Umoja Party ni CCJ iliyopotea na kupoteza umaarufu baada ya Usajili

kALEnga kidamali

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
542
733
Hivi vyama ambavyo huwa vikianza kwa mbwembwe na kusifiwa mapema kabla ya kutimiza hatua muhimu za usajiri huwaga vikipotea na kukosa mvuto baada ya kupata Usajili kamili, nakumbuka CCJ enzi za akina Sitta chama kilipata umaarufu kabla ya kusajiliwa ila baada ya kusajiliwa na kuitwa cck kilipoteza mvuto kabisa na sasa hakuna anayekiongelea Tena.

Yote ya yote niipongeze awamu ya sita kwa kuweka mazingira mazuri ya kisiasa hata ukapatikana uhuru wa kuunda chama kipya ambacho kinaonekana kupata matumaini makubwa ya kukua kutokana na dalili za kuruhusiwa kwa shughuli za kisiasa nchini kpind kifupi kijacho baada ya kuzuiwa kwa takribani miaka sita Hadi Sasa.

Ni ukweli usiopingika kuwa hakuna na hatukuona chama chochote cha siasa kikianzishwa AWAMU YA TANO licha ya uwepo wa chongamoto kadhaa za kiutawala zilizokuwa zikijitokeza zililizotosha kabisa kuanzisha chama kipya cha Siasa ili kuwasemea wananchi Kama ambavyo umoja party inaibuka kutokana na changamoto hizohizo za kiutawala Ila kwa Sasa imekuwa rahisi kwakuwa Utawala umetoa uhuru huo ambao ulikosekana.

Ushauri
hiki chama UMOJA PARTY hakikupaswa kushikamanishwa na jpm moja kwa moja ila kilipaswa kijinadi kwa sera na misimamo yake pia kupitia viongozi wake ambao wataonyesha kwa vitendo Yale yatakayo akisi utendaji wa JPM ili watu wenyewe waseme chama hiki kinamuelezea JPM tofauti na ambavyo wameanza kwa mbwembwe huku wakitumia picha ya JPM Kama nembo ya chama.

Kitendo ambacho ikitokea propaganda moja ndogo itakipoteza kabisa mfano mtu akisema je UMOJA PARTY kitakuwa chama cha watekaji, vipi kuhusu kununua wanasiasa kutoka vyama vingine?

Au ni cha sukuma gang hivyo tusio wasukuma tusijiunge? unaona kabisa namna ambavyo hicho chama kitapata shida kujitetea ili kieleweke.
 
Usiishi kwa kukariri, Mzee Mwinyi aliwahi kusemA; Kila zama na kitabu chake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom