Kubenea niliyemfahamu mimi. Je, atasahau alikotoka?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,638
697,929
Simchagulii wala kumpangia maisha yake nitakuwa mwehu kama sio mwendawazimu.. Ila kuna vitu ningependa nimkumbushe.. Pengine anavikumbuka pia.. Sio rahisi kuvisahau kwakuwa ni matukio vivid na mengine ya kutisha.

Nimesubiri kwa hamu kubwa press conference aliyoitisha leo. Nilitaka kusikia atasema nini.. Nilikuwa na hamu kubwa mno.. Sidhani kama kaifanya.. Naweza kuwa nimepotoka lakini sijaona popote mapya kumhusu

Kumbukumbu zangu zinanirudisha nyuma way back 2007 around June.. Sikumbuki tarehe lakini ilikuwa siku ya Jumatano.. Nina kila sababu ya kuikumbuka hii siku.. Siku hiyo ndio nilikutana na Saidi kubenea kwa mara ya kwanza.. Nilikutana naye kwenye ishu ya gari yake Suzuki Escudo iliyonusurika kuungua moto akiwa bar kati ya mitaa ya Mango garden kinondoni na Komakoma Mwananyamala.

Police report ilionesha fault kwenye battery kulikopelekea kupiga short na gari kuanza kuteketea.. Lakini kiuhalisia na kwa mujibu wa Kubenea mwenyewe gari ilikuwa imepaki bila tatizo lolote na kuna kitu ilifanywa na kuanza kutoa Moshi na hatimaye moto
Aliyeokoa ni kijana mlinzi au moshaji sikumbuki vema.. Huyu aliona moshi na kuomba msaada.. Saidi alifika kwenye gari yake ikiwa imeshaanza kuwaka moto upande wa battery...

Walevi waliokuwepo walifanikiwa kufungua bonnet na kuzima moto kabla haujasababisha madhara makubwa... Kesi ilifikishwa police Oysterbay na baada ya uchunguzi wa awali gari ilivutwa na kupelekwa mkwajuni mtaa wa pili nyuma ya iliyokuwa Masai bar.

Sina hakika sana kama Kubenea alikuwa anaishi hapo lakini nina hakika nyumba hiyo alikuwa akiishi Zitto Kabwe kama mpangaji ama kama mgeni wa Kubenea
Hii ni story ya 2007 ambapo Waziri mkuu alikuwa Edward Lowassa akiwa kwenye kilele cha mnga'o wa nyota yake na akiwa kwenye harakati za kuchangisha fedha na vifaa kwa ajili ya elimu (shule za msingi Tanzania).

Kampeni hii ilikuwa na mwitikio mkubwa mno na wananchi wa kawaida, makampuni, matajiri na taasisi mbalimbali zilichanga na kutoa kwa moyo mmoja.. Hapa ndio mahasimu wa kisiasa wa Lowassa waliona kitisho cha wazi.. Ilikuwa ni lazima kumfunga speed governor.. Lakini EL naye hakuwa boya... Ndio hapa alianza kumtumia Kubenea kupambana na mahasimu wake KISIASA kupitia magazeti ya MWANAHALISI NA MSETO nadhani

EL kupitia mtandao wake na wasiri wake waaminifu alifanikiwa kupata taarifa mbaya za siri za wabaya wake naye akamtumia SK kuzianika hadharani.. EL alikuwa na mkakati wa mbali... Alitaka2 kumu outsmart JK na hatimaye kuwa the next president
Licha ya kuwa na nia ya kuwa rais lakini pia alihitaji mno kupanua wigo wa ulinzi na usalama baada ya kumpiga boss wake Mzee Malecela kwenye tenda ya ku supply ma land cruiser Tanzania mara baada ya kuvunja mkataba na waingereza( kitu kilichokuja kugharimu maisha ya mwalimu Mchonga).

Baada ya dili kukaa sawa Wajep walileta cash kwenye ma brief case na Mmasai akazifanya zote zake... Mzee wa Kigogo alikuja kuambulia manyoya tuu... Bifu ya baadae ya hawa wawili ilitokana na kudhulumiana kwenye mlungula.

