chai ya raspberry leaf
chai ya anise seed

chai ya fennel seed

Umwone daktari kama:

Unatapika kupita kiasi mpaka unashindwa kubakisha chakula au maji tumboni au kama kutapika kunaambatana na homa au maumivu.

Source: MwanamkeUzazi
 
Mimi sio dr ila nilipatwa na hali kama iyo ya kutapika kuanzia mwezi wa kwanza hadi wa sita,nilijaribu kuzunguka hosp mbalimbali maana hiyo hali ilinidhoofisha sana.mwisho wa siku nilienda muhimbili nikaonana na Dr Ngarina akaniandikia dawa ya maji inaitwa PHAMACTIN toka siku iyo sikuwah tapika tena na nilikula vyakula vya kila aina.jaribu kumtafutia mkeo iyo dawa huenda ikamsaidia pia.ila ni vyema kabla hajaitumia mkaonana na gyner ili awaambie kama itamfaa.pole sana
 
Licha ya hayo kama hutaki atapike ulimpa mimba yanini? Wakati unajua fika kwamba ni lazima hiyo hali itokee. Na umeshaambiawa kuwa nusu ya wanawake wote huwa wanatapika wakiwa katika hali ya ujauzito. Cha kushangaza wewe unataka mtoto bila hali hiyo.
 
Mimi sio dr ila nilipatwa na hali kama iyo ya kutapika kuanzia mwezi wa kwanza hadi wa sita,nilijaribu kuzunguka hosp mbalimbali maana hiyo hali ilinidhoofisha sana.mwisho wa siku nilienda muhimbili nikaonana na Dr Ngarina akaniandikia dawa ya maji inaitwa PHAMACTIN toka siku iyo sikuwah tapika tena na nilikula vyakula vya kila aina.jaribu kumtafutia mkeo iyo dawa huenda ikamsaidia pia.ila ni vyema kabla hajaitumia mkaonana na gyner ili awaambie kama itamfaa.pole sana

Una namba ya huyo Dr Ngalina?! Na huyo gyner ni nani maana hapa huja mtolea maelezo lakini umeniambia nimuone! Labda kama sija kuelewa vizuri?
 
Una namba ya huyo Dr Ngalina?! Na huyo gyner ni nani maana hapa huja mtolea maelezo lakini umeniambia nimuone! Labda kama sija kuelewa vizuri?
Not neccesary umuone uyo ngarina..u can check with any gyner na umuulize khs iyo dawa.Namba ya NGARINA 0713406267
 
Una namba ya huyo Dr Ngalina?! Na huyo gyner ni nani maana hapa huja mtolea maelezo lakini umeniambia nimuone! Labda kama sija kuelewa vizuri?
gyner ni daktari anayedeal na akina mama wajawazito na magonjwa mengine ya kina mama
 
Habari zenu mabibi na mabwana.

Naomba msaada wenu wa hali na mali wenye michango yakinifu na yenye mashiko itakayo nisaidia kumtibu mke wangu.

Mwenzangu kila anapo kuwa mjamzito huwa anasumbuliwa sana na kutapika, mimba ya kwanza ilikuwa balaa sana maana alianza kutapika ikiwa na mwezi mmoja na hali hiyo ikaendelea mpaka alipofikisha miezi tisa. Ilikuwa kila anacho kula hakikai anatapika kiasi kwamba ilifika wakati akawa anatundikiwa drip ya maji ambayo imechanganywa na dawa ya kuzuia kutapika na haikuwa inampa nafuu ya kudumu.

Niliambiwa kwa sababu ni mimba ya kwanza nivumilie, nimekaa apumzike miaka 5 kwa kuwa niliigopa sana ile hali lakini pia kuweka interval nzuri kati ya mtoto wa kwanza nawa pili.

Tumeamua tupate mtoto wa pili ila kinacho nishangaza mwezi bado niwa kwanza na ameanza tena kutapika kama kipindi akiwa na ujauzito wa kwanza! Kwa sasa kila anachokula anatapika, hii inanipa woga kuwa huenda akazoofu kama jinsi alivyo kuwa kwenye mimba ya kwanza.

Wabobezi na wataalamu wa haya maswala naombeni msaada wenu. Miaka 5 iliyo pita sikuwa memba humu. Hivyo naomba jf dokta iwe msaada kwangu katika kipindi hiki kigumu kwangu.

Naomba watakao changia wawe ambao wako tayari kunisaidia kwa ushauri/dawa au matibabu. SITAKI DHIHAKA TAFADHARI.

Mpeleke Aghakhan utapewa vidonge vya kuzuia kutapika,mfanyakazi mwenzangu ana mimba ya miezi miwili alipewa dawa pale zimemsaidia sana kamuone gynacologist nitakuulizia jina la doctor alieenda kumuona
 
Mkuu siko Dar niko mkoani. Naomba kama unaweza kunisaidia uwasiliane na huyo dada akuambie ni dawa za namna gani alipewa ili nione kama zitamfaa huku nikiwa nafanya mpango wife aende kwa gynacologist kwa ajili ya ushauri na matibabu zaidi. Asanteni sana kwa kuonyesha kujali kwenye hili, msaada wenu bado ni muhimu sana kwangu.
 
Mimi sio dr ila nilipatwa na hali kama iyo ya kutapika kuanzia mwezi wa kwanza hadi wa sita,nilijaribu kuzunguka hosp mbalimbali maana hiyo hali ilinidhoofisha sana.mwisho wa siku nilienda muhimbili nikaonana na Dr Ngarina akaniandikia dawa ya maji inaitwa PHAMACTIN toka siku iyo sikuwah tapika tena na nilikula vyakula vya kila aina.jaribu kumtafutia mkeo iyo dawa huenda ikamsaidia pia.ila ni vyema kabla hajaitumia mkaonana na gyner ili awaambie kama itamfaa.pole sana

Sitakaa ni msahau Dr. Ngarina, alipotaka kuniua kwa kunipa dawa za ugonjwa nisioumwa..

Mwaka 2002 nilienda hospital ya Massana nilikuwa na sumbuliwa na kikohozi na homa kali wakati wa usiku na mafua yasioisha.

Nilipokelewa hospitalini hapo na kupangiwa kuonana na Dr. Nilipoingia chumba cha daktari ndipo nilipokutana na Dr. Ngarina na kumuelezea tatizo langu na yeye kunipima na kuniambia na sumbuliwa na Pumu na Vidonda vya tumbo.

Aliniandikia Dawa za magonjwa hayo na mimi kuanza kuzitumia pasipo kupata nafuu zaidi ya kizidiwa na ugonjwa alimanusra kufa.

Hadi nilipokwenda hospitali ya TMJ na kugundulika nilikuwa na limonia kali..
 
Hi jf

Mke wangu ni mjamzito kwa sasa namshukuru Mungu..ila anatapika sana,chakula hakikai tumboni.Naomba ushauri atumie dawa gani kukata hiyo kutapika maana ni hadi hatari..asante
 
Mpe pole sana ...mie nilipewa dawa zinaitwa Nosic na nikaambiwa ninywe kidonge kimoja asubuhi ,na kimoja jioni kwa siku kumi na nne inasaidia,
Kwa ushauri zaidi mpeleke kwa Gyna atapata msaada
 
hi jf

mke wangu ni mjamzito kwa sasa namshukuru Mungu..ila anatapika sana,chakula hakikai tumboni..........naomba ushauri atumie dawa gani kukata hiyo kutapika maana ni hadi hatari..asante

Pole sana ndugu yangu
 
Je, umri wa hiyo mimba ni wiki ngapi? Kama bado ni mimba changa(below or around 12 weeks) ni kawaida kwa mjamzito kuexperience hali hiyo.

Je, ameshaanza clinic? Kama bado, nakushauri aanze clinic, na huko atapata msaada zaidi kuhusu hali hiyo.

Mara nyingine kunakuwa na vitu vinavyosababisha hali hiyo ya kutapika kuzidi sana, kama vile mimba ya mapacha,na matatizo yanayohusiana na mimba.

Aende hospitali afanyiwe na vipimo ikiwemo ultra sound ya hiyo mimba ili ku-rule out vitu kama ujauzito wa mapacha(multiple gestation), then daktari atamuanzishia dawa kadri inavyofaa na kwa dosage sahihi, usikubali kumuanzishia dawa tuu kienyeji, kila mgonjwa ni tofauti na daktari atatoa dawa sahihi na dozi sahihi kulingana na ugonjwa, na atamuongezea dozi au dawa au kumpunguzia kadri ya maendeleo yake yatakavyokuwa.

Nakutakia malezi mema ya ujauzito wa mkeo, umtunze na kumuangali vizuri zaidi katika kipindi hiki, ahsante sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom