Mwalimu huyu alipwe bei gani?

kavulata pole sana kwa mashambulizi unayopata kutoka kwa wachangiaji wa uzi wako. Kwa maoni yangu ni kwamba walipaswa kujikita kujadili hoja (kama ipo) ili wajipambanue bara bara kama great thinkers. Ila kwa upande wangu uzi wako sitashughulika nao kwa sababu mbili:
i.

Hizo sababu mbili hujaziweka umeishia kuweka roman one alafu hukuendelea, huyu mleta uzi nadhani alikuwa na hoja flani alitaka kuwakilisha lakini ameileta kivingine, kwa mtazamo wangu na hoja yake ni moja kwa moja hata ndio kwanza amemaliza shule anategemea kuingia chuo hivi punde na anaamini kwamba mafanikio kwenye ajira ni kuwa na division 1 O level na A level anasahau kwamba mitihani ni sehemu ya kipimo cha mwanafunzi hivyo kama hukupata kiwango flani four four ndio maana baada ya kwenda A level mtu anakwenda Certificate course ya miaka 2 au mmoja ili akitoka hapo aweze kuendelea na Diploma mpaka elimu ya juu. Huu ni utaratibu tu wa maisha kama mwalimu aliingia ualimu bila kuwa na Division 1 maana yake hastahili kudai mafao yake hata kama ni kidogo na walimu hao hao anaowaponda ndio hao hao waliompa hiyo Division 1 ya O - level na A - level. Lazima aelewe kwamba kila kada ina umuhimu wake na ndio maana kuna vyuo vya certificate mpaka university hivyo hata kwenye ofisi nyingi mgawanyo wa kazi upo kulingana na educational background na kila mtu regardless ya elimu ana umuhimu kwenye kazi yake. Hata hao walimu wa UPE unaowadharau wametoa mchango mkubwa sana kwa wale waliosoma elimu ya msingi miaka ya 80 na mwanzo wa 90 wanatambua mchango wao na kiukweli unaweza kupata Division one na bado ukawa kilaza kwa utaratibu huu wa sasa wa mitihani mpaka hisabati ni multiple choice. Soma mchango aliotoa Lyimo na kimeloki nadhani wamesema kitu muhimu
 
Last edited by a moderator:
Sikutarajia majibu tofauti na haya niliyoyapata kwenye uzi wangu huu kwasababu ukweli unauma, lakini meseji sent. Walimu hawa ndo wanaosababisha watoto wetu hawajui kusoma na kuandika, kutokana na uwelewa wao mdogo wanashindwa hata namna ya kula rushwa kwa kumfaulisha mtoto asiyejua kusoma na kuandika kwenda kidato cha kwanza. Mtu mwenye division 4 point 28, tena hapo zamani kidogo ilikuwa hata darasa la saba ni mwalimu gani????. Mwalimu gani anauza karanga na ubuyu darasani hata kama ana mshahara mdogo. Mwalimu wa aina hii naye anataka kumiliki nyumba, gari, kusomesha watoto international school kwa kutumia mshahara wake, nchi gani umeiona hii?.

Acheni ujinga wenu wapondaji.
 
Sijui watu wanaandika wakiwa wameshapata kitu cha malawi. Bila shaka utakuwa na mtindio wa ubongo kama huna akili kabisa
 
Migomo, migomo, migomo ya walimu! Eti kuna mwalimu anagomemea sh. 250,000 kwa mwezi, kwani huyu mwalimu anayelipwa mshahara huu anazo sifa gani za kulipipwa zaidi? Yeye ni form 1V division IV point 28 na wengine ni darasa la saba (UPE), wakaenda kozi ya ualimu wiki 4-6, hivi wanategemea miujiza gani kwenye mishahara yao? binafsi watu hawa waelemishwe wajue sifa walizonazo kwanza, hii ni sawa na nurse attendants, CO anayelalamikia mshahara mdogo pia kwa kujilinganisha na madaktari waliopata division I form IV na form VI na kwenda kozi miaka 6. Binafsi hawa ndio wanaotakiwa kusikilizwa zaidi maana ndio wanaopunjwa na mfumo wa uchumi wetu.

Huna adabu. Hao hao tangu awali ndo walimu wa Tanzania na walitufundisha na tumekuwa CEOs na key board unajua kubonyeza. Huna shukrani wewe. Loohhh sorry nimesahau umesoma Academy au Arusha Schoo enzi zile waalimu wenu huko wazungu, wakenya na waganda. Usitukane wakunga na uzazi ungalipo, wale extended family wako wanafundishwa na waalimu hao hao unaowadharau. Wewe na division yako ya point 7 na 3 umevifanyia nini. "I respect you my teachers, you introduced me to the world of letters, words and books and now I am someboby. I dedicate my life success to you, late and alive!"
 
Rekebisha kiswahili chako anagomemea
Migomo, migomo, migomo ya walimu! Eti kuna mwalimu anagomemea sh. 250,000 kwa mwezi, kwani huyu mwalimu anayelipwa mshahara huu anazo sifa gani za kulipipwa zaidi? Yeye ni form 1V division IV point 28 na wengine ni darasa la saba (UPE), wakaenda kozi ya ualimu wiki 4-6, hivi wanategemea miujiza gani kwenye mishahara yao? binafsi watu hawa waelemishwe wajue sifa walizonazo kwanza, hii ni sawa na nurse attendants, CO anayelalamikia mshahara mdogo pia kwa kujilinganisha na madaktari waliopata division I form IV na form VI na kwenda kozi miaka 6. Binafsi hawa ndio wanaotakiwa kusikilizwa zaidi maana ndio wanaopunjwa na mfumo wa uchumi wetu.
 
Sikutarajia majibu tofauti na haya niliyoyapata kwenye uzi wangu huu kwasababu ukweli unauma, lakini meseji sent. Walimu hawa ndo wanaosababisha watoto wetu hawajui kusoma na kuandika, kutokana na uwelewa wao mdogo wanashindwa hata namna ya kula rushwa kwa kumfaulisha mtoto asiyejua kusoma na kuandika kwenda kidato cha kwanza. Mtu mwenye division 4 point 28, tena hapo zamani kidogo ilikuwa hata darasa la saba ni mwalimu gani????. Mwalimu gani anauza karanga na ubuyu darasani hata kama ana mshahara mdogo. Mwalimu wa aina hii naye anataka kumiliki nyumba, gari, kusomesha watoto international school kwa kutumia mshahara wake, nchi gani umeiona hii?.

Acheni ujinga wenu wapondaji.

Mkuu hapana kwa ujumbe wako. Tangu awali hata wale wa middle school waliochaguliwa kwa ualimu walikuwa na low grade points na hii imeendelea hadi leo. Tatizo la watoto kutojua kusoma linachangiwa na changamoto nyingi sana ikiwemo:
(a) Changamoto za ukali wa maisha ambozo hazikidhiwi na mshahara mdogo wa waalimu vimesababisa waalimu kutafuta mbinu nyingine mbadala za kutafuta hela na kupoteza seriousness ya kazi yao (uza ubuyu, tambi, vitumbua,tena darasani)
(b) Ongezeko ka kuzaliana Tanzania ni kubwa hivyo darasa linakuwa na wanafunzi hadi 100 sasa na mikondo kama mitatu hivi hasa shule za mijini. Sasa basi mwalimu huyu anaweza ku-deal na utitiri huu wa wanafunzi? Zingatia not motivated!!!
(c) Kwa ukali wa maisha inabidi waalimu wabuni mbinu za tution na michango ya ulinzi na wazazi wasio na uwezo watoto hawapati tution na wanafeli. Zamani tution hakuna na tulifaulu ndiyo maana tuna uwezo wa kugonga key board hapa.
(d) Watoto wenyewe maendeleo ya sayansi na teknolojia yanafanya wale wasio kuwa na TV majumbani basi wanatumia muda wa mchana kuhudhuria vibanda vya TV zinazolipiwa mitaani 100!!! Je mtoto huyu atajua ya shule? Ile hela ya dala dala ni kiingilio.

Mkuu yapo mengi but just preamble others can add on. Tuheshimu waalimu, tuwasikilize la sivyo badala ya watoto kutojua kusoma sasa watafundishwa kuandika na kusome kinyume kama Quran!!! Usicheze na walimu na walisema wamerudi kazini kwa kinyongo!!!!! Kinyongo gani, mimi na wewe hatujui.
 
Migomo, migomo, migomo ya walimu! Eti kuna mwalimu anagomemea sh. 250,000 kwa mwezi, kwani huyu mwalimu anayelipwa mshahara huu anazo sifa gani za kulipipwa zaidi? Yeye ni form 1V division IV point 28 na wengine ni darasa la saba (UPE), wakaenda kozi ya ualimu wiki 4-6, hivi wanategemea miujiza gani kwenye mishahara yao? binafsi watu hawa waelemishwe wajue sifa walizonazo kwanza, hii ni sawa na nurse attendants, CO anayelalamikia mshahara mdogo pia kwa kujilinganisha na madaktari waliopata division I form IV na form VI na kwenda kozi miaka 6. Binafsi hawa ndio wanaotakiwa kusikilizwa zaidi maana ndio wanaopunjwa na mfumo wa uchumi wetu.

Mfumo wako wa kufikiri na kutafsiri mambo haupo sahihi, na ipo haja ya kufundishwa, usione aibu hata humu jf kuna watu watakufundisha bila ya malipo ili usije ukawa sehemu ya tatizo.
 
sikutarajia majibu tofauti na haya niliyoyapata kwenye uzi wangu huu kwasababu ukweli unauma, lakini meseji sent. Walimu hawa ndo wanaosababisha watoto wetu hawajui kusoma na kuandika, kutokana na uwelewa wao mdogo wanashindwa hata namna ya kula rushwa kwa kumfaulisha mtoto asiyejua kusoma na kuandika kwenda kidato cha kwanza. Mtu mwenye division 4 point 28, tena hapo zamani kidogo ilikuwa hata darasa la saba ni mwalimu gani????. Mwalimu gani anauza karanga na ubuyu darasani hata kama ana mshahara mdogo. Mwalimu wa aina hii naye anataka kumiliki nyumba, gari, kusomesha watoto international school kwa kutumia mshahara wake, nchi gani umeiona hii?.

Acheni ujinga wenu wapondaji.
we ni wa kusamehewa bure tu nfikiri hata ukaelishwa huelimiki
unakosea adabu baba yako kwa kumuambia angechelewa kukuzaa ungemzaa
maana hao madaktari unao wasema wamezalishwa na walimu hawa hawa unaowadharau leo
hata hiyo div 1 unayoisema uwezi ukazaliwa tu na kuweza kuiandika bila kupitia awali kwa walimu wa div4.
Pole sana kijana laana inakutafuna

Migomo, migomo, migomo ya walimu! Eti kuna mwalimu anagomemea sh. 250,000 kwa mwezi, kwani huyu mwalimu anayelipwa mshahara huu anazo sifa gani za kulipipwa zaidi? Yeye ni form 1V division IV point 28 na wengine ni darasa la saba (UPE), wakaenda kozi ya ualimu wiki 4-6, hivi wanategemea miujiza gani kwenye mishahara yao? binafsi watu hawa waelemishwe wajue sifa walizonazo kwanza, hii ni sawa na nurse attendants, CO anayelalamikia mshahara mdogo pia kwa kujilinganisha na madaktari waliopata division I form IV na form VI na kwenda kozi miaka 6. Binafsi hawa ndio wanaotakiwa kusikilizwa zaidi maana ndio wanaopunjwa na mfumo wa uchumi wetu.

Dogo pole sana kwa mashambulizi bila hatia!

Kimsingi ulitakiwa kuelimishwa kwa upendo tu, maana kinachofanya mtu alipwe sio elimu tu bali kazi anayofanya mtu, kwa mfano bungeni wabunge wote wanalamba 200,000 kama sitting (signing) alowance kuanzia kwa ma-Prof mpaka kwa akina Livingstone Lusinde (Std VII). Hata kama una div I ya form VI na ukataka kwenda kusomea ualimu ngazi ya cheti hutatofautishwa na huyo wa form IV div IV pt 28 mwenye certificate. Kwa misingi hiyo walimu kama kada nyingine wanadai mishahara kulingana na kazi wanayoifanya lakini pia kwa kuzingatia viwango vya elimu walivyonavyo.

Otherwise, baada ya elimu hiyo sasa naomba upokee comments za wenzangu kwa moyo mmoja ikiwa ni pamoja na matusi.
 
Usiongee kulingana na ukubwa Wa mdomo wako...,ifike mahal uwe na akil bila mwalimu d naamin hata hayo maandish usingeyaandika niny ndo huwa mnawazarau hata wenu wazazi.....M**b
 
naafikiri kuna mda lazima tujifunze kuamua mambo kama watu wazima ni kipi bora kumlipa mtu kutokana na kazi anayoifanya au elimu aliyonayo? na je katika migomo ya walimu madai yao ya msingi unayafahamu au ndo ile kukaa na kuandika unachokiwaza bila kujua kina madhara gani kwa taifa, au umesahau haya yote yanatokana na serikali iliyoko madarakani maana kama wangeweza kudhibiti mfumuko wa bei na kupunguza kodi kwenye bidhaa muhimu kama cement na mafuta unafikiri haya yote yangetokea wapi? na je ww unataka walipwe bei gani ndo uridhike au unafurahia hao wanaokaa na kupiga makofi bungeni ndo wawe na mishahara mikubwa kuliko wengine?
 
Migomo, migomo, migomo ya walimu! Eti kuna mwalimu anagomemea sh. 250,000 kwa mwezi, kwani huyu mwalimu anayelipwa mshahara huu anazo sifa gani za kulipipwa zaidi? Yeye ni form 1V division IV point 28 na wengine ni darasa la saba (UPE), wakaenda kozi ya ualimu wiki 4-6, hivi wanategemea miujiza gani kwenye mishahara yao? binafsi watu hawa waelemishwe wajue sifa walizonazo kwanza, hii ni sawa na nurse attendants, CO anayelalamikia mshahara mdogo pia kwa kujilinganisha na madaktari waliopata division I form IV na form VI na kwenda kozi miaka 6. Binafsi hawa ndio wanaotakiwa kusikilizwa zaidi maana ndio wanaopunjwa na mfumo wa uchumi wetu.
tatizo Lako mtoa hoja ni ku register ID huku ukijua dhahiri hujatibu Maralia
 
Sina mchango zaidi, maana yote yeshasemwa! Labda nikushauri uombe radhi kwa kuwaudhi waungwana wa humu jf, na uwaombe moderators waondoshe aibu hii! Pole sana mkuu ndo jf hiyo, ugreat thinker una gharama zake!
 
Back
Top Bottom