Kapela Msonda
Member
- May 29, 2009
- 39
- 11
Kulundikana kwa magazeti ya MwanaHalisi kwenye baadhi ya vibanda vya magazeti jijini Dar es Salaam mpaka saa hizi za jioni ni dalili tosha ya kuisha mvuto wa gazeti hili lililokuwa kipenzi cha wapigania haki nchini pamoja na mhariri wake Kubenea kama ambavyo mvuto wa RAI/Mtanzania ulivyokwisha kwa mara moja na wahariri wake akina Mhingo na Balile kutokana na kutumiwa na Mafisadi.
Pamoja na kujitutumua safari hii na kichwa cha habari cha kudanganyia wasomaji "Mafisadi CCM sasa wageuka Mbogo", Kubenea bado anaonesha kubanwa koo na Mafisadi ambao inasemekana sasa wanammiliki kwa kurashiarashia habari hii na kuishia kuwananga wabaya wake wapya: Sitta, Mwakyembe na Nape!
Kilichonilazimu nijitose hapa JF ni tamko la MwanaHalisi kuwa litakuja wiki ijayo na taarifa nyeti juu ya hao wabaya watatu wapya wa Kubenea kuhusu chama kisichokuwepo cha CCJ kwa mujibu wa mtu mmoja aitwaye Dickson Ng'hily, anayetambulishwa kuwa naibu katibu mkuu wa CCJ wa zamani. Mimi na wenzangu tuishio Temeke pamoja na Mbunge wetu, tunamhakikishia Kubenea kuwa sasa anajiua mwenyewe kitaaluma kwani tunamjua sana huyo Ng'hily, si chochote, si lolote.
Bwana Dickson A. Mg'hily anajulikana sehemu mbalimbali hapa Dar es Salaam kama Mchungaji (sampuli ya akina Mtikila). Aligombea ubunge Temeke mwaka 2010 kwa tikiti ya CHADEMA, akabwagwa na CCM kwa sababu huyu jamaa ni TAPELI! Anajiita Mchungaji, lakini ukimpenyezea rupia tu yuko radhi kufunga ndoa na shetani. Nasema hivi kwa kuwa namfahamu sana msanii huyu.
Sitashangaa kuja kujua baadaye kuwa huyu baba hamfahamu Sitta, Nape wala Mwakyembe, ila kapenyezewa kitu yuko radhi kuapa kuwajua! Hafasi kabisa mtu huyu, lakini wiki ijayo ndo anapamba gazeti la MwanaHalisi!
Mtume! MwanaHalisi bye bye!