Ndugu yangu unayeamini maneno ya wanasiasa kuwa watasitisha matumizi ya ma land cruiser kuna mengi huyajui... Ukiambiwa chama kina wenyewe kuwa mpole wala usikaze misuli kubisha

Ni kipindi hiki cha EL ndio gazeti la MWANAHALISI lilipata nguvu na umaarufu mkubwa mno.. Huku SK akipata direct access na PM EL na pengine ulinzi.. Siku moja tukiwa na SK mitaa ya Mwananyamala mochwari alipigiwa simu na EL akipewa updates za michango ili achapishe kwenye gazeti lake kwakuwa wabaya walikuwa wameshaanza upotoshaji kwenye magazeti mengine
Naendelea

Inaendelea..
Kubenea kupitia MWANAHALISI akawa mwiba mchungu kwa wanasiasa wengine.. Lakini siasa za Tanzania ni MTAFUTANO.. kuelekea mwishoni mwa 2007 EL akaundiwa kashfa ya RICHMOND na kufika February 2008 ikabidi ajiuzulu uwazirj mkuu... Alizidiwa kwenye mapambano

Kilichofuatia kinajulikana wazi.. Visasi na kutafutana.. EL alikuwa kajiuzulu lakini bado alikuwa na nguvu na connection pia.. MWANAHALISI lilizidi kuwa mwiba... Kilichofuatia 2008 kinajulikana wazi.. Kubenea alinusurika kifo na hata kuwa kipofu baada ya kuvamiwa ofisini kwake Mwananyamala na kujeruhiwa na kumwagiwa tindikali machoni
Sababu zilizokuja kutolewa baadae zinachekesha sana.. Nitaweka makala yake hapa

SK alipona na kuendelea na maisha. EL hakukata tamaa bado alipania kuwa the next president... EL si mpinzani na hakuwahi kuwa mpinzani.. EL alikuwa na hasira na kisasi pande zote mbili UPINZANI NA kwenye chama chake CCM.. EL ni Mmasai asiyeamini kwenye kushindwa.. Aliipenda CCM lakini ikamtenda.. Hakuupenda UPINZANI kwanza ulishamsimanga kwenye list of shame.. Lakini sasa hakuwa na jinsi ilikuwa ni lazima chombo cha kutimiza ndoto zake..

Nguvu ya Dr Slaa CHADEMA ilichagizwa kwa kiasi kikubwa na EL na MWANAHALISI.. SK ni mkosoaji si mwanasiasa.. Connection za EL zilizidi kukatwa na hatimaye akaangukia CHADEMA na SK naye kumfuata huko.. SK baada tu ya kuingia kwenye siasa MWANAHALISI lilipoteza mvuto na umaarufu.. Mwishoni likafungiwa..
Yaliyotokea ni mengi baada ya hapo
Dr Slaa aliyemkaribisha EL CHADEMA alimkimbia.. Wanajuana vema wasingewezana hata kama CHADEMA ingeshinda
Ya Mwakyembe yalipita humohumo..
Kubenea kupitia CHADEMA akaingia rasmi kwenye siasa na kuwa mbungo kupitia jimbo jipya la Ubungo.. Huko kwenye siasa kapwaya.. Huyu si mwanasiasa ni mkosoaji tena wa kuletewa habari.. Hakuna vyanzo tena vya kumpa habari na mfadhili mkuu kaomba poo... Uandishi hauwezi kumlipa tena... Nyakati si rafiki sana.. Familia inahitaji kuishi bado na ni lazima maisha yaendelee

Je Kubenea yuko tayari kufumba macho na kula matapishi yake?
Je Kubenea yuko tayari kusamehe na kusahau ili akae na watesi wake waliomkosakosa kumdhulumu haki yake ya kuishi?
Je abaki CHADEMA iliyombeba na kumsitiri kipindi chote cha miaka mine au avae uso wa mbuzi na kuamua kuunga juhudi?
Wazaramo wanasema KUMKOMA NYANI JILADI... je Kubenea ataweza kufanya hivyo? Ni wazi yuko njiapanda kwakuwa pia ana hofu ya kuwekwa ghalani ama kupelekwa kwa jirani kwakuwa ni kama bohari kuu imejaa kama pishi la mchele... Imejaa WAUNGA JUHUDI BANDIA

Jr.

Jr
 
Kumekucha tena tuendelee
Kama inavyofahamika wazi kuwa EL alikuwa na kiu kubwa ya kuwa rais wa Jamhuri na kwa vyovyote waliunda umoja yeye na JK way back 1995 ili mmojawao awe akiwa raisi basi mwingine awe makamu ama Waziri mkuu.. Aliyetibua hii mission alikuwa hayati Mwalimu Nyerere.. Lakini tukirudi nyuma zaidi miaka ile ya 80 mwishoni kipindi cha mzee Mwinyi wakati huo Mzee Malecela akiwa na nguvu kubwa pia naye alishaonesha nia ya dhati ya kuutaka urais... Kama kwa EL tu aliyetibua mipango yote alikuwa Mwalimu Nyerere mchonga meno.

Malecela alikuwa kajijenga mno ndani ya ccm kuanzia chini mpaka juu.. Wajumbe wote wa mikoani na wilayani walikuwa team yake.. Tunatambua dhima ya wakuu wa wilaya na mikoa.. Hawa ndio wasimamizi wa kamati za ulinzi na usalama.. Na ripoti zote za kila siku walikuwa wanaziwasilisha kwa Waziri mkuu... Malecela pia alishawahi kuwa Waziri mkuu
Mbinu za Malecela ndio zilikuja kuwa mbinu za EL.. Ni kama alikopi na kupest na kumbuka Malecela alishawahi kuwa boss wake..... Nia ya dhati ya Kukaa magogoni haikuwahi kuwatoka vijana wawili machachari almaarufu kama BOYS II MEN.. Jakaya na Lowassa.. Waliendelea kujiwekeza na hatimaye 2005 JK akawa rais na kumteua Lowassa rafiki wa siku nyingi kuwa Waziri mkuu.

Mambo yalikuwa ok mwanzoni lakini uchapakazi wake ulianza kuwatia shaka wengi. Alikuwa na kila elements za hayati Edward Moringe Sokoine wajina wake.. Hili liliwatisha wengi... Taratibu waziri mkuu akawa maarufu kuliko boss wake
Mpango wa wananchi uliovumbuliwa na Waziri mkuu EL wa kuchangia elimu kwa hiari ulikuwa na matokeo chanya ya kutisha.

Ndipo hapa JK akatonywa kuwa ukimuachia huyu 2010 hutoboi atakutoa.. Hii pesa ya UJENZI wa madarasa na kuchangia elimu account zake zilikuwa chini ya PM.. Kwahiyo alikuwa na madaraka nazo kwa asilimia mia.. Ikaonekana wazi anaweza kutumia mwanya huo kujikita zaidi na kukusanya pesa kwa ajili ya uchaguzi 2010

Ni hapa sasa watu kama SK walihitajika kwa nguvu mno.. Hasa kwenye propaganda na kujiwekeza kwenye kukubalika na kuwabana wengine... EL angekuwa na uchaguzi wa watu wengine wenye UTHUBUTU.

Kulikuwa na Mchungaji Mtikila RIP wa Liberty desk lakini huyu alikuwa keshaharibu na akawa hatabiriki wala kuaminika na tayari akawa na chama cha SIASA.

Kulikuwa na Mrema lakini naye alikuwa na nia kama ya EL na tayari alikuwa keshamalizwa na kitengo alipokimbilia NCCR-MAGEUZI.

Kulikuwa na waandishi na wanasiasa wengi lakini akachagua the most potential one.. Na hapa SL akalamba dume.

Kama tunakumbuka Mwanahalisi liliripoti ishu ya Richmond kwa namna ya kumkinga EL
Habari ni ndefu lakini SK aliendelea kuwa bega kwa bega na EL na baadae wakafanikiwa kujipenyeza CHADEMA kupitia Dr. Slaa.. CHADEMA ikawa juu lakini nyuma yake kulikuwa na mkono wa EL hasa kwenye connection na kitengo

Mambo yalipoharibika kabisa CCM EL alikimbilia CHADEMA ili akatimize ndoto yake.. Lakini ujio wake haukumfurahisha hata kidogo Dr. Slaa kwakuwa kama EL angefanikiwa kuwa rais thamani ya Dr Slaa ingeshuka sana kwakuwa connection yake sasa ina connect yenyewe... Yaliyofuatia yote yanajulikana.

SK amekuwa kiungo muhimu sana kwenye siasa za upinzani hasa CHADEMA na EL na Slaa.. Amefaidika pia.. Ametengeneza na kujenga jina lake ana mchango wake mkubwa tu.. Ndio maana nikahoji kama anaweza kuvaa uso wa mbuzi na kumuua nyani... Bahati nzuri amekuwa na tafakuri kuu

Jr

Jr
 
Nakumbuka mwanahalisi kwenye ubora wake ,Vipi Kubenea ana rudi nyumbani??


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Dah Mie ushauri wangu kwake kama gazeti limekufa na hapo kwenye hicho chama anapumulia mashine kwa maana asije akatuwa ghalani inabidi ajifunze kuwa mwanasiasa hata kwa kuigiza ale matapishi yake ili mradi maisha yaendelee kwa upande wake
 
Back
Top Bottom